mfumo, kichwa chako kinafanya kazi lkn sio kazi nzuri. Mimi siko kwenye hoja yenu ya udini lkn nikukosoe kidogo kuhusu 'uzuri' wa mipango ya huyo mjombaako hadi umnadi kuwa kufanya mambo makubwa kwa jamii.
NSSF isomeke kwako kama National Social Security Fund yaani Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii.Lengo la uanzishwaji wa mifuko ya mfumo huu ni USTAWI wa JAMII.
Mifano yako ya uzuri wa Bwana Dau ni chukizo kwa wanachama maskini wa mfuko, kwa sababu ujenzi wa madaraja na vyuo vikuu ni kazi ya serikali na sio NSSF. Nikukumbushe kuwa, ustawi unaopaswa kusimamiwa na NSSF ni wa individual member na sio daraja la Kigamboni.
Ukihitimisha hoja yako mfu, umethubutu kulinganisha Deadly NSSF na mifuko mingine kiasi cha kuiita ni yenye vikao vya kula kitimoto. Hapo ndio unadhihirisha ukomo wa ubongo wako kuwaza.
Ingia kwenye tovuti ya PSPF, utakutana na tangazo la ONDOA STRESS, ONGEZA ASSETS. Ule ndio ubunifu ambao Mzuri Dau wako na NSSF wamekosa. Mwambie Dau akajifunze toka PSPF namna ya kuwahudumia wanachama wa NSSF badala ya kuihudumia serikali ambayo inakopesheka kwenye taasisi nyingine.
Watanzania wengi (hasa walioko NSSF) ni watu wa kipato cha chini, hawakopesheki kwenye taasisi za fedha sababu hawana dhamana. PSPF imetoa fursa kubwa na ya kupongezwa inayomuwezesha mnyonge kutumia amana yake iliyoko kwenye mfuko kumiliki ardhi, huu hasa ndio utumishi kwa jamii ambao unaleta natumaini. Wakati PSPF inawafaidisha wanachama wake kuona faida ya amana zao, NSSF iko bize na miradi isiyo na direct impact kwa watu wa kipato kidogo.
Kama DAU ni mjombaako, tafadhali mwambie kwamba, ni jambo linalotia uchungu kwenda Benki kukopa 5m ili ununue kiwanja ukakataliwa kwa kuwa huna dhamana at the same time unayo maana yako NSSF mara mbili ya kiasi unachotaka kukopa lkn huwezi kuikopa wala haiwezi kutumika kukudhamini badala yake inakopeshwa serikali ambayo inavyo vyanzo vingi vya mapato na dhamana.
Dau akiendelea kuiongoza NSSF, sisi wanachama wa NSSF tutaendelea kuwa wapangaji kwenye nyumba za wanachama wa PSPF. Najua hapa unaweza ukaleta ngonjera ya mikopo ya NSSF kupitia SACCOSS, ashakhum si matusi....uhuni ule. Saccoss ni kiini macho na huwezi kunigroup na watu wasio na shida inayofanana na ya kwangu.
Tukiliacha hili la kukosa ubunifu, uwajibikaji kwa wafanyakazi wa NSSF ni hiyari. Huu ndio mfuko ambao staff wake Hawana muda wa kuingiza entry za michango ya wanachama kwenye mfumo wa komputa. Ukienda kuangalia salio lwako, utakuta kuna entry mbili tatu za miaka ya nyuma, wanachofanya ni kukupa adjustment form umpelekee muajiri wako. Kwa maana hiyo wanategemea taarifa toka kwa muajiri wao database yao ni maandazi na chai yenye hiliki. Sasa ikiwa taarifa za michango yangu wao wanazitaraji kutoka kwa mwajiri, ikiwa michango yangu haipelekwi, kuna anayejua na kuchukua hatua kweli? Hapa ndio napata mashaka kuwa, upo uwezekano kweli ajira pale ni za namna ya kufahamiana badala ya kulenga uwajibikaji.
Nakuhakikishia kwamba, siku sheria kandamizi za nchi hii zikijaruhusu mwanachama kuhama kutoka mfuko mmoja kwenda mwingine, watu wengi watachagua fedha zao ziwawezeshe wao wenyewe kumiliki asset na sio kujenga madaraja.
Kwa kumalizia, kuhusu kitimoto na bia, nikwambie kwamba, mifuko mingine hii inapotangaza kuwa unapata FAO la kuanzia maisha haitanii, kweli unapata, tena fasta.
Mimi ni mhanga wa Dau kukosa maono na ubunifu. Fedha zangu hazininufaishi, Dau anataka akae nazo hadi wakati atakaponipa uwezo wangu usiwe wa kiuwekezaji bali zitumike kununulia sanda ya kuzika mwili wangu.
Mwambie mjombaako,
Mwana Mtoka Pabaya naye anatamani kumiliki kiwanja kilichopimwa kama anavyomiliki Ally Mzee, mwanachama wa PSPF, daraja la Kigamboni kwangu halina maana kwa kuwa hata ningetaka kwenda huko kukodi Shamba la kulima matikiti, serikali sikivu ya CCM ilishapiga marufuku kuiona pikipiki yangu ikikatiza mjini kwa kuwa inaleta foleni