Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

you be damned you can't say that to a deceased person

Expecially Mwalimu

Na ukome!

Nafikiri ni haki na ni kweli kuwa kwa ajili ya uchambuzi wa hoja ni kuangalia pande mbili zote kwa pamoja na kutoa hatimaye maoni.

Alifanya mema mengi amabayo si sahihi sana kuya ponda kama vile hakuna ubora wa msingi alioufanya. Ni haki pia kuangalia wapi palikuwa na mapungufu..na kuyalinganisha na mambo muhimu unayofikiri aliyafanya na kisha kutoa maoni yako unafikiri mambo yangepelekwa.

Kuja hapa na kusqush out all what Mwalimu did..and to the extent ya ku_mwish angekuwa hell etc! I dont thint if that is totaly wise!

Kufikiri serously kuwa Nyerere hakujali ubinaadamu na utu wake na wa Watanzania kwa moyo wake wote si haki. Swali wapi alikiuka Utu na ubinaadamu wa Taifa Hili kama inavyofanyika kwa viogozi wengi leo?

Kufikiri alifanya yote aliyofanya kwa ajili ya ubinafsi na kujiangalia yeye mwnyewe kama viogozi wengi wa sasa..that dosnt sound at all! Wapi haswa alifanya na kwa namna gani?

Kufikiri hakutekeleza kwa dhati kabisa dhana ya kumtakia kila Mtanzania kumiliki uchumi kwa kutumia rasilimali ya ARDHI kama shina pekee wakati ule wa mwanzo kabisa wa kupata uhuru ni kuwa sio sahihi sana. Nani na vipi leo kila mtanzania ataweza kwa njia nyingine yeyote zaidi ya kutumia ardhi...anaweza kuchangia na kumiliki uchumi wa taifa kuanzia mjini mpaka kijijini?

Kufikiri Nyerere hakujua kwa kina Maana ya Uongozi wa dhati usio kuwa na nia ya kuutumia kama mtaji wa kujinufaisha wewe kiongozi na kuwasaliti unaowaongoza na kuwatamanisha kuwa uongozi ni rasilimali na hivyo kuuufanya kitu cha kuhonga na kukifia kukipata ni kukosea, Nyerere aliliona hilo. Kwa wakati ule ilikuwa sahihi kabisa kuja na MIIKO YA UONGOZI..ambayo leo hii kila mmoja aliyeivunja is Paying the price!

Kama una kina cha mtizamo gundua kuwa Tanzania leo inachipua upya kama mbegu aliyopanda Nyerere. Ni kama kila ambachohakikueleweka wakati wake sasa kinaeleweka na WATU ...NGUVU YA UTU wa Kitanzania umepevuka na kuchipua kuhitaji Muongozo wote alioufundisha Nyrere!

Kilio Chochote cha wanachi kinachoandikwa magazetini, kujadiliwa bungeni...kinacholiliwa kwenye kila maadmano, migomo mbalimbali..nk..ni KILIO CHA UTEKELEZAJI FALSAFA YA NYERERE KWA VITENDO!

And you know What?

NGUVU YA UTU WA WATU WAKITANZANIA KATIKA MAONO YA NYRERE...very soon! ITASHINDA!!!HAKUNA WA KUZUIA! Presure is too huge to be blocked, mbegu iliyopandwa ardhini imevunja ganda la nje inaisukuma ardhi na itachipua tu! Nani haoni hilo?
SUBIRI NA UTAONA!
 
Nchi hii inauzwa kipande kimoja baada ya kingine wakati nasi tupo hapa hapa. Kuna siku niliwahi kusikia kwamba sehemu ya hifadhi ya Serengeti imefanyiwa udalali, sasa nasikia kuna mwekezaji anatarajia kutua Uwanja wa ndege JKNyerere Int Airport. Hivi ukishafanya hivyo umebakiza nini cha maana. Imebaki Ikulu. KASI MPYAtumeiona. Bado NGUVU MPYA, lakini hatujala dona ukitupa dona tutapata NDUVU MPYA. Tatizo kwenye ari hapo utapata shida kwani hakuna mwenye nia hiyo.
 
Nyerere alienda na chama chake cha wakulima na wafanyakazi kule ahera(R.I.P mwalimu),hiki kilichobaki ni chama cha wafanyabiashara na majambazi.Hawa hawana huruma kabisa kwa walalahoi.Wako tayari hata kuua mtu wapate madaraka na wazidi kupora rasilimali.

Tulitegemea mwandishi wa mwalimu angetusaidia,kumbe ndo akatunyamazisha tuache uvivu wa kufikiria na wivu wa kijinga kuwanyanyasa wawekezaji eti wanaleta maendeleo.Akiambiwa rushwa iko sehemu fulani,utajibiwa lete ushahidi.Sasa ni maana ya vyombo vya usalama mpaka raia adaiwe kuonyesha ushahidi.

Muujiza uliobaki ni kuwaondosha waliovamia kutuongoza kumbe hawana sifa kama za kiongozi kama Mwalimu JK.
 
Jamani leo usiku nlitafakari jambo kwa kina nikaona nije kuwashirikisha hapa,tumekua tukimtuhumu na hata KUMZOMEA huko mtaani Rais wetu mstaafu Mr. Clean-Mkapa (kutoka kuleee Lupaso) lakini naona tuangalie kiini cha yeye kuingia madarakani!!
Je twakumbuka kuwa BABA WA TAIFA aliamua kurudi mjini toka kule shambani kwake Butiama baada ya kuona mtoto wa kichagga ngunguli Augustine Lyatonga Mrema anaichukua nchi?
Nani kweli alikua ameisha ichachafya CCM mpaka pale MWENYEHERI,BABA WA TAIFA,MWALIMU, DR.NYERERE alipoamua kuzunguka na mgombea asiyeuzika Mhe. Mkapa mpaka wakahakikisha ushindi wa KISHINDO tehe tehe!!
Sasa je wanazuoni wenzangu hatuoni kuwa Nyerere alichangia kumwingiza Mhe.Mkapa madarakani akitumia ushawishi mkubwa alionao yeye kama BABA WA TAIFA hili?
Na wasi wasi kua hata kifo chake kilikuja baada ya kufanya kazi nzito mwaka 1995 kiasi kwamba akaishiwa nguvu akaugua,akafariki!!!!!
BY MWENDE JONAS
 
Ilikuwa ni LAZIMA kwa mujibu wa Katiba yetu tuwe na Rais mwingine baada ya Mzee Mwinyi kuwa amemaliza ngwe yake. Wakati huo (1995) CCM ilikuwa imevurugika kidogo na akina Mzee Cigwiyemisi na Kolimba walikuwa wameng'olewa KIAINA kwa juhudi binafsi za Mwalimu. Wakachukua fomu za kugombea Urais watu zaidi ya 15 na Mwalimu akawa ametaja SIFA za Rais tuliyekuwa tukimhitaji wakati ule. Mkapa hatimaye akaonekana ndiye alistahili kuchukuwa nafasi ile na wengi wengine mbali na Mwalimu tulidhani hivyo. Mkapa alikuwa hajachafuka na hakuwa na MASWAHIBA wala MAKUNDI ndani na nje ya CCM. Akawa hajulikani kwa wengi na hivyo Mwalimu ikabidi amsaidie sana kwenye kampeni akisaidiwa na watu wengi tu wasafi kama akina Waryoba, Jenerali, Kaduma,...
Kilichokuja kumbadili Mkapa nadhani ni baada ya Mwalimu kufariki na mchango binafsi wa FAMILIA yake kama anavyoteseka Mugabe sasa hivi. Mengine yatabaki kuwa ni historia.
 
Mwanakijiji,

Unakubali kwamba Nyerere alichemka hapa au?

Nimeona umebariki idea ya kwamba hakuna utata kwamba alichemka.

Kama unajali, naomba ueleze hapo kidogo.
 
Actual alichemka sana hata sasa hivi matatizo tunayoyapata na tutakayoendelea kuyapata yalitokana na uhamuzi wake usiokuwa na busara wa kumpigia kampeni Mkapa.

Sasa hivi tungelikuwa kwenye optimazations ambapo hata Nyatonga angeingia akaingia tena mwingine tofauti, tungelikuwa tumevunja mtandao na misululu ya watu waliojipanga kutoka katika vyanzo vya uhujumu uchumi.
 
Mwalimu akawa ametaja SIFA za Rais tuliyekuwa tukimhitaji wakati ule. Mkapa hatimaye akaonekana ndiye alistahili kuchukuwa nafasi ile na wengi wengine mbali na Mwalimu tulidhani hivyo.

Kilichokuja kumbadili Mkapa nadhani ni baada ya Mwalimu kufariki na mchango binafsi wa FAMILIA yake


Nami pia naamini mkapa alikuja kubadilika (sidhani kama alikuwa kaficha makucha yake). Mkapa alikuwa na 'both power and authority'. Angeweza kutuletea maendeleo makubwa Watanzania, kama Nyerere alivyotarajia, angetumia vipawa vyake hivyo alivyokuwa navyo. Kuna mchango wa familia na ulevi madaraka kama walivyo viongozi wengi wa Africa. Kwa maoni yangu sidhani kama Nyerere alichemka, bali watanzania ndio tulichemka (general public kwa woga maana tulielezwa--Netgroup, Madini etc) na wale waliokuwa na nafasi kunufaika na mfumo huo wa kujichotea fedha za umma.
 
Nyerere hajachemka Wananchi ndo walichemka!kwani Nyerere pamoja na ushawishi wake kwa nini na wananchi walimchagua!Heri yangu mimi sikupiga kura!
 
Mwalimu hakufanya makosa kwani wakati hule Mr clean alikuwa Mr clean kweli wizi kajifunza ukubwani ndo maana anaiba kama mlafi kila kinachopita mbele yake lazima apige panga.
 
Jamani leo usiku nlitafakari jambo kwa kina nikaona nije kuwashirikisha hapa,tumekua tukimtuhumu na hata KUMZOMEA huko mtaani Rais wetu mstaafu Mr. Clean-Mkapa (kutoka kuleee Lupaso) lakini naona tuangalie kiini cha yeye kuingia madarakani!!
Je twakumbuka kuwa BABA WA TAIFA aliamua kurudi mjini toka kule shambani kwake Butiama baada ya kuona mtoto wa kichagga ngunguli Augustine Lyatonga Mrema anaichukua nchi?
Nani kweli alikua ameisha ichachafya CCM mpaka pale MWENYEHERI,BABA WA TAIFA,MWALIMU, DR.NYERERE alipoamua kuzunguka na mgombea asiyeuzika Mhe. Mkapa mpaka wakahakikisha ushindi wa KISHINDO tehe tehe!!
Sasa je wanazuoni wenzangu hatuoni kuwa Nyerere alichangia kumwingiza Mhe.Mkapa madarakani akitumia ushawishi mkubwa alionao yeye kama BABA WA TAIFA hili?
Na wasi wasi kua hata kifo chake kilikuja baada ya kufanya kazi nzito mwaka 1995 kiasi kwamba akaishiwa nguvu akaugua,akafariki!!!!!
BY MWENDE JONAS


Mwacheni mzee wa watu apumzike, amefanya mengi mazuri kwa taifa hili.ukijaribu kumpaka mfu madoa ambayo hasitahili yatakurudia mwenyewe
 
Taifa Stars ilipoifunga Burkina Faso kwao,kila mtu alisema kuwa kocha tunae.Ilipotoa draw na Senegal Mwanza,ndio kabisa tukaona kuwa kombe la dunia tunaenda,wacha hio AFCON! Hapa juzi ilipochemsha mechi mbili za mwanzo wengi walisema kocha hafai,wengine kama mimi tulisema tatizo sio kocha ni wachezaji.Na hilo likaja kudhihirika kwenye mechi mbili vs Cameroon.Kocha haingii katika akili ya mchezaji,anamsoma kutokana na bidii yake ya mazoezi mentality yake na character pia.Lakini mchezaji anapovuka ule mstari na kuingia uwanjani,ni yeye na Mungu wake.Mwalimu ndivyo alivyoona kwa Mkapa
 
Kwa nini yeye ndio alikuwa anatuteulia wagombea kila wakati?

And he never got them right. Na hakukoma.
 
Hii thread ni ya kipuuzi! Kama kweli mnajua siasa ya Tanzania, Mkapa was Nyerere's student. Mkapa hakuwa na known "political" scandal kabla ya kuingia Ikulu. Nyerere kwa kutumia kigezo hicho na baada ya kuona kuwa ukimya wake mwaka 1985 ulitaka kuiua nchi katika mikono ya mzee ruksa, aliamua kusimama kidete ili mtu mchafu mwingine kama kikwete au Lyatonga wasiingie madarakani. Ninajua kuwa wakati anaaga dunia alishaona mabadiliko ya Mkapa na alikuwa nahuzunishwa sana na matamshi na vitendo vyake. Sasa hapa wa kumlaumu siyo Nyerere, ni yeye mwenyewe Ben na ubaradhuli wake.
 
Taifa Stars ilipoifunga Burkina Faso kwao,kila mtu alisema kuwa kocha tunae.Ilipotoa draw na Senegal Mwanza,ndio kabisa tukaona kuwa kombe la dunia tunaenda,wacha hio AFCON! Hapa juzi ilipochemsha mechi mbili za mwanzo wengi walisema kocha hafai,wengine kama mimi tulisema tatizo sio kocha ni wachezaji.Na hilo likaja kudhihirika kwenye mechi mbili vs Cameroon.Kocha haingii katika akili ya mchezaji,anamsoma kutokana na bidii yake ya mazoezi mentality yake na character pia.Lakini mchezaji anapovuka ule mstari na kuingia uwanjani,ni yeye na Mungu wake.Mwalimu ndivyo alivyoona kwa Mkapa

Asante kwa ufafanuzi wako
 
Pamoja Na Yote Huyu Mkapa Ndio Alietuzalia Jk Uongozini,mwanzo Tukawa Tunasema Taifa Limepata Mtu Atakae Likomboa,maisha Bora Kwa Kila Mtanzania!!
Na Kura Tukampa Tena Nyingi Tuuu!!lakini Sa Ivi Kimebaki Kilio,muda Unaenda Hatuoni Mabadiliko Ya Kweli Zaidi Ya Kulindana Na Hata Kuogopana.hii Yote Ni Kutoka Chama Chetu Cha Mapinduzi,je Si Sahihi Tukajaribu Mbadala Wa Chama?mnaonaje Ccm Hii Hii Ikawa Mpinzani Hapo Baadae?nchi Hii Ni Kubwa Iliyoneemeka Lakini Bado Tunang'ang'ania Chama Kilekile Na Watu Wale Wale Je Si Upofu Huo?
 
Naomba kusema kuwa ifike mahali wananchi na sisi tukubali kubeba mzigo wetu katika hili la matatizo ya taifa letu, lakini hatuwezi kukwepa ishu iliyopo mbele yetu kwa visingizio vya kitoto, ni lazima kukata ishu:-

1. Mwalimu alichemsha big time kumchagua Mkapa kuwa rais wetu, period! Kwa sababu records zipo very clear kuwa Mkapa alipokuwa Elimu ya Juu, alihusika sana na rushwa na maovu, against wananchi Mwalimu alijua haya kwa sababu aliwezaje kujua ya Lowassa, aliyekuwa waziri kama Mkapa na katika serikali moja ya Mwinyi? Waliokuwa wanampa habari za Lowassa, pia walimpa na habari za Mkapa, lakini kwa makusudi akaamua kuangalia upande mwingine, kwa sababu alimtaka Mkapa kwa manufaa yake binafsi kwanza, ambayo Mwinyi na kundi lake walikuwa wameanza kuyakata.

2. Wananchi ndio hasa tunaotakliwa kubeba hii lawama kwa sababu Mwalimu alituchagulia Mwinyi, tukajionea madudu, lakini tukamruhusu tena kuja kutuchagulia Mkapa, not only that pia akaamuru kuwa mkapa akimaliza amuachie Kikwete na here we are, sasa makelele ya nini tena kumbughudhi Mwalimu aliyetangulia kwenye haki tayari? Kwani Mwalimu alikuwepo kwenye uchaguzi wa Kikwete?

3. Maneno kwamba eti Mkapa alikuwa mr.Clean ni ujinga mtupu kama sio unafiki, ni kujaribu kukwepa ukweli kuwa Mwalimu alichemsha tena kwa makusudi kwa manufaa yake binafsi, hakuna kiongozi yoyote wa wakati ule aliyekuwa hajui tabia za Mkapa, kwa nini kila alipogombea ujumbe wa NEC na CC wajumbe walimgomea Mwalimu kata kata, Mwalimu alijaribu kila mbinu lakini haikuwezekana mpaka Mwalimu mwisho akaamua kuwalazimisha UV-CCM kumpa ubunge wa huko, nafasi ambayo ninakumbuka wao UV-CCM walitaka kumpa Mpigaji Mziki wao Mkulu Wangu Hemedi Maneti(RIP), akalazimishwa kukaa pembeni na kumuachia Mkapa,

Wa-Tanzania, tufike mahali tujifunze kuuangalia ukweli wa taifa letu, kwa macho mawili hatuwezi kutatua anything kama bado tunakwepa ukweli tena wa wazi, na sasa tunakubali kuhamishia huu ujinga mpaka kwa watoto wetu wa kukwepa ukweli na kujaribu kulaumu wasiohusika, Mwalimu alichemsha lakini kwa ajili ya manufaa yake, wananchi ndio hasa tuliompa hiyo nafasi, na mpaka leo bado hatujaamka,

Sasa tuamke ili tulikomboe taifa letu! Tukubali ukweli tuufanyie kazi na hatuweiz kuendelea kuangalia nyuma!
 
Back
Top Bottom