Punguza gharama za kutumia mafuta kwenye gari lako. Sasa unaweza kutembea kilomita 180 kwa gharama ya Tsh.15,000 tu

Nimeeleza hapo mkuu...kwa sasa kuna vituo 2 tu vinavyojaza gesi dar ambavyo ni ubungo na tazara...vingine vitatu vipp hatua ya mwsho... Kukamilika ila vyote vipo dar..

Mikoani ni ngumu kwa sasa
Installation Cost ya 1.8mil kwa gari ya 4 cylinder bado ni kubwa
 
Natamani vituo vienee nchi nzima hata walioko Nanjililinji wapate huduma, japo wazee wa tozo watafanya yao.
Nakumbuka mafuta taa yalikuwa gharama nafuu, kilichotokea ......
 
Baada ya utafiti na majaribio ya muda mrefu wa matumizi ya gesi kwenye vyombo vya usafiri tumefanikiwa kuongeza mfumo wa matumizi ya gesi kwny pikipiki za migut mitatu.
Kwa muda sasa tumekuwa tukiongezea mfumo wa matumizi ya gesi asilia katika magari.
leo hii ningependa kutambulisha huduma mpya ya kuongeza mfumo wa matumizi ya gesi kwenye bajaji.

FAIDA ZA KUONGEZEA MFUMO WA GESI KWENYE CHOMBO CHAKO
Ifahamike kwamba kuweka mfumo wa gesi hakuondoi mfumo wa matumizi ya mafuta bali unakupa fursa ya kutumia gesi asilia amcyo kiuhalisia gharama zake ni nafuu sana.
unapofungiwa mfumo wa gesi unawekewa mtungi wa kg 5.6 ambao kuujaza gharama yake ni Tsh 8,400 TU na kwa mtungi huu unaweza kutembea na chombo chako kwa umbali wa km 190 hadi 200.
jiulize kwa kutumia mafuta ungetumia lita ngpi za mafuta kusafiri umbali huo?
Bei ya kg 1 ya gesi ni tsh 1550 haijawahi badilika huku bei ya petroli ikiwa ni zaidi ya tsh 2800 huk ikiwa ni yenye kupanda kila uchao.

GHARAMA ZA KUWEKA MFUMO WA GESI
huduma hii ya kuweka mfumo huu wa gesi inatolewa kwa gharama ya TSH 1,200,000 kwa chombo cha pikipiki ya miguu mitatu (bajaji).
ambapo kwa kiasi cha pesa utakachookoa kwa matumizi ya mfumo wa gesi ni ndani ya miezi 3 hadi 4 utakuwa umerejesha pesa yako kisha kuendelea kula maisha na chombo chako cha usafiri.
kwa wale ambao wangependa kujua gharama za kubadili mfumo wa gesi kwnye magari
itategemeana na ukubwa wa engine ya gari husika
kwa magari ya injini yenye piston 4 gharama ni 1,800,000 pistoni 6 ni 2,200,000 na pistoni 8 ni 2,400,000

Huduma utazipata kutoka kwa wataalam wetu wanaopatikana dar es salaam ubungo maziwa kwenye kituo cha kujazia gesi.

Kwa maswali na maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia namba hii 0613 11 31 90.
 
KWA SASA TUMEANZISHA HUDUMA YA KUWEKA MFUMO WA GESI KWENYE PIKIPIKI YA MATAIRI 3 (BAJAJI)

KWA MAWASILIANO ZAIDI 0613 11 31 90
 
Back
Top Bottom