Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,546
- 843
Katika wiki mbili zilizopita naona kumekuwa na pilika mbalimbali toka serikalini pamoja na media Bongo za kumuenzi Ndugu JK Nyerere lakini pamoja na hayo still kuna sumu amabayo inapandikizwa ya kumfanya Mungu mtu amabaye hakukosea kitu..State Sponsored Propaganda. Mfano iweje leo hii kuna watu wanataka kujenga SANAMU za Mwalimu kila kona wakati yeye alikataa mamabo haya wakati wa uhai wake? Iweje kila jengo la Serikali linapewa majina ya Mwalimu huku maalim ABEID KARUME hapewi jina la haya uwanja wa mpira Mafia? yote ni kwa sababu Mwalimu hakutaka hizi sifa anazomwagiwa na hawa wanaompaka mafuta kwa mgongo wa chupa
Zaidi ya hayo Mwalimu hakuwa imortal na alikuwa na mapungufu yake ambayo yanaendelea kutu haunt leo hii kama yafuatayo:
1-MUUNGANO kati ya Tanganyika na bara bado una kasoro nyingi tu amabzo watawala hawataki kuyaangalia au hata kuyazungumza..vitu kama memorandum za Muungano haziko katika public domain na hii kama ilikwepo wazi tika awali basi tungejua kuwa tuna ungana nini na tukiachana tunaachana vipi after all Muungano ni contract kama ndoa amabyo ikishindaka basi mwapeana talaka tu je Mwalimu alifanya nini kuliaddress hili? najua watu watakuja na ile speech aliotoa pale Kilimanjaro hotel lakini hamuoni kama Mwalimu alilea gonjwa?
2-UDINI Hili ni moja kati ya sensitive issues amabzo wengi wanakuwa emotional kuliaddress bila kuangalia evidence zilizowasilishwa..mfano kuwa popular belief among muslims Tanzania kuwa serikali ya Mwalimu JK iliwaweka chini strategically na matokeo yake ni kuondoka kwa religious Harmony especially kati ya Waislam na Wakatoliki sasa Mwalimu kwa kweli hili alifeli kuliaddress na matokeo yake lilikuja kuwa addressed na bwana JK, Mkapa..je mnasemaje (Please hiii sio topic ya dini bali ni je Nyerere ana mkono katika hili?
3-UCHUMI Hili naamini halina upinzani mkubwa kwani tunajua kuwa UJAMAA na AZIMIO LA ARUSHA ni one of the biggest failures katika historia ya dunia na bahati mbaya Mwalimu alistuka too late kuwa hatukuwa tayari kuwa wajamaa in other words he tried to introduce SOCIALISM in a country its people were not prepared to be socialists
4-MILITARY ADVENTURES- kila kona africa Wazalendo wa Tanzania walipoteza maisha lakini je was it worth it? Je hizi nchi tulizopigania leo hii tunafaidika na nini in terms of Uchumi na mengineyo
5-UTAWALA Post Nyerere political leaders..wengi wao hawataki kubadilika kutokana na wakati..na wengine bado wako serikalini mpaka leo kwa kuteuliwa na si kwa ridhaa ya wananchi sasa hili linakuwa kikwazo kikubwa katika suala zima la democratic deficit NA wengi wao wako huko serikalini amabko wanafanya maamuzi mengi amabayo hayalengi national interests mfano mzuri ni mikataba ya uuzaji mashirika ya umma.Hii yote bado ni product ya mwalimu ambayo haitaki kupisha damu mpya
6-DEMOKRASIA- Still TZ bado mwendo wetu kuelekea katika demokrasia bado ni wa kusua sua kwa sababu hatuna independednt judiciary system na wanasiasa kutojua separation of powers. Hili halikupewa kipaumbele na mwalimu tangu mwanzo ndio maana mpaka leo tuna wapinzani amabo wao wanataka kupinga kila kitu na upande wa chama tawala tuna watu ambao wanawaona wapinzani kama maadui
7-EAST AFRICAN COMMUNITY- sidhani kama nahitaji kusema mengi haswa kuzingatia maoni ya wengi kuhusu Rwanda na Burundi kujiunga na EAC..In short Mwalimu hili nalo alifeli kwa kiasi kikubwa tangu mwanzo na wanasiasa waliomfuata ambao wanataka kutuingiza katika muungano kichwa kichwa bila kuangalia kama kuna consent ya wananchi hii yote ni kutaka kuweka Legacy on behalf of Mwalimu lakini ukweli ni kuwa kama ilikuwa ni kuweka legacy basi mwalimu angeweka Legacy wakati yuko madarakani na siyo kuyapa madaraja majina ya mwalimu
8-AFRICAN UNION- Nadhani mnajua kama mwalimu na Nkuruma walitofautiana katika hili kwa sababu kambi ya mwalimu ilitaka muungano kiduchu kiduchu wakati kambi ya Nkuruma amabyo ma Pa-Africanist wengi walikuwa wanalitaka muungano amabyo ulikuwa more radical wa pamoja hivyo still kuna deficit kwa mwalimu katika hili
9-UKABILA- hili nalo LIPO japo kuna propaganda kuwa hakuna lakini lipo na litaendelea kuwpo. Mfano angalia wizara nyeti zimejaaa makabila fulani fulani na hili lilikuwa likisemwa tulikuwa tunaambiwa kuwa watanzania hawana makabila na tumeunganishwa na lugha moja ..actually tulikuwa na muungano kabla ya mwalimu lakini divisions ziliongezeka baadaya kuja yeye ana hakufanya jitihada za kuliondoa hili..sisemi watu wasiwe na makabaila yao after all identity kwa Mwafrika ni muhimu lakini sasa kama ukabila unatumika kuwakandamiza watu basi nadhani hapo kuna mapungufu makubwa tu
Mwisho ningependa kuweka wazi kuwa pamoja na mapungufu hayo niliyataja hapo juu still Mwalimu alikuwa moja kati ya watawala wachache Afrika amabo walikuwa sio wezi lakini alizungukwa na wezi, wadini, wakabila, wabinafsi na hakuweza kuliondoa hili na matokeo yake ndio vitu kama IPTL na kadhalika lakini pia ni vizuri kama kizazi kijacho pia kikajua kuwa Mwalimu ALIKUWA NI BINADAMU kama mtu mwengine na alikuwa na mapungufu mengi tu na wala sio MUNGU MTU kama wanayomfanya sasa hivi