Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Rais Samia akizungumza na Wakazi wa Jiji la Mwanza baada ya kuwasili kwa Ziara ya Kikazi leo Juni 12, 2023.
Akitoa Salamu kwa Wananchi wa Jiji la Mwanza waliojitokeza kwenye uwanja wa Ndege kumpokea, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ni Nchi moja, haiwezi kugawanyika wala kuuzika.
“Baada ya kusema hayo jioni imeingia, na ninaambiwa wapo wengine wengi kule nilitaka tu niwasalimie, lakini salamu moja kubwa ni kwamba Mama huyu ni Mtanzania. Atafanya kila analoweza kufanya Tanzania iendelee. Na Tanzania ni moja, haigawanyiki wala haiuziki. Kwa hiyo ndugu zangu mama ni Mtanzania, maendeleo yetu ndio muhimu. Kila linalofanyika ni kwa maendeleo ya Watanzania” amesema Rais Samia.
Aidha, Rais Samia amesema pamoja na kukagua miradi ya Maendeleo Mkoani humo, atashiriki pia maadhimisho ya miaka miwili ya Uchifu aliopewa Mkoani humo, Uchifu Hangaya.
“Kama chifu Mkuu sikuwaza kama nisije. Kama chifu Mkuu lazima nije. Mwanza ndiko nilikokabidhiwa Uchifu na Uhanganya, kwahiyo tumekuja kwenye maadhimisho yetu ya Miaka 2 ya Uhangaya lakini sherehe zetu zile za Bulabo. Sherehe za kutunza Mila na utamaduni wetu.” ameongeza Rais Samia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza uliopo Ilemela Mkoani humo
Aidha, Rais Samia amesema pamoja na kukagua miradi ya Maendeleo Mkoani humo, atashiriki pia maadhimisho ya miaka miwili ya Uchifu aliopewa Mkoani humo, Uchifu Hangaya.
“Kama chifu Mkuu sikuwaza kama nisije. Kama chifu Mkuu lazima nije. Mwanza ndiko nilikokabidhiwa Uchifu na Uhanganya, kwahiyo tumekuja kwenye maadhimisho yetu ya Miaka 2 ya Uhangaya lakini sherehe zetu zile za Bulabo. Sherehe za kutunza Mila na utamaduni wetu.” ameongeza Rais Samia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wa Ilemela waliofika kumpokea katika uwanja wa Ndege wa Mwanza mara baada ya kuwasili
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makalla amesema kuna kundi kubwa la vijana wa Bodaboda zaidi ya 300 wamejiandaa kumpokea Rais Samia mkoani humo huku akiweka bayana pia kuwa hali ya Usalama ni Shwari.