"Maendeleo hayana chamaa"...


Uhuru Wa vyombo vya habari "....... Masud ananichora kichwa kimebonyea hadi naenda kujiangalia kwenye kioo kama ni kweli"........
 
Tanzania ni tajiri, sihitaji mikopo na misaada, siku si nyingi tutaanza kutoka misaada na mikopo kwa nchi zingine
 
Buku tano ni za..............................
Gadafi ni raisi wa ............................

Katika dunia ya sasa hakuna kitu kinaweza kupotea ili mradi kimewahi kutamkwa mbele ya jamii. Lakn pia tunaweza kupoteza vitu admu pale tu tutakaposhindwa kuweka kumbukumbu kwa vizazi vijavyo na vya sasa. Kwa kipindi kirefu tumekua na nukuu za Baba wa Taifa mwalimu nyerere. Ni wakati mwafaka kuweka kumbumbuku ya maneno mazuri ya mheshimiwa Rais Magufuli.

Duniani tuna nukuu (quotes) zawa watu maarufu kama Martn Luther king, Jr. Abraham lincoln na wengine wengi. Kwa hapa kwetu tuna nukuu za baba wa taifa mwalim Nyerere.

Sasa ni wakati mwafaka kuweka nukuu zake kwenye uzi huu. Usihofu iwe mbaya masikio mwako au iwe nzuri wewe weka tu maana lolote analo litamka mkuu wa nchi linapaswa kutunzwa.

Naweka maneno mawili matatu kuanzisha ukurasa wa maneno ya mkuu wetu.

Mimi ni raisi wa maskini wanaoshi kama malaika wataishi kama mashetani

serikali yangu haitawapa chakula Kila mtu atabeba msaba wake njaa haijaletwa na serikali

hakuna serikali iliyowahi kujenga nyumba za wahanga duniani pote. Nasisi hatujengi.

hakuna kufanya za siasa mpaka 2020 siasa huzuia maendeleo

siwezi kuwashirikisha wapinzani kwenye serikali yangu. Nakushangaa sheni kuwaingiza wapinzani

sijawahi kutamka katiba kwenye kampeni zangu za kuomba urais , katiba sio kipaumbele changu kwa sasa nainyoosha nchi kwanza

police mkukita mtu anaendesha gari kwenye njia ya mwendo kasi ng'oa tairi uzeni

watoto watasomeshwa bure kwenye utawala wangu hivyo fyatueni watoto wengi maana watasoma bure

Haya ni machache kati ya mengi aliyowahi kuyaongea . Ni wakati mwafaka kuweka maneno yake hapa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom