Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, amefariki akiwa fukara.
haya ni mambo kumi muhimu tunayaoweza kuyatafakati.
1.Hana kitu cha fahari cha kujivunia, mbali na busara na msimamo kwa kile alichokiamini.
2.Hana lolote la kuweza kunyooshewa kidole na binadamu yeyote kwamba alikuwa na mali nyingi kupindukia ambazo alizipata kwa njia ya udanganyifu.
3.Alikuwa, amekuwa na ataendelea kuwa mjamaa wa kweli asiye na mfano ndani na nje ya bara la Afrika. Alikuwa na msimamo usiotetereka wala hakuwahi kumpigia magoti mtu kwa mali au utajiri wake.
4.Aliwakemea wote waliojaribu kumwambia lolote kuhusu kuchota mali za umma kwa ajili yao na ndugu zao. Aliwapa ukweli tena usiokuwa na kificho; Aliwaambia hapana na kweli ikawa hivyo hadi mwisho na wao kukata tamaa.
5.Kwa wabinafsi na mafisadi, Mwalimu alionekana mjinga kwa kutotumia nafasi aliyokuwa nao kujichotea mali. Hakuweza kamwe kujilimbikizia mali pamoja na kwamba alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo.
6.Nyerere alikuwa ni binadamu tofauti. Kwa kawaida binadamu amezaliwa na tabia ya ubinafsi, lakini yeye hakuweza kuwa na tamaa ya kuiba ama kuchota raslimali zilizokuwapo wakati huo pamoja na umbumbumbu wa idadi kubwa ya wananchi wa Tanganyika, ambao wengi wao kwa wakati huo hawakuwa na elimu wala ufahamu wa kutosha juu ya mambo mengi.
7.Mwalimu alikemea utumiaji wa mitutu ya bunduki ama nguvu za dola katika kuzima ama kuzuia haki za watu, akieleza kuwa matumizi ya maguvu ya aina hiyo hayawezi kudumu milele kukandamiza na kuzuia haki kutendeka.
8.Alithamini haki za binadamu na kusema ni kigezo cha msingi katika kudumisha amani na mshikamano, katika nchi moja kwa upande mmoja na katika dunia kwa upande mwingine.
9.Mwalimu Nyerere hakutaka kuonea, lakini alikaripia pale palipojitokeza udhaifu.
10.Mwalimu Nyerere alikuwa baba, babu na mlezi wa kila mmoja. Wapo wanaokejeli ubaba, ubabu na ulezi wake ambao ameutoa kwa Tanganyika, na baadaye Tanzania, kwa zaidi ya nusu ya maisha yake yote.
HITIMISHO
Tabia hii ilifanya Mwalimu ajikusanyie mashabiki na marafiki wengi na alifanikiwa kuipenyeza kwa baadhi ya watumishi waliokuwa madarakani wakati huo.
Ufukara wa viongozi waliokuwa madarakani si dhambi; wala si kosa kwa viongozi walioko madarakani kutumia fedha halali za mishahra yao na masurufu mengine ya lazima kujijengea nyumba na mahitaji mengine muhimu.
Lakini ukweli unabaki pale pale kuwa kiongozi yeyote Tanzania au nchi nyingine masikini anayeweza kuwa na kasri ama gari la gharama kubwa wakati mishahara si mikubwa, isiyoruhusu kufanya vitu vya kuogofya; na kama anavyo vitu vya fahari kubwa ni wazi kuwa atakuwa akiiba ama mali ya umma au kula rushwa.
Nyerere 'aliwaambukiza' tabia hiyo viongozi wengi waliokuwa chini yake na ambao, hata leo baada ya kustaafu, wamebaki kuwa watu wasiokuwa na msimamo thabiti kwa maisha yao na familia zao kwa kuwa tu hawakuweza kujichotea mali kwa rushwa au wizi.
haya yote yanapatikana katika kitabu cha Nyerere Hazina Tanzania.na nimeyaleta hapa kwa nia moja na dhumuni moja la hasira juu ya wale wote wanaopenda kujilimbikizia mali.