Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Wakati Nyerere anachukua nchi alikuwa na watu walioelemika kiasi gani kupewa utawala wa kitu chochote? Ni wangapi walikuwa wamesomea utawala, biashara, banking n.k... nadhani Mwalimu angeomba wazungu na wahindi waliokuwa wasomi waiendeshe nchi kwa miaka kadhaa wakati tunaandaa wasomi wetu... au angechelewesha kidogo kudai uhuru hadi kama miaka ya themanini hivi.
 
Mindi,
hamna la maana lolote ktk post yako ndeeeeefu kama treni!!! mtoto wa darasa la tano wakati ule wa Nyerere, alikuwa anaweza kuandika uloandika hapo juu.........

kwahiyo unataka kutuambia kwamba Nyerere alikuwa na uwezo wa ki-mungu!!! kama yeye alikuwa starring wa kuona mbali, ikawaje akampigie debe fisadi Mkapa kuwa raisi!!! yaaani umekaa kipropaganda mno, ni vigumu kukuchukulia serious!!

Kaka inaelekea ama unamjua mindi hivyo unaprejudice na mitazamo yake ama ur another simple minded bongoist ambaye huamini kuwa mtu wa kawaida anaweza kufikiri kwa mapana zaidi kama ulivyo wewe......

Tanzanianjema
 
Wakati Nyerere anachukua nchi alikuwa na watu walioelemika kiasi gani kupewa utawala wa kitu chochote? Ni wangapi walikuwa wamesomea utawala, biashara, banking n.k... nadhani Mwalimu angeomba wazungu na wahindi waliokuwa wasomi waiendeshe nchi kwa miaka kadhaa wakati tunaandaa wasomi wetu... au angechelewesha kidogo kudai uhuru hadi kama miaka ya themanini hivi.

Are you trying to imply that tulilosti kwa vile hatukuwa na wasomi?
 
operation chaos kama ya Limbaugh........unakumbuka huyu jamaa alifanya nini kwenye mada ya kambona je historia itampa??
si yeye alitaka ifungwe?? akapiga majungu mpaka ikaamishwa toka jukwaa moja mpaka lingine?? hivi kuna tofauti gani kati ya yanaongewa hapa na kwenye ile mada!!??.... au kila kitu mpaka yeye tu akitaka kiwe ndio kiwe!!??
....ebu fikiria kwa kina kidogo ndugu yangu, haya mambo ya kuburuzana mpaka lini??? sie wengine sio ma-soldier by design, labda ndio maana tunakuwa hatuelewani na "the chosen ones."

kuhusu elimu, hivi nyerere alianzisha vyuo vikuu vingapi Tanzania!!?? aliwaenzi vipi wasomi? waarusha walipotaka kuanzisha 'versity miaka ya sitini, je ni nani aliyeweka mguu!?? mambo mengine bwana....nyerere alipokea system nzuri tu ya elimu toka kwa mkoloni, akashindwa kuindeleza na hatimaye kuvuruga kila kitu!!!

asante kwa ushauri wako bwana Ngabu, labda hii inaweza kuwa post yangu ya mwisho ktk mada hii iliojaa upuuzi!! LOL, bwahahahahahahahaha.

Ahahahahahaaaa....sasa hii operation chaos yako hapa objective(s) ni nini? Mwenzako Limbaugh anataka Barry na Mama wararuane ili ikifika Novemba wawe wamerahisisha kazi ya GOP....halafu Mac aingie kiulaini pale 1600 Penns. Ave...
 
YournameisMine,
Mkuu maadam umeniuliza nitakujibu kwamba pamoja na yote hayo nadhani Lugha unayotumia mkuu ni nzito!..haiwezi kuwa Shakespearian, labda wetu yule Tegesa Machumuirian! haaa haaa haaa!
 
Akina Mindi na wenzako !!!

Mimi sitaki kuwaadress kama wapiga propaganda. Ila naona nisiwaache bila darasa kidogo kumhusu Mwalimu Nyerere na uongozi wake 1961 - 1985. Najua utakuwa ukisubiri nikueleze kwa undani jambo moja moja ambalo Mwl alifanikiwa dhidi ya yale aliyokosea. Hilo sitafanya, ila nitakupa nahau kidogo ya kukulazimisha utafakari hoja yako dhidi ukweli halisi.

Mwalimu Nyerere ni mmoja wa viongozdi wengi wa Afrika ambao walikuwa na uwezo mkubwa wa kuwatawala bila upinzani watu wa nchi zao. Ninamtafakari Nyerere kama kiongozi aliyefanikiwa sana katika mambo kadhaa ikiwepo kuongozi harakati za ukombozi si tu Tanzania bali sehemu kubwa ya Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara.

Pamoja na mafanikio hayo na mengi ambayo si rahisi kuyataja haraka haraka hapa ni lazima nionyeshe jinsi udhaifu mmoja wa Nyerere unavyotugharimu hadi leo.

Mwalimu Nyerere alikuwa hawezi kukaa meza moja na mtu anayempa changamoto. Hii ilimfanya awafukuze hata wasomi kadhaa ambao tulikuwa nao mara baada ya uhuru kwa kuwa tu walionyesha kumpa changamoto.

Mwalimu alivijenga vyama vya siasa alivyoanzisha kwa mtindo ambao vingemheshimu na kumtii bila kuhoji alichofanya wala kutengua anachopanga.
CCM ya sasa inasemwa sana kuwa imeacha mwenendo wa Nyerere. Mimi nikuhakikishieni kuwa CCM imeacha tu mwelekeo wa kijamaa wa Nyerere. Lakini tabia za kuhodhi madaraka, kujiona miungu watu, siasa za kulindana, kupeana madaraka kwa fadhila, chuki na hujuma dhidi ya upinzani, ukabila wa kichini chini, siasa kuamua namna uchumi wa nchi utakavyoendeshwa na mengi mengi yanayotokea sasa yalizaliwa enzi za uongozi wa Nyerere. Kwa hiyo udhaifu wa CCM wa sasa hauwezi kutengwa kabisa na Mwl. Nyerere.

"Mti hutambuliwa kwa matunda yake"
Mwalimu alipanda mti, akaunyeshea, akaulinda usiharibiwe na yeyote. mti ukakua. Na sasa unazaa matunda. Sasa kama matunda yake ni machungu kwa nini mnajitahidi kuonyesha kuwa huo mti haukupndwa na mtu mzuri msiyetaka achafuliwe?? Mwembe huzaa maembe: Mpapai huzaa mapapai. Mchungwa huzaa machungwa. Ukiona ndimu basi limetokana na Mndimu na si Mwembe. Kama Mwl alitaka Maembe asingepanda mti wa ndimu. HAKWEPI LAWAMA HAPA!!

Inawezekana ndugu zangu ninyi hamna hata habari kuwa asili ya kushindikana kwa zoezi la kutengeneza katiba muafaka kwa mazingira ya siasa ya vyama vingi Tanzania ni Mwl. Nyerere.

Na inawezekana pia kuwa hamjui kuwa katiba yetu inatoa mianya kwa mafisadi kujiporea rasilimali za nchi yetu wanavyoona wenyewe yafaa ili mradi tu wakiimarishe chama cha Mwalimu.

Mngekuwa mnayaona hayo, basi mngegundua pia kuwa umasikini wetu unaanzia kwenye mianya ya katiba na mfumo mbaya wa Siasa na Uchumi wa nchi.

Kama binadamu wa kawaida sioni ufahari kumkejeli Mwl. wakati huu ambao hayuko nasi, wala sioni vema kumvunjia heshima mtu ambaye ametangulia mbele ya haki. Kikwetu kila mtu anapotutoka tunamwagia sifa kem kem.

kwa hiyo ndugu yangu uliyeanzisha hoja hii amini kabisa kuwa mimi sina mpango wa kumvunjia heshima Mwalimu bali nataka kukushawishi ujue kuwa matunda tunayokula ya CCM leo yametokana na mti aliopanda Mwl. Na kabla hujaleta hoja jukwaani nakuomba sana uifanyie utafiti. Usilete hoja tukakufikiria kuwa umetumwa na watu wachache. wanaotaka kuharibu ukweli wa historia ya nchi yetu.

Tchao
 
Yournameis Mine,
binafsi sintapenda kuingia ktk ubishi wenu isipokuwa umeniuliza mwenyewe kuhusu lugha yako..Assume wewe ni daktari uliyetaka ushauri wa daktari mwingine sasa nikisema nje ya jibu ulotegemea utaniona Dr. House..mwenzako nazijua symptoms za retinopathy tofauti na mtu aliyepigwa mchanga wa macho!..
 
Mwalimu Nyerere alikuwa hawezi kukaa meza moja na mtu anayempa changamoto. Hii ilimfanya awafukuze hata wasomi kadhaa ambao tulikuwa nao mara baada ya uhuru kwa kuwa tu walionyesha kumpa changamoto.

Sasa na wewe unakuja na kauli ambayo inatakiwa ichukuliwe kama factual. Ni wasomi gani "kadhaa" ambao tulikuwa nao baada ya uhuru na walifukuzwa kwa kumpa "changamoto". Na kuna ukweli gani kuwa Nyerere hakuweza "kukaa meza moja" maana sisi wengine tunakumbuka sana mijadala ya Chuo Kikuu ambayo hata Kikwete hawezi hata dakika moja kwenda pale Nkrumah (well anaweza baada ya kumuweka Mukandala)...

Mwalimu alivijenga vyama vya siasa alivyoanzisha kwa mtindo ambao vingemheshimu na kumtii bila kuhoji alichofanya wala kutengua anachopanga.

Once again, vyama vya kisiasa alivyovianzisha. Hivi hujui kuwa kuna watu walimpinga na kuna maamuzi yaliyobadilishwa? Inabidi urudi kwenye historia tu usiwe kama mtu mmoja humu anayetoa kauli za kuhukumu bila ushahidi wowote japo wa mantiki.
CCM ya sasa inasemwa sana kuwa imeacha mwenendo wa Nyerere. Mimi nikuhakikishieni kuwa CCM imeacha tu mwelekeo wa kijamaa wa Nyerere. Lakini tabia za kuhodhi madaraka, kujiona miungu watu, siasa za kulindana, kupeana madaraka kwa fadhila, chuki na hujuma dhidi ya upinzani, ukabila wa kichini chini, siasa kuamua namna uchumi wa nchi utakavyoendeshwa na mengi mengi yanayotokea sasa yalizaliwa enzi za uongozi wa Nyerere. Kwa hiyo udhaifu wa CCM wa sasa hauwezi kutengwa kabisa na Mwl. Nyerere.

Kuna uliyoyasema hapa ambayo naamini yana ushawishi wa ukweli. Hata hivyo madai ya rejareja kama tabia kadhaa zinazoendelea sasa ni matokeo ya Nyerere kunathibitisha vitu vichache; moja hakuna kiongozi ndani ya CCM ambaye yuko mbali na mweleko wa "kinyerere". Lakini hilo la kudai kuwa "siasa kuamua namna ya uchumi wa nchi unavyoendeshwa" ni mojawapo ya madai yasiyo na msingi. Dunia nzima ni siasa ndiyo inayoamua namna ya uchumi wa nchi unavyoendeshwa na ni wanasiasa wanaoamua nchi inaendeshwaje.

"Mti hutambuliwa kwa matunda yake"
Mwalimu alipanda mti, akaunyeshea, akaulinda usiharibiwe na yeyote. mti ukakua. Na sasa unazaa matunda. Sasa kama matunda yake ni machungu kwa nini mnajitahidi kuonyesha kuwa huo mti haukupndwa na mtu mzuri msiyetaka achafuliwe?? Mwembe huzaa maembe: Mpapai huzaa mapapai. Mchungwa huzaa machungwa. Ukiona ndimu basi limetokana na Mndimu na si Mwembe. Kama Mwl alitaka Maembe asingepanda mti wa ndimu. HAKWEPI LAWAMA HAPA!!

Mfano mzuri sana hapa, tatizo ni kuwa mti hukua unapopandwa! kama udongo hauna rutuba na hata mtu akitumia mbinu gani wakati mwingine mti haukui! Lakini wakati mwingine mtu anaweza akapanda vizuri mti wake lakini "akaja adui naye akapenda magugu"!

Inawezekana ndugu zangu ninyi hamna hata habari kuwa asili ya kushindikana kwa zoezi la kutengeneza katiba muafaka kwa mazingira ya siasa ya vyama vingi Tanzania ni Mwl. Nyerere.

Wewe unayejua utuambie miaka karibu nane tangu afe na ishirini na ushee tangu aachie madaraka mbona tumeshindwa. Na nikuhakikishie kwa kuendelea kumlaumu Nyerere usitarajie Katiba mpya. Angalia mada moja hapa inayomhusu mama Nagu aliyesema mwaka jana kuwa "hakuna haja ya Katiba mpya". Nyerere alimpanua mdomo kusema? Muulize kiongozi yeyote wa CCM akuambie kama ipo haja ya Katiba mpya...!

Na inawezekana pia kuwa hamjui kuwa katiba yetu inatoa mianya kwa mafisadi kujiporea rasilimali za nchi yetu wanavyoona wenyewe yafaa ili mradi tu wakiimarishe chama cha Mwalimu.

Yote hayo yanajulikana lakini Nyerere hayupo CCM leo; wabebeshe mzigo wahusika. Mwisho mtamlaumu Nyerere kwa Rada, Richmond, Buzwagi, Posta, NBC n.k!

Mngekuwa mnayaona hayo, basi mngegundua pia kuwa umasikini wetu unaanzia kwenye mianya ya katiba na mfumo mbaya wa Siasa na Uchumi wa nchi.

Mbona hayo yote yanajulikana? Tatizo kwanini CCM wanashindwa kubadilisha mambo hayo wakati Nyerere hayupo? Hivi unambebesha Mwinyi, Mkapa, na Kikwete lawama zozote za yale yanayoendelea hivi sasa? Kila mtu hubeba mzigo wake mwenyewe! Hivi mnataka Nyerere atoke kaburini kuja kutueleza kuwa kuua maalbino ni vibaya? Hivi Nyerere atoke kaburini na kutuambia kuna haja ya kujenga mitaro safi ya maji machafu? Unataka Nyerere atoke kaburini na kutuambia kuna haja ya kujenga shule zenye vyoo bora?

Kama binadamu wa kawaida sioni ufahari kumkejeli Mwl. wakati huu ambao hayuko nasi, wala sioni vema kumvunjia heshima mtu ambaye ametangulia mbele ya haki. Kikwetu kila mtu anapotutoka tunamwagia sifa kem kem.

Huo huitwa unafiki; yaani kumpa mtu sifa asizozistahili. Bora uwe kama YNIM kwa sababu yeye hana chema chochote cha Nyerere na hilo tumelikubali. Kama unaona Nyerere alikuwa hivi au vile sema tu usiogope au kumvisha kilemba cha ukoka.

kwa hiyo ndugu yangu uliyeanzisha hoja hii amini kabisa kuwa mimi sina mpango wa kumvunjia heshima Mwalimu bali nataka kukushawishi ujue kuwa matunda tunayokula ya CCM leo yametokana na mti aliopanda Mwl. Na kabla hujaleta hoja jukwaani nakuomba sana uifanyie utafiti. Usilete hoja tukakufikiria kuwa umetumwa na watu wachache. wanaotaka kuharibu ukweli wa historia ya nchi yetu.

Hivi unafikiri Nyerere alianza kuvunjia heshima leo au jana? Ukifanya hivyo utakuwa kwenye msururu wa watu wengine waliotangulia kabla yako na huo ndio uzuri wa uhuru wa maoni.

Nyerere aliupanda mti katika ardhi aliyopewa; aliupanda mti kwa utaalamu aliokuwa nao na kwa kutumia mbinu alizokuwa nao. Mti umekuwa na sasa tunaanza kuvuna matunda yake tunaanza kumlaani mpanzi ati kwa sababu mbona kuna magugu pembeni? Mbona hakung'oa magugu yote, mbona hakutuchumia matunda na kutusindikia; Yaani kwa mawazo yako Nyerere angefanya kila kitu ili wewe na mimi tubweteke na kula jasho la kazi ya Mwalimu!

Hayo ni mawazo ya watu wavivu. Jukumu lako na langu ni kuona wapi mwalimu alishindwa na kutengeneza kuanzia hapo badala ya kulia kuwa "mwalimu alipanda mtu mbovu mbona sasa tunakula matunda mabovu". Kama unaamini mti ulipandwa ni mbaya, ung'oe panda mwingine!

Nyerere asingeweza kupanda, kumwagilia, kutia mbolea, kuhamia ndege n.k halafu baadaye achume mazao na kutuwekea ghalani na tungemwomba atutengenezee chakula na sisi kama makinda yaliyodekezwa tupanue midomo yetu na kula tu! Hivi katika maelezo yako yote hayo Nyerere alikuwa anafanya kazi peke yake? Hivi muda wote huo Nyerere alikuwa anatembea kila kijiji, kila mkoa na kila nyumba kuangalia watu wanatendaje kazi? Ni kwa kiasi gani wasaidizi au watu wenyewe walishindwa kuteleleza majukumu yao? Je hali iliyopo sasa inaweza kuelezewa kuwa ni matokeo ya mchanganyiko wa sababu za mbalimbali na Nyerere ni mojawapo ya sababu hizo? au katika mawazo yako Ni Nyerere tu ndiye mbaya wa Tanzania kama anavyoamini YNIM?

Hata Yesu mwenyewe alishindwa kufikisha ujumbe wake kwa watu wote lakini akawatuma wengine wafanye kazi kwa niaba yake; Vivyo hivyo Mohammed naye ni mpaka alipokufa ndio kiini cha ujumbe aliopewa ndivyo ulivyoenezwa na wafuasi wake. Lakini je ujumbe wa wote wawili umefika leo hii bila kupitia wakati mgumu au hata kugawanyika? Je kwa sababu leo tunaona matatizo katika Ushia au Usunni, Ukatoliki au Uprotestanti maana yake Nyerere na Muhammad ndio waliopanda mbegu mbovu ambazo zimezaa matunda mabovu? Je ni kwa kiasi gani mapadre na watawa wanaolawiti watoto wadogo au maghaidi wanaojilipua na kuua watu bila hatia wanawajibika kwa vitendo vyao wao wenyewe?

Kuna wakati lazima ujifunze kuwajibika kwa matendo yako mwenyewe na vivyo hivyo watu wengine nao wawajibike kwa matendo yao wenyewe.
 
.......au ndio jaribio la makusudi la kujipendekeza kwa CCM iliwakupe ulaji?? maana from nowhere, Nyerere this, Nyerere that....utafikiri kuna jipya ambalo limegunduliwa leo juu ya huyu bwana, ambalo lilikuwa halijulikani!!!!
aibu sana, pale watu wazima(tena wajuaji wa mambo) wanapojitoa akili ili ku "pitch" kwa faida binafsi!!!.

I hope CCM wamekusikia, inshallah, labda watakuita kundini......

Njombi mbona una hasira hivyo na Nyerere...it's almost as if it's personal. Alikukosea nini lakini hadi umchukie hivi?

Yaani kutwa nzima unam-trash mzee wa watu...come on man...
 
"....as if its personal"!?? it is personal, I religiously hate the guy!!....it is a family affair, kuna vitu huyu babu alikosea sana. sijui mungu atam-judge vipi!!?? but I hope he's in hell right now, burning 24/7......

Lawd Hammercy!!! Are you serious?
 
Basi tumeshafahamu ukweli kumbe personal... Duh pole sana, bahati mbaya mzee wetu anajirusha na Hurulain.
 
Duh! I love Jambo Forums where we dare kumkoma nyani mchana kweupeeeee!

Yaaani haogopwi mtu hapa, wala kiongozi ni maweee tuuuu, duh! Ndugu yangu YRMN, imetosha mkuu, lakini I got you bro! damn!
 
Basi tumeshafahamu ukweli kumbe personal... Duh pole sana, bahati mbaya mzee wetu anajirusha na Hurulain.

Hii mbona imeonekana mapema sana hapa? Personal issues ndizo zinadrive matusi na sio facts
 
Field Marshall Es,
Mawe ya jamaa yetu ni ya kusimuliwa kwani hukumu ya kipofu haiwezi badilisha umbo la Tembo!..
Nyerere is large na Mungu mwenyewe katuonyesha ktk mazishi yake, wanaomwombea pepo ni kuliko urefu wa ulimi wake..dua zake zitaishia urefu wa sauti yake..
Mwenzetu yeye sana sana watajaa nzi!..(sijatukana) Naomba anielewe hivyo.
 
Ukweli huu mzito!!

Hapa ndipo umegongomelea msumari; watu hawataki kufikiri! wanataka kuchukua vitu at face value kama YNIM ambaye uchungu wake wote na Nyerere umetokana na Babu yake kunyang'anywa nyumba ya bati or something...

Mwanakijiji,

Sasa wewe mbona unaleta utani wa ukweli?😉
 
Back
Top Bottom