Rais Samia, Nyerere wa pili

Suphian Juma

Senior Member
Apr 2, 2019
133
546
Rais wetu Dkt Samia amelihutubia Bunge la Zambia leo baada ya kuoombwa ziara ya kuwa Mgeni Rasmi wa Siku ya Uhuru wa Nchi hiyo ya Zambia ambayo ndiye Mteja Mkuu wa Bandari yetu ya Dar es Salaam inayoenda kufanyiwa Mapinduzi ya kiufanisi na DP World ya Dubai.

Nafurahi kuona tuna Rais anayevaa viatu vya Mwasisi Mwl Nyerere kwa vitendo kwa kuimarisha kwa kasi mahusiano na Mashirikiano na mataifa.

Akiwa katika ziara ya Siku 3 nchini humo, Rais Samia amesisitiza Umoja baina ya nchi za Afrika na undugu wa Kiuchumi ambapo akiwa na Mwenyeji wake, Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ameongoza makubaliano ya kuanzishwa bomba jipya la gesi kutoka Dar es Salaam hadi Zambia, kuboresha bomba la Mafuta la TAZAMA na reli ya TAZARA ambayo vyote hivi ni miradi tegemewa na wananchi wa hali ya chini wa Zambia na Tanzania.

Kwa upande mwingine, Rais wetu ametoa kipande cha ardhi cha hekta 20 katika Bandari kavu eneo la Kwala mkoani Pwani kama zawadi ya Watanzania kwa Wazambia kama sehemu ya kuenzi Upendo baina ya nchi hizi mbili ulioundwa na waasisi wetu Mwalimu Nyerere na Mzee Kaunda.

Ziara hizi lukuki za Rais wetu katika mataifa ya nje zinazidi kuifanya Nchi yetu sasa kurejesha heshima yake ya kihistoria iliyokuwa nayo ya kuwa nchi Darasa duniani la kupanda Upendo baina ya nchi na nchi na kufungua fursa adhimu za kiuchumi hususani baina ya Tanzania na nchi za Kiafrika.

Katika Urais wa Mama Samia hakika naiona Tanzania mpya tegemewa ya kutatua migogoro kwa njia ya meza za mazungumzo baina ya nchi za Afrika zinazohasimiana na hata kufuta vita vinavyooendelea vya baadhi ya Serikali za nchi za Afrika na Vikundi vya waasi.

Mungu mbariki Rais wetu.
Mungu ibariki Tanzania.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Suphian Juma Nkuwi,
Simu: 0717027973
IMG_20231025_203826_781.jpg
 
Sijaelewa kuhusu kipande Cha ardhi ya bara sio zenji kilichotolewa kama Zawadi maana Sheria ya Ardhi hairuhusu mgeni kumiliki ardhi ya bongo!

Uchawa ni hatua inayokuja automatic njaa inapozidi! Mtu yoyote anaweza kujikuta Kawa chawa mkuu kulinda tumbo!!
 
Pesa inatafutwa Kwa namna nyingi Sana....maisha ya kutegemea uchawa ni magumu mno tujitahidi watoto wetu kuwatengenezea FUTURE Yao ili wasije ishi maisha haya
 
Back
Top Bottom