Rais anapata wapi mamlaka ya kuagiza Spika asilipe posho za Wabunge?

Simple and clear, sio sawa!

Kwa mujibu wa katiba yetu, Bunge linaundwa na pande mbili... Wabunge na Rais.

Utekelezaji wa mambo unategemea pande hizi mbili... Bunge na Rais

Ni kutokana na hilo, ndio maana hata kama serikali imejiridhisha pasipo na shaka yoyote kwamba tukiwa na sera fulani baada ya mwaka Tanzania itakuwa kama Brunei; bado Rais hawezi kuwatuma watu wake waitengeneze sera husika na yeye kuipitisha bali LAZIMA iende kwanza bungeni!

Na kwavile Bunge linaundwa na Wabunge na Rais, hata kama Bunge limekubaliana kwa 100% kupitisha muswada husika, lazima urudi kwa Rais aidhinishe kuwa sheria!

Chukulia hata Mamlaka ya Rais kutangaza hali ya vita... akishatoa tangazo tu, inabidi Bunge likutane ndani ya Siku 14 kujadili tangazo la rais! Na hapo Bunge linaweza kukubali au kukataa azimio la rais la kuiingiza nchi vitani!

Kwa kungalia mfano huo tu, utaona ni namna gani si Bunge wala Rais mwenye mamlaka ya kutekeleza jambo peke yake! Na tunaposema Bunge sio Spika wa Bunge bali Wabunge!

So, ukichukua issue ya jana kuhusu agizo lake kwa Ndugai... Rais hana mamlaka hayo kwa sababu suala la posho na mishahara ya Wabunge halipo kwenye Mamlaka ya Rais kwa mujibu wa katiba yetu.

Wacha kwanza nitafute Ibara husika!!
 
Tunaambiwa mihimili mitatu, na hiko sawa yaani Dola, Bunge na mahakama, je ni haki mwimili wa Dola kutoa maagizo "direction" hasa kwenye haki na maslahi ya wabunge, kama wasilipwe posho! Naamini Bunge kwenye kamati ya uongozi au nidhamu wangelikaa na kushughulika na jambo hili, uenda wangeona namna bora zaidi ya kulishughulikia bila ya kuleta maswali kwenye jamii juu ya namna mihimili inavyoingiliana!

mkuu ulivyoandika Mungua anakuona, Yaani jinsi unavyokibananga kiswahili
 
Natamani kusema kitu ila nikiwaza Ugali na Leshuu ya karanga ilivyo tamu duh wacha nikae kimya.
 
Ingependeza kama speaker wa bunge amjibu rais kama alivyofanya speaker wa Uganda juzi kwa rais Museven ili kuonesha nguvu ya bunge kama mhimili unaojitegemea na wenye maamuzi yake so rais auheshimu.
Spika gani mkuu? huyu huyu anayejisema ana cheti cha uchizi?
 
Wakuu, ile dhana ya uwepo wa Mihimili Mitatu inayojitegemea ni DANGANYA TOTO TU. Magufuli amedhihirisha hilo leo kwa kuagiza Ndugai asilipe posho za Wabunge walioamua kujiweka "karantini".

Kama Rais ana mamlaka ya kuliingilia Bunge, vipi kuhusu Mahakama? Atashindwaje kutoa maagizo yanayofanana na hayo kwenye Tume yake ya Uchaguzi hapo Oktoba?

My take: Tuna utawala wa Mkono wa Chuma, tusitarajie Uchaguzi Huru hapo Oktoba mwaka huu.

ebana we ndio unajua leo???? Pole sana Jiwe sasa sio kulewa tu ameamua na kututapikia, mhimili ni mmoja kwa utawala huu na wabunge wa upinzani wamwachie majimbo yote vinginevyo wataumia zaidi.
 
Ni kweli kabisa Mkuu. Ndiyo sababu tunajadili hapa, ili iwapo hakutakua na mabadiriko yeyote angalau kwenye Tume ya uchaguzi, basi tusishawishiane kuingia kwenye huo Uchaguzi.
 
Wakuu, ile dhana ya uwepo wa Mihimili Mitatu inayojitegemea ni DANGANYA TOTO TU. Magufuli amedhihirisha hilo leo kwa kuagiza Ndugai asilipe posho za Wabunge walioamua kujiweka "karantini".

Kama Rais ana mamlaka ya kuliingilia Bunge, vipi kuhusu Mahakama? Atashindwaje kutoa maagizo yanayofanana na hayo kwenye Tume yake ya Uchaguzi hapo Oktoba?

My take: Tuna utawala wa Mkono wa Chuma, tusitarajie Uchaguzi Huru hapo Oktoba mwaka huu.

Hivi nani alikwambia Tanzania tuna mihimili mitatu.

Tanzania tuna muhimili mmoja tu, usipopenda hilo hama nchi nenda Kenya palipo karibu au mbali zaidi. Over.
 
Wakuu, ile dhana ya uwepo wa Mihimili Mitatu inayojitegemea ni DANGANYA TOTO TU. Magufuli amedhihirisha hilo leo kwa kuagiza Ndugai asilipe posho za Wabunge walioamua kujiweka "karantini".

Kama Rais ana mamlaka ya kuliingilia Bunge, vipi kuhusu Mahakama? Atashindwaje kutoa maagizo yanayofanana na hayo kwenye Tume yake ya Uchaguzi hapo Oktoba?

My take: Tuna utawala wa Mkono wa Chuma, tusitarajie Uchaguzi Huru hapo Oktoba mwaka huu.
Kumbuka pamoja na ukweli Bunge ni mamlaka mengine lakini Serikali ndiyo inayolipwa mishahara na posho za wabunge kilichofanyika kuzuia ni mashauriano
 
Mkuu, umeuelewa mjadala? Ni wapi Rais alitamka kufanya majadiriano na Spika? Kwanini mnapenda kuficha ficha ukweli? Kutoa MAAGIZO na kufanya majadiriano wewe unaona ni mambo yanayofanana?
 
Wakuu, ile dhana ya uwepo wa Mihimili Mitatu inayojitegemea ni DANGANYA TOTO TU. Magufuli amedhihirisha hilo leo kwa kuagiza Ndugai asilipe posho za Wabunge walioamua kujiweka "karantini".

Kama Rais ana mamlaka ya kuliingilia Bunge, vipi kuhusu Mahakama? Atashindwaje kutoa maagizo yanayofanana na hayo kwenye Tume yake ya Uchaguzi hapo Oktoba?

My take: Tuna utawala wa Mkono wa Chuma, tusitarajie Uchaguzi Huru hapo Oktoba mwaka huu.
Hiyo .ni kwasababu wanafany mambo ya kitoto hakuna haja ya kumlipa m2 kama Huyo
 
Wakuu, ile dhana ya uwepo wa Mihimili Mitatu inayojitegemea ni DANGANYA TOTO TU. Magufuli amedhihirisha hilo leo kwa kuagiza Ndugai asilipe posho za Wabunge walioamua kujiweka "karantini".

Kama Rais ana mamlaka ya kuliingilia Bunge, vipi kuhusu Mahakama? Atashindwaje kutoa maagizo yanayofanana na hayo kwenye Tume yake ya Uchaguzi hapo Oktoba?

My take: Tuna utawala wa Mkono wa Chuma, tusitarajie Uchaguzi Huru hapo Oktoba mwaka huu.
Mkuu, umeuelewa mjadala? Ni wapi Rais alitamka kufanya majadiriano na Spika? Kwanini mnapenda kuficha ficha ukweli? Kutoa MAAGIZO na kufanya majadiriano wewe unaona ni mambo yanayofanana?

Ni kutoelewa mpangilio wa serikali na nchi ilivyo ndo tatizo lenu.
Pesa zote na bajeti ziko chini ya kamishna wa bajeti, Hazina. Kamishna ndo anafanya uchambuzi Bunge lipate ngapi, mahakama ipate ngapi na serikali ipate ngapi. Ndiye anayeamua vikomo vya bajeti kwa kila sehemu au mhimili unavyoita. Hapo ndo hata Bunge linapopata pesa.

Huyo kamishna hayuko chini ya Bunge yuko chini ya Rais. Rais wetu ni mkuu wa serikali na ni mkuu wa nchi. Ndo maana hata mbunge akihukumiwa kunyongwa, anayeweka sahihi ni rais, siyo spika.
 
Magufuli is our president and his level is people like Mr. TRUMP or any other head of state. Call him what you want, it doesn't change anything! He is a respectable and able president - one of the best in this era.
Trump is too far bright. This dude is shit
 
Wakuu, ile dhana ya uwepo wa Mihimili Mitatu inayojitegemea ni DANGANYA TOTO TU. Magufuli amedhihirisha hilo leo kwa kuagiza Ndugai asilipe posho za Wabunge walioamua kujiweka "karantini".

Kama Rais ana mamlaka ya kuliingilia Bunge, vipi kuhusu Mahakama? Atashindwaje kutoa maagizo yanayofanana na hayo kwenye Tume yake ya Uchaguzi hapo Oktoba?

My take: Tuna utawala wa Mkono wa Chuma, tusitarajie Uchaguzi Huru hapo Oktoba mwaka huu.
Watu huwa hamfatilii uendeleo wa mambo muhimu nchini.
 
Magufuli is our president and his level is people like Mr. TRUMP or any other head of state. Call him what you want, it doesn't change anything! He is a respectable and able president - one of the best in this era.
He is still a country bumpkin, that doesn't change just because he is president.
 
Ni kutoelewa mpangilio wa serikali na nchi ilivyo ndo tatizo lenu.
Pesa zote na bajeti ziko chini ya kamishna wa bajeti, Hazina. Kamishna ndo anafanya uchambuzi Bunge lipate ngapi, mahakama ipate ngapi na serikali ipate ngapi. Ndiye anayeamua vikomo vya bajeti kwa kila sehemu au mhimili unavyoita. Hapo ndo hata Bunge linapopata pesa.

Huyo kamishna hayuko chini ya Bunge yuko chini ya Rais. Rais wetu ni mkuu wa serikali na ni mkuu wa nchi. Ndo maana hata mbunge akihukumiwa kunyongwa, anayeweka sahihi ni rais, siyo spika.
Jielekeze kwenye hoja, suala siyo posho. Tunajadili mamlaka ya Rais dhidi ya Bunge na Mahakama, ni sahihi kwa muhimili mmoja kutoa MAAGIZO kwa mihimili mingine?
 
Back
Top Bottom