Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

ningekuwa mie nimeongea hivyo, mngesema kejeli, kebehi, oooh jamaa anatukana na maneno mingiii, lakini kwa kuwa ni ninyi hakuna kilichoharibika!!!
Nilijua tu utakuja na jibu hilo hii ndio hekima mkuu - tunaona mbali.. usiwe na haraka mkuu Nyerere yupo na Hurulain, hutaki!...
 
Hivi tujiulize yale mapungufu ya Nyerere yaliyekuwepo kipindi cha utawala wake kama ndiye yapo hivi sasa wananchi wa wakati huu wangeichukuliaje zama hizi?Je angeweza kutawala Tanzania ya leo?
Hizi zama uhuru wa vyombo vya habari,zama za kukosoa serikali katika kutoa huduma za jamii,zama kukosoa viongozi kwa wazi uwazi kabisa!zama za biashara huria dawa za meno na sabuni mpaka vijijini zama za nyerere ilikuwa almasi!Wananchi wa zama hizi wangeweza kuvumulia kama wale waliyo kuwa wakitawalia na Nyerere?

Nyerere amefanya mazuri lakini kwa mwananchi wa kawaida mwenye njaa hana sabuni,hana nguo hana maji wa zama za Nyerere unambia nyerere saint atakushangaa.

Mie nimesoma zama za Nyerere kulikuwa hakuna madaftari shuleni tuna madaftari 5 tuna ambiwa daftari moja masomo mawili!Leo hii nani anakubali hayo?
!

Sir Leem,

Ningekuwa mchumi au mtu wa pesa, hoja yako inaegemea kwenye purchase power na si supply versus demand.

Wakati ule wa kupanga foleni, tuliopanga wote kutokana na hali ngumu. Nikupashe sana kuwa hata Marekani baada ya vita kuu ya pili, kulikuwa na resheni ya kila kitu, mafuta ya gari, nguo, chakula na kadhalika.

Unadai dawa za mswaki, leo hii dawa kibao madukani lakini hakuna wanunuzi kutokana na kukosa pesa! Unazungumzia madaftari? Wiki mbili zilizopita tulikuwa tunazungumzia picha ya watoto washule wamekaa sakafuni!

Umeuliza hao waliozaliwa 1985 sasa hivi wana miaka 23, je ni wangapi wao ambao pamoja na "Uhuru" wa kuingiwa mzuka wa Nyerere wanaweza jitegemea kwa kukua katika mfumo wa Ruksa?

You are talking more of material stuff and absence of commodities. Sasa material stuff ambazo nyingi ni imports zimejaa madukani, zile local industry tumezigawa kwa bei powa and still, watu wanapiga mswaki kwa kutumia majivu, kwa kuwa it is better for them to spend the money kununua mbegu na si Colgate! Same is with clothing!

Kwa hiyo usidanganyike kwa kujaa maduka (mengi yana bidhaa bomu maana tumekuwa dampo) na kuona huko ni maendeleo! Ni sawa na wale wanaodai kuwep kwa magorofa ya kauri Dar ndio kuendelea!

Kama Mtanzania wa Malampaka, Nanjilinji, Kondoa, Wawi na Mchafukoge hali yake bado ni ile ile kama ilivyokuwa 1985, utaendeleaje kumlaumu Nyerere huku tumekuwa na miaka 23 ya ku-recover kutoka makucha na kunyanyaswa na Unyerereism?

Why Tanzania has failed to make drastic changes that are progressive for the benefit of Taifa in the last 23 years?

Hivi ukichukua inflation na devaluation ukafanya analysis na comparison kati ya 1985 na 2008 factor population increase and other indicators, kama life expectancy, literacy, infant mortality etc. si utakuta heri enzi za Nyerere? au utadai ni Ufisadi na Ukimwi? if so I stll ask you, we have been liberated and free of Nyerereism for the past 23 years or let say 9 years since his death, what have we achieved economically that all Tanzanians in rural and urban areas can boast and thump their chests vifua mbele and claim matunda ya uhuru kutoka Utumwa na Ukoloni wa Nyerere?
 
Reverend.. hilo somo haliwezi kuingia kwa sababu kwao wao Tanzania inatawaliwa na sheria za uchumi za ulimwengu sambamba..
 
I think Prof. Ali Mazrui sums up Nyerere's legacy quite well:

Nyerere's policies of Ujamaa amounted to a case of Heroic Failure. They were heroic because Tanzania was one of the few African countries which attempted to find its own route to development instead of borrowing the ideologies of the West. But it was a failure because the economic experiment did not deliver the goods of development.

On the other hand, Nyerere's policies of nation-building amount to a case of Unsung Heroism. With wise and strong leadership, and with brilliant policies of cultural integration, he took one of the poorest countries in the world and made it a proud leader in African affairs and an active member of the global community.

The rest of the article is here:
http://http://www.africaresource.com/content/view/56/222/
 
Rev.Kishoka said:
Sir Leem,

Ningekuwa mchumi au mtu wa pesa, hoja yako inaegemea kwenye purchase power na si supply versus demand.

Wakati ule wa kupanga foleni, tuliopanga wote kutokana na hali ngumu. Nikupashe sana kuwa hata Marekani baada ya vita kuu ya pili, kulikuwa na resheni ya kila kitu, mafuta ya gari, nguo, chakula na kadhalika.

Unadai dawa za mswaki, leo hii dawa kibao madukani lakini hakuna wanunuzi kutokana na kukosa pesa! Unazungumzia madaftari? Wiki mbili zilizopita tulikuwa tunazungumzia picha ya watoto washule wamekaa sakafuni!

Umeuliza hao waliozaliwa 1985 sasa hivi wana miaka 23, je ni wangapi wao ambao pamoja na "Uhuru" wa kuingiwa mzuka wa Nyerere wanaweza jitegemea kwa kukua katika mfumo wa Ruksa?

You are talking more of material stuff and absence of commodities. Sasa material stuff ambazo nyingi ni imports zimejaa madukani, zile local industry tumezigawa kwa bei powa and still, watu wanapiga mswaki kwa kutumia majivu, kwa kuwa it is better for them to spend the money kununua mbegu na si Colgate! Same is with clothing!

Kwa hiyo usidanganyike kwa kujaa maduka (mengi yana bidhaa bomu maana tumekuwa dampo) na kuona huko ni maendeleo! Ni sawa na wale wanaodai kuwep kwa magorofa ya kauri Dar ndio kuendelea!

Kama Mtanzania wa Malampaka, Nanjilinji, Kondoa, Wawi na Mchafukoge hali yake bado ni ile ile kama ilivyokuwa 1985, utaendeleaje kumlaumu Nyerere huku tumekuwa na miaka 23 ya ku-recover kutoka makucha na kunyanyaswa na Unyerereism?

Why Tanzania has failed to make drastic changes that are progressive for the benefit of Taifa in the last 23 years?

Hivi ukichukua inflation na devaluation ukafanya analysis na comparison kati ya 1985 na 2008 factor population increase and other indicators, kama life expectancy, literacy, infant mortality etc. si utakuta heri enzi za Nyerere? au utadai ni Ufisadi na Ukimwi? if so I stll ask you, we have been liberated and free of Nyerereism for the past 23 years or let say 9 years since his death, what have we achieved economically that all Tanzanians in rural and urban areas can boast and thump their chests vifua mbele and claim matunda ya uhuru kutoka Utumwa na Ukoloni wa Nyerere?

Kishoka,

..majibu uliyotoa yanalingana na yale aliyotoa Mwalimu alipokwenda kuzungumza na jamaa wa IMF.

..Mwalimu aliulizwa kwanini ali-fail. badala ya kujibu akawarudishia swali IMF kwamba mbona hata wao wamefeli!!

..sidhani watu kama Sir Leem wanaongelea "material" stuff. masuala ya NGUO,CHAKULA,na MALAZI ndiyo basic human needs duniani kote. tena kwingine wanasema hizo ni HAKI.

..kuna mataifa mengine yameongeza masuala kama ELIMU na AFYA kuwa haki za msingi za raia wake.

..mimi nafikiri kila sekta ya jamii ilidorora wakati wa utawala wa Mwalimu. Kwamba Mwinyi, na Mkapa, walishindwa kupata ufumbuzi wa matatizo aliyoyaacha Mwalimu, hakumuondolei lawama Mwalimu.

NB:

..when was the last time you bought a tooth paste,bar of soap,cooking oil, sandals,shoes, bicycle, etc etc made in Tanzania?

..kwanini watu wanazungumzia hivi viwanda as if vilikuwa at the peak of their production capacity?

..viwanda na mashirika ya umma mengi/majority yalikufa wakati wa utawala wa Mwalimu.
 
Jokakuu,
Ukisema hivyo basi kuna kila haki ya kusema aliye fail ni kati ya Mwarabu, Mjarumani, Muingereza maana hata mwalimu alikuta uchumi mbaya..
Hivi viwanda mkuu vilikuwa ndio kwanza vimejengwa... hata uwanja wa ndege kabambe la Uingereza limeshindwa kufanya kazi siku za mwanzo na technologia yote hiyo..
Ni uongo na uzushi mkubwa kuwa viwanda hivi vilikufa tazama list ya mali zote tulizouza kisha unambie kilichofa ni kipi, Vilikufa wakati wa Mwinyi, tulipoanza kuiba vipuri na kuviuza nje kama wanavyofanya RITTES, hata magari ya Polisi na mabasi ya UDA, transifoma za umeme na kadhalika.. mkuu tulikuwa Bongo katikati ya maswala haya yakitokea.
 
Lee Kuna Yew waziri mkuu wa zamani wa Songapore amepata kuitwa Dictator na Viongozi pamoja na vyombo vya habari vya nchi za Magaharibi.

Hatahivyo baada ya kuiondoa Singapore kwenye umasikini mkubwa kuliko Umasikini liyo kuwa nao Tanzania baada ya Uhuru. Kuen Lee Yew anaonekana ni mfano wa kuigwa.

Yeye pamoja na Kiongozi wa Dubai wanaonekana kama Viongozi wa mtindo wa very Smart CEOs.

Nyerere siwezi kumdiscredit completely katika mtazamo wake.

Lakini kuna mambo mengi sana ambayo sikubaliani naye hata kidogo.
Ujamaa na Azimio la Arusha yakiwemo.

Jambo jingine ni kukimbilia ndoto ya pili ya ukombozi wa Afrika na kusahau kabisa kuanisha ndoto zake katika mfumo unaotekelezeka na kurekebisha mengi yasiyotekelezeka.

Kwa sababu Nyerere katika siasa yake ya Ujamaa na kujitegemea alishindwa, tuna haki ya kurudi nyuma na kuangalia migongano mingi ya utawala wake, uzembe wa kulinda wahalifu na wezi na kuwapa adhabu kali wale wote waliopinga Ujamaa na Azimio la Arusha
Pia suala la kuwajaza Wajomba zake Wazanaki usalama wa taifa na Ikulu na kujifanya Tanzania ni moja kati ya nchi kiboko katika shughuli za usalama wa taifa, kumbe ni kundi la watu wachache wanao mlinda mjomba wao kama akina Butiku na wenzake.

My Freand who ever think NEGATIVE abt AZIMIO LA ARUSHA anatakiwa atueleze mabaya ya hilo azimio this was A VISSION OF THIS NATION azimio hata leo tunalihitaji and tunapo ongelea UJAMAA lazima Tutaje wazi na KUJITEGEMEA and we need that PRACTICALLY TODAY.

Kwahilo Mwalimu was Right leo tumeona impact ya the so called AZIMIO LA ZANZIBAR nashangaa anae pinga hilo my be hayupo ndani na hajui matokeo ya kuua azimio hilo.TOday we have a Nation without a VISSION also we dont have a MISSION.

Tusisahau AZIMIO was a VISSION and UJUMAA NA KUJITEGEMEA was a MISSION leo tuna nini?

In my opinion this was one of mwalimu success and kuondoa hilo we can see the price tunayolipa,UKO WAPI UZALENDO,UMOJA,UTAIFA, Nashangaa tunapohoji ju ya haya kuna TANGABLE na INTAGIBLE success za MZANAKI HUYU kwa TAIFA hili,Najiuliza unapo hoji why alitumia Muda mwingi kutafuta UHURU wa mataifa mengine DO YOU THINK UTAKUA SAFE WHILE ENEMIES WAPO NEXT DOOR? That was one of the success za mwalimu leo tunaona na kujadili SADC,COMESA kama wasinge pata uhuru wao tusingekua na ECONOMIC BLOCK HIZO the man ametengeneza msingi ameondoka mbaya tumeanza kuubomoa na kusahau kua ukuta tunaojenga utatuangukia na sasa umeonyesha NYUFA tunasema mjenzi wa msingi hakua makini while sisi ndio tuliurekebisha bila kujua/kwa kujua/makusudi/bahati mbaya/ kua tunauharibu
 
Sisi Waafrika tunapenda mno kulaumu wengine kwa failure zetu. Hapa tuko tunamlaumu mtu mmoja (Nyerere) kwa kutulostisha na tunasahau na kupuuzia kabisa common denominator ya nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara. Mnazidi kunishangaza!!
 
Nyani umesema jambo moja ambalo ni muhimu sana. Ukiangalia mjadala huu na ule wa fikra utaona mambo kadhaa:

a. Wanaosema "Nyerere alifeli" wanafanya hivyo wakijaribu kutafuta mtu wa kumbebesha mzigo ili wao wenyewe au watu wengine wasiwe na wajibu. Ukiona mambo ambayo wangependa Nyerere aweze kuyafanya miaka michache baada ya uhuru wanathibitisha aidha alikuwa na nguvu za kiungu kuweza kufanya yote.

b. Wanaozungumzia kuwa uchumi wa Tanzania ulikuwa mbaya wakati ule hadi hivi sasa hakuna hata mmoja aliyetupa comperative economic analysis ya uchumi miaka ya 70 hadi mwanzoni mwa 1980 mwa uchumi wa nchi nyingine jirani au uchumi wa dunia. Nitafurahi kuoneshwa jinsi gani uchumi wa nchi nyingine za Afrika ulikuwa mbali sana na wa kwetu miaka hiyo Uganda, Kenya, Zaire, Msumbiji, Angola, n.k Ili tuweze kulinganisha maana kama Uchumi wetu in isolation ulikuwa mbaya basi tunaweza kusema tatizo ni Nyerere.

Mafanikio ya miaka ya 80 baada ya Mwinyi je yalihusiana na kazi ya Mwinyi tu au kulikuwa na factors nyingine ambazo zilifungulia wingi wa bidhaa? Je ni nchi yetu tu iliyoonesha kukua kwa uchumi kusiko kwa kawaida miaka ya themanini na tisini ukilinganisha na nchi nyingine za dunia?

c. Leo hii credit crunch na mortgage crisis inayoendelea inaathiri ulimwengu mzima. Hivi Marekani na nchi nyingine ambazo ziko katika hali mbaya ya uchumi ni kwa sababu Rais Bush amefeli kiuchumi? Leo hii uchumi wetu ukianza kuyumba watu watamlaumu Kikwete kwa kufeli kiuchumi au tutaangalia factors zote na si mtu mmoja kama wengi wanavyojaribu.

d. Kuna majaribio ya demonization ya Mwalimu kwa vitu ambavyo vilikuwa nje ya uwezo wake. Hivi Nyerere angeweza kujenga madaraja, barabara, hospitali, kukabiliana na njaa, vita, hali mbaya ya uchumi, sabotages za economic hitmen, taifa la wasomi kiduchu, miundo mbinu kidogo n.k na apate maksi mia moja? Alikuwa na nguvu gani za kiungu za kumuwezesha kufanya mambo hayo yote?

e. Rais yeyote wa nchi ana uwezo na nguvu za aina fulani lakini siyo "mweza yote" wa nchi kama watu wanataka kuashiria.

Nyerere alikuwa na uamuzi na kuamua kuweka kipaumbele. Hili ndugu zetu hawataki hata kuliangalia kwa ukaribu kwa sababu wakifanya hivyo watapata picha kubwa ambayo itawapunguzia kisirani chao dhidi ya Mwalimu na hivyo watakosa mtu wa kumhukumu.

Na zaidi ya yote ni rahisi kumlaumu Nyerere kuliko kujiangalia sisi wenyewe. Mojawapo ya maneno ya mzee FMES ambayo ni signature yako pia yana ukweli na ya na maana sana kwamba kimsingi viongozi wetu ni sura na picha ya sisi wenyewe.
 
Hey...you nailed it! I just had to point it out and you came in and put it into perspective. Bravo!!
 
ndugu zangu,

..naona kila mara watu wana-move the goal post.

..ninavyoelewa mimi inapotokea uchumi wa nchi yoyote ile ukaanguka basi anayebeba mzigo mkubwa wa lawama ni Raisi na serikali yake.

..Mwalimu anapaswa kubeba lawama za kuporomoka kwa uchumi kutokana na maamuzi aliyoyafanya akiwa madarakani.

..tatizo siyo Mwalimu binafsi, bali maamuzi aliyochukua kukabiliana na economic challenges of his time.
 
ndugu zangu,

..naona kila mara watu wana-move the goal post.

..ninavyoelewa mimi inapotokea uchumi wa nchi yoyote ile ukaanguka basi anayebeba mzigo mkubwa wa lawama ni Raisi na serikali yake.

Anayemlaumu Rais na serikali yake ni mtu ambaye hajui kuchambua takwimu, factors za uchumi n.k. Mtu ambaye ana uwezo wa kuangalia historia, takwimu na hali halisi kwa njia ya upembuzi yakinifu hawezi kufanya makosa ya kumlaumu Rais wa nchi kwa hali mbaya ya uchumi wowote ule.

Hivi matatizo ya Mortgage sasa hivi ni makosa ya Bush? Kuna level ya lawama inapokuja kwenye masuala ya uchumi lakini the level that is raised against Nyerere is fundamentally flawed for it fails absolutely to admit the role of other factors in the near collapse of our economy during the said period. The attempt by some to put the economic hardship of the seventies and early eighties on Mwalimu's shoulders ni kinyume na ukweli wote wa kihistoria isipokuwa inafurahisha mioyo yao tu kuwa wamempata mtu wa kumlaumu.

..Mwalimu anapaswa kubeba lawama za kuporomoka kwa uchumi kutokana na maamuzi aliyoyafanya akiwa madarakani.

Maamuzi aliyoyafanya wakati tunaangalia in 20/20 tunaweza kusema mengine hayakuwa sahihi; lakini kuna wakati kiongozi lazima ufanya maamuzi ambayo unaamini are in the best of the nation. Nyerere was courageous enough to make decisions siyo kama hawa wa leo ambao wanasita kufanya hata maamuzi madogo kama kurudisha nyumba za serikali!

Ni bora kiongozi anayefanya maamuzi tukajua ameamua nini kuliko kiongozi anayeshindwa kufanya maamuzi na kutuacha tukisie ameamua nini. Nyerere alifanya maamuzi ambayo at the time yalikuwa ni kile alichokiita "clash of principles". Kati ya kujenga Chuo Kikuu kipya na kuhakikisha kuna chakula nchini Nyerere angechagua nini? Kati ya kuendelea na income gap kati ya weusi na walowezi wa wakati ule Nyerere angefanya nini ili kutoa nafasi kwa new educated blackmen and women? Endapo shule nyingi za sekondari na hospitali ni za binafsi (makanisa) na wengi wanaoenda kwenye shule hizo ni wakristu au wanacompromise imani zao yeye alitakiwa kufanya nini? Wakati njia zote za uchumi ziko mikononi mwa wageni Nyerere alitakiwa kufanya nini ili kutoa nafasi kwa watanzania weusi ambao walikuwa denied for many years kusimamia njia hizo angefanya nini?

Kwa maoni ya wengine ni kuwa Nyerere angeendelea kuwaacha wabongo waendelee kuwa the majority but holding a miniature sway katika uchumi wa nchi yao kama ilivyotokea Zimbabwe? Kama Asingeifanya ardhi kuwa mali ya Taifa zima hivi leo ni sehemu gani ya Tanzania ingekuwa mikononi mwa watu weusi? Kuna maamuzi ambayo leo tunayaona hayakuwa mazuri lakini in historical perspective were not only good but inherently necessary.

..tatizo siyo Mwalimu binafsi, bali maamuzi aliyochukua kukabiliana na economic challenges of his time.

As a single person and a limited being he could not have dealt with all economic challenges of his time superbly without failing in some. No way! Hakuna kiongozi yoyote duniani ambaye ameweza kufanya hivyo kwanini mnadhani Nyerere angeweza kufanya hivyo in the seventies!? This is the part that I don't understand.

In hindsight, tunaweza kusema "angefanya hivi au vile" lakini in reality hata akilini haiingii. Ni serikali ya nchi gani ambayo imeweza kushughulikia matatizo ya kiuchumi ya watu wake na kumalizana nayo? Japani? Ufaransa? China? Japan? Marekani? Uingereza? Ujerumani?

JokaKuu, I dare you to pick any nation or any leader at any time in history, who was able to deal with all social, economic, and political problem of his society ambaye watu hawakuweza kumlaumu huko baadaye kwa kutotimiza jambo lolote. Ukinionesha mmoja nitakubali tumbebeshe Nyerere lawama zote za kiuchumi kama unavyojaribu kufanya
 
Mkandara said:
Ukisema hivyo basi kuna kila haki ya kusema aliye fail ni kati ya Mwarabu, Mjarumani, Muingereza maana hata mwalimu alikuta uchumi mbaya..

..I am open to that debate.

..kukusaidia, mkoloni Mngereza ali-invest kidogo sana ktk masuala ya elimu. Baba wa Taifa alikuja kubeba mzigo wa kuwa na taifa lisilo na Wataalamu kutokana na utawala mbaya wa kikoloni..

Mkandara said:
Hivi viwanda mkuu vilikuwa ndio kwanza vimejengwa... hata uwanja wa ndege kabambe la Uingereza limeshindwa kufanya kazi siku za mwanzo na technologia yote hiyo..
Ni uongo na uzushi mkubwa kuwa viwanda hivi vilikufa tazama list ya mali zote tulizouza kisha unambie kilichofa ni kipi, Vilikufa wakati wa Mwinyi, tulipoanza kuiba vipuri na kuviuza nje kama wanavyofanya RITTES, hata magari ya Polisi na mabasi ya UDA, transifoma za umeme na kadhalika.. mkuu tulikuwa Bongo katikati ya maswala haya yakitokea.

..kiwanda kikijengwa halafu hata kisizalishe kinaweza kuwa ni hasara kuliko kisingejengwa kabisa.

..hebu tueleze sababu zilizopelekea viwanda hivi kujengwa na kufa mara moja. je, maamuzi gani ya serikali ya Baba wa Taifa yalisababisha hilo?

..pia kama kiwanda kinazalisha na wafanyakazi wanakitegemea kwa maisha yao hawawezi kuanza kuiba vipuri. kwa msingi huo yapo mazingira yaliyosababisha wafanyakazi wakose nidhamu kiasi hicho. sasa mazingira hayo yalisababishwa na siasa za Baba wa Taifa, au Mzee Mwinyi?

NB:

..kwa maoni yangu kulikuwa na siasa nyingi ktk uendeshaji wa viwanda, mashirika,na uchumi kwa ujumla.

..badala ya kushindana ktk uzalishaji mashirika yalikuwa yakishindana kwa vikundi vya ngoma, timu za mpira na netiboli, kwaya, matawi ya chama na juwata.

..pia kulikuwa na mashindano ya kudhamini shughuli za chama na serikali.

..viongozi wa chama na serikali walikuwa hawaishi kutafuta fadhila na zawadi toka kwa wakuu wa mashirika ya umma.

..Matawi ya chama na Juwata yaliwaingilia Mameneja ktk kufanya maamuzi ya kitaalamu.

..wengi tunashangaa kwanini kaburu ameweza kuendesha TBL. tunasahau kwamba ameondokana na vikundi vya sanaa, timu za mpira,juwata etc etc.

..Mameneja walikuwa hawaruhusiwi kupunguza wafanyakazi hata kama kiwanda/shirika limelemewa.

..sasa ukichanganya chama kushika hatamu[sera za Baba wa Taifa], under-capitalization ya mashirika yetu, utaona kwamba we were bound to fail.

..ukweli utabaki kwamba Baba wa Taifa alielezwa mazingira yaliyolikabili taifa, na maamuzi aliyopaswa kuchukua. alikataa ushauri ambao unaashria ungetusaidia. matokeo yake ni kuanguka kwa mashirika na uchumi wetu kwa jumla.

..kwa msingi nasema Mwalimu alifanya makosa na anastahili lawama.
 
..I am open to that debate.

..kukusaidia, mkoloni Mngereza ali-invest kidogo sana ktk masuala ya elimu. Baba wa Taifa alikuja kubeba mzigo wa kuwa na taifa lisilo na Wataalamu kutokana na utawala mbaya wa kikoloni..

Sasa kama alikuwa na "taifa lisilo na wataalamu" angeweza vipi kufanya yote ambayo angepaswa kufanya kikamilifu bila makosa hata chembe?

..kiwanda kikijengwa halafu hata kisizalishe kinaweza kuwa ni hasara kuliko kisingejengwa kabisa.

..hebu tueleze sababu zilizopelekea viwanda hivi kujengwa na kufa mara moja. je, maamuzi gani ya serikali ya Baba wa Taifa yalisababisha hilo?

nadhani maamuzi ya kujaribu kuanza kujenga viwanda vyetu wenyewe; angeamua kuacha kujenga viwanda kwenye Taifa huru ambalo alikuwa anajribu kulijenga.

..pia kama kiwanda kinazalisha na wafanyakazi wanakitegemea kwa maisha yao hawawezi kuanza kuiba vipuri. kwa msingi huo yapo mazingira yaliyosababisha wafanyakazi wakose nidhamu kiasi hicho. sasa mazingira hayo yalisababishwa na siasa za Baba wa Taifa, au Mzee Mwinyi?

Mwinyi na Nyerere hawako madarakani, je watu wameacha kuvihujumu vitu vya Taifa? Kwani walioiba EPA na idara nyingine wote walikuwa ni wanafunzi wa Nyerere au hata mtu akiiba kipuri kwa sababu ni mwizi basi tumlaumu Nyerere kwa wizi wake. Hivi malaya akienda kufanya shughuli zake za umalaya tumlaumu Nyerere kwa kutengeneza mazingira ya "umalaya" na hatuwezi kuweka lawama hizo kwa mtu mwenyewe au vyanzo vingine mbalimbali? Kwanini lazima iwe ni nyerere?

NB:

..kwa maoni yangu kulikuwa na siasa nyingi ktk uendeshaji wa viwanda, mashirika,na uchumi kwa ujumla.

Kuna mkweli mkubwa, je siaza hizo "nyingi" leo hazipo? Ni Nyerere chanzo cha siasa hizo au kuna factors nyingine ambazo zilichangia?

..badala ya kushindana ktk uzalishaji mashirika yalikuwa yakishindana kwa vikundi vya ngoma, timu za mpira na netiboli, kwaya, matawi ya chama na juwata.

couldn't have said it better..!

..pia kulikuwa na mashindano ya kudhamini shughuli za chama na serikali.

Ina maana hakuna tena? umesikia jinsi watu walichongia kule Mara CCM na kwa kufanya hivyo wanachangia Amani? Au Nyerere ndiye alielekeza kwa njia ya osmosis toka kaburini?

..viongozi wa chama na serikali walikuwa hawaishi kutafuta fadhila na zawadi toka kwa wakuu wa mashirika ya umma.

Walikuwa? wameacha lini...?

..Matawi ya chama na Juwata yaliwaingilia Mameneja ktk kufanya maamuzi ya kitaalamu.

Yaliwaangilia.. unafikiri influence ya CCM bado haipo kwenye viwanda na taasisi mbalimbali? Au hiyo ilikuwa wakati wa Nyerere tu?

..wengi tunashangaa kwanini kaburu ameweza kuendesha TBL. tunasahau kwamba ameondokana na vikundi vya sanaa, timu za mpira,juwata etc etc.

Mzee unajua ni kwa kiasi gani wamekuwa wakidhamini michezo na mambo mbalimbali ili wawe na uzuri? Unajua ni kwa kiasi gani wakubwa wa TBL wamelala kitanda kimoja na vigogo wa CCM; don't even get me started.

..Mameneja walikuwa hawaruhusiwi kupunguza wafanyakazi hata kama kiwanda/shirika limelemewa.

Si umesikia mambo ya TRL? Leo hii nani kafukuzwa kazi au hata kupunguzwa kazi wakati mzigo wa maisha umeelemea kwenye mashirika mbalimbali?

..sasa ukichanganya chama kushika hatamu[sera za Baba wa Taifa], under-capitalization ya mashirika yetu, utaona kwamba we were bound to fail.

that is gross generalization ya Nyerere; hivi huwezi kufikiri kuwa tuna viongozi dhaifu ambao wameshindwa kusimamia maslahi ya nchi yetu wengine wakita tangu chini ya Nyerere na if you think about it.. if they failed then, why should they succeed today. Don't you think that Baada ya Nyerere kufa na hawa kuendelea na uharibifu wao yawezekana wao ndio tatizo hasa la utekelezaji wa jambo lolote zuri na si mwalimu na fikra zake?

..ukweli utabaki kwamba Baba wa Taifa alielezwa mazingira yaliyolikabili taifa, na maamuzi aliyopaswa kuchukua. alikataa ushauri ambao unaashria ungetusaidia. matokeo yake ni kuanguka kwa mashirika na uchumi wetu kwa jumla
.

Ni kweli lakini uchumi ni uchumi hauna kanuni moja ambayo inaweza kujibu matatizo yote. Ingekuwa hivyo nchi ambazo zina maprofesa na washauri wa uchumi wengi zaidi na waliobobea wasingekuwa na matatizo ya mabenki, mikopo n.k Au unaelezeaje matatizo ya kiuchumi ambayo yameripotiwa leo na IMF?

..kwa msingi nasema Mwalimu alifanya makosa na anastahili lawama.

makosa ambayo si makosa? kama lengo ni kumlaumu Nyerere kwa kila kitu bila kufungua mwanya wa kuangalia ukweli wa kihistoria basi wewe endelea kwa sababu lengo ni kulaumu bila kufanya haki katika kulaumu huko.
 
Mwanakijiji,

..posting yangu hapo juu nimeituma kabla kusoma posting yako.

..naona mtu mwingine yeyote akisema Mwalimu alikosea ktk hili au lile basi huishi kulaumu.

..naomba basi utueleze kwa mtizamo wako Mwalimu alikosea wapi, na anawajibika kwa lipi ktk utawala wake.

NB:

..mfano wako wa morgage crisis una matatizo kidogo. hauendani na mazingira ya Tanzania ya wakati wa Baba wa Taifa.

..ktk morgage crisis kuna mabenki binafsi, halafu kuna loop-holes ktk sheria[serikali], speculators, na innocent individuals.

..Bush angebeba lawama zote kama mikopo ingekuwa imetolewa na mabenki yanayomilikiwa na serikali 100%, na zaidi kama serikali yake ingekuwa imeweka hizo loop-holes zilizotumika kutoa mikopo mibaya.

..lawama anazopewa Bush ni za kukataa ushauri bali alipoonywa kwamba kuna matatizo.

..wakati wa Nyerere chama kilikuwa kimeshika hatamu. serikali ilikuwa inatekeleza maamuzi ya chama. Nyerere alikuwa mwenyekiti wa chama na mkuu wa serikali. fikra zake zilikuwa zikidumishwa wakati wote.

..katika mazingira kama hayo unataka nani abebe lawama mambo yakienda kombo???

..unataka Kawawa ndiyo awajibike??
 
Hata mimi huwa nawaza katika "FIKRA" za Mwanakijiji sijui Nyerere alikosea wapi? Maana yeye kila siku hapa huwa anamtetea Nyerere kwa uwezo wake wote huku akikiri kuwa alikuwa (Nyerere) na mapungufu yake. Tuambie mzee makosa ya Nyerere ktk utawala wake ni yapi?
 
Finally, somebody asked me!

a. Nyerere aliamini mno watu kuwa wote walikuwa wanaitakia mema Tanzania na hivyo akawaamini kukamilisha mambo mengi. Hili lilitugharimu sana kwa sababu leo hii wale wale aliowamini na ambao waliiharibu nchi bado wako madarakani na wameanza kurithisha watoto wao nafasi. Hata hivyo ukweli ni kuwa he had to work with whatever he had sijui short of asking for wataalamu toka Sweden Nyerere angetoa wapi wasaidizi. Hilo ndilo lilikuwa tatizo kubwa kama Rais wa Kwanza..

b. Taifa lilikuwa halikujiandaa kuwa huru hivyo hatukuwa na wasomi wa kutosha na watendaji wa kutosha katika serikali hivyo tuko huru lakini kimawazo na kiutendaji hatukuwa huru hivyo wengi waliopewa madaraka hawakuwa na uwezo, elimu na ufundi wa kuongoza taasisi au idara nyeti. Hivyo tungechelewa kupata uhuru kwa sababu tofauti na nchi nyingine sisi hatukuwa koloni. Tungejadiliana na Waingereza kuandaa "A Plan for Independence" na tungepata uhuru may be at the end of sixties badala ya kudandia treni la uhuru.

Hili lingefanyika mazingira ya kisiasa ya eneo letu yangekuwa tofauti sana. Hivyo kosa la kuharakisha Uhuru (ingawa nakumbuka aliwahi kutoa ofa ya kuchelewesha uhuru lakini si kwa sababu niliyosema hapo juu)

c. Kosa lake la tatu ni kwenye Azimio la Arusha. Siyo Azimio lenyewe jinsi lilivyo au kanuni ilizolitangaza bali mguso wake katika jamii. Lilidumaza sana private investment na it was overreaching and over bearing. AR lililikuja na kanuni muhimu sana kwa Taifa lakini lilipoenda kutekelezwa liligusa vitu vingi na visivyo vya msingi (kama Kutaifisha Mashamba ya Mkonge kama JokaKuu ulivyosema hapo nyuma). Naamini kulikuwa na ulazima wa kutaifisha vitu fulani lakini not to the extent of what happened; na kama si kutaifisha ingeweza pia kufanya kile cha kuingia Ubia. So in hindsight nadhani hilo lilikuwa kosa.
 
Mwanakijiji,

..posting yangu hapo juu nimeituma kabla kusoma posting yako.

..naona mtu mwingine yeyote akisema Mwalimu alikosea ktk hili au lile basi huishi kulaumu.

..naomba basi utueleze kwa mtizamo wako Mwalimu alikosea wapi, na anawajibika kwa lipi ktk utawala wake.

Tatizo wanaposema "alikosea" wana oversimplify the truth kiasi kwamba the argument turns out to be absurd when looked closely.

NB:

..mfano wako wa morgage crisis una matatizo kidogo. hauendani na mazingira ya Tanzania ya wakati wa Baba wa Taifa.

Believe me kanuni za uchumi zinatawala wakati wowote ule. Na jinsi uchumi wa dunia ulivyofungamana usishangae hali ikawa ngumu kutokana na kuongezeka kwa bei ya mafuta sasa hivi au hudhani hilo linaweza kutuathiri kiuchumi na lisingeathiri uchumi wakati wa Nyerere?
..ktk morgage crisis kuna mabenki binafsi, halafu kuna loop-holes ktk sheria[serikali], speculators, na innocent individuals.

..Bush angebeba lawama zote kama mikopo ingekuwa imetolewa na mabenki yanayomilikiwa na serikali 100%, na zaidi kama serikali yake ingekuwa imeweka hizo loop-holes zilizotumika kutoa mikopo mibaya.

Sasa kwanini serikali inaingilia kati kama vile ni serikali ya Kijamaa? Si benki yao kuu imemwaga fedha zaidi.. si wao leo wametoa mpango wa kusaidia watu walipe mikopo? Kwanini serikali isikae pembeni? Una uhakika gani kuwa huko mbeleni watu wakalaumu kwanini serikali iliingilia kati?

..lawama anazopewa Bush ni za kukataa ushauri bali alipoonywa kwamba kuna matatizo.

..wakati wa Nyerere chama kilikuwa kimeshika hatamu. serikali ilikuwa inatekeleza maamuzi ya chama. Nyerere alikuwa mwenyekiti wa chama na mkuu wa serikali. fikra zake zilikuwa zikidumishwa wakati wote.

..katika mazingira kama hayo unataka nani abebe lawama mambo yakienda kombo???

..unataka Kawawa ndiyo awajibike??

Mtu abebe lawama anazostahili lakini ya kubebesha lawama alimradi abebe lawama ni kucheza kidali po ili apatikane mtu wa kulala nacho!
 
Mwafrika wa Kike,
Kwanza kabisa naomba unisamehe kwa hoja na swali langu, maana mie bado ni mgeni hapa JF. Nianze na swali. Nimevutiwa na title yako, "mwafrika wa kike". inagusia mapambano, maana neno "mwafrika" kwa kawaida huwa halihusishwi na jinsia, katika matumizi ya kawaida. ile punchline yako pale chini "well behaved women never make history" kwa upande mwingine inapunguza kidogo speed ya mapambano. unajua mapambano ni mapambano na wanasema vita havina macho. mfano wengi huwa wanapinga pale wapigania uhuru/ukombozi wa Mwafrika, walipotumia mtutu wa bunduki. wanasema huwezi kuhalalisha mauaji kwa namna yoyote. lakini wengine wanasema "everything is on the table", njia yoyote ni halali. sasa kwenye mapambano wanaomake history nadhani ndio hao ambao hawana time sana na kuwa "well behaved" maana utakuwa well behaved kwa macho ya nani? kwa hiyo hapo naona kama contradiction kidogo, lakini inanivutia maana unaleta hoja ya mapambano ya kistaarabu. Nimeona majibizano yako na "mwafrika" (huyu hana jinsia, anaweza kuwa jike, dume au hata jikedume - samahani mwafrika, sina nia mbaya, utandawazi si unajua tena)hayo majibizano yanaonesha pia ustaarabu fulani. nitapitia thread za nyuma ili nione ukweli wa hoja ya mwafrika kwamba wewe ni mvuruga mada. kwa sasa nakupongeza kwa ujasiri wako, aluta continua!
 
Finally, somebody asked me!

a. Nyerere aliamini mno watu kuwa wote walikuwa wanaitakia mema Tanzania na hivyo akawaamini kukamilisha mambo mengi. Hili lilitugharimu sana kwa sababu leo hii wale wale aliowamini na ambao waliiharibu nchi bado wako madarakani na wameanza kurithisha watoto wao nafasi. Hata hivyo ukweli ni kuwa he had to work with whatever he had sijui short of asking for wataalamu toka Sweden Nyerere angetoa wapi wasaidizi. Hilo ndilo lilikuwa tatizo kubwa kama Rais wa Kwanza..

b. Taifa lilikuwa halikujiandaa kuwa huru hivyo hatukuwa na wasomi wa kutosha na watendaji wa kutosha katika serikali hivyo tuko huru lakini kimawazo na kiutendaji hatukuwa huru hivyo wengi waliopewa madaraka hawakuwa na uwezo, elimu na ufundi wa kuongoza taasisi au idara nyeti. Hivyo tungechelewa kupata uhuru kwa sababu tofauti na nchi nyingine sisi hatukuwa koloni. Tungejadiliana na Waingereza kuandaa "A Plan for Independence" na tungepata uhuru may be at the end of sixties badala ya kudandia treni la uhuru.

Hili lingefanyika mazingira ya kisiasa ya eneo letu yangekuwa tofauti sana. Hivyo kosa la kuharakisha Uhuru (ingawa nakumbuka aliwahi kutoa ofa ya kuchelewesha uhuru lakini si kwa sababu niliyosema hapo juu)

c. Kosa lake la tatu ni kwenye Azimio la Arusha. Siyo Azimio lenyewe jinsi lilivyo au kanuni ilizolitangaza bali mguso wake katika jamii. Lilidumaza sana private investment na it was overreaching and over bearing. AR lililikuja na kanuni muhimu sana kwa Taifa lakini lilipoenda kutekelezwa liligusa vitu vingi na visivyo vya msingi (kama Kutaifisha Mashamba ya Mkonge kama JokaKuu ulivyosema hapo nyuma). Naamini kulikuwa na ulazima wa kutaifisha vitu fulani lakini not to the extent of what happened; na kama si kutaifisha ingeweza pia kufanya kile cha kuingia Ubia. So in hindsight nadhani hilo lilikuwa kosa.

Kwa hiyo ktk miaka yote hiyo aliyokaa madarakani ni makosa matatu tu aliyofanya?
 
Back
Top Bottom