Rais Samia ashiriki miaka 59 ya Uhuru wa Zambia, leo Oktoba 24, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zanzibar leo tarehe 24 Oktoba, 2023.


View: https://www.youtube.com/live/p8yX2IIpIGs?si=f1iByQWZfoe3Pf3d
Samia.jpeg

6e194b9d-e06a-4358-a54d-09117d880a2e.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akikaribishwa Ikulu ya Lusaka na Mwenyeji wake Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za miaka 59 ya Uhuru wa nchi hiyo tarehe 24 Oktoba, 2023.
c27f20c0-8cbe-4de7-91e2-cd9f6f74ff0b.jpeg

44ed05fe-8c06-4d6a-b42e-b4624d533da3.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema wakati wa Wimbo wa Taifa wa Tanzania na Zambia ukiimbwa mara baada ya kuwasili kwenye eneo la Mnara wa Kumbukumbu ya Wapigania Uhuru (Mashujaa) wa nchi hiyo kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa nchi hiyo, Mtaa wa Uhuru Jijini Lusaka tarehe 24 Oktoba, 2023.

0d996325-ed7a-4c49-94ff-4de558eab234.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya Wapigania Uhuru (Mashujaa) Lusaka Zambia tarehe 24 Oktoba, 2023.

c2cc27f1-a703-4f25-9391-51ea71c726e5.jpeg

a09fafc6-019a-42c8-9d41-9a2471fbc14b.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye kaburi la Rais wa Kwanza wa Zambia Hayati Kenneth Kaunda (Presidential Burial site, Embassy Park Jijini Lusaka tarehe 24 Oktoba, 2023.
a15dc586-ebe0-46d3-b5cc-00c2362ff19c.jpeg

Kikundi cha ngoma kutoka Lusaka kikitumbuiza katika Sherehe za miaka 59 ya Uhuru wa Taifa la Zambia katika Viwanja vya Ikulu ya Nchi hiyo tarehe 24 Oktoba, 2023.​
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameungana na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, kuweka mashada ya maua kwenye Mnara wa uhuru wa Zambia.

Rais Samia ameweka shada hilo ikiwa ni ishara ya kutoa heshima na kutambua walioongoza harakati za kuliltea uhuru Taifa hilo mwaka 1964.

Baada ya kuweka shada kwa mashujaa, Rais Samia pia ameweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa la Zambia, Dk. Kenneth Kaunda jijini Lusaka.

Leo Zambia inaadhimisha miaka 59 tangu ipate Uhuru kutoka kwa Waingereza mwaka 1964 na tukio la kuweka shada hufanywa kila mwaka wakati wa maadhimisho haya.

Rais Samia amealikwa kuwa mgeni rasmi kwenye tukio la maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru litakalofanyika baadaye leo kwenye Ikulu ya Zambia.
IMG-20231024-WA0026.jpg
IMG-20231024-WA0029.jpg
IMG-20231024-WA0019.jpg
IMG-20231024-WA0011.jpg
IMG-20231024-WA0010.jpg
IMG-20231024-WA0012.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom