Rais Samia ni mwanamageuzi ndani ya wakati sahihi

Billal Saadat

Senior Member
Nov 30, 2022
169
356
Baada ya kuapishwa Machi 19,2021 Rais Samia alitamani kuona Tanzania inasimama peke yake bila kutegemea mikopo, lakini ukitizama katika hali tulivyokuwa nayo ilikuwa ni sawa na kujichimbia shimoni!

Siku zote palipo na matatizo kuna mzizi wa tatizo lenyewe huo ndiyo wa muhimu kuukata! Matunda ya kuukata mzizi yanahitaji uvumilivu ili matokeo yake yaonekane Rais Samia ameukata mzizi na matunda yanaonekana!

1. Alijifunza makosa ya utawala kwa Serikali iliyopita ambayo alihudumu hakuchagua lawama alitengeneza njia ya kutatua matatizo kwa kufanya kazi Rais Samia alifahamu ili tuendelee tunahitaji mfumo mzuri wa kulipa kodi si ule uvamizi katika akaunti za watu na kubambika kodi utaokimbiza hadi wawekezaji.

2. Aliomba muda wa kufanya kazi! Hakujifunza kuamka asubuhi kufanyia kazi story za mitandao na magazeti na kuwafukuza kazi walioshutumiwa bila kufanyia due process katika uongozi kuna fitna, majungu na kuoneana kijicho Rais Samia amejifunza serikali iliyo bora ni ile inayoheshimu utawala bora.

3. Amewavuta World Class Talent kwenye kila kona ya utumishi wa Umma kwa ajili ya kumsaidia kufanya kazi! mifano ipo wazi inaonekana.

4. Nchi haipoi kama maji, Rais Samia ameonyesha uwezo mkubwa wa kusimamia usalama wa nchi pamoja na kuifungua nchi katika uhusiano wa kimataifa ni vigumu sana kwa maadui kupenyeza na kuleta chokochoko. Amemudu kubadili spy master wawili pamoja na kuleta sera mpya ya mfumo.

5. Kuipa thamani sekta binafsi,wafanyabiashara na wajasiriamali hawa ni watu muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu katika mengi yaliyokwishafanyika katika mipango ya maendeleo wamepata nafasi ya kushiriki kutoa mchango wa mawazo na kuijenga nchi.

6. Falsafa ya 4R

7. Serikali imeweka institutions perfomance kwa taasisi zote zinazoingiza kipato (generate income) kila taasisi imewekewa target ya kukusanya ikiwemo TRA kama zitashindwa kujiendesha na kuongeza kipato kwa Wakuu wa Taasisi watafute shughuli nyingine za kufanya jambo hili limeongeza efficiency kwa mashirika ya Umma.

8. Ameyafuta na kupunguza mashirika yanayoikwamua Serikali vilevile Rais Samia anataka kuunganisha mashirika ya Umma kuwa na idadi ndogo yenye ufanisi. Kupunguza utegemezi wa mashirika ya Umma kutoka Serikali kuu.

9. Ameweka zuio la uingizaji wa nafaka kama mchele, mahindi pamoja na Sukari isipokuwa kwa dharura kipindi cha majanga na hii ni kwa ajili ya kuhamasisha kilimo cha mazao hayo hapa nyumbani. Kibali cha kuingiza mchele ni adimu kama machozi ya Simba.

10. Benki kuu kununua dhahabu kwa ajili ya back up ya sarafu yetu lengo la Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia ni kununua tani 6000 za dhahabu kila Mwaka. Jambo hili limeimbwa sana muda mrefu Rais Samia amelitekeleza now tumeimarisha sarafu pamoja na akiba ya fedha za kigeni.

#MamaYuKoKazini

IMG_5261.jpg
 
2. ...Hakufanyia kazi story za mitandao na magazeti na kuwafukuza kazi walioshutumiwa bila kufanyia due process katika uongozi kuna fitna, majungu na kuoneana kijicho Rais Samia amejifunza serikali iliyo bora ni ile inayoheshimu utawala bora.
Hapa namsifu sana- fitina na majungu kayakataa kabisa. Hata zile story za mwenge na ukaguzi wa Miradi zimekaa kifitina na majungu. Hufuatilia mwenyewe kwa njia zake kupata ukweli. Mradi mkubwa wa mabilioni huwezi ukauchambua kwa safari ya siku moja.
5. Kuipa thamani sekta binafsi,wafanyabiashara na wajasiriamali hawa ni watu muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu katika mengi yaliyokwishafanyika katika mipango ya maendeleo wamepata nafasi ya kushiriki kutoa mchango wa mawazo na kuijenga nchi
Sekta binafsi ni muhimu. Ndio kuna matatizo ambayo yanarekebishika kwa kuboresha sheria na kuelimishana. Dhana kuwa matajiri watokomezwe ni potofu. Hapa Mama kafanya vizuri sana.
6. Falsafa ya 4R
Hii falsafa iwekwe (itafsiriwe) kiswahili kama ilivyokuwa kwa Azimio la Arusha. Ni falsafa muhimu sana, si tu ifahamike kwa wasomi tu bali kwa watanzania wote. Ni kazi ya BAKITA kuifanyia kazi, na wizara ya elimu kuifundisha toka darasa la kwanza, hata chekechekea ikibidi.
9. Ameweka zuio la uingizaji wa nafaka kama mchele, mahindi pamoja na Sukari isipokuwa kwa dharura kipindi cha majanga na hii ni kwa ajili ya kuhamasisha kilimo cha mazao hayo hapa nyumbani. Kibali cha kuingiza mchele ni adimu kama machozi ya Simba
Sina hakika. Uthibitisho zaidi utolewe.
10. Benki kuu kununua dhahabu kwa ajili ya back up ya sarafu yetu lengo la Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia ni kununua tani 6000 za dhahabu kila Mwaka. Jambo hili limeimbwa sana muda mrefu Rais Samia amelitekeleza now tumeimarisha sarafu pamoja na akiba ya fedha za kigeni
Sina hakika. Takwimu za Benki kuu zinahitajika kujua uhalisia.
 
Namba 3 world class talent ndio kina nani?

Au ndio kina Nape, January , Mwigulu na Mchengerwa?

You must be joking labda Samia anachoweza kuvuta ni hewa ya oxygen kama binadamu mwingine hao world class talent hawapo kwenye uongozi wake.

Sababu ni moja hawezi kuleta world class talent sababu watakua tishio kwake.

She is an academic dwarf with tons of honorary accolades to ensconce her impecunious academic qualifications.
 
Hatuwezi kuendelea Kama hatuwezi kubadili fikra na namna ya kufikiria!!. Upuuzi na maisha yakipuuzi yametukomaza wtz ndio maana mtu haoni aibu kusifia uongozi/kiongozi aliyefeli, ukisoma nyuzi nyingi humu ni upuuzi na usifiaji wakipumbavu Sana.
 
Aibu yako. Kama hujui maana ya mageuzi kaa kimya. Neno mwanamageuzi huenda kwa watu maalum na si kila mtu. Hapa hamna kitu zaidi ni mageuzi ya kusafiri na na kugeuza maisha kuwa magumu kwa wananchi. Na kama yupo kazini basi hiyo ni ya tumbo lako
 
unawaimiza wanachukia ukweli ujue..

wanatukana hao tsaatsaaatsaaaaatsssaaaahh 🐒
 
Umesahau kuweka namba ya simu. Nakukumbusha. Pia nikupongeze uchawa unalipa.
 
Back
Top Bottom