Rais Samia, naona kuna haja ya kulitazama upya Fao la Kujitoa katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii

Sasa kila mtu anaanza kuomba lake mama ataanza na lipi aache lipi? Mbona kama mnaanza kumpangia na hata mazishi bado.
 
Hili la kila mtu kumuomba mama amsaidie jambo hili au lile ni limesababishwa na katiba mbovu tulilyonayo
Marehemu alitumia na kufanikiwa vizuri ubovu hii wa katiba kwa kuhakikisha kila kitu maamuzi yanakuwa chini yake . na matokeo ndo haya

Mama atatatua mambo mengi sana kama akianzisha mchakato ili tupate katiba mpya.
 
Nashindwa kuelewa pale Mtu anaposema watanzania tunapenda vitu vya bure. Naomba nikuelimishe kidogo wewe unayesema tunapenda vitu vya bure. Kama kazini kwako au ulipoajiriwa unalipwa laki saba kama ndio mshahara wako NSSF wanachukua kutoka kwenye mshahara wako kiasi cha asilimia 10 ambapo itakuwa ni elfu 70 halafu mwajiri wako pia anakuchangia wewe mfanyakazi wake asilimia 10 ambapo itakuwa jumla 140,000 sasa hiyo hela ndio itakuwa inapelekwa NSSF kila mwezi hivyo kama utaongezewa mshahara basi hivyo hivyo kiwango cha fedha itakayopelekwa nssf itaongezeka ila asilimia ni kumi ya mshahara wako.

Sasa hicho kiwango cha mshahara kama utafanya kazi kwa miaka 15 ni kwamba unachukua 140,000*miezi 12 halafu utakayoipta ndio unazidisha kwa miaka 15. mfano (140,000*12=1,680,000 sasa hii unazidisha kwa 15=25,200,000 hivyo unapata zaidi ya milioni 25 kwani hapo nimepiga bila nyongeza ya mshahara hivyo kama mshahara utaongezeka utapata fedha nyingi zaidi. Tuje Kwa upande wa serikali, serikali inafaidika vipi na mshahara wako kama kodi?

Serikali baada ya kukata NSSF yako maana kama ulikuwa unapokea laki 70000 watatoa hapo hiyo asilimia 10 ya nssf (700000-70000=630000) hivyo hiyo 630,000 serikali inachukua hapo kiasi cha shilingi elfu 44500 kila mwezi kama kodi. Kwahiyo take home yako inakuwa 585500 (700000-70000ya nssf-44500 ya kodi ya serikali=585500) sasa hiyo 585500 ndio unaenda nayo nyumbani sasa hapa tunaanza kuifanyia kamchakato nikikosea mtanirekebisha

1. kodi ya nyumba chumba na sebule sehemu za kawaida 80,000
2. matumizi ya nyumbani kama matumizi ya kawaida 300,000
2. umeme kwa vile utakuwa umepanga na luku mnashare 10,000
3. Maji ya kutumia kwa mwezi 10,000
4. Nauli ya kwenda kazini tupigie gari moja 800*22= 17600
5. maji ya kunywa kazini 800*22= 17600
6. chakula kazini 2000*22 44000
JUMLA NI KIASI CHA 479200 JUMLA
Hivyo unabakiwa na kiasi cha elfu 106300
sasa hapa tuje kwa matumizi ambayo nikiweka hapa utalia
1. Ada ya watoto hapa kama watakuwa wanahitaji nauli mimi sijui wewe wajua
2. mjomba wangu yuko Mjini ngoja nimwombe fedha hao waliokusomesha utakuwa unawajua wewe mimi na Samiha Suluhu hatuwajui
3. kumetokea tatizo kijijini kwenu ngoja wakupigie simu mimi siju wewe wajua
4. bado kama hujaoa kuna wale tuma na ya kutolea unawajua wewe
sasa hapo mwaka wa 15 kuelekea wa 16 unasimamishwa kazi au unafukuzwa kazi bosi amekuchoka au kutokana na kusumbua sumbua na visababu kwamba naumwa leo siji kazini kumbe umeenda kufanya kibarua sehemu nyingine upate ada ya mtoto au utume mchango wa rambirambi kijijini hivyo bosi anachoka na ruhusa zako anakuandikia poor performance hivyo tunakufukuza kazi. unarudi kitaa hueleweki unasema ngoja nizame NSSF kuchukua mafao yako ukafungue kiduka unaambiwa hela haitoki mpaka ufikishe miaka 60 hapo unamiaka 35. keshokutwa baba mwenye nyumba anakuja na bili zote za kodi umeme maji, kodi sasa kwanini usichanganyikiwe ukaitelekeza familia na kukimbia? kwanini usisalimie michongoma? maana unaweza ukawa unatembea unaona kisiki cha mchongoma unaanza kusalimia habari ya hapo jamani. kumbe kisiki cha mchongoma
nimalizie kwa kusema NSSF sio msaada bali ni jasho lako.
 
Nashindwa kuelewa pale Mtu anaposema watanzania tunapenda vitu vya bure. Naomba nikuelimishe kidogo wewe unayesema tunapenda vitu vya bure. Kama kazini kwako au ulipoajiriwa unalipwa laki saba kama ndio mshahara wako NSSF wanachukua kutoka kwenye mshahara wako kiasi cha asilimia 10 ambapo itakuwa ni elfu 70...
Hongera sana Mku
 
Awali ya yote napenda kukupongeza kwa namna ulivyopokea kijiti cha mtangulizi wako Hayati Dkt. JPM, hongera na endelea hivyo hivyo.

Fao la kujitoa(withdraw benefits) kwa wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii imekua ndio mwokozi na chanzo kikubwa cha mitaji kwa wanachama wanaofukuzwa au kuachishwa kazi.

Sheria mpya ya hifadhi za jamii haina tija kwa mwanachama na pia haijulikani imetungwa kwa lengo la kumnufaisha mtu gani.

Fao la ukosefu wa ajira litolewalo kama mdadala wa fao la kujitoa limekua na lengo la kumfanya mtu aendelee kuajiliwa , tofauti na fao la kujitoa ambalo kwa zaidi ya asilumia 60 ya wanufaika wa fao hilo wamelua wakijiajiri na kuajiri wengine.

Wakati ukiendelea kuweka mambo sawa ofsini, mimi binafsi nakuomba sana kuiangalia vizuri sheria husika na ikibidi kurudisha fao la kujitoa kwa waajiriwa wa makampuni na mashirika binafsi ili kutengeneza mitaji kwa wananchi wakiwa bado na nguvu zao badala ya kuwapa hela nyakati za kustaafu wakiwa hawana hata nguvu za kuzifanyia kazi.

Nawasilisha.
 
Mama yetu, Rais wetu Mpendwa hili la Fao la kujitoa wahanga hapa tupo wengi mno hivyo kusababisha idadi kubwa ya watafuta ajira mitaani/nchini hivyo kusababisha mzigo mkubwa kwa Serikali of-which you declared it on your speech ulipo mwapisha makamu wako wa Rais.

Hivyo fao hili la kujitoa litatunufaisha wengi tuliowahi kupata ajira za mikataba ya muda mfupi na kuisha kujiajiri wenyewe katika shughuli mbali mbali za kujipatia kipato na kulipa kodi kwa serkali yetu.

Pia kufanikiwa kwa biashara zetu hizi ndogo ndogo zikikuwa zitasaidia kutengeneza ajira kwa wadogozetu wanaoendelea kuhitimu katika vyuo mbalimbali nchini hivyokupunguza mzigo na lawama kwa serikali. Naamini kati ya watu 10 watakao weza kuanzishabiashara au shughuli yoyote ya kiuchumi kuzalisha kipato baada ya miaka 5 atakuwa na uhitaji walau wa watu 2 kusaidia katika uzalishaji na utawala. hivyo kusaudia kutengeneza/kuzalisha ajira.

Pia mama nakushaurikutumia urafiki wa Zanzibar na nchi za kiarabu kufungua masoko ya nje ya viungo na matunda kwa nchi za Kiarabu pamoja na bidhaa zingine za kilimo ambapo uwepo wa masoko hayo na urahisi wa usafilishaji wa bidhaa hizo uta-amsha hari za sisi vijana kuwekeza kwa wingi ktk kilimo ambapo ndipo msingi/uti wa mgongo wa taifa letu kuzalisha bidhaa bora kwa wingi hivyo kujipatia kipato na hapo hapo kutengenezwa kwa ajira nyingi.

Mafao haya yakujitoa katika mifuko ya kijamii yatatufanya vijana kuweza kujiajiri katika kilimo cha Samaki, kilimo cha matunda,viungo,nafaka n.k, ufugaji wa mifugo hivyo kuzalisha nyama,mayai,ngozi n.k pia na biashara zingine ambazo zitachangia katika kodi hivyo kukuza pato la ndani.

Ahsante sana Mama yetu, kwakuwa wewe ni mama naamini utatusikia na kulichukulia hatua za haraka swala hili,
 
Hii Nchi ni ya ajabu sana, kila nikifikiria ile sheria wakati inatungwa ililenga kumnufanisha nani hasaa ?? Sipati jibu oh ! Mpaka uzeeke hivi kifo hawakukifikiria ??

Its obvious wamepanga kuwaibia wanachama na sio kuwasaidia.

Mh: Rais futa sheria zote kandamizi...
 
Hii Nchi ni ya ajabu sana, kila nikifikiria ile sheria wakati inatungwa ililenga kumnufanisha nani hasaa ?? Sipati jibu oh ! Mpaka uzeeke hivi kifo hawakukifikiria ??

Its obvious wamepanga kuwaibia wanachama na sio kuwasaidia.

Mh: Rais futa sheria zote kandamizi...
Zilikuwa na hatua za kuinusuru mifuko.. kama tulivyo sikia.. bado mifuko ina hali mbaya
 
Mheshimiwa Rais bila Shaka unafahamu sheria ya Sasa ambayo inazuia fao la la kujitoa jinsi inavyowanyima haki wafanyakazi wengi hasa wale walioko mashirika binafsi au wenye mikataba ya muda mfupi.

Tunaomba mheshimiwa urudishe FAO la kujitoa ili mikataba yetu inapokuwa imefikia tamati Basi tuweze kupata kile tulichokuwa tunachangia kwani kitatusaidia katika kuendeleA shughuli zetu, kuliko kuambiwa kwamba tutasubiri Hadi tufikishe miaka 60.

Mheshimiwa tunaomba usikilize kilio chetu kwani hii sheria Ni ya kikoloni na haifai kuendelea kuwepo
 
Hii Nchi ni ya ajabu sana, kila nikifikiria ile sheria wakati inatungwa ililenga kumnufanisha nani hasaa ?? Sipati jibu oh ! Mpaka uzeeke hivi kifo hawakukifikiria ??

Its obvious wamepanga kuwaibia wanachama na sio kuwasaidia.

Mh: Rais futa sheria zote kandamizi...
Kwa muda mrefu tumesikia kwamba hii mifuko ya hifadhi ya jamii, ambayo lengo lake kuu ni kutunza fedha za wastaafu, ina hali mbaya kifedha na sababu kuu ni serikali kuchukua fedha zake bila kuzirejesha.

Kwa maoni yangu hii ndiyo sababu iliyopelekea kuziunganisha hii mifuko kutoka kwenye ushindani wa mifuko mingi kwenda kwenye mifuko 2 tuu (wa serikali PSSPF na NSSF), na hii ni kwa sababu mifuko mingine ilikuwa na hali mbaya sana wakati mingine ikifanya vizuri.

Pia hili fao la kujitoa nadhani ililenga kubana pesa za mifuko kutoka kwa wingi kwenda kwa wafanyakazi kwa sababu hazipo, so bora ziwe zinatolewa kidogo kidogo. Sasa nimeshtuka sana jana kumsikia SSH akisema hajateuwa mkurugenzi wa ule mfuko mwingine kwa sababu una hali mbaya sana, mpaka waweke mambo sawa.
 
Well said! Nilimsikia mama jana wakati akiapisha makatibu wakuu na wakurugenzi alimwambia mkurugenzi mpya wa NSSF kuwa mwajiriwa akisitisha ajira yake kwa sababu yeyote ile apewe chake.Sasa tatizo wakitoka pale wanasahau walichoagizwa na kuanza kunyanyua mabega.
 
Rais Samia anaweza kufanya mengi kwa wafanyakazi hapa nchini ila bila kurudisha FAO la kujitoa, malalamiko ya wafanyakazi ndani ya nchi hii hayawezi kuisha na ataendelea kuonekena kwamba yeye na Serikali yake wanatumia sheria kandamizi na za kikoloni kuwakandamiza wafanyakazi wa nchi hii.

Mtu hawezi kupoteza kazi akiwa na miaka 25 au 30 umwambie kwamba mafao yake atasubiri Hadi akifika miaka 60.

Hivyo Rais afanye afanyavyo lakini bila Kuondoa huu upuuzi wafanyakazi tutazidi kumuona mnyonyaji wa wafanyakazi Kama walivyo wanyonyaji wengine.

Kama kweli wabunge wanaona hii sheria ina msaada kwa wafanyakazi basi wafanye marekebisho ya sheria hii ili na wao iwahusu na wawe wanasubiri mafaonyao wakifikisha miaka 60. Unatunga sheria unayoona ina tija ila wewe unajiondoa isikuhusu.
 
Rais Samia anaweza kufanya mengi wa wafanyakazi hapa nchini ila bila kurudisha FAO la kujitoa, malalamiko ya wafanyakazi ndani ya nchi hii hayawezi kuisha na ataendelea kuonekena kwamba yeye na Serikali yake wanatumia sheria kandamizi na za kikoloni kuwakandamiza wafanyakazi wa nchi hii....
Shida ni wabunge.

Wao mbona hawasubirii miaka 60? Mitano tu wanalamba pesa zao
 
Umeona eee. Haiwezekani bunge linatunga sheria kandamizi Kama Hizi. Kama wangejuwa zina tija kwa wafanyakazi basi wangeweka ziwahusu na wao
Wabunge ndio wakuambiwa, kikatiba mhimili wa bunge ndio unaweza kufanya mabadiliko kwa haraka na kwa uchambuzi zaidi.
 
Tunaomba mama yetu mpendwa mama samia tupia jicho lako kwenye fao la kujitoa, kunyimwa pesa yako mpaka ufikishe umri fulani ni uonevu hasa tuliopo kwenye sector binafsi, kazi zetu za mikataba, mikataba mingi ni ya muda mfupi tofauti na walio serikalini, kuna muda unatamani kuanzisha biashara ili uondokane kwenye ajira hizi zisizo tabirika.

Fao la kujitoa kwetu ni mtaji tosha kufanya biashara na hata kuongeza ajira kwa wengine, pesa inakaa tu bure haiongezeki waka kunufaika nayo mpaka uwe mzee ndio nn.

NSSF wamekosa ubunifu kwa wanachama kunufaika kwenye pesa tunayoweka kwao, wanafanya uwekezaji kwa kutumia pesa kwenye miradi mbali mbali kama za ujenzi wa nyumba ila sisi wanachama hatujawahi kutangaziwa au kuwekewa utaratibu wa kununua nyumba hizi basi hata kupangishwa kwa bei nafuu tukajisikia na sisi pia pesa yetu imewezesha kujenga majumba mazuri na kufurahia uwekezaji wa pesa zetu.

NSSF wanafanya biashara kwa pesa zetu na kutusahau wanachama, pili wamekuwa watu wa longolongo sana kufuatilia michango kwa waajiri, michango haipelekwi kwa wakati na mwajiri na hakuna linalofanyika na nssf ingawa wanayo sheria ya kumshurutisha mwajiri kupeleka michango ni kujisifia tu kuwa wanampiga faini mwajiri kama wanapigwa faini mbona bado hawapeleki hapa kuna kuna mchezo mchafu unaendelea kati ya nssf na waajiri, wanajuana.

Mwanachana unapoenda kufuatilia michango yako wanakimbilia kukupa adjustment form . ukipeleka adjustment form kwa mwajiri baada ya wiki unashangaa mfanyakazi kesi za ofisini zinakuwa nyingi mara mchelewaji, KPI zako zinashida, ili mradi tu wakutoe kazini ili usiwashtue wengine walio lala.

Mama tunaomba uruhusu fao la kujitoa tukajenge viwanda na kuajiri wengine na kujenga uchumi wa nchi ama nssf waruhusu kutumia dhamana ya pesa zetu kuchukua mikopo kwenye mabank.
 
Binafasi sikubaliani kabisa na huu utaratibu wa sasa wa NSSF kulipa fao la kukosa ajira kwa miezi 6, pesa ni zangu kwanini nisipewe zote kwa mkupuo ili niweze kupanga mambo yangu ya maendeleo ? Hiii sheria imekua kandamizi sana

Ajira za makapuni binafsi nyingi sio za uhakika na asilimia kubwa ni za mikataba, mmiliki wa kampuni muda wowote anaweza akaamua kufunga biashara zake na kurudi nchini kwake au asikuongeze mkataba hasa hasa kwa hawa wawekezaji wa kigeni.

Kwanini tuzungushane wakati lile ni jasho langu ? Inamana hii mifuko ya hifadhi ya jamii imelenga kutufanya tuwe watu wa kutegemea tu kuajiriwa miaka yote ? What if kama nataka pesa zangu niende nikajiajiri ?

Tunaomba muheshimiwa Rais mama Samia Suluhu Hassan amulike hizi sheria kandamizi na ikiwezekana azifanyie marekebisho na kurudisha fao la kujitoa.
 
Back
Top Bottom