Rais Samia awa mgeni rasmi katika Mkutano wa mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO) Dodoma

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565


Rais Samia: Nakushukuru Waziri wa Maendeleo ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Uongozi wa baraza la Mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kunialika kwenye mkutano huu wa mwaka wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali nataka nikiri kuwa nimefurahi sana kushiriki katika mkutano huu.

FAhR3awXoAElxT6

Rais Samia Suluhu Hassan ameshiriki Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO's) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma leo Septemba 30, 2021. Akiwa katika Mkutano huo Rais Samia amesema mambo yafuatayo:

Rais Samia: Najua na ilishasemwa hapa baadhi yenu mtakuwa mnajua kabla sijaingia kwenye masuala ya siasa niliwahi kufanya kazi kwa takribani miaka kumi kwenye Mashirika yasiyo ya kiserikali. Nilikuwa muanzilishi wa Taasisi ya kuendeleza wanawake Zanzibarya mwanzo Angoza. Kwahivyo mimi pia naweza kusema ni zao la Mashirika yasiyo ya Kiserikali.

Rais Samia: Nipende kuchukua nafasi hii pia kuipongeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa kubuni wazo la kufanya mkutano wa pamoja wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kila mwaka.

Rais Samia: Mikutano ya aina hii itakuwa inajumuisha wadau wengine zikiwemo taasisi za serikali, hili ni jambo zuri sana kama mnavyofahamu mara kadhaa kumekuwa kukijitokeza hali ya kutoelewana na kuaminiana kati ya serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Rais Samia: Mara kadhaa kumekuwa na hali ya kutoelewana na kuaminiana kati ya Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali, kupitia mikutano hii hali hiyo itaondoka. Tunaamini kwenye majadiliano hakuna linaloharibika.

Rais Samia: Masuala mengine yaliyopigiwa kelele ni masuala ya kodi, uhamiaji na ajira kwa mashirika yasiyo ya kiserikali. Ni imani yangu kwamba kupitia mkutano huu, haya yote mtayazungumza vizuri.”

Rais Samia: Tunafahamu zipo changamoto kwenye mifumo yetu ya kodi na pia kuna baadhi ya taasisi zinastahili kupata misamaha ya kodi. Tumeanza kufanyia kazi yote hayo. Tumeandaa kitini kitakachoeleza namna NGOs zinazofanya kazi kwa hisani zikakavyonufaika na misamaha ya kodi.

Rais Samia: Ni ukweli usiopingika kuwa mashirika yasiyo ya kiserikali yana mchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa na ustawi. Kama Serikali isingeruhusu kuwepo kwa masharika yasiyo ya kiserikali, kungekuwa na mzigo mkubwa katika suala la ajira

Rais Samia: Kuhusu vibali vya kazi na ukaazi utakumbuka hivi karibunu nilieleza hatua zilizochukuliwa na serikali kutatua changamoto hiyo ambapo tangu mwezi April 2021 Idara ya Uhamiaji na Idara ya Kazi wameanzisha mfumo wa kielektroniki ambao umepunguza sana urasimu. Nimeambiwa kwa sasa endapo muombaji atakuwa amekamilisha taratibu zote anapata kibali katika kipindi cha siku moja hadi tatu kutoka siku 14 na zaidi zilizokuwapo hapo nyuma.

Rais Samia: Kuhusiana na suala la urasimu wa vibali vya kutekeleza miradi natoa rai kwa sekretarieti za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa mashirika yasiyo ya kiserikali tufanyenao kazi kwa pamoja ili kwa pamoja tujenge nchi yetu. Waswahili wanasema kidole kioja hakivunji chawa. Kwahiyo kidole cha NGO na Serikali kikiungana chawa atavunjika tu atake asitake

Rais samia: Kabla ya kumaliza hotuba yangu ningependa kusisitiza kuwa Mashirika yasiyo ya kiserikali mjotahidi kuoanisha mipango yenu na vipaumbele na mipango ya kitaifa. Yaani mashirika yasiyo ya kiserikali yafanye kazi kwa kuangalia mipango ya kitaifa.

Rais Samia: Pili natoa wito kwa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kuongeza uwazi katika utendaji wa kazi zenu

Rais Samia: Aidha, nayahimiza mashirika yasiyo ya serikali, hususani ya ndani, kupunguza utegemezi. Ajenda za kidunia zinavyobadilika, wahisani wanabadilisha sera zao za kutoa fedha, unajikuta lile uliloanzishia taasisi, si kipaumbele kwao, mnajikuta hamna fedha za kujiendesha.

Rais Samia: Pia natoa wito kwa mashirika yasiyo ya Serikali kufanya kazi zinazoendana na tamaduni, mila, desturi na maadili ya Kitanzania.

Baada ya Hotuba Rais Samia azindua taarifa ya Mashirika ya kiserikali pamoja na kupiga picha za kumbukumbu na makundi mbalimbali.
 
Mama bado anaupiga mwingi sana......akiweza kufuta kesi Mbowe baasiiiio
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Tendo la kuifanya Buchosa kuwa wilaya ya Geita, imepokelewa vibaya sana na wakazi wa Buchosa.
 
Mh.Rais Chifu Mkuu na kipenzi chetu Chifu Hangaya amezikumbusha asasi za kiraia(AZAKI-NGO's) kufuata SHERIA ,MILA NA TARATIBU ZA NCHI.

My Take : Sheria na taratibu za UHAMIAJI zinawahusu pia....hawana mlango wa kuzikwepa.....

Sheria na taratibu za TRA....zinawahusu pia....hawana mlango wa kuzikwepa ......


N.B

AZAKI zikumbuke pia kuendana na AJENDA/ SERA ZINAZOIBULIWA NA SERIKALI na si tu kusubiri AJENDA ZA KIDUNIA ambazo huwa zinabadilika mara kwa Mara na kipindi kingine zinabadilika kabla ya Sera hizo KUTEKELEZWA ndani ya nchi zinazoendelea kutokana na WADAU WA MAENDELEO(watoa fedha) kuchelewesha KUTOA MAFUNGU(fedha) na mwishowe kutopatikana TIJA iliyokusudiwa.


#SiempreJMT
#NchiKwanzaKablaYaMaslahiMengineyo
#KaziIendelee
 
Back
Top Bottom