Sifael Mpollo

Member
Jan 20, 2018
24
34
Leo tarehe 20 Mei 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Samia Suluhu Hassan ataongoza uzinduzi rasmi wa Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma ambapo Rais wa JMT na watumishi wengine watahamia katika Ikulu hiyo.

Sherehe hiyo ya kihistoria inatarajiwa kuhudhuriwa na takribani watu 2,500.

Kupitia uzi huu, tutapeana dondoo, taarifa na pia kufuatilia matangazo ya moja kwa moja ya uzinduzi wa Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.​

UAMUZI WA DODOMA KUWA MAKAO MAKUU YA NCHI
Uamuzi wa Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi ulifikiwa katika Mkutano Mkuu wa 16 wa TANU uliofanyika tarehe 01 Oktoba 1973 ambao uliazimia Makao Makuu ya nchi yahamishwe kutoka Dar Es Salaam kwenda Dodoma.

Baadhi ya nyaraka/vitabu kama Sura ya Dodoma kilichoandikwa na Mamlaka ya Makao Makuu (1978) pamoja na A portrait of Dodoma - Capital Development Authority (1975) vinaeleza kuwa sababu za kuhamishia Makao Makuu jijini Dodoma ni kama ifuatavyo.​
  1. Dodoma iko katikati ya nchi na kwenye kitovu cha mawasiliano ya kitaifa (Hali ya kijiografia - Mji uko katikati ya nchi).
  2. Dodoma ipo karibu sana na Arusha ambayo ni Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
  3. Dodoma ipo mahali pema kwa hali ya usalama wa nchi na kuwa hewa yake nzuri ni muafaka zaidi katika hali ya ufanyaji wa kazi.
Akitoa hotuba katika Mkutano huo, Baba wa taifa na Rais wa Kwanza wa JMT Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema, "Makao Makuu ya kitaifa ya nchi ni kitu cha kudumu. Ikiwa tunakata shauri Makao Makuu yabakie hapa hapa Dar Es Salaam au yahamishiwe Dodoma, tutakuwa tunatoa uamuzi wa kudumu. Sababu ambazo ndiyo msingi wa uamuzi wetu, zinabidi kuwa ni sababu za kudumu. Tusizitumie sababu zisizokuwa za kudumu kufanya uamuzi wa kudumu."
IMG-20210805-WA0014.jpg
PICHA YA IKULU YA CHAMWINO
ikulu-pic.jpg

MATUKIO
Wananchi na Waalikwa

Shughuli ya uzinduzi imeanza alfajiri kwa wananchi na wageni mbalimbali kuanza kuwasili katika viwanja vya Ikulu mpya.

Saa 4:15 asubuhi
Rais Samia anawasili na kupokelewa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wastaafu akiwemo Ali Hassan Mwinyi na Jakaya Kikwete.

Mti wa Kumbukumbu
Rais Samia anapanda mti wa kumbukumbu ulio mbele ya jengo la Ikulu ya Chamwino ambalo lilianza kujengwa mwaka 2020 na kukamilika miezi 30 baadaye.
UZINDUZI WA IKULU
WhatsApp Image 2023-05-20 at 2.48.43 PM (1).jpeg

ikulu-pic (1).jpg

Kupandishwa kwa bendera
Rais Samia na viongozi wengine wanasimama mbele ya jengo la Ikulu kushuhudia bendera zikipandishwa juu ya mnara wa jengo hilo huku baragumu likipigwa.
Bendera tatu zinapandishwa ambazo ni bendera ya Rais, bendera ya Taifa na bendera ya Afrika Mashariki.

Upigaji wa ngoma, ishara ya ufunguzi
Rais Samia na Makamu wa Rais Dkt. Mpango wanaelekea kwenye lango kuu la kuingia ndani ya Ikulu na kupiga ngoma zilizowekwa hapo ikiwa ni ishara ya ufunguzi huo. Rais Samia anaingia ndani kukagua jengo lenyewe.
WhatsApp Image 2023-05-20 at 2.48.43 PM.jpeg

WhatsApp Image 2023-05-20 at 3.09.23 PM.jpeg

HUSSEIN MWINYI, RAIS WA ZANZAIBAR
Nampongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa mafanikio haya ya ujenzi wa majengo mapya ya Ikulu ambayo ni miongoni mwa hatua za kuendeleza dhamira za Baba wa Taifa, hayati Mwl. Julius Nyerere kupitia chama cha TANU mwaka wa 1973 ya kuweka azimio la kutaka Dodoma iwe Makao Makuu ya Serikali.

Hivi sasa sote tunashuhudia mafanikio ambayo tumeweza kuyapata katika utekelezaji wa mpango huo, ikiwemo leo katika ufunguzi wa Ikulu hii mpya hapa Chamwino jijini Dodoma.

Natumia fursa hii kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuipatia Serikali ya Mapinduzi Zanziba eneo hapa jijini Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa ofisi zake. Naahidi kuwa sisis nasi tutajenga ofisi za SMZ hapa Dododma ili kuwawezesha Watumishi wetu kupata mazingira bora ya kufanyia kazi.

Nikushukuru Mheshimiwa Rais kuwa katika Ikulu hii pia kumetengwa nafasi, au tuseme Ofisi ya Rais wa Zanzibar.

PHILIP MPANGO, MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA
Mh. Rais, Ikulu ulioizindua ni lulu ya Tanzania. Ni jingo lenye hadhi ya nchi yenye kipato cha kati. Nami naona ni taa ya kuipeleka nchi yetu ndani ya kipato cha juu ndani ya kipindi kifupi.

Ikulu hii ni kazi ya vichwa vya Watanzania. Ni kazi ya mikono ya Watanzania. Ni kazi ya kodi za Watanzania. Kwahiyo hongereni sana kwa kazi nzuri ya kupata Ikulu mpya yaChamwino.

Nawaomba (Watumishi wa Ikulu) jengo lile liheshimiwe. Na jingo lile litunzwe vizuri.

SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA TANZANIA
Tukio hili ni adhimu na kuleta faraja kwani kwa mara ya kwanza Watanzania tumeweza kujenga Ikulu yetu kwa kutumia rasilimali zetu na kutumia wataalamu wetu wa Kitanzania. Hii ni tofauti na Ikulu yetu ya Dar es Salaam ambayo ilielezwa vizuri hapa.

Sasa ndugu zangu, katika mchakato huu ni nguvu za awamu zote ziliingia katika mchakato wa kuifanya Dododma kuwa Makao Makuu yay a Serikali na kuwa Mji Mkuu wa nchi yetu. Ni ngu za awamu zote. Kabla sijaendelea nimkaribishe Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete.

JAKAYA KIKWETE, RAIS MSTAAFU WA TANZANIA
Leo historia imeandikwa, na imeandikwa kwa wino wa dhahabu. Hili ni jingo ambalo tumelijenga wenyewe. Wataaalamu wetu walichora. Wakasanifu. Tumetoa pesa zetu wenyewe kujenga na leo limekamilika.

Tukio hili umuhimu wake ni kuwa linahitimisha dhamira ya Baba wa Taifa ya kuhamishia makao makuu kutoka Dar es Salaam kuyaleta katikati ya nchi hapa Dodoma. Uamuzi ulifanyika mwaka 1971 lakini leo Mama yetu, umekamilisha.

Kilele cha uamuzi ule ni Rais kuhamia Dododma. Na si kuhamia Dododma kwa kupita tu, lakini Rais kuwa na ofisi yake Dodoma. Katika kila awamu kuna yaliyofanyika.

Katika kipindi change uamuzi wa msingi tulioufanya ni kuamua kwamba Ofisi ya Rais na makazi ya Rais yatakuwa hapa Chamwino. Wazo lililokuwepo mwanzoni ni kwamba pale Chimwaga ndipo yatakapokuwa makao makuu ya TANU na makao makuu ya Serikali.

Mimi nilipokuja nikaamua pale tujenge chuo kikuu. Kulikuwa na mjadala, mawazoo yalikuwa mengi lakini nikasema tutajenga chuo kikuu Dodoma.

Baada ya kuwa pale tumepatumia kwaajili ya chuo kikuu, Tulifanya mkutano na CBA. Mh. Lukuvi alikuwa Waziri wa Ardhi. Nikamwambia Ofisi ya Rais na Makazi ya Rais yajengwe Chamwino. Na ofisi za mawaziri zijengwe karibu na hapo.

Niliwaamba waende Kuala Lumpur. Kuala Lumpur, Malaysia wamejenga makao ya Serikali. Na kule walipojenga makao ya Serikali ndipo yalipo makazi ya Waziri Mkuu, ya Mfalme, huko huko. Nikawaambia nendeni mkaone. Na wamejenga vizuri. Unapita majengo ya ofisi za mawaziri halafu juu yake mwishoni ndiko ofisi ya Rais. Wamekwenda wamefanya hiyo kazi na ndiyo hii tunaiona sasa.

Rais wa Awamu ya Tano ndiyo ametoa msukumo mkubwa wa ujenzi.
 
Hongera sana Mwamba wa Africa John Joseph Pombe Magufuli A.k.A kajonii wanajaribu kukupoteza lakini hawatofanikiwa ulithubutu na ukaweza!
Nani anajaribu kumpoteza chadema, ACT au CUF? Maana CCM chini ya Samia ndo inamalizia miradi yake na kuizindua.
 
Ni jambo la kujivunia kufanya kitu chetu na sisi...matumaini yangu ujenzi wake umezingatia kuwa Dodoma ikipata tetemeko la ardhi itaendelea kusimama...
 
Ni jambo la kujivunia kufanya kitu chetu na sisi...matumaini yangu ujenzi wake umezingatia kuwa Dodoma ikipata tetemeko la ardhi itaendelea kusimama...
Kwa hakika, Ikulu Yetu, Fahari Yetu na Utambulisho Wetu. Ujenzi wake umezingatia mambo mengi, taarifa itakayotolewa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambaye ndiye mbunifu na msimamizi itakuwa na mengi ya kutujuza.
 
Dahh ila wabongo wahuni sana

Yaani wanajitahidi kukwepa kumtaja jpm kwa namna yoyote anapongezwa MAMA

Tazama Clouds TV
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Ikulu mpya iliyopo Makao Makuu ya Nchi, Dodoma, leo tarehe 20 Mei, 2023.

HUSSEIN MWINYI, RAIS WA ZANZAIBAR
Nampongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa mafanikio haya ya ujenzi wa majengo mapya ya Ikulu ambayo ni miongoni mwa hatua za kuendeleza dhamira za Baba wa Taifa, hayati Mwl. Julius Nyerere kupitia chama cha TANU mwaka wa 1973 ya kuweka azimio la kutaka Dodoma iwe Makao Makuu ya Serikali.

Hivi sasa sote tunashuhudia mafanikio ambayo tumeweza kuyapata katika utekelezaji wa mpango huo, ikiwemo leo katika ufunguzi wa Ikulu hii mpya hapa Chamwino jijini Dodoma.

Natumia fursa hii kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuipatia Serikali ya Mapinduzi Zanziba eneo hapa jijini Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa ofisi zake. Naahidi kuwa sisis nasi tutajenga ofisi za SMZ hapa Dododma ili kuwawezesha Watumishi wetu kupata mazingira bora ya kufanyia kazi.

Nikushukuru Mheshimiwa Rais kuwa katika Ikulu hii pia kumetengwa nafasi, au tuseme Ofisi ya Rais wa Zanzibar.

DKT. PHILIP MPANGO, MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA
Mh. Rais, Ikulu ulioizindua ni lulu ya Tanzania. Ni jingo lenye hadhi ya nchi yenye kipato cha kati. Nami naona ni taa ya kuipeleka nchi yetu ndani ya kipato cha juu ndani ya kipindi kifupi.

Ikulu hii ni kazi ya vichwa vya Watanzania. Ni kazi ya mikono ya Watanzania. Ni kazi ya kodi za Watanzania. Kwahiyo hongereni sana kwa kazi nzuri ya kupata Ikulu mpya yaChamwino.

Nawaomba (Watumishi wa Ikulu) jengo lile liheshimiwe. Na jingo lile litunzwe vizuri.

SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA TANZANIA
Tukio hili ni adhimu na kuleta faraja kwani kwa mara ya kwanza Watanzania tumeweza kujenga Ikulu yetu kwa kutumia rasilimali zetu na kutumia wataalamu wetu wa Kitanzania. Hii ni tofauti na Ikulu yetu ya Dar es Salaam ambayo ilielezwa vizuri hapa.

Sasa ndugu zangu, katika mchakato huu ni nguvu za awamu zote ziliingia katika mchakato wa kuifanya Dododma kuwa Makao Makuu yay a Serikali na kuwa Mji Mkuu wa nchi yetu. Ni ngu za awamu zote. Kabla sijaendelea nimkaribishe Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete.

JAKAYA KIKWETE, RAIS MSTAAFU WA TANZANIA
Leo historia imeandikwa, na imeandikwa kwa wino wa dhahabu. Hili ni jingo ambalo tumelijenga wenyewe. Wataaalamu wetu walichora. Wakasanifu. Tumetoa pesa zetu wenyewe kujenga na leo limekamilika.

Tukio hili umuhimu wake ni kuwa linahitimisha dhamira ya Baba wa Taifa ya kuhamishia makao makuu kutoka Dar es Salaam kuyaleta katikati ya nchi hapa Dododma. Uamuzi ulifanyika mwaka 1971 lakini leo Mama yetu, umekamilisha.

Kilele cha uamuzi ule ni Rais kuhamia Dododma. Na si kuhamia Dododma kwa kupita tu, lakini Rais kuwa na ofisi yake Dodoma. Katika kila awamu kuna yaliyofanyika.

Katika kipindi change uamuzi wa msingi tulioufanya ni kuamua kwamba Ofisi ya Rais na makazi ya Rais yatakuwa hapa Chamwino. Wazo lililokuwepo mwanzoni ni kwamba pale Chimwaga ndipo yatakapokuwa makao makuu ya TANU na makao makuu ya Serikali.

Mimi nilipokuja nikaamua pale tujenge chuo kikuu. Kulikuwa na mjadala, mawazoo yalikuwa mengi lakini nikasema tutajenga chuo kikuu Dododma.

Back
Top Bottom