Prof. Kennedy kutenguliwa siku moja baada ya kuapishwa kuwa Katibu Mkuu Wizara nyeti ya Mambo ya Nje kuna shida katika "Vetting" za Viongozi?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Juzi Mhe. Rais Rais alimteua Prof. Kennedy Gaston kuwa Katibu Mkuu wizara ya mambo ya nje (anayeshughulikia ushirikiano wa Afrika Mashariki). Ijumaa tar. 1 akaapishwa huko Zanzibar. Jumamosi akarudi nyumbani Dsm. Jana jumapili akaenda kanisani kutoa shukrani kwa kuteuliwa lakini jana usiku akafurushwa na kupelekwa ofisi ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali. Yaani ameondolewa kwenye nafasi hata hajaingia ofisini.

Kwahiyo Prof. Kennedy ndiye Katibu Mkuu ambaye amedumu kwa kipindi kifupi sana maana ametenguliwa kabla hata hajaingia ofisini. Wizara ya mambo ya nje inaingia kwenye historia ya kuwa na Katibu Mkuu ambaye haijui ofisi. Kwa kuwa tayari alishaapa, jina lake litakuwepo kwenye orodha ya Makatibu wakuu wa wizara. Lakini "tenure" yake itakua siku moja, maana aliapishwa September 1 na kufurushwa September 3 bila kuingia ofisini.

Anyway, nadhani timu ya Rais inayoshughulika na "vetting" za viongozi haifanyi kazi yake ipasavyo. Huwezi kumteua Katibu Mkuu wa wizara nyeti kama ya Foreign kwa kubahatisha. Kama walikua hawana uhakika nae wasingemteua. Bora nafasi ingebaki "vacant" kuliko kumteua mtu leo na kumuondoa kesho.

Inaonekana hakuna umakini kwenye teuzi. Maafisa wanaomsaidia mama wanapuga ramli. Na hii si mara ya kwanza. Kuna jamaa mmoja aliwahi kuteuliwa DED na DAS kwa wakati mmoja. Ikaleta gumzo hadi yakafanyika mabadiliko. Timu ya "vetting" imsaidie Rais vizuri. Iache kufanya betting. Taarifa ya Ikulu haipaswi kuwa ya kubahatisha, inapaswa iwe firm and legitimate. Isiwe kama taarifa ya vicoba vya Mburahati. Fanyeni vetting sio betting.!

Screenshot 2023-09-04 123717.png

Screenshot 2023-09-04 124503.png

Screenshot 2023-09-04 124127.png

Malisa JG
 
Kwahiyo Prof. Kennedy ndiye Katibu Mkuu ambaye amedumu kwa kipindi kifupi sana maana ametenguliwa kabla hata hajaingia ofisini. Wizara ya mambo ya nje inaingia kwenye historia ya kuwa na Katibu Mkuu ambaye haijui ofisi. Kwa kuwa tayari alishaapa, jina lake litakuwepo kwenye orodha ya Makatibu wakuu wa wizara. Lakini "tenure" yake itakua siku moja, maana aliapishwa September 1 na kufurushwa September 3 bila kuingia ofisini.
Kikubwa apewe haki zake za uhamisho kutoka Wizara hiyo kwenda ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali.
 
Juzi Mhe. Rais Rais alimteua Prof. Kennedy Gaston kuwa Katibu Mkuu wizara ya mambo ya nje (anayeshughulikia ushirikiano wa Afrika Mashariki). Ijumaa tar. 1 akaapishwa huko Zanzibar. Jumamosi akarudi nyumbani Dsm. Jana jumapili akaenda kanisani kutoa shukrani kwa kuteuliwa lakini jana usiku akafurushwa na kupelekwa ofisi ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa serikali. Yaani ameondolewa kwenye nafasi hata hajaingia ofisini.

Kwahiyo Prof. Kennedy ndiye Katibu Mkuu ambaye amedumu kwa kipindi kifupi sana maana ametenguliwa kabla hata hajaingia ofisini. Wizara ya mambo ya nje inaingia kwenye historia ya kuwa na Katibu Mkuu ambaye haijui ofisi. Kwa kuwa tayari alishaapa, jina lake litakuwepo kwenye orodha ya Makatibu wakuu wa wizara. Lakini "tenure" yake itakua siku moja, maana aliapishwa September 1 na kufurushwa September 3 bila kuingia ofisini.

Anyway, nadhani timu ya Rais inayoshughulika na "vetting" za viongozi haifanyi kazi yake ipasavyo. Huwezi kumteua Katibu Mkuu wa wizara nyeti kama ya Foreign kwa kubahatisha. Kama walikua hawana uhakika nae wasingemteua. Bora nafasi ingebaki "vacant" kuliko kumteua mtu leo na kumuondoa kesho.

Inaonekana hakuna umakini kwenye teuzi. Maafisa wanaomsaidia mama wanapuga ramli. Na hii si mara ya kwanza. Kuna jamaa mmoja aliwahi kuteuliwa DED na DAS kwa wakati mmoja. Ikaleta gumzo hadi yakafanyika mabadiliko. Timu ya "vetting" imsaidie Rais vizuri. Iache kufanya betting. Taarifa ya Ikulu haipaswi kuwa ya kubahatisha, inapaswa iwe firm and legitimate. Isiwe kama taarifa ya vicoba vya Mburahati. Fanyeni vetting sio betting.!

Malisa JG
Anaelewa alichokifanya, muulizeni.
 
makosa kama haya !!!???
 
Back
Top Bottom