Inakuwaje uelewa wa wafanyakazi juu ya jambo moja ni tofauti?? Hapa utapewa huduma fulani ila pale watakataa.
 
NMB mobile Service nawapongeza kwa huduma zenu kwani zinatusaidia. MAKALAMIKO YSNGU KWENU NI PALE MNAPOKATA FEDHA ZA MTEJA KUTOKA SALIO LAKE KWENYE SIMU HATA PALE AMBAPO MUAMALA HAUJAKAMILIKA.

Mfano, mteja anataka kununua muda wa maongezi, kutokana na tatizo la kiufundi kutoka NMB muamala hujakamilika. Sasa kwa nini MKATE FEDHA WAKATI HUDUMA HAIKUKAMILIKA?
 
Hii NMB loan advance imekuwa tatizo toka Jana.NMB wako kimya kama wamefuta huduma waseme kuliko kusumbua wateja
 
Hili tatizo limekuwa sugu.Kama wameishiwa pesa waseme
 
Duuuh!! Umejilipua haswa. Why usiwatumie hizo details pm? Au ndio vyuma kukaza
 
Leo yamenikuta nimekwenda kwenye ATM moja katika jiji la Mwanza na kutaka kutoa shs.400000/=ajabu pesa haijatoa wala hata risiti pia haijatoka lakini nimetumiwa meseji kwamba nimetoa kiasi hicho cha fedha kuangalia salio nikaona wamekwisha kata pesa!

Mbaya zaidi nilikuwa na dharura ambayo kukosa pesa hizi kumenifanya nipate hasara kubwa. Swali langu je, nikifungua madai kutokana na usumbufu nilioupata nitakuwa na cause of action?

Au njia gani ya kunirudisha nilipokuwa? Au ni halali kwa bank kujifanyia wapendavyo katika kutunza pesa za mteja? Je, pesa yangu ipo salama?
 
Nenda kwa Wakala wa NMB hayo mambo hutayaona,kwakuwa wewe no mvivu wa kuandika Fanya hivo
 
Hili Jukwaa bado halina msaada siku ya tatu leo toka pesa zangu zizuiwe na ATM pamoja na kujaza form lakini nimeshuhudia unyanyapaa wa hali ya juu kiukweli najuta kuwa mteja mzuri wa NMB mbaya zaidi kitendo cha kuzuia pesa kimenipa hasara kubwa na usumbufu sana kila nikimuona mtumishi wa benki hiyo napata hasira kuu mbaya zaidi wao wanaona ni kitu rahisi sana.

Hivi nchi zilizoendelea Wanafanyaje? Hivi huduma katika Bank nyingine zikoje katika kumuhudumia mtu maskini? Hivi kosa langu ni lipi? au wamelewa madaraka? Mbona hainiingii akirini hivi kwa teknolojia ya sasa unaweza kuchukua zaidi ya siku tatu hujarudisha pesa ambazo umezikata kimakosa! Sasa manufaa ya kutumia Bank ni yapi? au Ubepari unazidi kutamaraki? Bado nauliza hivi hakuna sheria ya kumlinda mteja aliyeonewa kwa kiwango changu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…