Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
499
1,000
"Katika mazishi Wazee Chato walimuomba Rais Samia mkoa wakidai ni ahadi ya mtangulizi wake.kwa hekima akasema ataangalia vigezo.Kama Mbunge Mstaafu jirani Muleba Kusini najua vigezo havipo.Wazo halitekelezeki. Wazee jirani na sisi naamini tutapewa nafasi kushauri"Anna Tibaijuka

1622354699288.png
---
Anaandika PROF. ANNA K. TIBAIJUKA

Ramani inaonyesha Chato ni sehemu ya Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera. Kiuhalisia. Na kihistoria. Mengine ni kulazimishalazimisha tu.

Naendelea kusisitiza hakuna hoja yoyote ya kiuchumi kuunda mkoa wa Chato. La sivyo basi tuelimishwe.

Ila kama mnapenda siasa za upendeleo wa sehemu fulani ama kwa kuwa mkubwa aliwahi kuzaliwa pale au mtu apewe nafasi kwa sababu ni mtoto wa kiongozi endeleeni kuwabebesha wananchi mizigo ya kulipa kodi kusudi wateule wajichane. Period.

Kwanza ikumbukwe Mkoa wa Geita ulianzishwa kusudi Chato iwe Makao Makuu. Ikakosa vigezo. Geita mjini ikaonekana ndiyo yenye sifa za kuwa Makao Makuu ya Mkoa mpya wa Geita. Hii ilikuwa 2010. Sasa 11 years later Chato ati ina vigezo kuwa Makao Makuu ya Mkoa wake wenyewe? Are we serious with our development? Really? Na Rais wetu mpendwa SSH tunataka kweli kumtwisha zigo la kuamua jambo hili na controversy zake? Elimu haina mwisho. Mimi kama kuna vigezo naomba viorodheshwe. Labda ndiye sina taarifa. Ila so far Hoja ya kuwaletea maendeleo Kakonko, Biharamulo, Ngara na Muleba inayokatwa vipande ninazikataa. Mkoa unaweza kuleta maendeleo gani kwa Wilaya yake wakati Mkoa unategemea bajeti ya Serikali Kuu. Mkoa una mapato gani zaidi ya kutumia kodi? Lets be serious. Maendeleo yanatokana na uwekezaji na uwezeshaji kwa wananchi. Siyo watumishi wa Serikali tena baadhi bila maadili wanaweza kuishia kuwabugudhi wananchi badala ya kuwa msaada.

Njia pekee kumuenzi Hayati Magufuli ni kurekebisha mambo ambayo kama binadamu hakufanya vizuri. Mengine yote ni ubinafsi. Na kufifisha sifa zake katika historia ya nchi hii. Tumuache apumzike.

Miundombinu iliyowekwa Chato siyo kigezo kuunda mkoa hapo. Tuikamilishe na kuitafutia matumizi mbadala ya kitaifa. Mfano Airport ya Chato inaweza kufanywa Hub ya kilimo cha contract floriculture na horticulture...(kilimo mkataba cha maua na mboga) ili tuwe na ndege za mizigo kuja kubeba. Na maziwa .

Hospitali ya Kanda Chato.... naomba tutathmini kwanza maendeleo ya hospitali ya Mloganzila. State of the Art buildings only 40km away from Dar City Centre na Muhimbili. Mojawapo ya mafanikio makubwa ya Awamu ya nne. Lakini Angalia changamoto zake. Uhaba wa madaktari hadi leo. Sasa hao specialist doctors watakaokubali kuishi Chato mtawalipa fedha kiasi gani?. A hospital is not just buildings. Its manpower resources and the economy surrounding it. Katika dhana ya mipango miji na maendeleo ya makazi lazima vigezo vyote hivyo kuangaliwa. Kwa uelewa wangu Chato haina vigezo. Tusidanganyane.
 

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
12,116
2,000
"Katika mazishi Wazee Chato walimuomba Rais Samia mkoa wakidai ni ahadi ya mtangulizi wake.kwa hekima akasema ataangalia vigezo.Kama Mbunge Mstaafu jirani Muleba Kusini najua vigezo havipo.Wazo halitekelezeki. Wazee jirani na sisi naamini tutapewa nafasi kushauri"@AnnaTibaijuka
Mama pumzika zako makongo Dar ya huko waachie wana Chato na Mama Mkoa Geita wameshakubali .....acha iwe utaambiwa ya kuambiwa wilaya mojawapo au 2 Kagera itamegwa kwenda Chato....pambana na wajukuu mama awamu 6 hii sukuma gang wanalia huko legacy ......ya kulazimishia
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
105,688
2,000
"Katika mazishi Wazee Chato walimuomba Rais Samia mkoa wakidai ni ahadi ya mtangulizi wake.kwa hekima akasema ataangalia vigezo.Kama Mbunge Mstaafu jirani Muleba Kusini najua vigezo havipo.Wazo halitekelezeki. Wazee jirani na sisi naamini tutapewa nafasi kushauri"@AnnaTibaijuka
Chato haina sifa hiyo na hata uwanja wa ndege pale zilitumika fedha za watanzania vibaya.
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
105,688
2,000
Mama pumzika zako makongo Dar ya huko waachie wana Chato na Mama Mkoa Geita wameshakubali .....acha iwe utaambiwa ya kuambiwa wilaya mojawapo au 2 Kagera itamegwa kwenda Chato....pambana na wajukuu mama awamu 6 hii sukuma gang wanalia huko legacy ......ya kulazimishia
Mkoa wa geita hawana mamlaka ya kumlazimisha mkuu wa nchi atumie fedha za umma kwenye mambo yasiyo na tija kwa umma.

Chato haina sifa ya kuwa mkoa maana chato ni kiwilaya sawa na kibondo au ukerewe
 

Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
14,525
2,000
Chato haina vigezo vya kuwa Mkoa, kwanza hii italeta picha mbaya ya ubinafsi kwa JPM, kwa mfano, je JK nae angetaka Msoga iwe Mkoa, Mkapa nae angetaka Masasi iwe Mkoa, Mzee Mwinyi nae angetaka Mkuranga iwe Mkoa, Mwalimu Nyerere angetaka Butiama iwe Mkoa, tungefika wapi? Ila hawakufanya hivyo hata kidogo, Ili kuwa Mkoa ni vigezo, sio will tu ya Mkuu wa nchi kwa wakati husika. Chato haijakidhi vigezo kabisa kuwa Mkoa. Tusilazimishe
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
10,466
2,000
"Katika mazishi Wazee Chato walimuomba Rais Samia mkoa wakidai ni ahadi ya mtangulizi wake.kwa hekima akasema ataangalia vigezo.Kama Mbunge Mstaafu jirani Muleba Kusini najua vigezo havipo.Wazo halitekelezeki. Wazee jirani na sisi naamini tutapewa nafasi kushauri"@AnnaTibaijuka
Prof Tibaijuka naomba unywe kret nzima ya Heineken hapo. Umeongea madini tupu.

Japo najua Sukuma gang watanuna.

Shubamiti! Eti Kijiji cha Chato kiwe mkoa. Mkoa my foot!
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,112
2,000
Kiukweli lipo tatizo la kufikirika,ni Bora kuongeza halmashauri na kupandisha hadhi palipo na vigezo, ofisi ya RC Haina impact kubwa kwa ustawi wa Jamii. Kwa dunia ya leo mawasiliano hata wazo la kuhamia Dodoma halina tija Bora fungu like lingetumika boresha sector kilimo, SGR ingepata mizigo ya kutosha mbeleni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom