Rais Museveni awaomba rasmi msamaha Waganda. Bado nyie CCM!

Rais Museveni awaomba rasmi msamaha Waganda. Bado nyie CCM!

CCM haiamini kama kuna wa kumuomba msamaha
Hasa wakati huu wapo kwenye kilele kabisa cha kiburi. Ukisikiliza matamshi yao wote, utadhani hawa viumbe Tanzania hii ni mali yao binafsi.

Ni lazima tuseme "CCM', kwa sababu hata hayo yaliyomo humo, na hayakubaliani na ujinga huu yamekaa kimya kama mataahira!
 
Rais Yoweri Museveni na Mkewe Janet Museveni wameomba msamaha hadharani, wakikiri kuwepo kwa mapungufu katika utawala wao, rushwa, na kuwatelekeza wananchi, hasa wa eneo la Buganda, wakati joto la kisiasa likizidi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2026.

Katika tukio lililoandaliwa na binti yao, Mchungaji Patience Rwabwogo, wawili hao walisimama bega kwa bega na kusoma sala ya pamoja ya toba waliyoiandaa, walikiri uzembe na kasoro zilizopo serikalini katika awamu ya uongozi wao.
“Tunakubali kuwa sisi ni binadamu, tumewakosea, na tumefanya makosa kwa namna moja au nyingine. Utusamehe, Ee Bwana,” walisema Museveni na mkewe.
Aidha, mtoto wao, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye ni Mkuu wa Majeshi hakuudhuria ambaye amekuwa gumzo kutokana na ndoto zake za kisiasa na taswira yake tata. Hali hiyo imezidi kuchanganya mjadala wa uongozi baada ya Museveni, huku serikali ya sasa ikilinganishwa na tawala za zamani za Idi Amin na Milton Obote – ambapo Museveni mwenyewe alipinga vikali.

===================For English Audience====================

President Museveni and First Lady Janet Museveni have issued a rare joint public apology, acknowledging failures in governance, corruption, and alienation of citizens, especially in Buganda, as political tensions mount ahead of the 2026 general elections.

In a carefully choreographed moment at a national evangelical convention organised by their daughter, Pastor Patience Rwabwogo, the couple stood side by side and read from a prepared joint prayer of repentance, admitting negligence and lapses within their government.
"We acknowledge that we're human, have missed you and have made mistakes in one way or the other. Forgive us, oh Lord," the Musevenis

Notably absent from the event was their controversial son and military forces chief, Gen Muhoozi Kainerugaba, whose political ambitions and divisive image have complicated the post-Museveni narrative, often leading to comparisons of the ruling government to the regimes of Idi Amin and Milton Obote- which Museveni opposed.​
 
Mbona kama wanamuomba Mungu awasamehe na sio wananchi
 
Ccm nao waige mfano, miaka zaidi ya 60 si michezo. Makosa ni mengi na yanazidi kuimarika
 
Mzee anakaribia kufa au karma? Kama anamaanisha basi amdhibiti mtoto wake Kainerugaba ambaye huwa anatoa vitisho hadharani na amuachie huru Besigye.

Habari kamili;

Rais Yoweri Museveni na mkewe kwa pamoja wiki hii walikiri kuwepo kwa mapungufu katika uongozi, kutokea kwa ufisadi na kuomba msamaha kwa makosa ambayo yametokea katika kipindi cha uongozi wao.

"Kama viongozi wakuu wa National Resistance Movement (NRM), tunawajibika kwa makosa yote tuliyofanya sisi wenyewe, mawakala wetu na wawakilishi wetu. Kwa hiyo, tunasimama hapa kutubu na kuomba radhi hasa wananchi wa Buganda na nchi nzima. Tunaomba urejesho na upendeleo.

Nchini Uganda, raia wengi walionekana kwenye mitandao wa kijamii wakipuuza msamaha huo na kuashiria kuwa mchezo wa kisiasa uliokosa nia ya kweli au mabadiliko ya kumaanisha.

Akizungumza katika mji wa Gulu, Bobi Wine aliishutumu serikali kwa ukiukaji wa haki za binadamu. Alisema kuwa msamaha wa kweli lazima uanze na kukomesha ukandamizaji, akiongeza kuwa hakuna mazungumzo yanayoweza kutokea wakati raia wanabaki kuwa waathirika wa vurugu za serikali.

"Wakati anaomba msamaha, ndugu zetu wako gerezani wanateswa. Dada zetu wanabakwa. Watu wetu bado wanapokonywa ardhi zao... wakati ninasimama hapa, ninasema kwa Museveni, msamaha haukubaliki."
Wengine walikuwa na wingi wa matumaini kwamba huu huenda ukawa ndio mwanzo mpya.
Chanzo: BBC Swahili
 
Huyu mzee atakuwa ameona siku zake za kuishi sio nyingi sana duniani. Atakuwa amejua atakapoondoka watakaobaki watakuwa kwenye hali mbaya sana. Jana kwenye ibada maalum yeye na mke wake wamesoma speech maalum ya kuwaomba radhi Waganda kwa madhira waliyowafanyia na Chama chao.

Rai yangu kwa CCM. Museven ameona arekebishe na Waganda kabla haijawa too late. Nyie endeleeni tu kututeka na kutuua. Endeleeni tu kusema wazi bungeni kuwa sisi ni Kenge na tushughulikiwe na vyombo vyenu vya dola. Ushauri wangu kwenu andaeni ndege za kutosha kuwasafirisha na familia zenu tutakapoamua rasmi kuwashughulikia.

===
Rais Yoweri Museveni na Mkewe Janet Museveni wameomba msamaha hadharani, wakikiri kuwepo kwa mapungufu katika utawala wao, rushwa, na kuwatelekeza wananchi, hasa wa eneo la Buganda, wakati joto la kisiasa likizidi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2026.

Katika tukio lililoandaliwa na binti yao, Mchungaji Patience Rwabwogo, wawili hao walisimama bega kwa bega na kusoma sala ya pamoja ya toba waliyoiandaa, walikiri uzembe na kasoro zilizopo serikalini katika awamu ya uongozi wao.
“Tunakubali kuwa sisi ni binadamu, tumewakosea, na tumefanya makosa kwa namna moja au nyingine. Utusamehe, Ee Bwana,” walisema Museveni na mkewe.
Aidha, mtoto wao, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye ni Mkuu wa Majeshi hakuudhuria ambaye amekuwa gumzo kutokana na ndoto zake za kisiasa na taswira yake tata. Hali hiyo imezidi kuchanganya mjadala wa uongozi baada ya Museveni, huku serikali ya sasa ikilinganishwa na tawala za zamani za Idi Amin na Milton Obote – ambapo Museveni mwenyewe alipinga vikali.

===================For English Audience====================

President Museveni and First Lady Janet Museveni have issued a rare joint public apology, acknowledging failures in governance, corruption, and alienation of citizens, especially in Buganda, as political tensions mount ahead of the 2026 general elections.

In a carefully choreographed moment at a national evangelical convention organised by their daughter, Pastor Patience Rwabwogo, the couple stood side by side and read from a prepared joint prayer of repentance, admitting negligence and lapses within their government.
"We acknowledge that we're human, have missed you and have made mistakes in one way or the other. Forgive us, oh Lord," the Musevenis

Notably absent from the event was their controversial son and military forces chief, Gen Muhoozi Kainerugaba, whose political ambitions and divisive image have complicated the post-Museveni narrative, often leading to comparisons of the ruling government to the regimes of Idi Amin and Milton Obote- which Museveni opposed.

View attachment 3348683
Inawezekana ni 'guilty conscience'.
 
Back
Top Bottom