benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan amewasili Nchini Zambia kwa Ziara ya Kitaifa ya Siku tatu kuanzia leo tarehe 23-25 October 2023 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Hakainde Hichilema.
Katika Ziara hiyo Rais Samia atashiriki Matukio mbalimbali ikiwemo Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Uhuru wa Zambia,ufunguzi wa Kongamano la Biashara kati ya wafanyabishara wa Tanzania na Zambia.
Aidha Rais Samia amepewa heshima ya kuhutubia Bunge la Jamhuri ya Zambia tarehe 25 Oktoba, 2023 na anakuwa kiongozi mashuhuri wa wanne kuhutubia Bunge hilo.
Ziara hiyo inalenga Kuimarisha mahusiano baina ya mataifa haya Mawili.