Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

I wish Lyatonga angeshinda 1995 maana mzee wa kiraracha naamini angesafisha hizi tabia za kifisadi na leo tungekuwa na true democracy na ningekuwa labda upande wa CCM mana CCM wangekuwa ni watu wenye akili
 
Mzee MwanaKijiji,

Kwa hakika Salim Ahmed Salim angelipewa nchi hii hivi sasa tusingelikuwa tunazungumzia haya ya mafisadi wasiochukuliwa hatua. Rais Kikwete angeweza sana kuliongoza Taifa hili kwa ufanisi iwapo angelizingatia yale yote aliyoyasema mwanzo wakati anapokea kijiti! Lakini, cha kusikitisha ni kwamba ameelemewa! Salim anao uzoefu wa siasa za ndani na za kimataifa. Anaweza hata kumwambia Kingunge "Hapana bwana" na Bush "No". Bado Waafrika tunahitaji viongozi wanaoweza kusema hivyo.

Pamoja na hayo, hata tukiamua kumpigia debe mtu yeyote tunayemuona anafaa, bado tunayo miaka 3 na mingine 5 maana kwa hali ilivyo uwezekano wa CCM ama Rais Kikwete kutoendelea kwa kipindi cha pili haupo. Pengine tusaidiane kutoa mawazo kwa viongozi wetu ama tuombe muujiza utokee ili wabadilike na kuangalia matatizo ya nchi na wananchi kwa ujumla kwa umakini zaidi.
 
1. Mwalimu alichemsha big time kumchagua Mkapa kuwa rais wetu, period! Kwa sababu records zipo very clear kuwa Mkapa alipokuwa Elimu ya Juu, alihusika sana na rushwa na maovu, against wananchi Mwalimu alijua haya kwa sababu aliwezaje kujua ya Lowassa, aliyekuwa waziri kama Mkapa na katika serikali moja ya Mwinyi? Waliokuwa wanampa habari za Lowassa, pia walimpa na habari za Mkapa, lakini kwa makusudi akaamua kuangalia upande mwingine, kwa sababu alimtaka Mkapa kwa manufaa yake binafsi kwanza, ambayo Mwinyi na kundi lake walikuwa wameanza kuyakata.

Mkuu FMES,
Hapa mimi sikubaliani na wewe kabisaa. Mkapa hii wizara wakati ule alipopewa ilikuwa haina chochote cha kuiba zaidi ya kusaidia watu scholarship. Ilikuwa ile sehemu ya kumpuzisha asiyetakiwa kwenye cabinet lakini inashindikana kumuacha nje. Mkapa alikuwa anamdharau Mwinyi na walikuwa hawashabihiani kabisa kwenye cabinet meetings.

Binafsi nakumbuka nilibahatika kualikwa nyumbani kwake kwenye mnuso, nafikiri ilikuwa graduation ya mtoto wa mama Mkapa, labda 1993 hivi, nilishangaa sana nyumba yake ilivyokuwa ya hali ya kawaida pale Seaview. Hata rangi ilikuwa imepauka-pauka na bustani zilionyesha kabisa kutokuwepo kwa gardener. Hii ni baada ya yeye kuwa na zaidi ya miaka 30 ya kuitumikia nchi tena katika nyadhifa za juu sana.

Wakati huo huo, Lowassa ambaye ndio tu alikuwa kanusa uwaziri wa Ardhi kwa muda mfupi nafikiri akitokea AICC, alikuwa keshajilimbikizia mali kibao ikiwa ni pamoja na lile bungalow lake la Masaki ambako South Africa walianzishia ubalozi wao. Ukweli ni kuwa Mr. Clean was really very clean na awamu yake kabla ya kifo cha Mwalimu ilikuwa mizuri sana.

Hili la kusema kuwa eti Nyerere (JKN) pia yuko responsible na uchaguzi wa Kikwete (JMK), nafikiri litamfanya ageuke huko aliko. Maana, ingawa JKN alimpenda JMK, sidhani kama angekubaliana naye na wana mtandao wake including Lowassa na mbinu zao walizotumia kuingia Ikulu.

Tusimsingizie mzee wa watu ili apumzike salama. Let us be fair.
 
Nami pia naamini mkapa alikuja kubadilika (sidhani kama alikuwa kaficha makucha yake). Mkapa alikuwa na 'both power and authority'. Angeweza kutuletea maendeleo makubwa Watanzania, kama Nyerere alivyotarajia, angetumia vipawa vyake hivyo alivyokuwa navyo.


Uko sahihi kiasi cha kutisha.

Mchukue malaika yeyote..kutoka duniani au kuotoka mbinguni.

Mtungie azimio la zanzibar Mfanye aliamini na kulitiii!

AND WHAT DO YOU GET?

Several Mkapas, hundreds of EL, Milions of RA and milions of Vijisent

Get to know what is azimio la zanzibar
.
 
in 20/20 vitu vingi kweli tusingevifanya

- Tusingepata Uhuru 1961 tungekubali kutawaliwa kwa muda kidogo angalau hadi 1980
- Tusingeungana na Zanzibar
- Tusingeanzisha siasa za kutofungamana na upande wowote
- Tusingetangaza Azimio la Arusha
- Tusingepigana vita na Amini
- Tusingerudisha mfumo wa vyama vingi
- Nyerere angejiuzulu mapema zaidi kama 1971 hivi
- Tusingepinga utawala dhalimu wa makaburu
- Mwingi asingekuwa Rais
- Warioba asingekuwa Waziri Mkuu
- Salimu asingekuwa Waziri Mkuu
- Msuya asingekuwa Waziri Mkuu
- Malecela asingekuwa Waziri Mkuu
- Sumaye asingekuwa Waziri Mkuu
- Tusingefanya hivi na vile... n.k

Hivyo in hindsight naamini kuna mambo mengi yasingefanyika na kuna watu ambao wasingepata nafasi ya kushika madaraka kabisa... yote hayo ni rahisi kuyahukumu in 20/20.... bahati mbaya even God can not change the past!

Swali: Ni nani kiongozi ambaye tunaweza kumpata leo hii ambaye kwa asilimia 50% tunajua kuwa hatobadilika? Na kiongozi huyo ni yupi ambaye atamfurahisha kila mtu kwa asilimia 100? Nyerere alifariki 1999 na mwaka 2000 Mkapa alichaguliwa tena tuendelee kumlaumu Nyerere? Kuna watu ambao pia wamejaribu kumbebesha Nyerere mzigo wa Kikwete na sitoshangaa akija Rais Mpya Slaa au Seif na wenyewe wakaboronga huko mbeleni watetezi wa 20/20 watatuambia "Ni Nyerere ndiye aliyetufanya tuwachague".

Naomba yeyote mwenye uhakika kuwa kuna kiongozi ambaye tunaweza kumuaminisha Taifa letu na ya kwamba hatoharibu au hatofanya jambo lolote kwa maslahi yake au ya watu wa karibu yake na tukamuamini hivyo kwa asilimia 100. Nionesheni na miye nitaanza kumpigia debe!!! Mmoja tu.

See, this is what I'm talking about!! Tell them man...tell them....Lol
 
I wish Lyatonga angeshinda 1995 maana mzee wa kiraracha naamini angesafisha hizi tabia za kifisadi na leo tungekuwa na true democracy na ningekuwa labda upande wa CCM mana CCM wangekuwa ni watu wenye akili

Na hizi zinaitwaje....?
 
Kilichokuja kumbadili Mkapa nadhani ni baada ya Mwalimu kufariki na mchango binafsi wa FAMILIA yake kama anavyoteseka Mugabe sasa hivi. Mengine yatabaki kuwa ni historia.

Mkuu WildC,
Nakubaliana na wewe kabisaa. Mwanzoni mwa utawala wa Mkapa ilishasemekana kuwa mama Mkapa tayari alishataka kuanza kufanya biashara kama mama Sitti. Mkapa akamjia juu sana na hilo likatoweka. Lakini inaelekea mama Mkapa hakuacha kuendelea na nia yake na mlango ulipofunguka, akafanya kweli. Kuwepo kwa wanafamilia wake kwenye mradi wao wa Kiwira ni uthibitisho mzuri sana wa nani aliyekuwa na ushawishi mkubwa wa zile biashara za Ikulu.
 
Mwalimu HAKUCHEMKA kumpigia debe MKAPA,kipindi kile jamaa kweli alikuwa CLEAN
Kasheshe ilianza baada ya jamaa kuingia ikulu akajifanya MJASIRIAMALI akajikopesha na kujichotea vya kutosha na akatoka ameshiba kwelikweli
Kama alichemka ,wewe ulitaka ampigie debe nani MREMA,KIKWETE?
 
Last edited:
Kwanza, mpaka hapo alipokuwa anampendekeza Mkapa alikuwa poa kabisa. Mkapa alibadilika second term ndiyo ushetani wa hela ukamuingia

Pili, Kubadilika kwa Mkapa ilikuwa nje ya control ya Nyerere.

Tatu, katika wagombea wa 1995 ndani ya CCM, Mkapa was the best choice and was the least devil

Nne, hata leo, kwa CCM Mkapa is far better than the current ruling cligue members. In fact, mimi ukiniambia nichague kati ya Mkapa na JK, nitamchagua Mkapa kwa kuweka tick nyingi sana.

My conclusion: Kwa kuzingatia kwamba ilikuwa lazima achague/apendekeza mgombea kutoka CCM na raia wa Tanzania aliyepo Tanzania, Nyerere hakuchemka hata kidogo- he was more tha right kumsukumiza Mkapa kwenye urais!

Kitila!

I appriciate the observation na niongezee.

Kama hukujailiwa werevu MKUU ni naamini wengi wetu hapa JF tungeweza kuingia kwenye kiza na mtego uliomfika Mkapa baada ya kuingia madarakani.

Kama Mtu huna papara na kufuatilia kwa karibu na kwa kina kiini hasa cha ufisadi..kwanza kaa chini na pitia AZIMIO LA ZANZIBAR...utagundua Uchochoro uliokuwepo pale kumtengeneza fisadi wa leo na hasa kama alitokea kuwa kiogozi wa Awamu ya Kwanza.

Hakuna namna KIONGOZI YEYOTE aliyekuwa "AMETESWA" na AZIMO LA ARUSHA akaja kubamizwa Azimio la zanzibar..AZ alafu asilitumie "KAMA CHOMBO CHA KUJIPOOZEA NA KUONYESHA MAKUCHA YAKE YALIYOKUWA YAMEJIFICHWA KWNYE AZIMIO LA ARUSHA"

Angalia kwa makini Vifungu Vitatu kwenye AZ ona lilivyokuwa chombo cha "KUUUTUA MZIGO" ULIOKUWA UMEMLEMEA KIOGOZI yeyote tokea awamu ya kwanza na kumpelekea kuwa fisadi wa kutupwa.

Get to go deep on the azimio la zanzibar hekima na werevu wa haki na ukweli utakuonyesha...Kuwa Hakuna Yeyote amabaye angeliamini..huku akitokea kwenye kichaka cha azmio la arusha na akose kuwa kama alivyokuwa BWM

Na hata kama AZ litaachwa kuoparate kama lilivyo na kutokufanyiwa marekebishao..yatakayo jumuishwa kwenye katiba mpya ya nchi..au kitu kama hicho...bado Lots of Mkapas,chenges, El, Ra etc are destined to germinate anytime anyhow!
 
inawezekana kuwa nyerere hakuchemka, bali katika wote waliokuwa wamegombea urais wakati yule mkapa ndio alikuwa afadhali kidogo.
kama si mkapa alikuwa awekwe Lowassa? au Kikwete?

nyerere hakuwa na choice (LABDA), wote walikuwa utumbo....akaamua kutuchagulia aliyekuwa afuweni kidogo ambae ni mkapa. kumbe LOH!
 
Taifa Stars ilipoifunga Burkina Faso kwao,kila mtu alisema kuwa kocha tunae.Ilipotoa draw na Senegal Mwanza,ndio kabisa tukaona kuwa kombe la dunia tunaenda,wacha hio AFCON! Hapa juzi ilipochemsha mechi mbili za mwanzo wengi walisema kocha hafai,wengine kama mimi tulisema tatizo sio kocha ni wachezaji.Na hilo likaja kudhihirika kwenye mechi mbili vs Cameroon.Kocha haingii katika akili ya mchezaji,anamsoma kutokana na bidii yake ya mazoezi mentality yake na character pia.Lakini mchezaji anapovuka ule mstari na kuingia uwanjani,ni yeye na Mungu wake.Mwalimu ndivyo alivyoona kwa Mkapa

Well Said Zanaki...
 
Just thinking aloud;
  1. Kwa wale wanaokubali kuwa Mkapa alifanya kubadilika baadaye, je kuna alama zozote hivi sasa tukiangalia nyuma tunaziona ambazo tunaweza kuzitumia kumdadisi muungwana aliye kitini?
  2. Are the pouses key to ufisadi wa Ikulu, Sitti and Anna for example, or the husbands are just hidding behind wake zao?
  3. If the prez is constitutionally somewhat immune from prosecution, kwa nini tusiende after wake zao na ndugu wao wengine ambao hawana veto ya katiba?
 
Just thinking aloud;
  1. Kwa wale wanaokubali kuwa Mkapa alifanya kubadilika baadaye, je kuna alama zozote hivi sasa tukiangalia nyuma tunaziona ambazo tunaweza kuzitumia kumdadisi muungwana aliye kitini?
  2. Are the pouses key to ufisadi wa Ikulu, Sitti and Anna for example, or the husbands are just hidding behind wake zao?
  3. If the prez is constitutionally somewhat immune from prosecution, kwa nini tusiende after wake zao na ndugu wao wengine ambao hawana veto ya katiba?

Why don't you just keep your thoughts to yourself.....
 
So what the hell is your problem and who the hell do you think you are to tell me (how) to use my brain?

Hay, cool down Nyani. That was just an advise. But if cheering is better than using your brain, do it, man. After all, sometimes is no good to help a blind. Let's go back to the subject.
 
katika uongozi wake wote Mwalimu alikuwa halali usingizi mzuri kwa kuwaza matatizo ya wananchi....Alijitahidi kwa kadri ya uwezo wake kama binadamu kuingoza nchi si kwa manufaa yake wala ya familia yake na hili nadhani hata wasiokubali juhudi zake, hakuna anayeweza kulipinga. Kwa hiyo tunapomuhukumu, tuzingatie kwamba ni vigumu mno katika nchi zetu hizi masikini, kupata kiongozi ambaye kwa dhati kabisa anaweza akaweka maslahi yake pembeni na kujali yale ya wananchi anaowaongoza, kwa asilimia mia kwa mia.

Kwa hiyo unasema hakuchemka kwa sababu Mwalimu alikuwa na nia nzuri siku zote. Na kwamba, hata hivyo hakuna watu wasafi Afrika, anyway.

Nadhani hiyo thrust ya hoja yako (nimeisoma posti yote kwa makini).

Kama hivyo ndivyo unavyosema, basi hujui maana ya kuchemka, kwa sababu unadhani ni mwenye nia mbaya tu ndio anaweza kuchemka.

Na hata kama unajua maana ya kuchemka, hapa umekubali bila kujijua, kwamba, Afrika yenyewe watu wasafi ni vigumu kuwapata, kwa hiyo atakae chagua koroma asilaumiwe. Hapo unatetea sababu za kuchemka kwake, wakati swali halifiki huko. Linaishia hapa: Je kachemka. Umetwambia kachemka. Ahsante kwa mawazo yako.
 
Back
Top Bottom