Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,753
- 218,343
Taarifa nilizonazo zinaeleza kwamba Freeman Mbowe na timu yake iliyoko bungeni na hazina wanajipanga kuuthibitisha umma kwamba wabunge wa Tanzania wameongezewa mshahara kutoka milioni 13 hadi milioni 18, nyongeza ya milioni 5 kamili.
Ikumbukwe kwamba wafanyakazi wa Tanzania waliongezewa kati ya Tsh elfu 8 na elfu 18, kutegemeana na ngazi ya mshahara, hii ilitokana na ahadi ya nyongeza ya mishahara ya mtukufu rais aliyoitoa kwenye sherehe za Mei Mosi na kupigiwa makofi mengi na wafanyakazi wakiwemo walimu.
Baada ya uthibitisho huo unaopangwa kutolewa wakati wowote kuanzia sasa, unadhani ni hatua gani zifuate?
Ikumbukwe kwamba si mara ya kwanza kwa Bunge la Tanzania kuukanusha ukweli , kuna wakati waliwakusanya wanawake wanaowajua wenyewe na kwa kutumia nyaraka za kufoji wakawaapisha kuwa Wabunge wa Viti maalum wa Chadema , hata hivyo baadaye ikaja kuthibitika kwamba wanawake hao hawakuteuliwa na Chadema .