Mtazamo: Rais samia endelea kuongeza mishahara kimyakimya

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,032
KAMA ilivyozoeleka kwa baadhi ya wafanyabiashara, huwa wanapandisha bei ya bidhaa mara tu wanaposikia serikali imeongeza msha-hara na marupurupu kwa wafanyakazi kila mwaka. Uviziaji huo hufanyika wakati wa Sikukuu Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), kwani wafanyabiashara walishajua kuwa hicho ndicho kipindi ambacho serikali huwa inatangaza nyongeza hiyo.

Mtindo huo kwa namna moja au nyingine, umekuwa ukichangia kuumiza watumishi na watu wengine hasa wa hali ya chini, kutokana na ukweli kwamba wengi wao ni maisha ya kawaida, kwa maana ya kipato kidogo. Pamoja na hayo, fedha ndio kila kitu katika maisha ya dunia hit, lakini pia mtindo wa baadhi ya wafanyabiashara kupandisha bei ya bidhaa bila kuangalia kundi lingine la watu wenye hali ya chini, unaumiza.

Hata hivyo, Serikali imeshtukia janja yao na sasa imeamua kuja na utaratibu mpya ambao utatumika kuongeza mishahara ya wafanyakazi au watumishi wa umma bila wafanyabiashara hao kujua. Lengo la utaratibu mpya ambao serikali imebuni ni kutaka kukabiliana na mtindo wa kuvizia nyongeza za mshahara na kupandisha bei ya vitu, kwa madai kwamba mishahara imekuwa mikubwa.

Huo ni utaratibu uliotangazwa na Rais Samia, katika maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Mei Mosi, ambayo kitaifa mwaka huu ilifanyika mini Morogoro hivi karibuni. Tofauti na jinsi ambavyo watumishi wamezoea kutangaziwa nyongeza ya mshahara wakati wa sikukuu hiyo, safari hi Rais anasema sasa utaratibu huo umewekwa pembeni, badala yake wanaongezewa kimya kimya.

Katika ufafanuzi wake, Rais Samia anasema serikali yake itakuwa inaongeza mshahara kila mwaka na kulipa malimbikizo katika kipindi cha bajeti ya mwaka wa fedha ujao. Anaongeza kuwa si rahisi wafanyabiashara wanaovizia atangaze mshahara mpya, ili wapandishe bei ya bidhaa kushindwa kujua kinachoendelea na hivyo wateja kupata bidhaa kwa bei ya kawaida. Kwa msemo wa mitaani, ni kwamba wafanyabiashara waliozoea mtindo huo Unaoumiza watu wote, hasa wa hali ya chini, 'imekula kwao', kwani ni wazi utaratibu huo mpya hauwapi mwanya kujua kinachoendelea.

Ninaamini kwamba hata wale wamilikii wa nyumba kupangisha nao itakuwa imekula kwao, kwani hao nao huwa ni wepesi kuwapandishia kodi wapangaji wao mara tu wanaposikia mishahara mipya. Wote kwa pamoja wakiwamo wafanyabiashara, huwa wana vizia maeneo mawili, Mei mosi au mwanzo wa mwaka wa serikali ambao ni Julai ambapo hupandisha bei za bidhaa au kodi za pango. Lakini kwa mfumo ambao Rais amekuja nao, ninaamini unaweza kuwa na mchango mkubwa, katika kuwapunguzia 6 wananchi makali ya maisha ambao wamekuwa wakikumbana nayo.

Kitendo cha kuwapa nyongeza ya asilimia 23 wafanyakazi wenye mishahara ya chini bila kutangaza, ni dalili tosha kwamba ameamua kufanya mambo yake kimya, kimya. Hatua hiyo inaonyesha jinsi alivyodhamiria kuboresha maisha ya watanzania, kwani tangu akabidhiwe usukani wa kuongoza nchi, daima amekuwa akibuni mbinu mbalimbali za kutimiza lengo hilo.​
 
KAMA ilivyozoeleka kwa baadhi ya wafanyabiashara, huwa wanapandisha bei ya bidhaa mara tu wanaposikia serikali imeongeza msha-hara na marupurupu kwa wafanyakazi kila mwaka. Uviziaji huo hufanyika wakati wa Sikukuu Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), kwani wafanyabiashara walishajua kuwa hicho ndicho kipindi ambacho serikali huwa inatangaza nyongeza hiyo.

Mtindo huo kwa namna moja au nyingine, umekuwa ukichangia kuumiza watumishi na watu wengine hasa wa hali ya chini, kutokana na ukweli kwamba wengi wao ni maisha ya kawaida, kwa maana ya kipato kidogo. Pamoja na hayo, fedha ndio kila kitu katika maisha ya dunia hit, lakini pia mtindo wa baadhi ya wafanyabiashara kupandisha bei ya bidhaa bila kuangalia kundi lingine la watu wenye hali ya chini, unaumiza.

Hata hivyo, serikali imeshtukia janja yao na sasa imeamua kuja na utaratibu mpya ambao utatumika kuongeza mishahara ya wafanyakazi au watumishi wa umma bila wafanyabiashara hao kujua. Lengo la utaratibu mpya ambao serikali imebuni ni kutaka kukabiliana na mtindo wa kuvizia nyongeza za mshahara na kupandisha bei ya vitu, kwa madai kwamba mishahara imekuwa mikubwa.

Huo ni utaratibu uliotangazwa na Rais Samia, katika maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Mei Mosi, ambayo kitaifa mwaka huu ilifanyika mini Morogoro hivi karibuni. Tofauti na jinsi ambavyo watumishi wamezoea kutangaziwa nyongeza ya mshahara wakati wa sikukuu hiyo, safari hi Rais anasema sasa utaratibu huo umewekwa pembeni, badala yake wanaongezewa kimya kimya.

Katika ufafanuzi wake, Rais Samia anasema serikali yake itakuwa inaongeza mshahara kila mwaka na kulipa malimbikizo katika kipindi cha bajeti ya mwaka wa fedha ujao. Anaongeza kuwa si rahisi wafanyabiashara wanaovizia atangaze mshahara mpya, ili wapandishe bei ya bidhaa kushindwa kujua kinachoendelea na hivyo wateja kupata bidhaa kwa bei ya kawaida. Kwa msemo wa mitaani, ni kwamba wafanyabiashara waliozoea mtindo huo Unaoumiza watu wote, hasa wa hali ya chini, 'imekula kwao', kwani ni wazi utaratibu huo mpya hauwapi mwanya kujua kinachoendelea.

Ninaamini kwamba hata wale wamilikii wa nyumba kupangisha nao itakuwa imekula kwao, kwani hao nao huwa ni wepesi kuwapandishia kodi wapangaji wao mara tu wanaposikia mishahara mipya. Wote kwa pamoja wakiwamo wafanyabiashara, huwa wana vizia maeneo mawili, Mei mosi au mwanzo wa mwaka wa serikali ambao ni Julai ambapo hupandisha bei za bidhaa au kodi za pango. Lakini kwa mfumo ambao Rais amekuja nao, ninaamini unaweza kuwa na mchango mkubwa, katika kuwapunguzia 6 wananchi makali ya maisha ambao wamekuwa wakikumbana nayo.

Kitendo cha kuwapa nyongeza ya asilimia 23 wafanyakazi wenye mishahara ya chini bila kutangaza, ni dalili tosha kwamba ameamua kufanya mambo yake kimya, kimya. Hatua hiyo inaonyesha jinsi alivyodhamiria kuboresha maisha ya watanzania, kwani tangu akabidhiwe usukani wa kuongoza nchi, daima amekuwa akibuni mbinu mbalimbali za kutimiza lengo hilo.​
23% ipi unayoisema, mwenye mshahara wa mil 1.3 aliyeongezewa elfu 8500 hapo mmefanyaje Hesabu hadi kuiita 23% ?

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom