Hizo nizako tu hamna cha udini hapa ni utanzania tu ni haina nafasi shule yako basi
Unatakiwa utafakari hoja sio kupuuza hii nimesikia kwa zaidi ya watu kumi wame sense kitu kama hicho... Hili jambo ni serious kwa mustakabali wa Taifa letu.
Hizo nizako tu hamna cha udini hapa ni utanzania tu ni haina nafasi shule yako basi
Kinachowasumbua watanzania wala hawakijui, na ndio maana kila mtu anasema lake, na huu ni kwa ajili ya mfumo kandamizi,
Nchii hii kama unafuatilia kwa undani utakuja kuona kwamba inapita kwenye vipindi vingi na hili tufike kwenye mafanikio lazima tupate vidonda na vikipona lazima viache makovu, na kovu siku zote halifutiki linabaki kama historia.
Nchii hii wakati tunajenga ujamaa tuliona jinsi haki za binadamu zilivyopuuzwa, umaskini njaa,maradhi na ujingga vilivyotamalaki ktk maisha ya watanzania, watu walipuuza shule tuliona maazimio mengi yalikuja juu ya elimu yalivyokuwa yanazidi kuua elimu badala ya kuijenga, shule hazkujengwa, wanafunzi 70% waliishia darasa la saba,leo hii watanzania walio wengi wenye elimu bora walizipata kwa juhudi binafsi ndani na nje ya nchii na wengi wao nje ya nchi, ambayo ndio bora na hao wawekezaji au matajiri ndio wanazitaka, kibaya zaidi kile kizazi kilichopata elimu bora na mabaki ya elimu ya kikoloni au wale waliopata elimu ya chuo kikuu mwanzoni mwa miaka ya sabini wanaisha ama kufa au kustahafu kitakachobaki ni makanjanja watu wenye phD ambazo hazina elimu bora ya msingi na sekondari
Na hii miemko ya kidini naweza kuifananisha na muungano wa tanzania na zanzibar, muungano huu hauna msingi imara ukiangalia vizuri utaona ubabe ulikuwa mwingi kuliko utaratibu na ndio sasa, dhama mpya za uhuru wa mawazo na kidemocrasia zimekuja watu wako huru, mawazo yanatolewa, na watu wanahoji na sababu za msingi zinatolewa, ila watawala kwa maslahi au makusudi hawataki wanatumia mbinu na mikakati ileile ya wakati wa giza yaani 70 na 80 ktk dunia yenye mwaka ya wakati huu, mwisho wa siku wanazidisha mihemuko ya chuki na hisia za utaifa, na ni vitu ambavyo uwa havifi kwani hisia inashindwa pale mhimili imara ya haki na demokrasia utakapo fuata mkondo wake,
Kwa upande wa dini hili halina tofauti sana kwani baadhi ya watu wa dini furani walinyimwa elimu kwa makusudi na ukiwauliza sababu za msingi nao wanazo,kibaya zaidi ebu ndugu msomaji jiulize katika mazingira mabovu ya elimu hii mbovu tuliyonayo bado kuna wana wa jamii furani wanalalamika hiyo hiyo inayolalamikiwa kuwa elimu mbovu wao wamenyimwa sasa hapo ndio ufiklie aina ya jamii ambayo watanzania tumeijenga na tunaendelea kuijenga, sasa hapa hoja ipo tena ya msingi, sasa rejea kwenye point yangu pale juu kuwa ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu, na mibinyo mikali ya kisiasa iliyotokea wakati tunausimika ujamaa ambao baadae ukaja kufa kifo ambacho hata kaburi lake hatulijui liliko, na pia kuzaliwa kwa demokrasia, watu kuelimika tena kwa jitihada zao ndio sasa watu wanafumbua macho na kujitathmini kwamba wao kina nani wanatoka wapi na wafanye nini ili kujiletea maendeleo chanya na ndio hapo sasa uwezi kuzuia. Hisia kali za kizalendo, udini. Utaifa, ukabila na ueneo, rejea kampeni kwenye uchaguzi uliopita utagundua haya.
Watanzania tutoke tulipo tuje tuponye vidonda tulivyopata wakati tunasimika ujamaa, na hizi hisia za udini na utaifa, uwa havizimwi kwa watu kupotea au kubambikiwa kesi, lazima viongozi wetu waligundue hilo kisha tutafute njia za pamoja kujiondoa hapa ambako naweza kupaita tulipokwamia.
Mungu ibariki tanzania .
UDINI NSSF upo tangu kwa mtangulizi wa Dau na dau analiendeleza, huu ni ukwweli japo naona wengine povu linawatoka kwa kubisha hata wasichokijua! Acheni kubisha fanyeni uchunguzi mdogo tu mtagundua hilo
Wadau,
Kama tunavyofahamu Tanzania ni nchi isiyoongozwa kwa misingi ya dini fulani japokuwa wanaoutuongoza wana dini.
Kwangu mimi naona ni jambo jema endapo hatutaangalia dini zetu ili tupate au kutoa huduma mbalimbali za kijamii. Ni hivi majuzi mfuko wa jamii ya watanzania wote NSSF imetangaza nafasi lukuki za kazi lakini zimo tuhuma ambazo zinatolewa na watu wanaodai ni wafanyakazi na wenginesio wafanyakazi kuwa NSSF kuna udini eti kama hauna 'sigda' haupati kazi au kama wewe si Abubakari au Hamisi haupati kazi.
Tuhuma hizi ni mbaya na kubwa kwa mfuko unaoitwa wa jamii. Eti ili wakuajiri si kwamba umefaulu interview bali kwa majina na dini yako. Ni jambo linalohitaji ufafanuzi na ushahidi wa kutosha aidha kukubali au kukataa kuwa kuna udini au hakuna maana litaleta mpasuko kwa taifa.
Moto wa dini ni rahisi kuuanzisha na kuuchochea lakini ni ngumu kuumaliza. Kesho tutaskia na PPF kuna 'UDINI' Keshokutwa tutaskia mahakamani kuna udini na mwisho itakuwa ni jeshi na ikulu kuna udini huku mamlaka zikiwa kimya.
Sasa ni dhahiri uongozi wa Dr Dau unaendekeza udini katika taasisi ya umma ya NSSF.
Katika matokeo ya usaili idadi kubwa ya waliochukuliwa ni wa dini ya kiislamu ni kama asilimia 80 ya waajiriwa wapya ni waislam.jambo la kusikitisha ni kuwa udini unatumika kwani baadhi walikuwa hawana sifa stahili na hata wengine wamechukuliwa wakiwa bado ni wanafunzi wa chuo kikuu sasa sijui walitumia vyeti gani.
1.Serikali ipitie upya ajira ya watumishi wa NSSF
2.Serikali ipitie upya ugawaji wa vyeo na uhamisho wa watumishi wa nssf kwani kuna malalamiko kuwa wakristo wananyanyaswa.
Bila kufuatilia haya shirika lipo taabani kiutendaji na hata makusanyo yapo chini ya asilimia 40![]()
Kama ndiyo ilivyo nalo ni kosa serikali ifanyie kazi pia..Hebu nenda pspf na ppf ni zaidi za vigango, ajira ni kwa waimba kwaya tu