Rais, kwa mara nyingine unatukosea Watumishi wa Umma nyongeza ya mshahara

Black Legend

Senior Member
Jul 28, 2015
103
130
Ni wazi kuwa sasa ni mwaka wa 8 watumishi hawapati shahiki yao ya nyongeza ya mshahara. Matamko mbalimbali hususani kwenye sherehe za Mei Mosi, Rais kupitia majibu ya hotuba ya wafanyakazi alitoa kauli ya kurudisha japo Annual Increment kwa watumishi ifikapo July mwaka mpya wa bajeti.

Tofauti na matarajio ya wengi, hali imekuwa tofauti. Malalamiko na manung'uniko yamekuwepo kila kona. Watumishi wanabeba watu walio wengi; Arican extended families macho yote yapo kwa watumishi.

Mwaka jana hali ilikuwa mbaya na mwaka huu pia hali imekuwa mbaya. Rais wetu, tunajua una mambo mengi, lakini hili la mishahara duni linakupa sifa hasi mbele ya jamii ya watumishi (watendaji) wataifa hili.

Keki ya taifa ni ndogo lakini isiwe yenu tu watembelea V8. 🙏

Pia, Soma;

TUCTA: Nyongeza ya Mshahara "Annual increment" Itaanza Kulipwa Mwezi wa 8
 
Mambo mengi aliyonayo Rais ni yepi hayo? wao wanakula kwa urefu wa kamba zao wacha wale, mwalimu kamba fupi mno tena haina madhara kwao.

Nchi za kiafrika na watu weusi hawajipendi ndio maana mara mia mtu afe katika safari mbaya baharini akielekea kutafuta maisha mazuri Ulaya.

Mwalimu wa Tanganyika huwezi hata mlinganisha na mwalimu wa hapo Kenya kwa Ruto, hali ni mbaya sana ni ujinga na upumbavu kudharau sekta ya elimu.
 
Kwamba hakuna anayemjali mwalimu wa Tanganyika nchi iliyojaa rasilimali nyingi kuliko nchi zote Africa!

Lini mwalimu wa Tanganyika atafurahia kazi yake na aifanye kwa amani na ufanisi zaidi!? Huwezi fanya kazi kwa ufanisi wakati una matatizo ya kiuchumi tusidanganywe hapa!
 
Back
Top Bottom