Nyerere na Magufuli wanatoa machozi baada ya azimio la bunge kuibinafsisha bandari za Tanzania kwa nchi ya Dubai

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
Hayati Rais Magufuli alinunua mitambo miwili kwa ajili ya bandari ya Dar es Salaam, ambayo ni World first class yenye thamani ya trillion 3.2 na imefungwa juzi tu wakati ameshafariki,ajabu katika maelezo ya mkataba uliopitishwa na bunge,wanasema Dp World wataleta mitambo na kuendeleza bandari!? hivi sisi tumeshindwa kununua mitambo hiyo kidogo kidogo kuweza kuendesha bandari yetu sisi wenyewe,nilipata kusoma juu ya mkataba wa kilaghai aliosaini babu yangu Chifu Mangungo wa Msovelo,kwa kuwa alilaghaiwa na Dr Karl Peters aka mkono wa damu,nilimsamehe,leo siamini kusikia bunge letu lenye wasomi wamepitisha mkataba unaosema "kuhusu muda,makubaliano haya yatakuwa hai mpaka pale ambapo shughuli za miradi zitasitishwa au kuisha kwa muda wa mikataba ya nchi mwenyeji na mikataba ya miradi" kama kweli bunge limepitisha mkataba wenye maneno hayo basi tumsamehe sana Chifu Mangungo wa Msovelo.

Katika mkataba huo,ibara ya 23(1) ni jambo la hatari kwa taifa kukubali na kiridhia mkataba ambao hauna ukomo wa utekelezaji wake,kifungu kinaeleza kuwa ukomo wa mkataba ni mpaka hapo shughuli za mradi zitakapokuwa zimekamilika au muda kwisha wa Host Government Agreement (HGAs),sasa Intergovernmental Agreement (IGA) inachukua maeneo yote ya bandari nchini kama inavyofafanuliwa katika ibara 1,ibara ya 2 na ibara ya 4,haya ni mamlaka makubwa sana anayopewa Dubai rasilimali ya nchi yetu haiwezekani mkataba kutokuwa na muda,rejea tena ibara ya 22,hii ndio ibara inayoruhusu marekebisho,ibara hii inaipa mamlaka nchi ya Dubai kukataa baadhi ya marekebisho ya Tanzania kama nchi ambayo ndio wenye rasilimali za bandari na hivyo Tanzania itaendelea kupata hasara ikiwa haina la kufanya,nini faida ya IGA? Ubinafsishaji uliliathiri taifa la Tanzania na kuua viwanda, uchumi,mashirika ya reli TRL, TTCL,Tanesco,NBC ATCL,kupokonya ajira na kuwapa wa-Asia viwanda na sasa vimegeuzwa kuwa magodown,tuliona Tanesco walivyopewa makaburu,ikaja symbion,iptl na tukapata jibu kwenye kashfa ya Richmond na Escrow.

Azimio la bunge kuridhia mkataba wa IGA,kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendeshaji na uboreshaji wa Utendaji kazi wa Bandari za bahari na maziwa makuu ya Tanzania unakwenda kinyume na sheria za nchi na unakinzana na sera na msimamo wa nchi yetu katika mahusiano ya kimataifa,hakuna utafiti wala tathmini ya kina iliyofanyika kubaini mahitaji ya uwekezaji na fedha zinazohitajika kuboresha bandari zetu na kwa kuwa mkataba huo haujaweka wazi kiasi cha fedha inachokwenda kuwekezwa na pia jukumu la nchi ya Dubai halijawekwa wazi katika mkataba huu,rejea ibara ya 20 kutokutumia sheria za Tanzania kwenye usuluhishi wa migogoro,usuluhishi wa migogoro kufanyika Afrika kusini na kwa kutumia sheria za usuluhishi za kamisheni ya Umoja wa mataifa juu ya sheria zinazohusika na biashara za kimataifa (Unicitral arbitration rules) kifungu hiki kinakwenda kinyume na kifungu cha 11 cha sheria ya mamlaka ya nchi kuhusiana na umiliki wa rasilimali na maliasili ya mwaka 2017 (the natural wealth and resources (permanent sovereignty) Act no.5 of 2017) ambapo inaelezwa mgogoro wowote unaotokana na matumizi ya rasilimali na maliasili ya nchi ya Tanzania,hautatatuliwa katika mahakama na mabaraza ya nchi za nje,bali utatatuliwa na vyombo vya sheria vya Tanzania na kwa kutumia sheria za Tanzania.

Ibara ya 25(1) inaeleza kuwa shughuli za awali za kufanya upembuzi yakinifu na kufanya tathmini itafanyika baada ya mkataba wa IGA kusainiwa,hii si sawa maana tunao uzoefu wa kubinafsishwa kwa benki ya Taifa ya biashara,tuliambiwa benki ina madeni mengi,jibu lipo kichwani kama nanunua kampuni yako yenye madeni basi gharama za ununuzi nitatoa madeni kinachobaki ndio nakupa kisipobaki basi unanipa bure, Mkataba unahusisha maeneo yote ya bandari za bahari ya Hindi na maziwa makuu,Dubai walipaswa kupewa eneo moja tu phase 1,badala ya kumpa maeneo yote,kwa mujibu wa sheria ya bandari na 17 ya mwaka 2004 lazima Dubai ataje aina ya uwekezaji anaokwenda kufanya kwenye mkataba sio kutaja kiujumla eti kuendeleza,kusimamia na kuendesha bandari,lazima mkataba ueleze Tanzania itanufaika vipi,sio kusema DP World inakuja kuwekeza kibiashara,kama ni hivyo hakuna umuhimu wa IGA,Dp World ilipaswa kupewa kazi kwa utaratibi wa kawaida tu kupitia TPA na kwa sheria za Public private partnership (PPP) act na public procurement act,no 7 of 2011 badala ya kupitia mgongo wa IGA,

Nimalizie kwa kusema IGA inayoingiwa ni kwa ajili ya kuwekeza katika bandari za Tanzania na sio makubaliano ya uendeshaji wa bandari za Tanzania na bandari za Dubai, kwenye mkataba huu jukumu la nchi ya Dubai halijafahamika bayana ukiondoa makampuni yake yanayokuja kuwekeza nchini,utiaji sahihi unamuonesha Waziri wa Tanzania na CEO wa mamlaka ya bandari wa Dubai,hapa hatujazingatia ibara ya 28 ya sheria za mikataba(International Laws) nashauri kuvunja mkataba wa IGA na badala yake mamlaka ya bandari Tanzania (TPA) na kampuni ya DP World waingie makubaliano HGAs kwa kufuata taratibu zote na tuone,nawaona Chadema mkirudi kumsafisha Hayati Rais Magufuli kwa alivyovipigania na baada ya kuondoka vinatokea,hivi tumeshindwa kuboresha au kuendesha bandari,Mwalimu Nyerere alisema "Nia tunayo,Hali tunayo na Uwezo tunao" kipi ambacho tukitia nia tunashindwa!? ndugu zangu wabunge msiongee kwa tumia hamasa na kufukuzia kurudi kwa jina kwenye uchaguzi 2025 nawasihi kutumia weledi maana huku mitaani kuna WASOMI wa kila aina kuliko huko bungeni hivyo lazima mjue kuwa kila mnachoongea na kuchambua watu huku mitaani wanafanyia performance appraisal kwa maslahi mapana ya Tanganyika.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Nchi hii hakikisha familia yako iko salama basiii, mengine hatuyawezi tunaishia kuongea midomoni tu.Wameshafanya na hakuna kitu cha kuwafanya sababu kusahau, uoga na ujinga tumeshavizoea hili nalo litapita
 
Hiko ndo muhimu serekali ya ccm inajua hatuna cha kuwafanya
 
Magufuli anapashwa kufurahia kinachotokea sasa kuhusu mkataba wa bandari. Yeye binafsi ndiye alinajisi uchaguzi wa 2020, maccm yakamwita mwamba. Matokeo yake bunge la chama kimoja linapitisha kila uchafu sawa na maelekezo ya Magufuli.
 
NONDO ZA PASKALI MAYALA KUHUSU UTAPELI WA MKATABA WA KUBINAFSISHA BANDARI.

1.Utapeli wa kwanza mkubwa, ni hakuna mtu yoyote kati yetu aliyefanya a due diligence report ya DP World, tunaelezwa ni Governmental Organisation, wakati sii kweli, it's a private company!. Kabla ya kuingia mkataba wowote, lazima kwanza kufanyike kitu kinachoitwa a due diligence process na kutolewa a due diligence report. Hili halikufanyika hivyo serikali yetu kujikuta inaingia mkataba wa kimataifa na parties to contract which has no capacity to contract hivyo ku vitiate makubaliano kugeuka void hivyo makubaliano hayo yanakuwa null and void ab initio!.

DUBAI SIO NCHI,NCHI NI UAE,TUMEPIGWA

Mkataba wa IGA na HGA inaingiwa kati ya serikali na serikali, hivyo ukisoma documents za makubaliano utaona ni kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya UAE, lakini signatories kwa serikali ya Tanzania ni serikali kweli, lakini kwa serikali ya UAE, signatories ni Mwarabu wa Dubai wa DP World na sio serikali ya UAE, kwenye mkataba wameandika serikali ya Dubai, Dubai hivyo hapa tunatapeliwa!, serikali yetu inaingizwa mkenge kuingia mkataba na a private company disguised as a government of UAE kumbe ni kampuni binafsi!. 1686460927642.png
Mkataba Kati ya serikali ya Tanzania na Dubai ni batili kwenye sheria za kimataifa. Maana Dubai sio nchi, a sovereign state kama ilivyo Tanzania, Dubai hapa inajitambulisha kama a State Party, Dubai is not a state hivyo haiwezi kuwa a state party, it has no the capacity to transact as an international IGA, haiwezi kuingia mikataba ya kimataifa na nchi, inaweza kuingia mkataba wa kimataifa na mamlaka ya Bandari, taasisi kwa taasisi, kama ilivyofanya hapa 1686461228426.pngambapo DP World iliingia mkataba na Mamlaka ya Bandari TPA, mkataba ambao Rais Samia aliushuhudia ukisainiwa kule Dubai during Expo Dubai.
Sasa kampuni hii ya DP World iliyoingia mkataba na mamlaka ya Bandari, sasa inajigeuza nchi, sovereign state of Dubai, imeingia mkataba wa kimataifa na serikali yetu!, huku ni kututapeli!. Dubai is not a state, it's not a nation na nchi isiyo na sovereignty!. DP World is not a state, it's a private company, hapa imejigeuza ni nchi!. Huu ni utapeli!. 1686466691966.png
Mikataba ya kimataifa inaingiwa kati ya nchi na nchi, na Falme ya Kiarabu inayotambulika kwenye sheria za kimataifa na sio Dubai ambayo ni sehemu ya UAE, hivyo hapa kuna utapeli!. Due diligence ingefanyika, hili lingeonekana.
Status ya Dubai kwe UAE ni sawa na status ya Zanzibar ndani ya JMT, Zanzibar has no capacity to transact an international treaty kwasababu Zanzibar sio sovereign. Dubai pia sio sovereign, hivyo mikataba yote ya kimataifa ya Zanzibar, inaingiwa na JMT kwaniaba ya Zanzibar, IGA na HGA inapaswa kuingiwa kati ya Tanzania na UAE na sio Tanzania na Dubai!.
DPW ni kampuni kama inavyoonyesha hapa1686466821809.png

WANASHERIA MAGUMASHI WAMETUINGIZA CHOO CHA KIKE,

Wanasheria wanapoamua kufanya magumashi ya kisheria, wanakuzuga kwa maneno ya kweli kwenye mkataba, mfano hapa Dubai inatambulishwa kama nchi,1686466895812.pnglakini mkataba wetu hii iliyoandikwa kama nchi, sio nchi kweli bali ni kampuni ya DPW!.
Kwa vile kwa upande wetu ni serikali yetu, ili kuonyesha IGA ni kati ya serikali mbili, hapa wameitaja kampuni ya kiserikali ili kuiserikalisha kampuni binafsi ya DPW kuwa ni serikali 1686466969407.png
Hivyo mikataba ya HGA utaokuja kuingiwa na serikali yetu, sio mkataba wa kimataifa wa kiserikali kati ya serikali yetu na serikali ya UAE, lakini hakuna chochote cha UAE bali kampuni binafsi ya DPW iliyoserikalishwa na kujifanya ni serikali!.1686467041823.png1686467116175.png
Kwa vile mikataba ya kimataifa inahusisha state parties, HGA inayokwenda kuingiwa ni HGA kati ya nchi ya Tanzania ambayo ni state na kuingia na DPW iliyo ji stetisha kama a state ambapo huu pia ni utapeli!.1686467223681.png
Kwa Tanzania mamlaka yote ya nchi, mtu yoyote ili asaini mkataba wa kimataifa wa kuiingiza nchi, anapaswa apewe the Power of Attorney na Rais wa JMT. Hii hapa chini ni POA ya Rais Samia kumpa mamlaka Prof. Mbarawa kuingia huo mkataba kwa niaba ya Tanzania,
 
Nchi hii hakikisha familia yako iko salama basiii, mengine hatuyawezi tunaishia kuongea midomoni tu.Wameshafanya na hakuna kitu cha kuwafanya sababu kusahau, uoga na ujinga tumeshavizoea hili nalo litapita
Umemaliza.

Kupitia uoga wetu wanafanya wanachotaka. Ni swala la muda tu litakuja jambo lingine haya ya bandari yatasahaulika.

Watanzania ni mithili ya mtoto mdogo anaelilia gari la kuchezea, ukimuonyesha pipi tu anasahau gari.

Tuendelee kubwabwaja mitandaoni kama desturi yetu huku wenye akili wakila nchi yao.
 
NONDO ZA PASKALI MAYALA KUHUSU UTAPELI WA MKATABA WA KUBINAFSISHA BANDARI.

1.Utapeli wa kwanza mkubwa, ni hakuna mtu yoyote kati yetu aliyefanya a due diligence report ya DP World, tunaelezwa ni Governmental Organisation, wakati sii kweli, it's a private company!. Kabla ya kuingia mkataba wowote, lazima kwanza kufanyike kitu kinachoitwa a due diligence process na kutolewa a due diligence report. Hili halikufanyika hivyo serikali yetu kujikuta inaingia mkataba wa kimataifa na parties to contract which has no capacity to contract hivyo ku vitiate makubaliano kugeuka void hivyo makubaliano hayo yanakuwa null and void ab initio!.

DUBAI SIO NCHI,NCHI NI UAE,TUMEPIGWA

Mkataba wa IGA na HGA inaingiwa kati ya serikali na serikali, hivyo ukisoma documents za makubaliano utaona ni kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya UAE, lakini signatories kwa serikali ya Tanzania ni serikali kweli, lakini kwa serikali ya UAE, signatories ni Mwarabu wa Dubai wa DP World na sio serikali ya UAE, kwenye mkataba wameandika serikali ya Dubai, Dubai hivyo hapa tunatapeliwa!, serikali yetu inaingizwa mkenge kuingia mkataba na a private company disguised as a government of UAE kumbe ni kampuni binafsi!. 1686460927642.png
Mkataba Kati ya serikali ya Tanzania na Dubai ni batili kwenye sheria za kimataifa. Maana Dubai sio nchi, a sovereign state kama ilivyo Tanzania, Dubai hapa inajitambulisha kama a State Party, Dubai is not a state hivyo haiwezi kuwa a state party, it has no the capacity to transact as an international IGA, haiwezi kuingia mikataba ya kimataifa na nchi, inaweza kuingia mkataba wa kimataifa na mamlaka ya Bandari, taasisi kwa taasisi, kama ilivyofanya hapa 1686461228426.pngambapo DP World iliingia mkataba na Mamlaka ya Bandari TPA, mkataba ambao Rais Samia aliushuhudia ukisainiwa kule Dubai during Expo Dubai.
Sasa kampuni hii ya DP World iliyoingia mkataba na mamlaka ya Bandari, sasa inajigeuza nchi, sovereign state of Dubai, imeingia mkataba wa kimataifa na serikali yetu!, huku ni kututapeli!. Dubai is not a state, it's not a nation na nchi isiyo na sovereignty!. DP World is not a state, it's a private company, hapa imejigeuza ni nchi!. Huu ni utapeli!. 1686466691966.png
Mikataba ya kimataifa inaingiwa kati ya nchi na nchi, na Falme ya Kiarabu inayotambulika kwenye sheria za kimataifa na sio Dubai ambayo ni sehemu ya UAE, hivyo hapa kuna utapeli!. Due diligence ingefanyika, hili lingeonekana.
Status ya Dubai kwe UAE ni sawa na status ya Zanzibar ndani ya JMT, Zanzibar has no capacity to transact an international treaty kwasababu Zanzibar sio sovereign. Dubai pia sio sovereign, hivyo mikataba yote ya kimataifa ya Zanzibar, inaingiwa na JMT kwaniaba ya Zanzibar, IGA na HGA inapaswa kuingiwa kati ya Tanzania na UAE na sio Tanzania na Dubai!.
DPW ni kampuni kama inavyoonyesha hapa1686466821809.png

WANASHERIA MAGUMASHI WAMETUINGIZA CHOO CHA KIKE,

Wanasheria wanapoamua kufanya magumashi ya kisheria, wanakuzuga kwa maneno ya kweli kwenye mkataba, mfano hapa Dubai inatambulishwa kama nchi,1686466895812.pnglakini mkataba wetu hii iliyoandikwa kama nchi, sio nchi kweli bali ni kampuni ya DPW!.
Kwa vile kwa upande wetu ni serikali yetu, ili kuonyesha IGA ni kati ya serikali mbili, hapa wameitaja kampuni ya kiserikali ili kuiserikalisha kampuni binafsi ya DPW kuwa ni serikali 1686466969407.png
Hivyo mikataba ya HGA utaokuja kuingiwa na serikali yetu, sio mkataba wa kimataifa wa kiserikali kati ya serikali yetu na serikali ya UAE, lakini hakuna chochote cha UAE bali kampuni binafsi ya DPW iliyoserikalishwa na kujifanya ni serikali!.1686467041823.png1686467116175.png
Kwa vile mikataba ya kimataifa inahusisha state parties, HGA inayokwenda kuingiwa ni HGA kati ya nchi ya Tanzania ambayo ni state na kuingia na DPW iliyo ji stetisha kama a state ambapo huu pia ni utapeli!.1686467223681.png
Kwa Tanzania mamlaka yote ya nchi, mtu yoyote ili asaini mkataba wa kimataifa wa kuiingiza nchi, anapaswa apewe the Power of Attorney na Rais wa JMT. Hii hapa chini ni POA ya Rais Samia kumpa mamlaka Prof. Mbarawa kuingia huo mkataba kwa niaba ya Tanzania,
Hiyo due deligence wakiifanya wanaripoti kwa Mayala?
Mayala anajuaje kuwa hawakuifanya wakati hahusiki na huo mchakato? Ramli chonganishi. Zipuuzwe.
 
Jamaa wanachungulia dirishani kuona kama Watanganyika wamelala au wawapigie hadithi walale.
 
Je Bandari ni suala la Muungano!? Kama sio iweje Wazanzibari wasaini kuibinafsisha bandari ya Watanganyika!?
 
Fatima anasema tunawafukuza waarabu bure eti hao waarabu wameweza kufanya Mapinduzi ya kiuchumi kwa muda mfupi sana,Sasa kwa nini baba ake alifanya Mapinduzi kumfukuza mwarabu,ebu kwanza akamuulize baba baada ya hapo ndio aje kutufundisha uzuri wa mwarabu.
 
Back
Top Bottom