Rais Yoweri Museveni ampa zawadi Rais Samia ikulu ya Zanzibar

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
1710451563720.png
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais William Ruto wa Kenya wakiangalia picha ya Viongozi wa Nchi mbalimbali za Afrika wakati Rais Museveni alipomkabidhi Rais Samia zawadi hiyo baada ya mazungumzo yao Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 14 Machi, 2024.

Kwenye mazungumzo yao wamezungumzia masuala ya mtangamano wa Afrika Mashariki hususan umuhimu wa kuharakisha zoezi la kukusanya maoni ya Wananchi Juu ya muundo na maeneo ya kuangaliwa katika Rasimu ya Katiba ya Fungamano la kisiasa la Afrika Mashariki (EAC Political Confederation). Zoezi hilo limeshafanyika katika nchi za Burundi, Uganda na Kenya na linatekelezwa na Timu ya Wataalamu inayoundwa na Wajumbe watatu kutoka kila nchi Mwanachama.
 
Baba wa Afrika Mashariki wa sasa. H.E YKM

Geopolitiking

Naona safari hii wanataka "Baba Odinga" apite kule.

Nchi za Afrika Mashariki zincheleweshwa maendeleo na siasa za Uharakati.
 
Nimependa hilo la kukusanya maoni.
Vipi kuhusu maamuzi ya wananchi kutaka kujiunga ama kutojiunga na Jumuiya? Au tunaenda Kiafrika ambapo Mkuu wa nchi ndiye fina and conclusive?
 
mpaka sasa tanzania tuna ikulu 3 ambapo rais ana amua jambo fulani alifanyie dodoma jingine tunguu jingine dar er salaam
 
Watanzania mnaoshiriki kwenye Hilo zoezi kuweni wazalendo na mtumie akili zenu zote.

Lindeni maslahi yetu.
 
Coallion of willing.....tulinde ardhi na maliasili zetu kuna ufisi hapo nauonaaa
 
Nimependa hilo la kukusanya maoni.
Vipi kuhusu maamuzi ya wananchi kutaka kujiunga ama kutojiunga na Jumuiya? Au tunaenda Kiafrika ambapo Mkuu wa nchi ndiye fina and conclusive?
wawakilishi wetu bunge la Africa mashariki wanatosha kuwakilisha maoni ya waTz🐒
 
Back
Top Bottom