Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Jokakuu,

Shukran kubwa mkuu umerudia hoja ambayo kwa miaka karibu mitano nimekuwa nikijibu na wala sintapotosha maelezo yangu ya awali..na pengine nitajaribu kutumia mtindo wa Mzee mwanakijiji ambaye kakupa maelezo yake kulingana na ufahamu wake..
sasabasi ngoja nianze na kipengele cha kwanza, kumbuka tu mimi sifanyi theories ambazo zinabuniwa hapa kutafuta sababu ya kunyoosha kidole bali ni reality na hali halisi iliyotokea..

kiwanda kikijengwa halafu hata kisizalishe kinaweza kuwa ni hasara kuliko kisingejengwa kabisa.
..
Mkuu unachoshindwa kuelewa ni kwamba Nyerere alitawala kwa miaka 23, hivyo huwezi pima maisha ya viwanda nchini kwa kutazama miaka minne 4 ya mwisho..
Sikubaliani na usemi wa wengi kwamba viwanda hivi vilijengwa tukiwa hatuna wasomi, mkuu hili sio kweli kwa sababu Nyerere alihakikisha vijana wanakwenda soma ndani na nje kupata ujuzi ktk kila kiwanda alichojenga. Hawa wazee wetu, kaka zetu, wajomba zetu wengi leo hii watakwambia alisoma Israel, Urusi, Cuba, Uturuki, Uk, Marekani, France na hata Canada tena vyuo vya hali ya juu sana na wote hawa waulize vizuri upate kujua walisomea kitu gani... utakuta specific kwa kile Mwalimu alichotaka kujenga nchini.
Kifupi hata wapishi wa TRC ama Hotel zetu wote walisoma nje..hata watandika vitanda walisoma nje..Madaktari wakubwa wote leo hii Bongo wamesomeshwa na Mwalimu, hata Ma lawyer wazuri ni wale wa mwalimu kwa sababu leo hii hakuna mtu binafsi kama sio fisadi anaweza kulipia ada ya shule alizotupeleka mwalimu.. hii ni fact sifanyi kuzusha!...
The downside ya hoja yako kwa hawa wasomi wetu ni kwamba hawahawa aliyewaamini ndio leo wamekuwa mafisadi!..sasa kama kosa ni kuwapa elimu hapo nipo nawe hata hivyo yeye hakuwa mtume kuyajua yote haya..
Mimi naamini kabisa kwamba kwa asilimia ya wasomi wetu Nyerere alipeleka wanafunzi nje zaidi ya kiongozi yeyote ktk Utawala uliomfuatia, leo hii vijana wengi wanakwenda nje kusomea lugha Kiingereza wengine hizo Open Univesiuty na College mabzo hata UK ama USA kwenyewe hazifahamiki.. zaidi ya kuitwa community college utafikiri za misaada ya IMF, Tofauti kabisa na wakati wa mwalimu na pengine naweza kusema ndio viongozi wetu wa leo hii ktk nafasi zote kubwa.

hebu tueleze sababu zilizopelekea viwanda hivi kujengwa na kufa mara moja. je, maamuzi gani ya serikali ya Baba wa Taifa yalisababisha hilo?
Nitarudia kusema kwamba viwanda vyetu na mashirika havikufa hili nalipinga mpaka kesho kwa sababu Mwinyi anaingia madarakani mimi niko Bongo..viwanda vya nguo vyote toka Urafiki hadi Mutex..vilikuwa vikifanya kazi tena jamaa yangu marehemu sasa (Ismail) alipatia Utajiri wake pale Mwanza kwa kuuza kanga za Mwatex na Mutex...
Viwanda vyote toka Urafiki, UFI, Bandari, Tenesco - tulicheza Mbowe hadi asubuhi hakuna kukatiwa umeme, hizo Posta, Bima, ATC zote zilikuwepo na zikifanya kazi vizuri sana na vijana wote wa mjini ndiko tulifanya kazi.
- Tatizo kubwa la mfumo wa Ujamaa ilikuwa miradi yote hii ni kwa sababu ya matumizi ya ndani zaidi ya kusafirisha nje kwa sababu SIASA za wakati wa Mwalimu ziliambatana na uchumi wa nchi..
Nitarudia kusema kwamba wakati wa Nyerere hapakuwepo na hii kitu UTANDAWAZI!.. inaopnyesha watu wengi mnasahau hili kwamba Tanzania kwa kujikita Na nchi za mashariki Kisiasa moja kwa moja tulitangaza kufungwa kwa milango mikubwa ya kibiashara...
Pamoja na makosa yote ya Mugabe, nitasema hakuna kiongozi yeyote anayeweza kucheza Kiuchumi Zimbabwe bila kuwepo suluhu ya Kisiasa kuhusiana na ardhi za wazungu. Huko Gaza, Palestina hakuwezi kuwepo suluhu yoyote kiuchumi kama wataendelea kutoitambua Israel...
Kwa hiyo, makosa ya Nyerere makubwa yanaweza kuwa yamesababishwa na kwanza Kutaifisha mali za watu na kisha kujitangaza kuwa sisi ni Wajamaa jambo ambalo alikatazwa na kina Mtei..Hii ikiwa na maana kujitangaza tu kuwa sisi ni Wajamaa tayari alikwisha weka doa. Hivi vitu viwili ndio vimekuwa sumu ya Ubepoari na hasa nchi za magharibi kwani ukitazama nchi zote za Kijamaa ziliyafanya haya na ndio ugonvi mkubwa ulipotokea kati ya wanamapinduzi dhidi ya nchi hizi za magharibi..Tuliyaona Cuba na sasa hivi tunayaona Venezuela..
Pia kama kiwanda kinazalisha na wafanyakazi wanakitegemea kwa maisha yao hawawezi kuanza kuiba vipuri. kwa msingi huo yapo mazingira yaliyosababisha wafanyakazi wakose nidhamu kiasi hicho. sasa mazingira hayo yalisababishwa na siasa za Baba wa Taifa, au Mzee Mwinyi?

Mku unaponiuliza mimi kuhusu mazingira hayo sijui nikwambie kitu gani maanake hapa leo hii mada kibao zinambana Kikwete hali yeye kuyakuta mazingira hayo...
Nitasema hivi wizi wa vipuli umetokana na RUKSA! miaka mitano ya kwanza ya utawala wa Mwinyi hapakuwepo na wizi huo.. meaning Nyerere kisha ondoka miaka mitano ndio tuklaanza kuona vifo vya viwanda vyetu, sasa nambie huyo Mwinyi kwa zaidi ya miaka mitano alikuwa bado hawezi kurekebisha kitu?... na inakuiwaje leo tunamlaumu Kikwete ambaye yupo madarakani miaka miwili tu.
Mkuu changes zinaweza fanya na kiongozi ktk siku 100 tu kama tunavyoona huko Cuba leo hii..Na sio huyu Mwinyi aliyewapeleka waziri wa mabo ya ndani na mkuu wa majeshi kumuuliza mwalimu kwa nini anazungumza na wapinzani kina Mrema na Seif Hamad?..hadi akataka kurudisha kadi ya chama.. who else can do that!..

NB:
..kwa maoni yangu kulikuwa na siasa nyingi ktk uendeshaji wa viwanda, mashirika,na uchumi kwa ujumla.
..badala ya kushindana ktk uzalishaji mashirika yalikuwa yakishindana kwa vikundi vya ngoma, timu za mpira na netiboli, kwaya, matawi ya chama na juwata.
..pia kulikuwa na mashindano ya kudhamini shughuli za chama na serikali.

..viongozi wa chama na serikali walikuwa hawaishi kutafuta fadhila na zawadi toka kwa wakuu wa mashirika ya umma.

Mkuu hapa ndipo unapokosea, haya mashirika yangeshindana na nai katika Uzalishaji ikiwa mwenye mali ni huyo huyo?..Pili soko lipo ndani ya nchi na sio nje kutokana na masharti hayo ya standard na kadhalika ambayo yalitawaliwa sana na kutazama msimamo wa nchi kisiasa...
Miaka ya kati hadi mwisho wa 70's unajua bia yetu safari iliwahi kuibuka na gold medal kama bia bora ktk maonyesho ya bia Ujarumani?.. Mvinyo wetu wa Dodoma uliwahi kushinda vile vile lakini kutokana na siasa zetu milango ilikuwa imefungwa, zaidi tuliachiwa kidirisha cha kutuwezesha kukopa tusije kufa kwa njaa....

Matawi ya chama na Juwata yaliwaingilia Mameneja ktk kufanya maamuzi ya kitaalamu
.
Mkuu hata Ulaya Union pamoja na Taasisi za wafanyakazi huingilia kati maamuzi ya kitaalam pale kwenye haki..Kwa maoni yako basi sionmi hata haja ya kuwepo Polisi maanake nao huingilia sana maamuzi ya wataalam ktk Ufisadi na Ujambazi..maanake wakati wa Nyerere hawa wataalam walitaka kutumia sana nafasi zao hata kutoa ajira. Leo hii, mwanamke kama hatoi vitu kesho kazi hana na hana pa kwenda! huu utaalam ni utaalam gani unaohusiana na watu badala ya kazi...
Nitasema hivi, mkosa ya mwalimu ktk kazi yalihusiana na MISHAHARA..lakini sio iliyosababisha kuanguka kiuchumi ama kuanguka kwa viwanda hivi isipokuwa ulikuwa mtaratibu mbaya sana kiasi kwamba watu walikuwa wakifanya kazi masaa labda manne 4 kwa siku. Watu walikuwa wakilala kazi kila siku kusingizia magonjwa na hapakuwepo na utaratibu wa kuhakikisha Uzembe na Upuuzaji kazi utapigwa vita hadi tukajenga Utamaduni huo wa Uzembe na Upuuzi.
Wengi tunashangaa kwanini kaburu ameweza kuendesha TBL. tunasahau kwamba ameondokana na vikundi vya sanaa, timu za mpira,juwata etc etc.
Unaendelea kusahau kwamba mazingira ya biashara duniani wakati wa mwalimu na leo hii ni tofauti sana. Kisha wakati kaburu anaingia kampuni yetu ya Bia haikuwa imekufa wala imeingiza hasara isipokuwa ni kati ya asilimia 10
za mafisadi..Najua kabisa aliyelitengezeza deal hilo... labda nikupe hint (ex balozi wetu huko South).. Kwa hiyo bado unarudia pale pale kuwa hatungeweza kufanya kitu tofauti ikiwa kiwanda cha bia ni mali ya serikali...na huna Mtanzania hata mmoja aliyewekesha ktk bia kabla ya Uhuru..Jambo jingine ni kwamba leo hii kuna wanywaji bia mara tatu ya miaka ya mwalimu soko limeongezeka..hivyo demand ya bia imekuwa kubwa sana kiasi kwamba miaka ile ya mwalimu bia ilikuwa sii hivyo.. Mchagga alkitamani Mbege yake zaidi ya bia labda tu iwe baada ya chakula. Leo hii hata Gongo lina wateja kuliko wakati wowote ule hata Konyagi ambayo ilikuwa haina soko ndani wala nje pmaoja na kwamba ilikuwa ikisafirishwa nje toka enzi za mwalimu,sasa ni hadithi nyingine kabisa...hivyo basi tunarudi palepale ktk Demand na Supply. Ukiwambia Mwalimu leo Gold ni dollar 1000 kwa ounce anaweza omba arudi kutawala Tanzania...na pengine furaha na kicheko kikubwa kiasi kwamba malaika wanamshangaa kufikiria katuachia mtaji safi.

..Mameneja walikuwa hawaruhusiwi kupunguza wafanyakazi hata kama kiwanda/shirika limelemewa.
Nitarudia kusema kwamba mwalimu alitengeneza viwanda ktk stage ya kwanza ambayo ilikuwa kwanza kutosheleza matumizi yetu sisi wenyewe kabla hatujafikiria kuingia ktk soko la mashindano, hivyo ilikuwa ni kutujenga sisi zaidi kuelewa ufundi wa vitu hivi kama walivyokuwa wakifanya China. Biashara wasn't a main objective isipokuwa kuunda jeshi la kiuchumi ambapo viwanda hivyo vilikuwa kama ndio silaha. Mwanajeshi kubeba silaha sii lazima awe vitani laa anajifunza namna ya kuitumia kwanza (kama unakumbuka tulisema Muingereza alituacha sisi watupu bila elimu wala viwanda hivyo hatungeweza kuingia sokoni ghfla bin vuuu tukitegemea kuuza mali iliyotengenezwa na wanafunzi.

Sasa ukichanganya chama kushika hatamu[sera za Baba wa Taifa], under-capitalization ya mashirika yetu, utaona kwamba we were bound to fail.
..
Haya ni mawazo yako kwa sababu tayari jibu ni kwamba - Tuli fail kiuchumi...
sababu ni nyingi sana tena zinaambatana na sisi wenyewe kuwa Wazembe na Wapuuzi kama tunavyopuuza leo maswala ya Mafisadi, kesho tutakuja mnyooshea tena mkono mwalimu... Kwa mtaji huu tuta fail tena na hapo wengine tutaanza kumtafuta sijui Mkapa na FIKRA zake za UWAZI na Globolization kuwa ndio sababu ya sisi kushindwa tena...
Ukweli utabaki kwamba Baba wa Taifa alielezwa mazingira yaliyolikabili taifa, na maamuzi aliyopaswa kuchukua. alikataa ushauri ambao unaashria ungetusaidia. matokeo yake ni kuanguka kwa mashirika na uchumi wetu kwa jumla.
..kwa msingi nasema Mwalimu alifanya makosa na anastahili lawama.
Kwa hiyo leo hii tunavyo fail pamoja na kwamba tunafuata mashauri ya hao wajuzi waliomshauri mwalimu enzi hizo bado utasema nini?...ama ktk kamusi yenu mtu akisha fail hawezi tena kuamka ndio tumeshakuwa doomed!
 
Bob Mkandara,

Hawa jamaa hata leo ukiwaonyesha zao bora la wao kutembea huru na kuweza kubwabwaja hapa kwa uhuru kabisa watasahau kuwa mwasisi wa msingi wa sisi kufika hapa tulipo ni Nyerere.
 
Sikubaliani na usemi wa wengi kwamba viwanda hivi vilijengwa tukiwa hatuna wasomi, mkuu hili sio kweli kwa sababu Nyerere alihakikisha vijana wanakwenda soma ndani na nje kupata ujuzi ktk kila kiwanda alichojenga.
Hawa wazee wetu, kaka zetu, wajomba zetu wengi leo hii watakwambia alisoma Israel, Urusi, Cuba, Uturuki, Uk, Marekani, France na hata Canada tena vyuo vya hali ya juu sana na wote hawa waulize vizuri upate kujua walisomea kitu gani... utakuta specific kwa kile Mwalimu alichotaka kujenga nchini.!

Hilo swala ni kweli kabisa nakumbuka kuna jirani yetu mmoja alishawahi kupelelwa kusoma Ujerumani mashariki kusoma na aliporudi akawa yupo pale Urafiki

Nitarudia kusema kwamba viwanda vyetu na mashirika havikufa hili nalipinga mpaka kesho kwa sababu Mwinyi anaingia madarakani mimi niko Bongo..viwanda vya nguo vyote toka Urafiki hadi Mutex..vilikuwa vikifanya kazi tena jamaa yangu marehemu sasa (Ismail) alipatia Utajiri wake pale Mwanza kwa kuuza kanga za Mwatex na Mutex...

Viwanda vyote toka Urafiki, UFI, Bandari, Tenesco - tulicheza Mbowe hadi asubuhi hakuna kukatiwa umeme, hizo Posta, Bima, ATC zote zilikuwepo na zikifanya kazi vizuri sana na vijana wote wa mjini ndiko tulifanya kazi

Ni kweli kabisa mkuu nasikitika ni watendaji tu ndio waloharibu na ile ruksa alipoachia kila kitu kutoka nje viingie bila controll...angalia Kenya au India au China

Nitasema hivi, makosa ya mwalimu ktk kazi yalihusiana na MISHAHARA..lakini sio iliyosababisha kuanguka kiuchumi ama kuanguka kwa viwanda hivi isipokuwa ulikuwa utaratibu mbaya sana kiasi kwamba watu walikuwa wakifanya kazi masaa labda manne 4 kwa siku.
Watu walikuwa wakilala kazi kila siku kusingizia magonjwa na hapakuwepo na utaratibu wa kuhakikisha Uzembe na Upuuzaji kazi utapigwa vita hadi tukajenga Utamaduni huo wa Uzembe na Upuuzi.

UZEMBE NA UPUUZI NDIO NIDHAMU NA DINI YETU WABONGO PERIOD

Nitarudia kusema kwamba mwalimu alitengeneza viwanda ktk stage ya kwanza ambayo ilikuwa kwanza kutosheleza matumizi yetu sisi wenyewe kabla hatujafikiria kuingia ktk soko la mashindano, hivyo ilikuwa ni kutujenga sisi zaidi kuelewa ufundi wa vitu hivi kama walivyokuwa wakifanya China.

Biashara wasn't a main objective isipokuwa kuunda jeshi la kiuchumi ambapo viwanda hivyo vilikuwa kama ndio silaha.

Mwanajeshi kubeba silaha sii lazima awe vitani laa anajifunza namna ya kuitumia kwanza (kama unakumbuka tulisema Muingereza alituacha sisi watupu bila elimu wala viwanda hivyo hatungeweza kuingia sokoni ghfla bin vuuu tukitegemea kuuza mali iliyotengenezwa na wanafunzi.

Naunga mkono kabisa maelezo yako Mkuu Mkandara hizo ni facts and no doubt at all.

Kila mara huwa napiga kelele nikisema hizi siasa za CCM za kubebana ni product za mzee JKN. Lakini mzee JKN naweza kusema kuwa alikuwa ni MZALENDO halisi na MTANZANIA damu kuliko mtuyeyote sasa hivi, alikuwa na vision na alituwekea steel foundation.....bahati mbaya waliomfuatia nia yao ni kubomoa.
 
sasa mbona Chuo Kikuu humlaumu Nyerere? Na kule kwa Waberbeig wanaotimuliwa na DC si makosa ya Nyerere yale? Walipotimuliwa watu Bulyanhulu si Nyerere aliamuru hayo? Na ule mkataba wa Richmond ni Nyerere aliwaambia wausaini; na Chenge aliweka hela zake Jersey kwa sababu ya Nyerere. Kwa mawazo yako Balozi Mahalu alitumwa na Nyerere kuweka hela huko Monaco na Ditopile aliamuriwa na Nyerere kumlipua dereva wa daladala.

Sasa, unashauri nini ili tuondokana na hawa watu wanaofanya kila wanaloambiwa na Nyerere au kufuata mwelekeo wa Nyerere?
 
Rev,
ni nini hasa lengo lako la ku-post hiyo document ya heritage foundation?? eager to know...

YNIM,

I always try to be objective and acknowledge different opinions. Yes I am Pro-Nyerere, a Nyerereist, however I will be deceiving myself if I will hold my foot down and claim Mwalimu was an absolute perfect man and his legacy and Ideas are irrevesible!

Hii makala ni very informative. Inatoa maoni kutoka kwa mtu mwingine, ni macho mengine yanayoangalia Nchi ya Tanzania na kutoa tathmini.

Ni mawazo ya kujenga na kukosoa. Najifunza kutoka mawani ya huyu jama, ni wapi tulikosea na kwa siye wenye kusema zidumu Fikra, ikiwa tunataza kuzienzi Fikra, basi ni heri tuangalie kwa makini ni mapungufu gani tuliyoyaona sisi wenyewe na waliyoyaona wenzetu.

Does this answers your question?
 
YournameisMine,
Hee mkuu hakuna aliyepinga kwamba Nyerere hana mapungufu na hili la Kubebana tumelizungumzia siku zote kwamba limetokana na Muundo wa serikali zote za Kijamaa. Mwanatanu anachojaribu kusema hapa ni pamoja na yote mazuri na mapungufu yake lakini hayahusiani na Uzembe wetu sisi wenyewe kudondoka...
Kumbuka tu kwamba kwa ajiri ya ujenzi wa Political muscle na National security (ambalo sii jambo).. hawa jamaa walijenga Mafia na Kigamboini ndiko kulikuwa darasa na makao makuu ambako mbali na kujijenga kisiasa walijenga familia zao, wakaona wao kwa wao ama kutafutiana viwanja sehemu moja kuwa majirani kama walivyofanya China, Urusi na nchi nyingine zote za Kijamaa. Badala ya kujenga viongozi bora walijenga Watawala weusi wenye uchu kama mafisi wakisubiri mwisho wa Nyerere ama Ujamaa!

Kubomoa Mafia kama hizi ni kazi kubwa sana na hakuna hata sehemu moja ya mada hii inazungumzia tatizo hili isipokuwa mnachotafuta ni kupaka tope tuuu bila hata kuonyesha wapi tunaweza kurekebisha yaani kama vile mnakubali kuwa imeshakuwa laana na haiwezi kuepukwa.
Hapo juu nimeorodhesha vizuri mabaya ya mwalimu pamoja na kwamba yeye mwenyewe hakuwa na nia mbaya hata uundaji wa Mafia hiyo.
Imekuwa kama kama ilivyokuwa kesi ya Vito Corleone na Barzini ktk GodFather!...Vito Corleone ambaye utawala wake ulijihusisha sana biashara za mvinyo (wakati huo ukiwa haramu), lakini mara tu alipoondoka kina Barzini waliiingia katika madawa ya kulevya ambayo mzee Vito katika Uhai wake wote alikataa katakata kujiingiza ktk biashara hiyo. Likawa kosa na ndio mwanzo wa mtafaruku baina ya familia hizo mbili lakini hata hivyo hatuwezi kumshutumu Corleane kuwa karibu na watu kama Barzini ama Tataglia ama kwa nini alikataa kuingia ktk biashara ya Cocaine ambayo ilisababisha madhara mengi zaidi.
Tutawahukumu hawa jamaa kwa matendo yao na sio umoja wao kwani azma ya mwalimu kuunda Mafia hii ilikuwa kuhakikisha Uhuru wetu haurudi mikononi mwa Mkoloni mweusi.... He was very wrong!
 
30uve6s.jpg

Huu mjadala mzuri sana na ningependa sana kujadili na kutoa mawazo yangu lakini unfortunately siwezi kwa sababu kadhaa wa kadhaa...Ila najifunza mengi kwenye mijadala kama hii especially inayohusiana na waasisi wa Taifa letu.
Kudos kwa wachangiaji wote.
Weekend njema
 
Mkandara na Rev,
saaaaaaafi sana,mpo kwenye record na nimependa hicho kihitimishi chako Mkandara, "he was very wrong..."!! that's all I can say for now...shukrani nyingi na wkend njema!
thanx!!

yaani umedandia neno "he was wrong" and you missed the whole point..! try to use rational mind badala ya kureact kila kitu emotionally. Ni ushauri tu, itakusaidia sana.
 
haya nimekusikia, na response yako is very emotional. Nothing wrong with that.. I always enjoy your posting na tatizo langu nawe haliko kwenye kutokubaliana, tatizo langu liko kwenye jinsi unavyojenga hoja. Naweza kuona potential kubwa sana ndani yako only once you cross the personal and emotional barrier unapoangalia issues. Kuna wakati una michango mizuri sana Kama kwenye suala la wanafunzi.. to tell u the truth I was more than impressed.
 
Nashangaa sana sisi watanzania tunaosema Mwl alikuwa na mapungufu, kweli yeye kama binadamu yawezekana yalidhihirika, ila Mwl alijitahidi sana kukinzana na siasa za nje ili kulinda watu wake, Mwl alijitahidi kuhakikisha watu wake wanakuwa salama
 
Huu utumbo mwingine. Watu wake hawakufaidika chochote kwa yeye KUKINZANA (kukinzana - sijuhi ina maana gani) na siasa za nje. Na kama ulikuwa na maana kuwa alipinga siasa za nje, basi hilo ni kosa moja kubwa sana alilofanya.

Uchumi wa Tanzania ulijengwa na utategemea siasa za nje. Kukataa siasa za nje niku-lostisha watu tu. Na mfano mkubwa angalia Mugabe anavyotapatapa.
 
Bin Maryam,

Sasa tutaamka lini usingizini? tufanye nini turudi kwenye njia sahihi?

Rev:

Nadhani umefika wakati tuwe na viongozi watakaofanya kazi hili nchi iweze kuendelea na kuacha wachambuzi wa siasa za dunia. Nyerere ni mfano mzuri wa mchambuzi wa siasa za dunia lakini ufanisi wa kazi alikuwa hana. Na hii ndio siasa ya Tanzania ilivyo toka tumepata uhuru mpaka sasa. Huwezi kuendelea kwa maneneo.
 
"....as if its personal"!?? it is personal, I religiously hate the guy!!....it is a family affair, kuna vitu huyu babu alikosea sana. sijui mungu atam-judge vipi!!?? but I hope he's in hell right now, burning 24/7......

you be damned you can't say that to a deceased person

Expecially Mwalimu

Na ukome!
 
you be damned you can't say that to a deceased person

Expecially Mwalimu

Na ukome!

Nyerere alifanya mambo makubwa sana kwa nchi hii. Hata kama kuna mambo alikkosea. ambayo yapo kwa kweli, hakukosea kwa makusudi. Kwamba alikuwa anajua hapa nafanya hivi ili kumkomesha fulani? Hapana. Hata ugomvi wake na Kambona, ninaamini ilikuwa ni imani aliyokuwa nayo ya kujenga Taifa imara lenye amani na umoja na wala sio kwa faida yake binafsi ya mali au hali.

Hata Muungano ambao tunausherekea leo, kuna makosa kadhaa alifanya. Ni jukumu letu kuyarekebisha bila kuvunja alichoanzisha. He tried to build a strong, prosperous and agrarian nation. I am proud to be associated with his achievements and mistakes in the course of building our nation.
 
Hujambo mtoto wa Shida?
 
Bin Marium,
Nadhani umefika wakati tuwe na viongozi watakaofanya kazi hili nchi iweze kuendelea na kuacha wachambuzi wa siasa za dunia. Nyerere ni mfano mzuri wa mchambuzi wa siasa za dunia lakini ufanisi wa kazi alikuwa hana. Na hii ndio siasa ya Tanzania ilivyo toka tumepata uhuru mpaka sasa. Huwezi kuendelea kwa maneneo.

Nadhani mkuu hapa ndipo tunaposhindwa kuelewana. Tunazungumzia Nyerere na wakati wake ambao ulikuwa ni lazima uzungumzie siasa za Nje kisha uchague Upande!..nje ya hapo wewe sii mgeni wa mtu yeyote na siasa hizo ziliendana na Uchumi yaani siasa ilitangulia Uchumi...
Hivyo basi pamoja na Nyerere kuchagua Ujamaa bado tulitegemea nchi zenye mrengo sawa na wetu na wao wakatumia nafasi ile kuendeleza ukoloni wa kiuchumi...Huu ulikuwa ni wakati mpya baada ya nchi kuwa huru hivyo ktk kugawana mataifa madogo nchi kama Urusi, China, UK na Marekani ambao walikuwa ndio Super power wetu walianza kugawana nchi kwa kutumia siasa zao kama walivyogawana Utawala enzi za Ukoloni..Wewe tazama historia ya nchi zetu utakuta hawa jamaa waligawana nchi kama vile zao wamepewa na Mungu..
Tofauti na leo hii hakuna tena Siasa za pande mbili, lakini tamaa ya kushika uchumi wa nchi maskini bado imesimama pale poale na ndio maana tunaita Ukoloni mamboleo......
Hivyo bado kabisa utahitaji kutazama siasa za nje Kiuchumi na kosa la kutofanya hivyo ndilo limetuingiza hapa tulipo kuingia mikataba feki ambayo kwa sheria za kitaifa hatuwezi kuivunja...Pili, viongozi wa ndani watu kama kina Mkapa na Lowassa ni jaribio jingine ambalo lipo ktk hatua nyingine tofauti na wale machief enzi za mkoloni ama viongozi kama Nyerere waliotupatia uhuru wetu.
Siku zote ni lazima umfahamu mbaya wako!
 
Our Problem, we dont translate in action which the most intellegent person , Mwalimu nyerere said in Arusha declaration:

"Everybody wants developments but no t everyone understands and accepts the basic requirement for Development, the Basic requirement for development is hard work"

Today our contry is feeded by womens, while men sitting in Baraza and piga zoga, We Lazzy mans, The GDP of Tanzania we talking about today is what hard women have done , nad we men we wait and trade the hard work from them'Hard work start from talking Ideas and Implimenting them effectively,

Right now we Know corruption being a killer of our Economy , we have done something good so far but we need to stand beyond that , and we need to see courts action na ufirisishaji una happen,

At the same time let keep giving Mwalimu nyerere Credit for what he has seen it before and he done it before and he taught us to say it out ,

Remember 1995 press conference at Kilimanjaro hotel mwalimu said this"AFP, 14 March 1995
DAR ES SALAAM, March 14 (AFP)

- Former Tanzanian president Julius Nyerere on Tuesday accused the government of President Ali Hassan Mwinyi of corruption and violating the constitution and urged Tanzanians to vote differently in the next elections.

Addressing a gathering of local and foreign journalists at the Kilimanjaro International Hotel here, Nyerere also accused Mwinyi's administration of condoning religious differences and tribalism.

"This would not only lead to collapse of the now-sensitive 30-year-old union between the twin-islands of Zanzibar and Pemba and Tanzania mainland, but would also plunge the country into chaos," Nyerere warned and urged Tanzanians to ensure that they voted for "a president able to correct the situation and put the country on the right track."

Nyerere, who ruled Tanzania for 24 years after independence from British colonial rule in 1961, described Tanzania as a country "stinking with corruption." "Corruption in Tanzania has no bounds. Every country I visit they talk about corruption in Tanzania. Tanzania is stinking with corruption," Nyerere told journalists gathered at the Tanzania Press Club. Referring to a tax fraud in the country that recently led to aid suspension by donor countries and organisations, Nyerere declared: "This was one quality of corruption."

Lastly as we marking this holiday our aim is to mark as a revolutionary year of a war against corruption by turn the country on right direction, We can come up with the impletementation and let us work nowASANTENI
 
Mkandara:

Nyerere alitakiwa awe Prof. pale UDSM abishane na Shivji mchana kutwa lakini sio kuwa kiongozi wa kuleta mabadiliko ya nchi.

Ninachompendea Nyerere ni kuwa mkweli. Sikiliza maneno aliyomwambia ROBERT MUGABE wakati Zimbabwe inapata uhuru "You have inherited a jewel, keep it that way". Na aliyasema haya kwa sababu alivyorithi yeye aliviboronga.

Lakini nyinyi wapenzi wake mnampenda kwa vitu mwenyewe alivyoona kuwa alichemsha.
 
Our Problem, we dont translate in action which the most intellegent person , Mwalimu nyerere said in Arusha declaration:

"Everybody wants developments but no t everyone understands and accepts the basic requirement for Development, the Basic requirement for development is hard work"

Today our contry is feeded by womens, while men sitting in Baraza and piga zoga, We Lazzy mans, The GDP of Tanzania we talking about today is what hard women have done , nad we men we wait and trade the hard work from them'Hard work start from talking Ideas and Implimenting them effectively,

Right now we Know corruption being a killer of our Economy , we have done something good so far but we need to stand beyond that , and we need to see courts action na ufirisishaji una happen,

At the same time let keep giving Mwalimu nyerere Credit for what he has seen it before and he done it before and he taught us to say it out ,

Remember 1995 press conference at Kilimanjaro hotel mwalimu said this"AFP, 14 March 1995
DAR ES SALAAM, March 14 (AFP)

- Former Tanzanian president Julius Nyerere on Tuesday accused the government of President Ali Hassan Mwinyi of corruption and violating the constitution and urged Tanzanians to vote differently in the next elections.

Addressing a gathering of local and foreign journalists at the Kilimanjaro International Hotel here, Nyerere also accused Mwinyi's administration of condoning religious differences and tribalism.

"This would not only lead to collapse of the now-sensitive 30-year-old union between the twin-islands of Zanzibar and Pemba and Tanzania mainland, but would also plunge the country into chaos," Nyerere warned and urged Tanzanians to ensure that they voted for "a president able to correct the situation and put the country on the right track."

Nyerere, who ruled Tanzania for 24 years after independence from British colonial rule in 1961, described Tanzania as a country "stinking with corruption." "Corruption in Tanzania has no bounds. Every country I visit they talk about corruption in Tanzania. Tanzania is stinking with corruption," Nyerere told journalists gathered at the Tanzania Press Club. Referring to a tax fraud in the country that recently led to aid suspension by donor countries and organisations, Nyerere declared: "This was one quality of corruption."

Lastly as we marking this holiday our aim is to mark as a revolutionary year of a war against corruption by turn the country on right direction, We can come up with the impletementation and let us work nowASANTENI

Hapo sijuhi unataka kusema nini? Maana kama yeye alikuwa ni kiongozi mzuri basi wakati wa utawala wake angetoa ruhusa watu kumkosoa hadharani kama yeye alivyokuwa anafanya baada ya kuachia ngazi.

Na kibaya zaidi akatuchagulia Mkapa.
 
Back
Top Bottom