Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO's) 200 Mwanza hatarini kufutwa

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO's) 200 kati ya 613 mkoani Mwanza, yamewekwa chini ya uangalizi wa Ofisi ya Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kutokana na kutowasilisha taarifa za utendaji kazi na kutolipa ada kwa wakati.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa usajili wa mashirika hayo, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mussa Sanganya, wakati wa mafunzo ya jinsi ya kusimamia na kuendesha NGOs.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makalla amekemea mashirika hayo aliyoyaita 'Mashirika ya Maokoto na Familia' huku akiyataka kujikita katika shughuli zilizoainishwa katika taarifa za usajili wa mashirika hayo kabla hayajachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufutwa.

Naye, Katibu Mtendaji wa Shirika la Synergistic Globe, Tabu Angelina amesema tabia ya baadhi ya mashirika kuvizia na kutumia fedha za wahisani kwa matumizi binafsi inaunyima Umma hasa watu Wenye uhitaji fursa ya kupata huduma na misaada huku akiyataka kutofanya hivyo.
 
Back
Top Bottom