Rais Samia aipa Zambia ardhi hekari 20 katika bandari kavu Kwala mkoa wa Pwani

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,830
21,460
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imetenga eneo la hekari 20 za ardhi katika Bandari kavu eneo la Kwala Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuhudumia mizigo kutoka Zambia ambapo amesema hiyo ndio zawadi ya Tanzania kwa Zambia katika wakati huu wa sherehe za Uhuru wa Zambia.

Rais Samia amesema hayo kwenye hotuba yake akiwa ni Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zambia iliyofanyika Ikulu ya Lusaka, Zambia.

“Kwa nia ya kuwaweka Watu wa Zambia kama kipaumbele katika mipango yetu na kutokana na azma yetu ya kurahisisha biashara kati ya Nchi hizi mbili, Serikali yangu imefanya maamuzi ya kutenga eneo la hekta 20 katika Bandari kavu ya Kwala katika ukanda wa pwani ya Tanzania kwaajili ya shehena maalum kwaajili ya Zambia”

“Zambia itakuwa na uwezo wa kuhifadhi bidhaa kwa muda mrefu na pia hatua hii itaondoa msongamano, ucheleweshaji na kupunguza gharama za kufanya biashara nchini Zambia ikipelekea kukuza biashara kati ya Nchi zetu mbili na kutengeneza fursa za kibiashara kwa Wananchi kutokea Zambia na Tanzania na hii ni zawadi yetu kutoka Tanzania katika wakati huu wa sherehe za uhuru wa Taifa lenu”

Zambia ni Mteja mkubwa wa Bandari ya Dar es Salaam, ikichukua asilimia 34 ya mizigo yote inayopitia Bandari hiyo kwenda nje ya Tanzania.

Millard Ayo

----
Maoni yangu

Hadi tukifika mwaka 2030 Tanganyika itabidi kuomba uhuru upya ili tujikomboe kwa sababu nchi nzima itakuwa mikononi mwa wachache.

Je, kwanini hakutoa bure eneo la zanzibar!
 
Nimesoma thread nikaona manyotanyota.
Nikaona nikuite lakini pia nimaanishe vile nilivyomaanisha 🤣🤣🤣🤣
😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Daaah nimebaki nacheka tuu
Kwahiyo umeona thread huwelewi kabisa
 
Sasa wasichoelewa ni nini?
Kila safari moja huanzisha safari nyingine.
Tanzania si maliyawata....................
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom