Watu wameumizwa sana.
Kama ni kuomba msamaha kweli, ni lazima wote walioguswa moja kwa moja na makosa ya huyu mzee aombwe msamaha moja kwa moja, bila ya huo msamaha wa kijumla jumla tu.
Walio athiriwa moja kwa moja wana haki ya kusamehe au kutosamehe.
Hata hivyo; kama ni kweli huyu Mseveni kaona ni muhimu aombe msamaha, ni jambo jema. Lakini asiishie hapo.
Kwa wakati huu ambapo bado yupo hadi hapo atakapo achia madaraka ni lazima afanye jitihada zote za kutubu. Ajitahidi sana kuiacha Uganda ikiwa na amani na utulivu kwenda mbele.
Sasa sijui kama Muhoozi Kainerugaba, kweli atamruhusu kufanya hivyo.