Mbishi 4 real
JF-Expert Member
- Jan 16, 2014
- 616
- 548
Kwako Muheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tunakuomba uondoe hii sheria kandamizi ya fao la kukosa ajira na uterejeshe fao la kujitoa ambapo mwanachama wa NSSF atakua na uwezo wa kuchukua pesa zake zote bila kujali kwamba ameacha kazi mwenyewe au ameachishwa.
Sheria hii ya fao la kukosa ajira inazidi kuwaweka vijana kwenye wimbi la umaskini na kuendelea kukumbatia ajira za manyanyaso sababu hata kama una mpango wa kuacha kazi ili uchukue pesa zako na kuweza kujiajiri na kutengeneza ajira kwa wengine huwezi sababu sheria ya fao la kukosa ajira inakubana sababu hutoweza kuchukua pesa zako zote na badala yake utapata tu asilimia 33.3% ya basic salary kwa muda wa miezi sita tu kisha wanaacha kukulipa.
Kuna watu wanafanya kazi kwenye mazingira magumu sana na wanatamani leo kesho waache kazi ili wajaribu kujiajiri lakini wakifikiria kuhusu ugumu wa kupata viinua mgongo vyao NSSF inabidi waendelee tu kuzikumbatia ajira zao hata kama zina manyanyaso kiasi gani sasa kwa hali hii tutaendelea kuwa na taifa la watu maskini kila kukicha.
Sina uhakika kama utaona huu ujumbe wangu ila naamini kuna watu wako watakufikishia haya malalamiko yetu.
Ahsante