Wabunge: Serikali iagize magari yanayotumia mfumo wa gesi uliofungwa toka kiwandani moja kwa moja

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,328
8,243
Screenshot_20240315_222341_Instagram Lite.jpg

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, imeishauri Serikali kuagiza magari yenye mfumo wa gesi ambao una gharama nafuu, hali itakayosaidia kupunguza gharama za mafuta kutokana na uwepo wa Gesi Nchini.

Ushauri huo, umetolewa hii leo Machi 15, 2024 na Mwenyekiti wa kamati hiyo, David Mathayo wakati wa ziara ya kutembelea vituo viwili vya kuzalisha gesi vya Master gas na Taqa Dalbit vilivyopo jijini Dar es salaam.

Amesema, “Tunaishauri Serikali iangalie uwezekano wa magari yake kutumia mfumo wa Gesi, hii itapunguza gharama za mafuta inazotumia na rasilimali ya gesi tunayo ni yetu.”

3c081846-d4b6-4f4f-8ef1-176f84d0c194.jpg

Naye Naibu waziri wa Nishati, Judithi Kapinga amesema amepokea ushauri na maelekezo kutoka kwenye kamati hiyo ya Bunge na kwamba tayari wamejipanga kuongeza vituo 15 vya kujazia gesi vitakavyokamilika ndani ya mwaka huu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Petroli Tanzania – TPDC, Mussa Makame amesema mpango wa kununua vituo vya gesi vitano vyenye uwezo wa kuhama unaandaliwa kuanzia na vitatawanywa maeneo mbalimbali.
 
Viazi kweli hawa! yaani Toyota wawekeze kwenye RnD ya magari ya gesi kwakuwa kuna demand ya magari 200 kutoka serikali ya Tanzania?

Labda kama wako tayari kutembelea magari ya kichina. Hakuna kampuni kubwa ya magari wanafanya ujinga huo.
 
View attachment 2935706
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, imeishauri Serikali kuagiza magari yenye mfumo wa gesi ambao una gharama nafuu, hali itakayosaidia kupunguza gharama za mafuta kutokana na uwepo wa Gesi Nchini.

Ushauri huo, umetolewa hii leo Machi 15, 2024 na Mwenyekiti wa kamati hiyo, David Mathayo wakati wa ziara ya kutembelea vituo viwili vya kuzalisha gesi vya Master gas na Taqa Dalbit vilivyopo jijini Dar es salaam.

Amesema, “Tunaishauri Serikali iangalie uwezekano wa magari yake kutumia mfumo wa Gesi, hii itapunguza gharama za mafuta inazotumia na rasilimali ya gesi tunayo ni yetu.”

3c081846-d4b6-4f4f-8ef1-176f84d0c194.jpg

Naye Naibu waziri wa Nishati, Judithi Kapinga amesema amepokea ushauri na maelekezo kutoka kwenye kamati hiyo ya Bunge na kwamba tayari wamejipanga kuongeza vituo 15 vya kujazia gesi vitakavyokamilika ndani ya mwaka huu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Petroli Tanzania – TPDC, Mussa Makame amesema mpango wa kununua vituo vya gesi vitano vyenye uwezo wa kuhama unaandaliwa kuanzia na vitatawanywa maeneo mbalimbali.
Viongozi wa serikali ndiyo wenye sheli main road ni ngumu sn
 
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, imeishauri Serikali kuagiza magari yenye mfumo wa gesi ambao una gharama nafuu, hali itakayosaidia kupunguza gharama za mafuta kutokana na uwepo wa Gesi Nchini.
Serikali ikikataa wataifanya nini
 
Sasa hivi soko kubwa la hiyo gesi wanatumia sekta binafsi ndio wengi wamefunga huo mifumo

Issue kubwa ni vituo vya kujaza haviko nchi nzima .Wawekezaji waliojitosa nchini kuanzisha vituo ni wachina Kwa Dar naona Kuna kimoja tu Cha mchina Serikali wanacho kimoja kama sikosei

Uwekezaji uhimizwe ili vijengwe na sehemu za kuweka mitungi ziongezeke
 
Back
Top Bottom