Miaka ya 64 ya Rais Samia, safari ya kusisimua kutoka Karani wa Masijala hadi Mkuu wa Nchi

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Na Bwanku M Bwanku.

Jumamosi Januari 27, 2024 Rais wa Awamu ya 6 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alitimiza miaka 64 toka kuzaliwa kwake akihudumu nyadhifa ya juu kabisa nchini toka achukue mikoba hiyo Machi 19, 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya 5 Hayati John Pombe Magufuli.

Kwa wasiyemfahamu sana, Rais Samia ndiye Mwanamke wa kwanza katika historia ya Tanzania kushika nafasi ya Urais wa Tanzania baada pia kuandika historia ya kuwa Mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Makamu wa Rais mwaka 2015 hadi 2021, nafasi kuu za juu kabisa katika Taifa letu.

Wakati huu akisherehekea miaka 64 ya kuzaliwa kwake na miaka isiyozidi mitatu toka ashike hatamu ya kuongoza Taifa, Rais Samia ameshatunukiwa Shahada 3 za Heshima pamoja na Tuzo na kutajwa kwa zaidi ya mara 5 kutoka kwa majarida na taasisi mbalimbali kubwa za kimataifa kwa kutambua kazi yake kubwa anayoifanya kusukuma maendeleo kwenye Taifa lake.

Tayali Rais Samia ametunukiwa Shahada 3 za Heshima (Honoris Causa) na Vyuo Vikuu mbalimbali ndani na nje ya nchi. Walianza UDSM Novemba 30, 2022 kumtunuku Shahada ya Juu ya Heshima kwenye Humanitia na Sayansi Jamii (Social sciences), Oktoba 10, 2023 wakafuata Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru cha nchini India na wiki hii Desemba 28, 2023 Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) kumtunuku Shahada nyingine ya Uzamivu ya Usimamizi wa Utalii na Masoko (Doctor of Philosophy in Tourism Management and Marketing- Honors Causa).

Si jambo linalotokea mara nyingi kwa kiongozi mmoja ndani ya Taifa kutunukiwa Shahada 3 za Heshima kwa mpigo ndani ya muda mfupi wa uongozi wake. Wote tunakumbuka Hayati Rais Magufuli wakati wa uongozi wake wa Awamu ya 5 alitunukiwa mara moja Shahada ya Heshima na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) mwaka 2019 na Mstaafu Rais wa Awamu ya 4 Jakaya Kikwete pia mwaka 2011 alitunukiwa mara moja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Hii inaonyesha kazi kubwa aliyoifanya na jamii inaona inatunuku.

Kwa miaka ya karibuni, anakuwa Rais wa kwanza wa kizazi kipya wa Tanzania kutunukiwa Shahada ya Heshima na Chuo kikubwa chenye heshima kubwa duniani cha Jawaharlal Nehru use cha India huku akiandika historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kutunukiwa Shahada ya Heshima na Chuo hicho na Rais wa 3 pekee baada ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin pamoja ya Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan Hayati Shinzo Abe kutunukiwa na Chuo hicho.

Tayali majarida makubwa kama lile la Avance Media la Ghana limemtaja mara mbili kama mmoja wa wanawake wenye ushawishi mkubwa Afrika na duniani kwa ujumla, huku Kamati ya Chama Cha Waandishi wa Habari za Miundombinu na Fedha Afrika (MIFA) mwaka 2022 likimchagua kuwa mshindi wa tuzo ya Rais aliyefanya mapinduzi makubwa zaidi ya uwekezaji wa miundombinu barani Afrika huku pia majarida makubwa yanayosomwa kote ulimwenguni kuanzia lile la Times na Forbes likimtaja kama moja ya watu wenye ushawishi mkubwa duniani kwa kazi zake kubwa zilivyoacha alama kwenye jamii yake.

Rais Samia Suluhu Hassan alizaliwa Januari 27, 1960 katika Kijiji cha Kizimkazi kilichopo Jimbo la Makunduchi, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja Visiwani Zanzibar, kabla ya kuanza masomo yake ya Msingi katika shule mbalimbali ikiwemo Shule ya Msingi Chwaka kuanzia mwaka 1966 hadi 1968, kisha Ziwani mwaka 1970 na baadae Shule ya Msingi Mahonda mwaka 1972.

Baadae akajiunga Sekondari ya Ng'ambo kwa masomo ya kidato cha kwanza hadi cha tatu kisha Shule ya Sekondari Lumumba alikomaliza Kidato cha nne mwaka 1976.

Kwa maelezo yake mwenyewe Rais Samia wakati akihojiwa na Kituo cha Habari cha TBC, kuanzia shule ya awali mpaka anafika kidato cha nne alisoma kwenye shule zaidi ya 10 na anataja sababu ya hiyo kutokea ni kwasababu baba yake mzazi alikuwa mwalimu kwahiyo alipokuwa anahamishwa kwenye vituo vya kazi na yeye alihama na familia yake kwenda kwenye shule au eneo alilohamishiwa baba yake.

Kwa mara ya kwanza Rais Samia anasimulia aliajiriwa mwaka 1977 katika ofisi moja ya kwenye Wizara ya Mipango na Maendeleo- Zanzibar akiwa na umri mdogo sana wa miaka 17 lakini alirudishwa nyumbani baada ya kuonekana kuwa na umri mdogo lakini baadae aliitwa tena kufanya kazi eneo hilo na ndiyo ilikuwa ajira yake ya kwanza na mwanzo wa safari yake ya kusisimua ya utumishi wake katika ofisi hiyo ya maendeleo.

Baadae alijiendeleza kimasomo kwa kusoma Ngazi ya Cheti (Certificate) alipohitimu mwaka 1983 kwenye masuala ya Uchumi na Takwimu kwenye Chuo cha Uchumi Zanzibar na ndipo alipoajiriwa kufanya kazi kwenye Wizara ya Mipango na Maendeleo mwaka 1983 hadi 1986 na baadae kwenda Chuo Cha Maendeleo ya Uongozi Mzumbe (IDM) kufanya Advanced Certificate ya Utawala, kabla ya kwenda kusoma Kozi ndogondogo za miezi mitatu mitatu kwenye Chuo cha Utawala wa Umma kule Lahore, Pakistan mwaka 1987, kisha Taasisi ya Eastern and Southern African Management Institute (ESAMI) mwaka 1991 na Taasisi ya Uongozi ya Hyderabad, India mwaka 1998 kwa ajili ya Astashahada ya Utawala.

Baadaye, alikwenda sasa Chuo Kikuu cha Manchester, Uingereza alikosoma Undergraduate Diploma ya Uchumi kisha akafanya Masters Degree (Uzamili) kwenye Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Southern New Hampshire, Marekani.

Kama nilivyoanza kueleza pale juu kidogo, mwaka 1977 aliajiriwa kwa mara ya kwanza kwa nafasi ya chini akiwa Karani Masijala lakini kwa maelezo yake mwenyewe, aliona pale sio mahali pake maana alikuwa anafanya kazi zaidi ya aliowakuta pale kwa kufanya hata zile zilizofanywa na watu wa Juu wenye vitengo na ndio maana akaamua kwenda kuongeza elimu ili aendelee zaidi na baada ya kuongeza elimu kama nilivyoeleza pale Juu ndipo akaajiriwa na Shirika la Chakula Duniani (World Food Program) kwenye project zao mbalimbali pale Zanzibar, akafanya hapo kazi kwa miaka 9 kuanzia mwaka 1988 hadi 1997.

Baada ya kutoka Umoja wa Mataifa kwenye Shirika la Chakula Duniani, akaingia sasa kwenye Taasisi zisizo za Kiserikali (NGO's) akafanya kazi kubwa sana kuziendeleza ukuzaji wake wa NGOs za Zanzibar mpaka kuwa Mkurugenzi wa kwanza wa Taasisi zisizo za Kiserikali Zanzibar (ANGOZA) mwaka 1995 mpaka mwaka 2000 huku akifanya shughuli zingine mbalimbali na kushika nafasi zingine kama Mlezi wa Jumuiya ya Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Zanzibar kutoka mwaka 1997 hadi 2000, Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Fursa sawa kwa wote- EOTF kutoka 1996 hadi 2000, Mwanachama wa Lions Club Zanzibar kutoka 1991 hadi 1998, Mjumbe wa Kamati ya Uundaji wa Sera ya Elimu Zanzibar mwaka 1996, Mwanachama Mwanzilishi wa Taasisi ya Kuchochea Maendeleo ya Wanawake Zanzibar kutoka 1991 hadi 1994 na nafasi zingine kama Mjumbe wa Kamati ya Msamaha wa Wafungwa (Parole Committe).

Baada ya safari yote ya elimu ndani na nje ya nchi, kuzunguka kote huko na kufanya kazi kubwa na nzito kwenye Serikali, Taasisi za Kimataifa, NGO's na Taasisi zingine, hatimaye mwaka 2000 ndipo akapata mawazo ya kuingia kwenye siasa na sababu moja tu anasema iliyomvuta kuingia kwenye siasa, ni kwamba alikuwa anaangalia Baraza la Wawakilishi ile mijadala inavyoendelea, kama inavyofahamika Zanzibar upinzani umepamba moto kwahiyo kilichomsukuma ni kuingia tu kule nikasaidie kupeleka hoja za wananchi na kuisimamia serikali.

Mwaka 2000 akajitosa kwenye siasa na kufanikiwa kushinda kuwa Mbunge wa Viti Maalum vya Wanawake baada ya watu wengi kwenye Mkoa wake wa Kusini Unguja kumkubali sana baada ya kazi kubwa aliyoifanya ya kuwasaidia wananchi wakati akiwa na Shirika la Chakula Duniani kusaidia masuala ya chakula kwa wingi kwenye eneo hilo baada ya kuwa na uhaba wa chakula, akaingia Baraza la Wawakilishi na Rais wa Zanzibar wa wakati huo Mhe. Abeid Amani Karume akamteua kuwa Waziri katika Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira, Maendeleo ya Wanawake na Watoto kwenye Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ambako alifanya kazi kwa miaka mitano mpaka 2005 ambapo tena wananchi waliendelea kumuamini kuwa Mbunge wa Viti Maalum na kisha tena 2005, Rais Karume akaendelea kumuamini na kumteua kuwa Waziri kwenye Wizara ya Utalii, Biashara na Uwekezaji ambako nako alihudumu kwa miaka mitano bila kubadilishwa wala kutumbuliwa mpaka 2010.

2010 kwenye Uchaguzi Mkuu akaamua kuachana na Ubunge wa Viti Maalum na kwenda kugombea Ubunge wa Jimbo kwenye Jimbo la nyumbani Makunduchi na kushinda kama kawaida yake na sasa kuwa Mbunge wa Jimbo na si tena wa Viti Maalum na kuingia moja kwa moja kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sasa akateuliwa kuwa Waziri kwenye Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano mpaka mwaka 2015.

Mwaka 2014 wakati Taifa likipambana kupata Katiba Mpya na Rais wa kipindi hicho wa Awamu ya 4 Dkt..Jakaya Mrisho Kikwete kuunda Bunge Maalum la Katiba. Bunge la nyumbani la Wawakilishi la Zanzibar likampendekeza kuwa Msaidizi wa Bunge la Katiba na hivyo yeye kuteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba na Hayati Samwel Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tanzania akiwa Mwenyekiti wa Bunge lile la Katiba.

Ilipofika mwaka 2015 wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikimsimamisha Hayati John Pombe Magufuli kuwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Kamati Kuu ya CCM chini ya Mgombea mwenyewe wa CCM Hayati Dkt. John Pombe Magufuli walimteua yeye kuwa Mgombea Mwenza wa Mgombea Urais wa CCM na baada ya CCM kushinda kwenye Uchaguzi Mkuu ule wa mwaka 2015 ulimfanya yeye moja kwa moja kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania chini ya Hayati Magufuli, akiwa Mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo ya juu ya pili kwenye uongozi wa nchi yetu kabla ya Machi 17, 2021 ambapo aliyekuwa Rais, Hayati Magufuli alipofariki dunia na yeye kuwa rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mpaka sasa, Tanzania ikisherehekea miaka 64 ya maisha yake toka kuzaliwa mwaka 1960, maisha ya Rais Samia Suluhu Hassan yamekuwa ya utumishi tosha kwa watu huku akifanya kazi nyingi sana ndani ya nchi kwenye taasisi zisizo za kiserikali, ndani ya serikali kwenye nyadhifa kubwa kubwa na nzito kitaifa pamoja na kazi kubwa alizozifanya nje ya nchi hasa kwenye Shirika la Chakula Duniani.

Maisha yake yamekuwa msisimko tosha, darasa na inspirational tosha kwa watoto wa kike na wanawake kuamini kwamba wanawake ni Jeshi kubwa na kwa vijana kuamini kwamba kila kitu kinawezekana chini ya jua iwe umetoka kwenye familia maskini, uwe wa jinsia yoyote ile na mengine, muhimu ni kuweka malengo yako na kufanya kazi kwa bidii na kujituma. Historia yake imejaa upekee na uimara wa wanawake kwani licha ya yote lakini Rais Samia ameweza kuhimili mpaka sasa akiwa Mkuu wa Nchi iliyotoka kwenye majanga ya kuondokewa na Mkuu wake wa nchi na majanga ya maradhi ya Uviko-19 yaliyoleta athari kwenye uchumi lakini bado Taifa liko imara.

Kwenye Chama chake cha siasa (CCM) ambacho ni moja ya Chama kikubwa kabisa cha Siasa Barani Afrika na Duniani kwa ujumla, Rais Samia ameshika nafasi nyeti sana na za juu kabisa kabla ya sasa yeye mwenyewe akiwa ndiye Mkuu wa Chama kama Mwenyekiti wa Chama hicho. Amepita kwenye nafasi mbalimbali nyingi na kubwa sana ndani ya Chama toka ajiunge nacho mwaka Juni 10, 1987.

Ndani ya CCM, Rais Samia kabla ya sasa kuwa Mkuu wa Chama hicho kama Mwenyekiti, amewahi pia kushika nafasi za juu kabisa ndani ya Chama ambazo zingine anaendelea kuzishika mpaka leo kama kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, nyadhifa alizonazo mpaka sasa. Nyadhifa hizi ni za juu sana na zote zikiwa ndizo zenye maamuzi ndani ya CCM.

Pia amewahi kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja, Mjumbe wa Kamati za Siasa Mkoa na Wilaya ya Kusini Unguja, Mwanachama wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) na zaidi kushiriki kwenye tukio muhimu na nyeti la kuandika Ilani ya CCM mara 4 mfululizo kuanzia mwaka 2005/2010, 2010/2015, 2015/2020, 2020/2025.

Nje ya maisha yake toka kuzaliwa, elimu na utumishi, Rais Samia ameolewa na Bwana Hafidh Ameir na wamejaaliwa watoto wanne, watatu wakiwa wakiume na mmoja wa kike.

Huyu ndiye Mwanamke wa Shoka, asiyelaza zege, Muumini wa Vitendo kuliko maneno, Mtaalamu wa Maridhiano na shujaa wa kulinda demokrasia mbeba maono na msikivu kwelikweli ambaye tunasherekea miaka yake 64 iliyotukuka.

FB_IMG_1707205817466.jpg
status_me_status_IMG-20240131-WA0018.jpg

bwanku55@gmail.com.
 
Baadae alijiendeleza kimasomo kwa kusoma Ngazi ya Cheti (Certificate) alipohitimu mwaka 1983 kwenye masuala ya Uchumi na Takwimu kwenye Chuo cha Uchumi Zanzibar na ndipo alipoajiriwa kufanya kazi kwenye Wizara ya Mipango na Maendeleo mwaka 1983
Kwa nini umekwepa kuelezea kuhusu alivyoolewa, na sababu ya yeye kutotumia jina la ubini wa mumewe?
 
Na Bwanku M Bwanku.

Jumamosi Januari 27, 2024 Rais wa Awamu ya 6 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatimiza miaka 64 toka kuzaliwa kwake akihudumu nyadhifa ya juu kabisa nchini toka achukue mikoba hiyo Machi 19, 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya 5 Hayati John Pombe Magufuli.

Nchi ipo gizani wewe unaleta porojo za kichawa hapa?!

Bandıko lote hili hakuna sehemu uliyozungumzia changamoto za wananchi ambazo zimefanyiwa kazi.

Nchi nzuri watu HOVYO.
 
.

Maelezo mengii, ila ulicho andika hakieleweki..

🤒🤒🤒🤒

HAbari Bwana Bwanku!
Nitazungumzia kuhusu Honorary Causa na Awards Mbalimbali..

Kwangu mimi sio Thamani Yake umeandika kuwa Ni rais wachache waliotunukiwa Hapo ndo imenifanya kuja Kuweka sawa..

Rais Nyerere Alikuwa na Honorary Degree(PhD) zisizopungua 23 huku akiwa na Awards 23 na Hakuwahi kujiita Doctor..

Nyerere Alikuwa na Honorary Zifuatazo..

1. University of Edinburgh (United Kingdom)

2. University of Dugueshe (United States of America)

3. Cairo University (Egypt)

4. University of Nsukka (Nigeria)

5. University of Ibadan (Nigeria)

6. University of Monrovia (Liberia)

7. Toronto University (Canada)

8. Havard University (United States of America)

9. Howard University (United States of America)

10. Ljubliana (Yugoslavia) - Honorary Doctoral of Law (26 March 1985)

11. Pyongyang University (Korea) - Honorary Doctorate of Philosophy (28th March 1985)

12. National University of Lesotho (Lesotho)

13. The State House Dar es Salaam (Tanzania) - Honorary Degree for Diplomacy (20th Sept, 1985)

14. Havana University of Cuba (Cuba) - Honorary Degree of Doctor Of Philosophy (30th Sept 1985)

15. University of Dar es Salaam (Tanzania) - Honorary Degree of Literature Honoris Causa (13th Sept 1986)

16. Universities of Philippines (Philippines) - Honorary Doctorate of Humanities (12th July 1991)

17. Manila (Philippines) - Honorary Doctor Degree (12th October 1992)

18. Makerere University Kampala (Uganda) - Honorary Doctor of Laws (29th January 1993)

19. Open University of Tanzania (Tanzania) - Doctor of Letters Honoris Causa (15th March 1997)

20. Claremont University Centre (United States of America) - Doctor of Laws for Claremont graduate School California (17th May 1997)

21. Sokoine University of Agriculture (Tanzania) - Doctor of Philosophy Honoris Causa (28th November 1997)

22. University of Fort Hare (South Africa) - Doctor of Laws Honoris Causa (23rd April 1998)

23. Lincoln University (United States of America) - Honorary Degree of Laws (5th May 1998)

sources: JULIUS nyerere Honorary and Awards

Mkapa Alikuwa na Honorary PhD 15 zifuatazo ni.chache kati ya hizo

  1. Sōka University JapanHonorary degree1998
  2. Morehouse College United StatesHonorary degree1999
  3. Open University of Tanzania TanzaniaHonorary degree2003
  4. National University of Lesotho LesothoDoctor of Law2005
  5. Kenyatta University KenyaDoctor of Education2005
  6. University of Dar es Salaam TanzaniaHonorary degree2006
  7. Newcastle University United KingdomDoctor of Civil Law2007
  8. University of Cape Coast GhanaDoctor of Letters2008
  9. Makerere University UgandaDoctor of Law2009

Kikwete alikuwa Doctorate za Honorary PhD zaidi ya 27 hizi hapa.chache au Baadhi..
  1. 2006University of St. Thomas, Minnesota United StatesDoctor of Law[
  2. 2008Kenyatta University KenyaDoctor of Humane Letters
  3. 2010Fatih University TurkeyDoctorate in International Relations
  4. 2010Muhimbili University TanzaniaDoctor of Public Health
  5. 2010University of Dodoma TanzaniaHonoris Causa
  6. 2011University of Dar es Salaam TanzaniaDoctor of Law
  7. 2013University of Guelph CanadaDoctor of Law
  8. 2014China Agricultural University ChinaHonorary Professor
  9. 2014Nelson Mandela–AIST TanzaniaHonoris causa
  10. 2015University of Newcastle, New South Wales AustraliaDoctor of Laws
  11. 2016Open University of Tanzania TanzaniaHonorary doctorate in leadership.
Mwinyi (Alhassan Mwinyi "Mzee Ruksa) alikuwa na honorary chache kuliko hao alikuwa nazo kama sikosei 7 hivi..

  1. The Open University of Tanzania Tanzania Doctor of Letters 2012
  2. The East African University Kenya Doctor of Philosophy in Business Management 2013
  3. Honorary Doctorate of Political Science at the International University of Africa (IUA) in Khartoum, Sudan mwaka 2016

Hivi wahariri wa Siku hizi huwa mnatoa wapi Hizo Makala Bila kuichunguza Habari unaweka mbele utashi unaandika kile unachoona kichwani mwako ndiyo habari 😀😀
Dah inasikitisha sana..
 
kila mtu ana cv yake akielezea hapa kila mmoja wetu atampongeza.
bora na la maana ni nini ulicho fanya chenye impact kati hizo cv.

umakamu wa urahisi ni hisani ya watu, urahisi ni nasibu, matokeo baada ya urais haya sadifu cv yake yote.

taifa linahitaji mtu mmoja hivi ambaye hajawahi kuwepo kinywani mwa watu wala kwenye taswira zao aweze kubomoa mfumo tulio nao tuanze moja.

kupotea wakati wa kwenda sio mbaya ila wakati wa kurudi ukipitea huo ndio ujinga.
 
maelezo marefu na hakuna kitu cha maana ndani yake zaidi ya maisha magumu tu kwa watu.
umeme shida, sukari hakuna, dola hakuna, mfumko wa bei unaongezeka siku hadi siku.
 
a mtu ana cv yake akielezea hapa kila mmoja wetu atampongeza.
bora na la maana ni nini ulicho fanya chenye impact kati hizo cv.

umakamu wa urahisi ni hisani ya watu, urahisi ni nasibu, matokeo baada ya urais haya sadifu cv yake yote.

taifa linahitaji mtu mmoja hivi ambaye hajawahi kuwepo kinywani mwa watu wala kwenye taswira zao aweze kubomoa mfumo tulio nao tuanze moja.

kupotea wakati wa kwenda sio mbaya ila wakati wa kurudi ukipitea huo ndio ujinga.
Umeongea vzr sana ndugu yangu.
 
Hii CV ina walakini.
Kuzaliwa 1960 plus miaka saba kabla ya kuanza shule ni 1967. Shule ya msingi ameanza 1966 au 1967?
Kuanza shule ya msingi ni 1967 plus 7 alimaliza msingi 1974?
Secondary kama ameanza 1975 plus 4 maana yake alimaliza kidato cha nne 1979?
Kama aliajiriwa mwaka 1977, ina maana alikuwa anafanyakazi huku akihudhuria masomo ya upili? 😲😮
 
Back
Top Bottom