Rais, kwa mara nyingine unatukosea Watumishi wa Umma nyongeza ya mshahara

kwani lini mmefanya kazi??kila siku tunakuja maofisini kwenu kutafuta huduma tunaambiwa mara mnakunywa chai,mara chakula!ratiba ya mfanyakazi wa serikali;
saa 2 asbh - anaripoti
saa 2.05 - chai mpka saa 4
saa 4 - anapiga story mpk saa 7
saa 7 lunch mpka saa 9
saa 9 kugusagusa kazi mpk saa 10

Kuna kazi hapo kweli?wanahitaji ongezeko kweli?
wadau tujadili
wewe ni mchawi
 
watumishi wa levels za kawaida wanapitia magumu sana
wenzetu walioendelea wanalipaa house allowance
transport allowance
hivi kama vingewekwa vingewapunguzia ukali wa maisha kwa sababu ndipo muda wao wa maisha unapoishia mm mijitu inayokejeli watumishi uwa inanikeraga sana
 
Niko kazini kwangu hapa. Watumishi wameishiwa hamu ya kazi. Wamekata tamaa.

Mama unaua taifa. Ahadi unatoa lakini hutimizi. Nyongeza ya mshahara haipo.

Mungu anakuona.
Waache ujinga sisi wenyewe atujaongezewa kitu na tutaenda na mama adi 2030
 
ni haki yake mkuu maana huko ndio anaposhinda na kupoteza masaa mengi nchi zilizoendelea mtumishi wa umma ana furaha analipwa mshahara unaoendana na hali ya maisha ya wakati husika ndio maana amna wapigaji ni haki yake kuulizia nyongeza mkuu samahani kama umekwazika
Uko sahihi kabisa. Na ni haki yake kudai. Nilichokifanya mimi ni kumkumbusha ty kubadili huo mtazamo wake.
Maana katika nchi zetu za ulimwengu wa tatu, watumishi wa umma wanachukuliwa kama manamba tu. Hivyo ni bora na wenyewe wakajiongeza.

Haileti mantiki mbunge mwenye sifa ya kukua tu kidoma na kuandika alipwe milioni 12 kwa mwezi, halafu mtumishi wa umma alipwe laki kadhaa tu kwa mwezi, huku akifanyishwa kazi kwa muda mrefu na katika mazingira magumu.
 
Ni wazi kuwa sasa ni mwaka wa 8 watumishi hawapati shahiki yao ya nyongeza ya mshahara. Matamko mbalimbali hususani kwenye sherehe za Mei Mosi, Rais kupitia majibu ya hotuba ya wafanyakazi alitoa kauli ya kurudisha japo Annual Increment kwa watumishi ifikapo July mwaka mpya wa bajeti.

Tofauti na matarajio ya wengi, hali imekuwa tofauti. Malalamiko na manung'uniko yamekuwepo kila kona. Watumishi wanabeba watu walio wengi; Arican extended families macho yote yapo kwa watumishi.

Mwaka jana hali ilikuwa mbaya na mwaka huu pia hali imekuwa mbaya. Rais wetu, tunajua una mambo mengi, lakini hili la mishahara duni linakupa sifa hasi mbele ya jamii ya watumishi (watendaji) wataifa hili.

Keki ya taifa ni ndogo lakini isiwe yenu tu watembelea V8. 🙏
Watumishi mnapenda kulalamika hamna subra ,hetu tulieni kwanza muwe na subira msiwe wepesi wa kulaumu
 
Kwamba hakuna anayemjali mwalimu wa Tanganyika nchi iliyojaa rasilimali nyingi kuliko nchi zote Africa!

Lini mwalimu wa Tanganyika atafurahia kazi yake na aifanye kwa amani na ufanisi zaidi!? Huwezi fanya kazi kwa ufanisi wakati una matatizo ya kiuchumi tusidanganywe hapa!
Ndiyo maana watoto wao hawasomi kwenye hizo shule
 
Ni wazi kuwa sasa ni mwaka wa 8 watumishi hawapati shahiki yao ya nyongeza ya mshahara. Matamko mbalimbali hususani kwenye sherehe za Mei Mosi, Rais kupitia majibu ya hotuba ya wafanyakazi alitoa kauli ya kurudisha japo Annual Increment kwa watumishi ifikapo July mwaka mpya wa bajeti.

Tofauti na matarajio ya wengi, hali imekuwa tofauti. Malalamiko na manung'uniko yamekuwepo kila kona. Watumishi wanabeba watu walio wengi; Arican extended families macho yote yapo kwa watumishi.

Mwaka jana hali ilikuwa mbaya na mwaka huu pia hali imekuwa mbaya. Rais wetu, tunajua una mambo mengi, lakini hili la mishahara duni linakupa sifa hasi mbele ya jamii ya watumishi (watendaji) wataifa hili.

Keki ya taifa ni ndogo lakini isiwe yenu tu watembelea V8. 🙏
Msubiri hela za kusumamia achaguzi🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom