Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

2.
3. Maneno kwamba eti Mkapa alikuwa mr.Clean ni ujinga mtupu kama sio unafiki, ni kujaribu kukwepa ukweli kuwa Mwalimu alichemsha tena kwa makusudi kwa manufaa yake binafsi, hakuna kiongozi yoyote wa wakati ule aliyekuwa hajui tabia za Mkapa, Mwalimu alichemsha lakini kwa ajili ya manufaa yake, wananchi ndio hasa tuliompa hiyo nafasi, na mpaka leo bado hatujaamka,
Kweli kabisa maana kura ya mwalimu peke yake isingemuweka mkapa ikulu!
Asante
Hollo
 
mwalimu nyerere hakuwa Mungu, na hata mtikila aliwahi kutamka hilo, kwa hiyo kufanya makosa alifanya kama binadamu wengine, pia kuna mambo aliwahi kufanya yakawa chukizo mbele ya mwenyezi Mungu, mnakumbuka kuwa aliwahakikishia waliohudhuria ile birth day yake pale diamond jublee, 1997 kuwa alikuwa anakula vizuri, na kuwa alikuwa ana uhakika wa kuishi hata miaka 100. tena akasema kuwa alikuwa na uhakika wa kuona rais ambaye angekuja kumrithi mkapa, yaani angekwenda mpaka nyakati hizi za kikwete. watu wakamwambia mwalimu hapo umeteleza, lakini wapambe wake waaanza kula ugali wa mtama(chakula cha mwalimu), eti ili waishi maisha marefu, ulikuwa ni april 1997, mwishoni mwa 1997 tayari leukemia ikawa imethibitishwa na ahadi yake ya kuishi kwingi ikawa imekwenda na maji.

lakini mwalimu, alikuwa ni mtu anayekubali makosa, kwa kipindi cha kwanza tu alishagundua makosa ya mkapa

mfano alipinga wazi wazi kuuzwa kwa benki ya NBC, hatujui kama angekuwawepo mpaka sasa angepinga mangapi.

mkapa alikuwa ni mwanafunzi mnafiki wa mwalimu. ni wale wanafunzi wanaokuwa wanafiki wa ajabu. wawapo darasani na mbele ya mwalimu hushtaki wengine na kujipendekeza kwa mwalimu, lakini wawapo nje ya darasa ni wale wavuta bangi wakuu.

ni unafiki wa mkapa uliomfunika mwalimu asijue kuwa huyu alikuwa chui ndani ya ngozi ya mwanakondoo. ni yeye aliyemfuata mwalimu usiku kumtonya kuwa akina njelu kasaka na wenzake walikuwa wanapeleka hoja ya serikali tatu bungeni. na nyie aliyehariri kwa siri kitabu cha mwalimu UONGOZI WETU NA HATIMA YA TAIFA LETU.

mrema ni tofauti kidogo, ni mwanasiasa asiye mnafiki. asiye weza kuficha hasira yake(mfano : nikichaguliwa kuwa rais ccm watakunywa maji na karai), asiyeweza kufucha furaha yake hata kama kwa kufanya hivyo kutamfanya awe kituko, mfano, alifurahia wazi wazi na kutamka wazi wazi kuwa, yule mbunge wa mchinga mudhiri m. mudhihir ambaye alikatika mkono kwa ajali muda mfupi, baada ya kumshambulia zito kabwe bungeni , alipata adhabu ya mwenyezi mungu.
mrema pia hawezi kuficha hudhuni yake, akiugua kisukari anasikitika wazi wazi. sifa hizi zilitosha kumpa signal mwalimu na kumwelewa kirahisi kuliko mkapa
 
mwalimu nyerere hakuwa Mungu, na hata mtikila aliwahi kutamka hilo, kwa hiyo kufanya makosa alifanya kama binadamu wengine,

Hakuna aliyesema alikuwa Mungu, au alikuwa shetani, au hakuwa binadamu. Swali wala halina utata: Alichemka?

Hatu debate sababu zilizofanya achemke, na hatusemi yeye ni shetani kwa kuchemka, au Nyerere hakutakiwa kuchemka.

Alichemka au hakuchemka? Nadhani unasema alichemka, sio ndio?
 
Jamani leo usiku nlitafakari jambo kwa kina nikaona nije kuwashirikisha hapa,tumekua tukimtuhumu na hata KUMZOMEA huko mtaani Rais wetu mstaafu Mr. Clean-Mkapa (kutoka kuleee Lupaso) lakini naona tuangalie kiini cha yeye kuingia madarakani!!
Je twakumbuka kuwa BABA WA TAIFA aliamua kurudi mjini toka kule shambani kwake Butiama baada ya kuona mtoto wa kichagga ngunguli Augustine Lyatonga Mrema anaichukua nchi?
Nani kweli alikua ameisha ichachafya CCM mpaka pale MWENYEHERI,BABA WA TAIFA,MWALIMU, DR.NYERERE alipoamua kuzunguka na mgombea asiyeuzika Mhe. Mkapa mpaka wakahakikisha ushindi wa KISHINDO tehe tehe!!
Sasa je wanazuoni wenzangu hatuoni kuwa Nyerere alichangia kumwingiza Mhe.Mkapa madarakani akitumia ushawishi mkubwa alionao yeye kama BABA WA TAIFA hili?
Na wasi wasi kua hata kifo chake kilikuja baada ya kufanya kazi nzito mwaka 1995 kiasi kwamba akaishiwa nguvu akaugua,akafariki!!!!!
BY MWENDE JONAS

Hawa Ndio wakufungiwa.....
Ok!!Nafikiri hii ni kwasababu Mzee wetu JK Nyerere alifariki!!
 
Nyerere hakuchemka, kuchemka ni kufanya kosa kwa makusudi. yeye hakufanya kwa makusudi, bali alifanya lile ambalo alidhani ni sahihi kwa taifa lake. aliyechemka ni mkapa kwa kuwa aliendekeza unafiki hata baada ya kukabidhiwa kiti cha enzi
 
Mnamsikia huyu mtu anavyo chemka?
 
Nyerere alifikia Mpaka kumrudisha Mama Anna (ambaye alikuwa amechoka na visa vya Mkapa na alikuwa anataka talaka) kwenye fikira za kuendeleza ndoa ili tu Mkapa awe hana doa la ndoa na awe presentable kwa wananchi.

Bila ya races za urais 1995 na Nyerere kuingilia probably Mkapa na Mama Anna wasingekuwa pamoja.

Hivi kama mtu anaweza kwenda kumbeba mtu mlevi arrogant ambaye ndoa yake mwenyewe ilikuwa inamshinda anaweza kusema kuwa hakujua kuwa Mkapa alikuwa ana character flaws?
 
makosa ya mkapa ni ya mkapa, yanaongezeka mengine ya kuvunja uaminifu na dhamana alioonyeshwa na baba wa taifa.
sio namtetea nyerere.
Mkapa was over 18 then so quite responsible for all his actions.
Nyerere aliwapa dhamana watz wengi tu na wakamuangusha, wachache walikuwa na nae hadi mwisho.
Wengi walikuwa wanafiki na ndio tunawaona mafisadi wengi tu walikuwa watu wazuri sana siku zile, japo wengine walishindwa kujificha.
Mfano Lowasa, alikataliwa na nyerere, mbona baadaye tulimkubali?
 
Kwanza, mpaka hapo alipokuwa anampendekeza Mkapa alikuwa poa kabisa. Mkapa alibadilika second term ndiyo ushetani wa hela ukamuingia

Pili, Kubadilika kwa Mkapa ilikuwa nje ya control ya Nyerere.

Tatu, katika wagombea wa 1995 ndani ya CCM, Mkapa was the best choice and was the least devil

Nne, hata leo, kwa CCM Mkapa is far better than the current ruling cligue members. In fact, mimi ukiniambia nichague kati ya Mkapa na JK, nitamchagua Mkapa kwa kuweka tick nyingi sana.

My conclusion: Kwa kuzingatia kwamba ilikuwa lazima achague/apendekeza mgombea kutoka CCM na raia wa Tanzania aliyepo Tanzania, Nyerere hakuchemka hata kidogo- he was more tha right kumsukumiza Mkapa kwenye urais!
 
Nyerere alifikia Mpaka kumrudisha Mama Anna (ambaye alikuwa amechoka na visa vya Mkapa na alikuwa anataka talaka) kwenye fikira za kuendeleza ndoa ili tu Mkapa awe hana doa la ndoa na awe presentable kwa wananchi.

Bila ya races za urais 1995 na Nyerere kuingilia probably Mkapa na Mama Anna wasingekuwa pamoja.

Hivi kama mtu anaweza kwenda kumbeba mtu mlevi arrogant ambaye ndoa yake mwenyewe ilikuwa inamshinda anaweza kusema kuwa hakujua kuwa Mkapa alikuwa ana character flaws?

Labda alikua anataka Talaka wakati huo kwasababu Mkapa ali kua sio Fisadi!! Hakua ana kidhi mahitaji ya Mama Anna!!...
 
Mimi nasubiri passionate defence (of Nyerere, of course) ya Mwanakijiji tu....wengine wote mnaboa.....
 
Mimi nasubiri passionate defence (of Nyerere, of course) ya Mwanakijiji tu....wengine wote mnaboa.....
BASI ANZISHA THREAD MCHANGIE NYIE WAWILI TU....!
(habari yako/shkamoo...... nakusalimia ili jibu utakalotoa ni-jaji hiyo lugha yako hapo juu)
 
in 20/20 vitu vingi kweli tusingevifanya

- Tusingepata Uhuru 1961 tungekubali kutawaliwa kwa muda kidogo angalau hadi 1980
- Tusingeungana na Zanzibar
- Tusingeanzisha siasa za kutofungamana na upande wowote
- Tusingetangaza Azimio la Arusha
- Tusingepigana vita na Amini
- Tusingerudisha mfumo wa vyama vingi
- Nyerere angejiuzulu mapema zaidi kama 1971 hivi
- Tusingepinga utawala dhalimu wa makaburu
- Mwingi asingekuwa Rais
- Warioba asingekuwa Waziri Mkuu
- Salimu asingekuwa Waziri Mkuu
- Msuya asingekuwa Waziri Mkuu
- Malecela asingekuwa Waziri Mkuu
- Sumaye asingekuwa Waziri Mkuu
- Tusingefanya hivi na vile... n.k

Hivyo in hindsight naamini kuna mambo mengi yasingefanyika na kuna watu ambao wasingepata nafasi ya kushika madaraka kabisa... yote hayo ni rahisi kuyahukumu in 20/20.... bahati mbaya even God can not change the past!

Swali: Ni nani kiongozi ambaye tunaweza kumpata leo hii ambaye kwa asilimia 50% tunajua kuwa hatobadilika? Na kiongozi huyo ni yupi ambaye atamfurahisha kila mtu kwa asilimia 100? Nyerere alifariki 1999 na mwaka 2000 Mkapa alichaguliwa tena tuendelee kumlaumu Nyerere? Kuna watu ambao pia wamejaribu kumbebesha Nyerere mzigo wa Kikwete na sitoshangaa akija Rais Mpya Slaa au Seif na wenyewe wakaboronga huko mbeleni watetezi wa 20/20 watatuambia "Ni Nyerere ndiye aliyetufanya tuwachague".

Naomba yeyote mwenye uhakika kuwa kuna kiongozi ambaye tunaweza kumuaminisha Taifa letu na ya kwamba hatoharibu au hatofanya jambo lolote kwa maslahi yake au ya watu wa karibu yake na tukamuamini hivyo kwa asilimia 100. Nionesheni na miye nitaanza kumpigia debe!!! Mmoja tu.
 
Salim Ahmed Salim.

Comment..........
 
Naomba kutofautiana na wale wanaosema kwamba Mwalimu alimtaka Mkapa kwa manufaa yake mwenyewe (Mwalimu). Mwalimu hakuhitaji lolote kutoka kwa Mkapa zaidi ya kutaka nchi ipate kiongozi safi atakayeiongoza nchi bila ubinafsi kama alivyofanya yeye Mwalimu katika kipindi chote cha uongozi wake. Kama yapo ambayo Mwalimu alishindwa kuyafanya katika kipindi chake hayakutokana na ubinafsi wake. Kama Mkapa hakufanya vizuri kama wananchi walivyotarajia kutokana na 'kubebwa' na Mwalimu katika uchaguzi ule, siamini kwamba hilo ni kosa la Mwalimu. Kama walivyosema wengine humu Mwalimu aliamua kumbeba Mkapa kwa sababu ya matatizo yaliyokuwa yamejitokeza ndani ya CCM wakati huo. Mkapa hakuwa na kundi maalum ndani ya CCM ndio maana zilikuwepo kelele za kusema kwamba Mkapa hauziki kwa wananchi, hajulikani sana,.... itakuwa vigumu kwa mgombea CCM kupata ushindi iwapo Mgombea wa chama hicho atakuwa Mkapa.

Ninachopenda kusisitiza ni kwamba, katika uongozi wake wote Mwalimu alikuwa halali usingizi mzuri kwa kuwaza matatizo ya wananchi. Wote waliomfahamu Mwalimu vyema na waliofanya naye kazi kama ni wakweli watalithibitisha hili. Alijitahidi kwa kadri ya uwezo wake kama binadamu kuingoza nchi si kwa manufaa yake wala ya familia yake na hili nadhani hata wasiokubali juhudi zake, hakuna anayeweza kulipinga. Kwa hiyo tunapomuhukumu, tuzingatie kwamba ni vigumu mno katika nchi zetu hizi masikini, kupata kiongozi ambaye kwa dhati kabisa anaweza akaweka maslahi yake pembeni na kujali yale ya wananchi anaowaongoza, kwa asilimia mia kwa mia. Ndio maana hata hivi sasa tumo humu tunajaribu kutafuta dawa kwa ajili mustakabali wa nchi yetu kutokana na ubinafsi uliokithiri walionao baadhi ya viongozi wetu, uliozaa ufisadi na madudu mengine yanayokwamisha maendeleo ya wananchi.
 
Bibi Ntilie... asante kwa hilo... leo hii tuna viongozi siyo wanalala bali wanalala huku wanatembea!
 
Unajua yanayo mkuta Mkapa? ni kwa sababu alimgeuka baba/godfather wake Jkambarage! Na kwa hili Mungu anamlipa hapa hapa duniani, Nyerere hakuchemka hata, ni mwenza na swahiba wa mwenza wake walo mfundisha mkapa wizi na ufisadi! hakuwa hivo, na ndo maana kabla hajachaguliwa hakuwa na kashfa kubwa kama hizi.

Ila bahati yake mbaya, wizi wa kujifunzia ukubwani ndo ka kwapua bila hata kunawa sasa yanamkuta!
 
Back
Top Bottom