Rais Samia kuna Rais mwenzangu aliniambia nimbadilishe Balozi, aliyepo kazini haendi na Mikutano hashiriki

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Mabalozi Wateule Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.

RAIS SAMIA: MAFUNZO YA UBALOZI YASIWE YA JUMLAJUMLA
Rais Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Mabalozi Wateule Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma, leo 16 Agosti, 2023 amesema mafunzo ya Mabalozi yawe yanaendana na maeneo wanayopangiwa kwa kuwa mahitaji hayapo sawa.

RAIS SAMIA: RAIS MWENZANGU ALINIAMBIA NIMBADILISHE BALOZI
Akiwaapisha Mabalozi Wateule Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma, Agosti 16, 2023, Rais Samia Suluhu Hassan amesema “Katika Nchi nyingine Mabalozi wetu sijui niseme hawajui wanachokifanya, wapo tu, nilikutana na Rais mwenzangu ndani ya #SADC akaniambia nimbadilishie Balozi kwa kuwa aliyepo kazini haendi na mikutano hashiriki.”

Amesisitiza baadhi ya Mabalozi hawatoi ripoti muhimu katika maeneo yao, ndio maana aliunde Kamati ya kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ili kubaini mambo kadhaa ikiwemo kasoro, mazuri na ugawaji wa Mabalozi.

RAIS SAMIA AWATAKA MABALOZI KUFUATILIA HATI ZA MAKUBALIANO ZILIZOSAINIWA
Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo wakati akiwaapisha Mabalozi Wateule Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Amesema “Mnapokwenda angalieni tumesaini nao kitu gani na vimefikia hatua zipi, mnapopeleka Hati za Utambulisho mkikaa na Rais au Mfalme wa Nchi husika zungumzeni mawili matatu ambayo yametekelezwa au yapo njiani.”

RAIS SAMIA: WIZARA ZOTE ZIFUNGIWE MTANDAO NA VIONGOZI TUWE NA ‘PASSWORD’
Akitoa mfano amesema Wizara ya Mambo ya Nje iwe na ubao wa mtandaoni unaoonesha Mikataba, Hati za Makubaliano na mengine yote yanayoendelea kisha Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Katibu Mkuu Kiongozi wawe na Neno Siri (password) ili waweze kusoma na kujua kinachoendelea.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Mabalozi Wateule Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma tarehe 16 Agosti, 2023.

RAIS SAMIA: MAFUNZO YA UBALOZI YASIWE YA JUMLAJUMLA
Rais Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Mabalozi Wateule Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma, leo 16 Agosti, 2023 amesema mafunzo ya Mabalozi yawe yanaendana na maeneo wanayopangiwa kwa kuwa mahitaji hayapo sawa.

RAIS SAMIA: RAIS MWENZANGU ALINIAMBIA NIMBADILISHE BALOZI
Akiwaapisha Mabalozi Wateule Ikulu Chamwino, Mkoani Dodoma, Agosti 16, 2023, Rais Samia Suluhu Hassan amesema “Katika Nchi nyingine Mabalozi wetu sijui niseme hawajui wanachokifanya, wapo tu, nilikutana na Rais mwenzangu ndani ya #SADC akaniambia nimbadilishie Balozi kwa kuwa aliyepo kazini haendi na mikutano hashiriki.”

Amesisitiza baadhi ya Mabalozi hawatoi ripoti muhimu katika maeneo yao, ndio maana aliunde Kamati ya kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ili kubaini mambo kadhaa ikiwemo kasoro, mazuri na ugawaji wa Mabalozi.

RAIS SAMIA AWATAKA MABALOZI KUFUATILIA HATI ZA MAKUBALIANO ZILIZOSAINIWA
Rais Samia Suluhu Hassan amesema hayo wakati akiwaapisha Mabalozi Wateule Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Amesema “Mnapokwenda angalieni tumesaini nao kitu gani na vimefikia hatua zipi, mnapopeleka Hati za Utambulisho mkikaa na Rais au Mfalme wa Nchi husika zungumzeni mawili matatu ambayo yametekelezwa au yapo njiani.”

Unapanga balozi nchi ya kiarabu kwa kuzingatia jina la kiarabu? Tumefika huku tena?
 
Dar es Salaam.
Walioapishwa ni Balozi Gelasius Byakanwa (Burundi), Balozi Habib Awesi Mohamed (Qatar), Balozi Imani Njalikai (Algeria), Ramson Mwaisaka (Rwanda), Hassan Mwamweta (Ujerumani), na Mohamed Juma Abdallah (Saudi Arabia).
Ewaaaa,
Sio kama aliepita
 
Ameiponda CHADEMA,eti ni ya matukio,halafu kamponda na balozi aliyerudishwaga.
 
Kwa 99% hapo anayetajwa ni Humphrey Pole Pole ambaye alikuwa ni balozi wa Tanzania nchini Malawi.

Binafsi simkubali kabisa Pole Pole katika harakati zake za kisiasa, lakini katika hili nitamtetea. Hapa Samia anamsingizia tu ili amtimue kwa aibu. Sio busara kumnanga mteule wako hadharani (hata kama hakufai).
 
Huyo balozi itakuwa amechukizwa na upuuzi unaofanyika hapa nyumbani wa ukandamizaji wa haki za binadamu na uuzwaji wa maliasili ndiyo maana ameamu kutokufanya kazi ipasavyo.we we mtu auze maliasili ategemee kuungwa mkono?Hiyo haiwezekani
 
Kwa 99% hapo anayetajwa ni Humphrey Pole Pole ambaye ni balozi wa Tanzania nchini Malawi.

Binafsi simkubali kabisa Pole Pole katika harakati zake za kisiasa, lakini katika hili nitamtetea. Hapa Samia anamsingizia tu ili amtimue kwa aibu. Sio busara kumnanga mteule wako hadharani (hata kama hakufai).
Polepole ni balozi huko Cuba
 
“Nilishakutana na Rais mwenzangu ndani ya nchi za kiafrika, ndani ya Sadc, akaniambia nimbadilishie balozi, akisema uliyeniletea hata kazini haendi, mikutano hashiriki, yupo yupo tu, hatuelewi, Tanzania hatujawazoea hivyo, sasa labda umbadilishe, nikamwambia nimekusikia,” amesema Rais Samia na kuongeza;

Hayo maneno yamekaa kizushi mnoo.
Yaani rais wa nchi anawezaje kufuatilia ratiba za kuja kazini za balozi wa kigeni nchini wake?
 
Kwa 99% hapo anayetajwa ni Humphrey Pole Pole ambaye ni balozi wa Tanzania nchini Malawi.

Binafsi simkubali kabisa Pole Pole katika harakati zake za kisiasa, lakini katika hili nitamtetea. Hapa Samia anamsingizia tu ili amtimue kwa aibu. Sio busara kumnanga mteule wako hadharani (hata kama hakufai).
Hivi uko na taarifa sahihi juu ya Pole Pole alipo kwa sasa?.Mbona ni muda mrefu sana alishatolewa hapo Malawi na yupo Cuba sasa.
 
Kwa 99% hapo anayetajwa ni Humphrey Pole Pole ambaye alikuwa ni balozi wa Tanzania nchini Malawi.

Binafsi simkubali kabisa Pole Pole katika harakati zake za kisiasa, lakini katika hili nitamtetea. Hapa Samia anamsingizia tu ili amtimue kwa aibu. Sio busara kumnanga mteule wako hadharani (hata kama hakufai).

Breaking! TANESCO yashindwa kesi Marekani na kutakiwa kuilipa IPTL billioni 320!
 
Polepole ni balozi huko Cuba
Nimedit nikilenga kuwa hapo alilengwa yeye japokuwa Samia aliweka kama fumbo ili tubakie kufikirie sasa. Na tukihoji aseme mabadiliko yalishafanyika zamani na hiyo ilikuwa ni story tu wakati wa kuwaapisha mabalozi hawa wapya.
 
Kwa 99% hapo anayetajwa ni Humphrey Pole Pole ambaye alikuwa ni balozi wa Tanzania nchini Malawi.

Binafsi simkubali kabisa Pole Pole katika harakati zake za kisiasa, lakini katika hili nitamtetea. Hapa Samia anamsingizia tu ili amtimue kwa aibu. Sio busara kumnanga mteule wako hadharani (hata kama hakufai).
Yeye Samia mwenyewe anahitaji kubadilishwa. Hili ni suala la ''nyani haoni kundule''.
 
Hivi uko na taarifa sahihi juu ya Pole Pole alipo kwa sasa?.Mbona ni muda mrefu sana alishatolewa hapo Malawi na yupo Cuba sasa.
Nisome vyema utanielewa.
Pole Pole ndio target, muda sio mrefu hata huko Cuba atafukuzwa na mama halafu kisingizio cha Mama kitakuwa, aliharibu Malawi nikamrudisha nyumbani (kimyakimya) na kumpeleka Cuba, sasa na huko Cuba ameharibu.
 
Breaking! TANESCO yashindwa kesi Marekani na kutakiwa kuilipa IPTL billioni 320!
Duh!
Soon nchi itafilisika
 
Breaking! TANESCO yashindwa kesi Marekani na kutakiwa kuilipa IPTL billioni 320!
Wewe ndiye uliyekuwa unakejeli MIGA
 
Breaking! TANESCO yashindwa kesi Marekani na kutakiwa kuilipa IPTL billioni 320!
Symbion katupiga Bilioni 300 na IPTL Bilioni 320!
Hizi dili za Watu,Tena zinasukwa humuhumu ndani ya nchi!
 
Back
Top Bottom