benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,503
- 2,980
SHIRIKISHO la Vyama Vya Wafanyakazi (TUCTA), limempongeza Rais Dk. Samia Suluhu. Hassan kwa mabadiliko na maboresho makubwa kwa wafanyakazi wa sekta binafsi na umma, ikiwemo kuogeza kiwango cha mshahara kwa mwaka ambacho kilikuwa hakijaongezwa kwa miaka tisa iliyopita.
Pia, TUCTA imemshukuru Rais Dk. Samia kwa dhamira yake ya dhati ya kuendelea kushirikiana na TUCTA kwa kufungua milango ya majadiliano, kusikiliza changamoto kupitia vikao ambavyo wamekuwa wakifanya na serikali, ikiwemo mkutano wa hivi karibuni walipokutana na Rais.
Hayo yamesemwa na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa TUCTA, Said Wamba, alipozungumza na waandishi wa habari, juu ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei Mosi, iliyofanyika mkoani Morogoro hivi karibuni.
"Katika kipindi cha awamu ya sita cha uongozi wa Rais Dk. Samia, kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kushughulikia changamoto mbalimbali za wafanyakazi, ikiwemo nyongeza ya mishahara ambayo ilisimama tangu mwaka 2013,"alisema.
Alisema, wanaipongeza serikali kwa jitihada zake za kuboresha maslahi ya wafanyakazi, kushirikiana na TUCTA kupitia majadiliano mbalimbali yanayolenga kuendelea kuboresha maslahi ya kundi hilo nchini.
Wambwa alisema, jambo la kutia moyo kwao ni kwamba serikali imekuwa na utayari na imefungua milango kwa TUCTA, hivyo watatumia vyema fursa hiyo kufanya majadiliano yenye tija kwa wafanyakazi.
"Vyama vya wafanyakazi siyo chombo cha mapambano, bali ni sehemu mojawapo inayowaunganisha watumishi katika kufanya majadiliano ya changamoto zao yatakayo zaa matunda ya kero walizonazo, wala siyo sehemu ya mapambano na serikali, alisema.
Alieleza kuwa katika kudhihirisha hilo, hivi karibuni walikutana na Rais Dk. Samia na kujadiliana naye masuala mbalimbali ya wafanyakazi, ambapo aliahidi kuendelea kufanya maboresho ya maslahi yao kwa kushirikiana pande zote mbili. Aidha, alisema Rais Dk. Samia alitoa maagizo kwa Wizara husika kukutana na TUCTA, kufanya mazungumzo ya kuendelea kuzifanyia kazi changamoto zilizopo na kutumia vyema fursa iliyopo.