Mfuko Wa Hifadhi ya Jamii -Zanzibar Zssf ni Mfuko wa Kinyonyaji na kandamizi dhidi ya raia wanyonge sekta binafsi

Emanueli misalaba

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
1,107
1,648
Bila shaka mnaendelea vizuri wana familia ya JF pia mnaendelea kuchukua tahadhari za kujilinda na Covid-19.
Bila kuwachosha niingie moja kwa moja kwenye kero na dukuduku nililonalo.

Mfuko wa Zssf Zanzibar una kero nyingi sana kwa wanachama hasa wa sekta binafsi 1) Mfuko huu ukiwa mwajiliwa utake usitake lazima ujiunge nao, kosa lipo kwa Serikali ya Smz na serikali ya Muungano kwa sababu kwanini kusingekuwa na utaratibu wa waajiliwa kuwa na changuo la mwajiliwa ajiunge na Zssf au Nssf nk km ilivyo kwa Tanzania bara?

Kero 2) Mfuko huu hauna fao la kujitoa pindipo mkataba wa mwanachama ukikoma, unaambiwa ni mpaka mda wa kustaafu utimie miaka 55-60 au mauti imfike mwajiliwa, hii ni challenge sana kwa watu wa sekta binafsi kwani wao mikataba yao iko tofauti na wafanyakazi wa serikalini ,hivyo palikuwa na ulazima wa kuwa na fao la kujitoa lkn sivyo.

Kero 3) Kuna watanzania bara wengi sana sana wapo sekta binafsi upande wa Zanzibar hasa kwenye utalii unakuta Mtanzania bara akiwa zanzibar amepata kazi Tanzania bara au mkataba umekoma serikali zote mbili Smz na ya Muungano hawajaweka utaratibu kwa wanachama km hawa hela yao iliyoko Zssf Zanzibar ihamishiwe mfuko wa Nssf au mfuko wowote ambao mwanachama huyu amekuja kujiunga nao tena baada ya kurudi Tanzania bara.

Zssf Zanzibar wanamwambia mfanyakazi huyu aende zake Bara asubirie hadi utimu mda wake wa kustaafu miaka 55-60 halafu aje kufuatilia mafao yake zanzibar, ni aibu kwa serikali zetu kusema kweli.

Kero 4) Wafanyakazi wa kigeni kwenye sekta binafsi zanzibar Wakenya, Waganda, Wahindi, Wazungu nk mikataba yao ya kazi ikikoma tu mara moja hupewa fedha zao na Zssf Zanzibar, mbona hawa hawawaambii kama ndugu zao watanzania bara warudi kwenye mataifa yao hadi mda wa kustaafu? Sisi kama wafanyakazi wa sekta binafsi zanzibar tunasikitika sana na mioyo yetu ikibumbujika damu ya maumivu dhidi ya stahiki yetu.

Kero 5) Serikali ya Smz na ya Muungano wako kimya wala hawaoni umuhimu wa kupeleka mswaada kwenye Baraza la Wawakilishi kwenda kubadilisha sheria kandamizi zinazolalamikiwa na wafanyakazi.

6) Kwenye kipindi hiki cha janga la coronavirus (Covid -19) Sekta binafsi nyingi hasa utalii zanzibar na sehemu nyingi hotels, tours nk zimefungwa wafanyakazi hawana kazi wapo nyumbani wengi wa wa ajili wao wamerudi kwao ulaya hivyo kampuni nyingi kutotoa mshahara kwa kipindi hiki, hatuoni Serikali ya Smz wala mfuko wa Zssf kuchukua hatua za kuwasaidia wanachama wake kipindi hiki

Ninawaomba/tunawaomba taasisi za kiraia na watetezi wa haki za kiraia watusaidie juu ya hili ili pawe na usawa na papatikane asilimia fulani ya ya kutupatia, asanteni sana.
 
Wadau hasa watu wa sheria, taasisi zenye kutetea haki za binadamu na yeyote yule mwenye ushauri au kutusaidia kupanza sauti zaidi tunaomba msaada wenu wenu.
Kwani taasisi hii ya Zssf inatesa sana kwa mda mrefu wanachama wake hasa raia wa kawaida sekta binafsi.
 
hao ZSSF ni wizi, hilo jambo ni kero kubwa na wanasiasa wamelika kimya. Kwanini wanyang'anye watu fedha zao kwa nguvu?
 
Pole sana..sasahivi hakuna wakuwasemea watu wa zenji..mana act wana mnofu mdomoni.

Pambaneni kwa kubemba hata mabango tu.

Mana hela za hiyo mifuko ni mtaji wa kisiasa wa chama cha mashetani kipindi cha kampeni.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hata CHADEMA nao hua wanakaa kimya tu, ishu kama hizi ndio fursa za wao kueneza ushawishi wao
 
Back
Top Bottom