hekimanyingi
JF-Expert Member
- Jul 12, 2013
- 679
- 573
Wadau,
Kama tunavyofahamu Tanzania ni nchi isiyoongozwa kwa misingi ya dini fulani japokuwa wanaoutuongoza wana dini.
Kwangu mimi naona ni jambo jema endapo hatutaangalia dini zetu ili tupate au kutoa huduma mbalimbali za kijamii. Ni hivi majuzi mfuko wa jamii ya watanzania wote NSSF imetangaza nafasi lukuki za kazi lakini zimo tuhuma ambazo zinatolewa na watu wanaodai ni wafanyakazi na wenginesio wafanyakazi kuwa NSSF kuna udini eti kama hauna 'sigda' haupati kazi au kama wewe si Abubakari au Hamisi haupati kazi.
Tuhuma hizi ni mbaya na kubwa kwa mfuko unaoitwa wa jamii. Eti ili wakuajiri si kwamba umefaulu interview bali kwa majina na dini yako. Ni jambo linalohitaji ufafanuzi na ushahidi wa kutosha aidha kukubali au kukataa kuwa kuna udini au hakuna maana litaleta mpasuko kwa taifa.
Moto wa dini ni rahisi kuuanzisha na kuuchochea lakini ni ngumu kuumaliza. Kesho tutaskia na PPF kuna 'UDINI' Keshokutwa tutaskia mahakamani kuna udini na mwisho itakuwa ni jeshi na ikulu kuna udini huku mamlaka zikiwa kimya.