Rais anapata wapi mamlaka ya kuagiza Spika asilipe posho za Wabunge?

Jimbi

JF-Expert Member
Aug 16, 2010
3,951
4,264
Wakuu, ile dhana ya uwepo wa Mihimili Mitatu inayojitegemea ni DANGANYA TOTO TU. Magufuli amedhihirisha hilo leo kwa kuagiza Ndugai asilipe posho za Wabunge walioamua kujiweka "karantini".

Kama Rais ana mamlaka ya kuliingilia Bunge, vipi kuhusu Mahakama? Atashindwaje kutoa maagizo yanayofanana na hayo kwenye Tume yake ya Uchaguzi hapo Oktoba?

My take: Tuna utawala wa Mkono wa Chuma, tusitarajie Uchaguzi Huru hapo Oktoba mwaka huu.
 
Tuliwaasa Chadema

Wabunge wa Chadema wakichaguliwa na Watanzania wakawawakilishe bungeni

Ila Mbowe kwa ubabe wake bila kushirikiana na Spika amewakataza wabunge wa Chadema wasihudhurie vikao

Kwanza ieleweke Mbowe huwakata wabunge wake zaidi ya milion kwenye mshahara wa mbunge

Leo anawakataza wasichukue hata posho ?

Mbowe ajitathimini akae pembeni akili imefika kikomo
 
Kwani posho ni nin mkuu? Me nazani chadema walijua kabisa kujiisolet watakosa posho na wamekubaliana na hilo, nachojua unalipwa posho baada ya kusaini mahudhilio pindi uingiapo bungeni sio otherwise. Jiwe anatafuta kiki tu za.kishamba kwenye hilii.
 
Kwani posho ni nin mkuu? Me nazani chadema walijua kabisa kujiisolet watakosa posho na wamekubaliana na hilo...nachojua unalipwa posho baada ya kusaini mahudhilio pindi uingiapo bungeni sio otherwise....Jiwe anatafuta kiki tu za.kishamba kwenye hilii.
Kitendo cha kutamka hadharani kwamba ametoa agizo hilo, huoni namna ambavyo amedhihirisha Utawala wake wa Mabavu?
 
Ingependeza kama speaker wa bunge amjibu rais kama alivyofanya speaker wa Uganda juzi kwa rais Museven ili kuonesha nguvu ya bunge kama mhimili unaojitegemea na wenye maamuzi yake so rais auheshimu.
Thubutu anaanzaje kujibu wkt yeye ni mzee wa ndio mzee hawez hata kuulinda mhimili wake labda kama angekuwa mzee six ndo sabufa

Its not over until its over...
 
Spika Bosi wake ni Mkuu wa CCM, ambaye ni Raisi wa JMTZ, na fedha yote ya Serikali ya JMTZ msimamizi wake ni Raisi wa JMTZ, Bunge linapewa fedha za walipa kodi wa JMTZ na msimamizi wa Kodi zetu ni Raisi wa JMTZ, ...
 
Back
Top Bottom