NSSF tunataka majibu ya tuhuma kuhusu 'udini'

NSSF tunataka majibu ya tuhuma kuhusu 'udini'

Status
Not open for further replies.
mfumo, kichwa chako kinafanya kazi lkn sio kazi nzuri. Mimi siko kwenye hoja yenu ya udini lkn nikukosoe kidogo kuhusu 'uzuri' wa mipango ya huyo mjombaako hadi umnadi kuwa kufanya mambo makubwa kwa jamii.

NSSF isomeke kwako kama National Social Security Fund yaani Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii.Lengo la uanzishwaji wa mifuko ya mfumo huu ni USTAWI wa JAMII.

Mifano yako ya uzuri wa Bwana Dau ni chukizo kwa wanachama maskini wa mfuko, kwa sababu ujenzi wa madaraja na vyuo vikuu ni kazi ya serikali na sio NSSF. Nikukumbushe kuwa, ustawi unaopaswa kusimamiwa na NSSF ni wa individual member na sio daraja la Kigamboni.

Ukihitimisha hoja yako mfu, umethubutu kulinganisha Deadly NSSF na mifuko mingine kiasi cha kuiita ni yenye vikao vya kula kitimoto. Hapo ndio unadhihirisha ukomo wa ubongo wako kuwaza.

Ingia kwenye tovuti ya PSPF, utakutana na tangazo la ONDOA STRESS, ONGEZA ASSETS. Ule ndio ubunifu ambao Mzuri Dau wako na NSSF wamekosa. Mwambie Dau akajifunze toka PSPF namna ya kuwahudumia wanachama wa NSSF badala ya kuihudumia serikali ambayo inakopesheka kwenye taasisi nyingine.

Watanzania wengi (hasa walioko NSSF) ni watu wa kipato cha chini, hawakopesheki kwenye taasisi za fedha sababu hawana dhamana. PSPF imetoa fursa kubwa na ya kupongezwa inayomuwezesha mnyonge kutumia amana yake iliyoko kwenye mfuko kumiliki ardhi, huu hasa ndio utumishi kwa jamii ambao unaleta natumaini. Wakati PSPF inawafaidisha wanachama wake kuona faida ya amana zao, NSSF iko bize na miradi isiyo na direct impact kwa watu wa kipato kidogo.

Kama DAU ni mjombaako, tafadhali mwambie kwamba, ni jambo linalotia uchungu kwenda Benki kukopa 5m ili ununue kiwanja ukakataliwa kwa kuwa huna dhamana at the same time unayo maana yako NSSF mara mbili ya kiasi unachotaka kukopa lkn huwezi kuikopa wala haiwezi kutumika kukudhamini badala yake inakopeshwa serikali ambayo inavyo vyanzo vingi vya mapato na dhamana.

Dau akiendelea kuiongoza NSSF, sisi wanachama wa NSSF tutaendelea kuwa wapangaji kwenye nyumba za wanachama wa PSPF. Najua hapa unaweza ukaleta ngonjera ya mikopo ya NSSF kupitia SACCOSS, ashakhum si matusi....uhuni ule. Saccoss ni kiini macho na huwezi kunigroup na watu wasio na shida inayofanana na ya kwangu.

Tukiliacha hili la kukosa ubunifu, uwajibikaji kwa wafanyakazi wa NSSF ni hiyari. Huu ndio mfuko ambao staff wake Hawana muda wa kuingiza entry za michango ya wanachama kwenye mfumo wa komputa. Ukienda kuangalia salio lwako, utakuta kuna entry mbili tatu za miaka ya nyuma, wanachofanya ni kukupa adjustment form umpelekee muajiri wako. Kwa maana hiyo wanategemea taarifa toka kwa muajiri wao database yao ni maandazi na chai yenye hiliki. Sasa ikiwa taarifa za michango yangu wao wanazitaraji kutoka kwa mwajiri, ikiwa michango yangu haipelekwi, kuna anayejua na kuchukua hatua kweli? Hapa ndio napata mashaka kuwa, upo uwezekano kweli ajira pale ni za namna ya kufahamiana badala ya kulenga uwajibikaji.

Nakuhakikishia kwamba, siku sheria kandamizi za nchi hii zikijaruhusu mwanachama kuhama kutoka mfuko mmoja kwenda mwingine, watu wengi watachagua fedha zao ziwawezeshe wao wenyewe kumiliki asset na sio kujenga madaraja.

Kwa kumalizia, kuhusu kitimoto na bia, nikwambie kwamba, mifuko mingine hii inapotangaza kuwa unapata FAO la kuanzia maisha haitanii, kweli unapata, tena fasta.

Mimi ni mhanga wa Dau kukosa maono na ubunifu. Fedha zangu hazininufaishi, Dau anataka akae nazo hadi wakati atakaponipa uwezo wangu usiwe wa kiuwekezaji bali zitumike kununulia sanda ya kuzika mwili wangu.

Mwambie mjombaako, Mwana Mtoka Pabaya naye anatamani kumiliki kiwanja kilichopimwa kama anavyomiliki Ally Mzee, mwanachama wa PSPF, daraja la Kigamboni kwangu halina maana kwa kuwa hata ningetaka kwenda huko kukodi Shamba la kulima matikiti, serikali sikivu ya CCM ilishapiga marufuku kuiona pikipiki yangu ikikatiza mjini kwa kuwa inaleta foleni
 
Last edited by a moderator:
KakaKiiza pata hekima ya Qur'an hapa, na shukuru unapomuona Kiongozi wa Kiislaam na anafanya Uislaam kwa ukamilifu, juwa huyo hawezi fanya dhulma.

Mwisho hapo chini Dalai Lama anamalizia kwa wale wanao hangaika na tamaa za kidunia !

'Wala msifanye viapo vyenu ni njia ya kudanganyana baina yenu. Usije mguu ukateleza badala ya kudhibiti, na mkaonja maovu kwa sababu ya kule kuzuilia (haki) Njia ya Mwenyezi Mungu na mkapata adhabu kubwa.

'Wala msinunue ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa thamani ndogo. Hakika kilichopo kwa Mwenyezi Mungu ndicho bora kwenu, ikiwa mnajua.

'Mlivyonavyo vitakwisha na vilivyoko kwa Mwenyezi Mungu vitabakia. Na kwa yakini Sisi tutawapa walio subiri (watu wasio na tamaa !) ujira wao kwa bora waliokuwa wakiyatenda.

'Mwenye kutenda mema Mwanamume au Mwanamke, tutamhuisha maisha mema, na tutawapa ujira wao kwa bora walio kuwa wakiyatenda.

Qur'an: 16:94-97

attachment.php

 

Attachments

  • Dalai Lama- Health.JPG
    Dalai Lama- Health.JPG
    45 KB · Views: 514
Uongo mwingine hauna kichwa wala miguu.

Kwa kuwa Dau ni Muislaam, basi staff wote wa NSSF ni Waislaam?

Hiyo ni Islamophobia.

dau sio tu kuwa muislam ila mdini na mbaguzi kmanin watu wakandie tu NSSF?kwan ndo taasis pekee inayoongozwa na muislamu?
 
Kuna Kazi zilitolewa July za operation officers mpaka leo hawajaita watu....hii inakaaje?

Lazima watu waamini hizo tuhuma.

"Mi huwa nasema ni rahisi sana kwa mtu aliyeajiliwa anayelipwa vizuri kumpuuza mtafuta ajira"


mkuu huitwi kama we una jina la bara nyeupe
 
Usipende kusikiliza habari za vijiweni ....subiri nafasi zikitoka na kama una sifa peleka CV yako. ......watu mnakuwa hamjatimiza vigezo na mkitimiza mnakuwa mmefanya vibaya kwenye interview halafu mnakuja hapa na habari za kuokoteza kuwa kuna udini.
Mi nna rafiki yangu amesoma vizuri hapo Tanzania na ni muislam lakini alikosa kazi nssf, sasa na huyu nae alalamike kuwa kuna udini?

acha ujinga wewe mbwa mwitu,hutaki kaa pembeni,nssf udini umekithiri,ni kazi ya magufuli kumshughulikia dau kabla nssf haijafa
 
..........wamekalia wizi tu na kulewa ! wanashirika mpaka Kanisa, Benki ya Kanisa na Maaskofu kwenye wizi ! :hand:
Wanaitaka NSSF ili waibe tu, maana miaka yote hiyo ya Dr Dau pamoja na kumiliki Bilions, shirika halina scandals ! KakaKiiza

subiri scandle utazisikia mda ukifika no utajua dau ni wa aina gani
 
Last edited by a moderator:
subiri scandle utazisikia mda ukifika no utajua dau ni wa aina gani

.......... scandal huwa zinasubiri mda ! ..........?? !! Dr. Dau ni muungwana tu, muadilifu na hujisikia fahari na Dini yake, wala hamkeri mtu wala kumnyima pumzi ! shinyangakwetu mtabakia na vijiba vya roho tu.
 
Last edited by a moderator:
Kweli unaweza kuwepo, lakini tutajuaje?
Unaweza kuleta vielelezo kwamba ktk waajiriwa 5000 90% ni waislam ambao haakufaulu ktk interviews au hawakufanya interview kabisa!
Tanzania zipo shutuma nyingi sana panapotokea kiongozi muislam! Hata akifanya mema kiasi gani huwa hajadiliwi kwa uzuri wake, Bali kwa kila baya litalozushwa!
Mfano Nehemiah wa NHC anasifiwa sana kwa ujenzi wa makazi, hakuna anayemsifia Dau kwa uimarishaji wa taasisi ya NSSF! Kuna kashfa nyingi kwa dau kuliko sifa ambazo zote zinakuwa ni uzushi!
Hii nchi ina idara za umma zenye watu wa kabila moja zaidi ya 40% na bado watu watasema kuwa wao ni wasomi, ingawa ukitazama records za mashuleni sifa hizo hazipo!
Acheni kuwanyanyasa waislam, na hili mnaliaznisha kila mkiwa na kiongozi wa juu ambaye ni mkristo! Please acheni nchi iendelee na hali ya utulivu iliyonayo! Si jambo zuri kuleta mifarakano ya aina hii, kama una maswali ya aina hii, weka institution by institution na tone uwiano vs population na uone uwiano kama upo sawa! Narudia si vizuri unapotaka kutumika vibaya kwa manufaa ya vikundi Fulani au watu wachache mnaowania nafasi za uongozi baada ya wenzenu kutimuliwa!

Nehemiah Mchechu na Dau wote wawili ni watu waliokosa ubunifu.

Nianze na Mcheche: Nyumba zile ambazo zipo katika maeneo ambayo kodi kwa apartment moja ni $3000+ kwa mwezi kuziuza ni kuua future ya NHC na kuwamilikisha mabepari wachache mji.

Pili, hizo nyumba mnazoziita za gharama nafuu kwa akili ya wenye kipato kidogo hazilingani na mshahara wa mwenye kipato kidogo. Mshahara wa kima cha chini haufikii masharti ya mtu kukopeshwa 48m aweze kununua nyumba ya Mcheche ya tuvyumba tuwili. Kwa hiyo Mchechu hana mtumishi wowowte wa mfano kwa jamii, labda kwa wa chache wenye uwezo wa kukopa mamilioni Benki kwa dhamana na vyeo vyao.

Namna pekee ya mnyonge kuwa na kajumba kake ni kutafuta kiwanja, angalau kile cha high density 400sqm na kuwekeza hapo around 10m utapata kibanda cha kujisetiri.

Ramadhan Dau: anaendesha mfuko wa hifadhi ya serikali. Wakati mifuko mingine ikiwa bize na wellbeing ya members wake, NSSF iko bize na miradi ya serikali. Kwa kuwa walalahoi hawakopesheki kwenye taasisi za fedha basi si vibaya bwana Dau akafanya la maana kwa kuwapa wanachama haki ya kutumia amana zao kama dhamana wanapotaka kukopa ktk taasisi za fedha badala ya kuikopesha serikali tajiri.

Kwa hy, hoja ya fulani na fulani kati ya hao unaowataja hapa ni thuufri.
 
KakaKiiza

Mheshimiwa Dr Ramadhani Dau ni Muislaam thabiti, na anajua kuwa hiyo kazi ina mwisho. Muislaam wa kweli haogopi watu bali anamuogopa Mwenyezi Mungu.

Qur'an:16:90

'Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa (haki) jamaa: na anakataza uchafu, uovu, na dhulma. Na anakuwaidhini ili mpate kukumbuka (ya kwamba ipo siku ya Kiama).
Dr Shein ni dini gani? mbona yeye anang'ang'ania?
 
Dr Shein ni dini gani? mbona yeye anang'ang'ania?

.........anang'ang'ania nini !? Hivi una habari Maalim Seif Sharrif Hamad akiwa Waziri Kiongozi - Zanzibar, aliwahi kususiwa nchi ya Zanzibar na Rais Idris Abdul Wakil kwa wiki nzima !?? mama kubwa
 
Last edited by a moderator:
Nilishafanya interview pale, tulikuwa watu maelf na maelf, ila waliitaji watu wawili tu!, lakini nalo hilo wanalisemaga, sina uhakika nalo!
 
.......... scandal huwa zinasubiri mda ! ..........?? !! Dr. Dau ni muungwana tu, muadilifu na hujisikia fahari na Dini yake, wala hamkeri mtu wala kumnyima pumzi ! shinyangakwetu mtabakia na vijiba vya roho

hilo linajulikana, watu tumefuatwa sana tuombe kazi halo,wengine hatu mind mambo ya udini
 
Dr. Dau ni mchapa kazi na aliteuliwa na kiongozi wa dini tofauti na yeye na hajamuangusha kwenye utendaji wake. Angalia performance yake alipolitoa shirika na mpaka sasa lilipo. Projects ambazo ameshazikamilisha na ambazo zinaendelea ni mchango mkubwa sana katika nchi. Hakuna hizo habari za ubaguzi wa kidini pale zaidi ya qualifications
 
Nehemiah Mchechu na Dau wote wawili ni watu waliokosa ubunifu.

Nianze na Mcheche: Nyumba zile ambazo zipo katika maeneo ambayo kodi kwa apartment moja ni $3000+ kwa mwezi kuziuza ni kuua future ya NHC na kuwamilikisha mabepari wachache mji.

Pili, hizo nyumba mnazoziita za gharama nafuu kwa akili ya wenye kipato kidogo hazilingani na mshahara wa mwenye kipato kidogo. Mshahara wa kima cha chini haufikii masharti ya mtu kukopeshwa 48m aweze kununua nyumba ya Mcheche ya tuvyumba tuwili. Kwa hiyo Mchechu hana mtumishi wowowte wa mfano kwa jamii, labda kwa wa chache wenye uwezo wa kukopa mamilioni Benki kwa dhamana na vyeo vyao.

Namna pekee ya mnyonge kuwa na kajumba kake ni kutafuta kiwanja, angalau kile cha high density 400sqm na kuwekeza hapo around 10m utapata kibanda cha kujisetiri.

Ramadhan Dau: anaendesha mfuko wa hifadhi ya serikali. Wakati mifuko mingine ikiwa bize na wellbeing ya members wake, NSSF iko bize na miradi ya serikali. Kwa kuwa walalahoi hawakopesheki kwenye taasisi za fedha basi si vibaya bwana Dau akafanya la maana kwa kuwapa wanachama haki ya kutumia amana zao kama dhamana wanapotaka kukopa ktk taasisi za fedha badala ya kuikopesha serikali tajiri.

Kwa hy, hoja ya fulani na fulani kati ya hao unaowataja hapa ni thuufri.
Mtoka pabaya,Real Estate ni wigo mpana.
Kuuza apartment ni moja tu ya strategy zao na pia ni beneficial.kumbuka price set huwa imeshaangalia lufe span ya mjengo,na factor nyinginezo.hiyo ni sawa na kusema serikali au kampuni isiuze gari zake bado zinaonekana zinadai,huku maintenance cost imeshakuwa kubwa karibu nusu ya thamani ya gari lenyewe.
 
Usipende kusikiliza habari za vijiweni ....subiri nafasi zikitoka na kama una sifa peleka CV yako. ......watu mnakuwa hamjatimiza vigezo na mkitimiza mnakuwa mmefanya vibaya kwenye interview halafu mnakuja hapa na habari za kuokoteza kuwa kuna udini.
Mi nna rafiki yangu amesoma vizuri hapo Tanzania na ni muislam lakini alikosa kazi nssf, sasa na huyu nae alalamike kuwa kuna udini?

mkuu umemjibu vizuri kabisa big up
 
hawa wasio waislam(makafiri) wana tabu kweli!!!!sehemu ikiongozwa na waislamu,utasikia udini,rejea udom.mini nipo chuo cha serikali,malecture woote wanaonifundisha makafiri.utasikia waislaam wamekosa vigezo luwa malecture.ila sehemu ikiwa na waislaam wengi,udini.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom