Akili Unazo!
JF-Expert Member
- Feb 18, 2009
- 3,930
- 4,893
Katika maadhimisho ya Mei Mosi katika maombi yaliyowasilishwa kwa Rais Wetu Rais wa Tucta hakuzungumza lolote juu ya FAO la kujitoa NSSF baadala yake alijikita kuzungumza matakwa ya wafanyakazi wanaofanya kazi katika taasisi za Imma tu.
Nilijiuliza maswali mengi sana na mojawapo lilikuwa hivi TUCTA inafahamu kuwa Taasisi zilizoathirika na upunguzwaji wafanyakazi ikiwa Ni pamoja na baadhi kufunga oparesheni zao Tanzania Ni Taasisi na Makampuni binafsi? Je, wale wafanyakazi ambao hawajafikia huo umri wa kustaafu wanadai Hela Nyingi kwenye Hiyo mifuko ya Hifadhi ya Jamii?
Kweli TUCTA ilishindwa kuliangalia Hilo la kuwa sehemu ya hoja ya kuiwasilisha kwa Mama ili Hawa wahanga waruhusiwe kuchukua mafao Yao wakajifie Huko mbele?
Kweli TUCTA ilishindwa kujua kuwa taasisi binafsi imeathirika mno na watumishi wao wapo majumbani bila ajila Wala biashara huku wakiwa na fedha zao Nyingi zilizo kwenye hizo taasisi?
Kweli TUCTA imeshindwa kukuona Hilo ilihali inapokea Michango mingi ya wanachama kupitia TUICO, CHODAWU na Vyama vingi ambavyo vyote vinasimama wafanyakazi katika Taasisi binafsi?
Kweli hakuna Umoja wowote unaoweza kuundwa kwa ajili ya kuwawakilisha hili kundi lilosahaulika la wafanyakazi wasio na Akira kutoka Taasisi binafsi kuwasilisha ombi hili kwa Mama ili waruhusiwe kuchukua malikbikizo Yao kwenye hizo taasisi za hifadhi ya Jamii..
Nimekuja nikisikia Mh Jenista Mhagama akisema anatetea wanyonge? Ni wanyonge gani anaowasema Kama siyo Hawa walioathirika kwa kukosa ajira toka sekta binafsi?
TUCTA hamkuwatendea haki wafanyakazi wa sekta binafsi kwa kutoliona Hilo na kuwasilisha mahitaji yenu ya Watu waliopo kwenye ajira na ambao wanalilia kuongezewa mishahara na kupandishwa madaraja na kuwasahau hawa waliowengi ambao wamekuwa wakikosa wakuwasemea.
Ifike mahala Serikali ichunguze madhara ya Corona kwa watumishi wa sekta binafsi na Ione jinsi ya kurekebisha Sheria kandamizi ya kumlazimisha Mtu awe na umri wa miaka 55 ndiyo aweze kuchukua fao Hilo... Nani anajua ya kesho?
Kama wameweza kuwafungulia Akaunti zikizokuwa zimefungwa na TRA naamini na hili limawezekana kulifanyia kazi .
Shime viongozi unyesheni uteteze wa wananchi wanyonge kwa vitendo na siyo kwa maneno yasiyoakisi uhalisia.
Nawasilisha
Cc. Rais wa TUCTA