Wana JF,
Nimekuwa nawaza kwa muda mrefu kuwa nani Rais bora tulishewahi kupata Tanzania. Baada ya kufikiri pamoja na maoungufu yao nimeona kwanza ni Nyerere. Pia anafuata Mkapa na kama siyo Anna Mkapa kumfundisha UFISADI basi leo hii angelikuwa kamzidi hata Nyerere na JK angelikuwa anafokewa na Mkapa. Lakani Nkapa akaona heri PESA kuliko heshima ya kweli na kukumbukwa milele kwa WEMA.
Sasa ukija angalia unajikuta wamebaki wawili yaani Shemeji aka Ngapulila aka Mzee wa ruksa aka Mwinyi akishindana na Msanii or Smiling handsome president SoulJAH-KAYA. Yes , yeye ni EX-JWTZ. Katika hawa wawili Mwinyi aling'ang'ania MADARAKA wee hadi akamaliza miaka 10 na ilipofika akaanza vikampeni vya chinichini ili kubadili katiba na ashike URAIS kwa miaka mingine 3 na jumla iwe 15. Mhhh, Mchonga meno akamshtukia na kumpandishia. Nakumbuka alisema "Ni nchi gani mambo ya IKULU yanaamuliwa kitandani...." Sitti Mwinyi inasemekana ndiyo alikuwa Rais wetu. Halafu watu wanafikiri yule mama wa Liberia ndiyo rais wa kwanza mwanamke Africa. Waambieni kabla yake alikuwepo Sitti Mwinyi.
Sasa tofauti ya MWINYI na KIKWETE ni kuwa Kikwete hana UCHU wa madaraka kwa muda mrefu kuwa Rais wetu. Kaona mambo yanamshinda na yamekuwa magumu. Sasa hivi anavuta zake za mwishomwisho na ikifika mwaka 2010 anajiendea zake Msoga na kula za Uzeeni. Hekalu lake kweli zuri na hadi kwenye GOOGLE EARTH unaliona.
Mwaka 2010 unakaribia. Tuanze kufikiri tutamuenzi vipi Kikwete kwa busara zake za kutoendelea na madaraka na kupisha wengine waje wapambane na UFISADI, Mauwaji ya Albino, tatizo la umeme, maji, maisha bora kwa Watanzania, usafiri hasa kwa wanafunzi mijini, nk. Yeye atakuwa Rais wa Pili baada ya Mandela kwa kufanya term 1 na kupisha wengine. Bravo Kikwete.