Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Koba,
Alimdiktate nani?

kwamba unabisha Nyerere hakuwa dikteta?? yeye na Mugabe kwangu mimi sioni tofauti ilipo kati yao......mi-viongozi ya Afrika 99.999% ni midikteta!!! kama unabisha haya, maana kuna wengine hapa wanasema Jongwe ni mzalendo! kaazi kwelikweli.
 
Koba,
Alimdiktate nani?

..dikteta mkubwa sana yule,alicontrol tunachokula,tunachoweza kumiliki,tunachotaka kusoma&kuangalia,alituweka ndani bila mashtaka tuu maana wakikuhisi tuu umekwisha,alinyang'anya mali zetu kuanzia nyumba mpaka mashamba kuwagawia wazembe ili kuwa popular au ni ndoto zake tuu za mchana,alitulazimisha tuishi sehemu alizotaka etc bila idhini yetu au makubaliano na sisi,hizo ndio tabia za dikteta kama sio niambie wewe.
 
...he deserve that,he was a big time dictator!

And forever we will be greatful kutokana na yeye kuwa' Dictator' Tanzania tupo hapa tulipo kwa sasa...

Hivi kuna Kiongozi aliyekuja baada ya Nyerere hata mmoja ambaye alifuata Legacy and beliefs za JKN kunufaisha umma wa Watanzania? Ni nini maana ya Dictator? maana Fasheni ya Politics za Afrika za miaka hii ni kupitisha Uchaguzi ambao unaitwa Free and Fair na baada ya hapo wanaochaguliwa katika Chaguzi za Kidemocrasia wanaitwa Madictator.

Sijasoma kitabu hicho na kwa sasa nadhani ntafika pale Mlimani nipate Nakala yake niweze soma hayo matusi...

Kitu anachofanya Shivji ni kama wafanyavyo baadhi ya Wanamuziki wa Kimarekani, kuanzisha "Beef" na kuwatusi wanamuziki waliowatangulia ambao ni Mashuhuri ili tu waweze kutoka. Kwa hilo Nakupongeza Shivji!!!
 
JKN has never been the saint we have always thought he was.He never accomplished the so called three setbacks to the developmental of this nation.Poverty,Ignorance and Disease.He only made us poor with his Ujamaa policy but one thing he never failed and for that reason we are respected worldwide is how he united the more than 100 ethnic tribes in Tanzania.We are a one great nation and peaceful.
 
Tupunguze tabia ya kutafuta wa kumlaumu.
Btw, did you originally placed this under JOKES/UTANI?

.
 
Tupunguze tabia ya kutafuta wa kumlaumu.
Btw, did you originally placed this under JOKES/UTANI?

.

Hell no saa hivi ndio nashtukia ipo humo.Niliiweka kwenye Jukwaa la Siasa nadhani hawa moderators wamei move thinking its a joke while its something damn serious.
 
I'm looking forward to get recommendation from others of whether it is wealth buying/reading this book.

.
 
I think that you bought a very serious issue Kevo, nashanga imeenda kwenye udaku.
But there are other threads that discussed the legacy of Nyerere. Labda tutumie thread hii kujadili kitabu cha Shivji.
 
I think that you bought a very serious issue Kevo, nashanga imeenda kwenye udaku.
But there are other threads that discussed the legacy of Nyerere. Labda tutumie thread hii kujadili kitabu cha Shivji.

Usijali mkuu Invincible anairudisha kwenye Jukwaa la Siasa nadhani ni an error ilifanyika.
 
Jamani kitabu cha Shivji kinapatikana wapi? tunataka na sisi tusome! Asante
 
Mwalimu alikuwa DICTATOR kwa yafuatayo:
1. Maliasili za nchi; hapana kuzichezea, kuziuza hovyo bila ridhaa ya WaTz.
2.Rushwa; hakuna kuitoa wala kuipokea iwe ni kwenye huduma, uchaguzi au vyovyote vile.
3. Ufisadi; iwe ni kwa nafasi yako au ya mjomba wako.
4. Elimu; Wote tusome hadi ukomo wa akili yetu bila mikopo au kuchangia.
5. Ukabila, Udini; Haya yakusaidie wewe mwenyewe kutambika, kuzikana na kuoa/kuolewa.
6. Matabaka; Masikini na matajiri, rangi.
7. AMANI na USALAMA wa NCHI yetu na WATU wake.
8. AJIRA; Alianzisha mashirika ya UMMA zaidi 400 hadi ya mayai na vifaranga (NAPOCO).
9.HUDUMA muhimu kwa WOTE; maji,elimu, barabara ingawa hazikuwa za lami, matibabu.
ORODHA ni ndefu; kwa tuliokuwepo kabla ya AZIMIO LA ARUSHA na bado TUPO ni mashahidi wa haya niliyoyaandika, HATUTAKUWA NA NYERERE MWINGINE.
 
You think so?!

Otherwise post yako bomba sana when reflecting our current mess.

.
 
Isaac Mruma, Caracas, Venezuela
Daily News; Saturday,July 05, 2008 @00:03

Rais Hugo Chavez wa Venezuela amezisifu sera za hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na kusema anazitumia katika kuendeleza ushirikiano miongoni mwa nchi zinazoendelea.

Chavez aliwaambia mawaziri wa habari kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NATO), kwamba utekelezaji wa sera za Mwalimu alipokuwa Mwenyekiti wa Tume ya Nchi Zinazoendelea, utawezesha nchi masikini kupata maendeleo makubwa.

Mkutano huo wa saba wa mawaziri wa habari unafanyika katika kisiwa cha Margarita, dakika 45 kutoka Caracas kwa ndege ndogo na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika anawakilisha Tanzania.

Akinukuu taarifa ya Tume ya nchi zinazoendelea iliyotolewa baada ya utafiti katika nchi hizo mwishoni mwa miaka ya 1980 na ambayo alisema aliisoma akiwa gerezani kama mfungwa wa siasa, Rais Chavez amesema mapendekezo ya kuwa na taasisi za pamoja miongoni mwa nchi masikini bado yana mantiki.

"Ripoti ya Nyerere ilitaka kuwapo na vyombo vya habari vinavyomilikiwa pamoja na nchi zinazoendelea, kuwe na benki ambazo nchi hizi zitahifadhi fedha, kuwe na mashirika ya kulinda maslahi ya nchi hizi katika soko la vitu muhimu kama mafuta. Lazima tuitekeleze taarifa hiyo sasa," alisema Chavez.

Alikosoa mfumo wa sasa ambamo nchi nyingi zinazoendelea zinahifadhi akiba za fedha za kigeni katika benki za nchi tajiri na kusema ingawaje hata Venezuela iko katika mkumbo huo, lazima jitihada zifanyike kubadili hali hii. Rais Chavez alipendekeza njia za kuifufua taarifa ya Mwalimu Nyerere kwa kuiwekea taarifa ya utekelezaji na kuanzisha upya mijadala kuhusu ushirikiano.

"Hakuna haja ya kuwa na mikutano ya kila mara kila tunapokwenda," alisema katika hotuba yake iliyochukua saa mbili na nusu. Chavez alieleza kuwa kama sehemu ya kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Nyerere, ameanzisha televisheni ya kusini, inayojulikana kama Telesur na Yutaka nchi wanachama wa NATO kuiendeleza televisheni hiyo kwa kufungua vituo vya kikanda. Waziri Mkuchika leo atahutubia mkutano huo

[I]Nafikiri Mkuchika kimoyomoyo atawasihi waige mifano ya utanndawazi,napia atawajulisha kuwa sela za Nyerere zimepitwa na wakati bongo kwakuwa hazikuwa zinaruhusu mianya ya ufisadi,na kwamba kwa kubadili sela hizi tanzania imepiga hatua kubwa na kuna watu wanitwa waheshimiwa badala ya ndugu, vijisenti badala ya hela/feza/pesa,nakwamba sela ya kupata vijisenti ndo umekuwa uti wamgongo kwa waheshimiwa wakati kwawalalauchoju jembe limeendelea kuipinda migoongo yao.[/I]
 
................mwalimu Nyerere ...unaenziwa Mbali...nyumbani Kina Kikwete Wanafanya mzaha Tena Na Mafisadi Juu Ya Kaburi Lako........

Nabii Hakubaliki Kwao??????

R.i.p Mwalimu....we Will Always Love You!!
 
Last edited by a moderator:
Hivi huyu mwandishi umakini wa habari uko wapi? Umoja wa nchi zinazoendelea si unaitwa NAM? Mimi nadhani NATO ni jeshi la kujihami la nchi za magharibi na Marekani.Lile lililomng'oa Slobodan Milosevick wa Yugoslavia ya zamani
 
Nadhani hiyo ni typing error tu.

Naam, Nabii hakubaliki kwao. Pamoja na baadhi ya viongozi wa Tanzania kutokujali umuhimu wa misingi aliyoiweka Mwalimu katika suala zima la kupatikana kwa maendeleo ya kweli kwa wananchi, ukweli wa yale aliyokuwa aliyahubiri Mwalimu utaendelea kudhihirika. Cha kushangaza ni kwamba Watanzania wakipewa majukwaa ya katika mikutano ya kimataifa wanaona soni kutaja jina la Baba wa Taifa lao! Ni aibu kwa taifa letu kwa sababu iweje viongozi ama watu wa nchi zingine wanaona umuhimu wa yale aliyosimamia Mwalimu Watanzania tusiuone? Huenda wanashangaa sana kuona hata viongozi wa nchi aliyotoka Mwalimu hawazitumii busara za uongozi wake kusisitiza yale wanayoyasema kwenye mikutano wanayohudhuria, bali wanaofanya hivyo ni watu wa nchi zingine.
 
Hivi huyu mwandishi umakini wa habari uko wapi? Umoja wa nchi zinazoendelea si unaitwa NAM? Mimi nadhani NATO ni jeshi la kujihami la nchi za magharibi na Marekani.Lile lililomng'oa Slobodan Milosevick wa Yugoslavia ya zamani

Ndio press hiyo, safari bado ndefu...Hongera Chavez kwa kuuthamini mchango wa mmoja wa wazalendo na mwana halisi wa Afrika.
 
Huwa Ni Vigumu Mtu Asiyeitakia Mema Afrika Kujua Nyerere Ni Nani...!
 
Back
Top Bottom