NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania

NMB Tanzania

Verified Member
Sep 13, 2014
93
150
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
 
pitbull

pitbull

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
582
225
Nendeni TPB Bank siku moja tu unafungua mkuu
Nmb kwanini Kufungua account ya kikundi ni mzunguko sana? yaani hadi unawezakukata tamaa, nikipiga hesabu nauli tu inakaribia hela ya kufungulia, nenda rudi ni nyingi hadi tunachoka.
 
Mponda 02

Mponda 02

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
447
500
ATM nyingi hazina pesa siku ya Jumapili na Jumamosi, kwanini mnafanya hivi?.. maana ni kero isiyoisha.
 
gerit

gerit

JF-Expert Member
Jul 16, 2016
280
250
Nmb tawi la Tukuyu Rungwe Mbeya ATM zinaharibika Mara kwa mara na ni za miaka mingiii. Unalazimika kulipia gharama kubwa ndani SBB ya ubovu wa hizo Mashine. Wateja wanaomba ziwekwe mpya na ikiwezekana zingine zifungwe eneo la Ushirika pia kwani kuna Wateja wengi.
 
BABA PAROKO 92

BABA PAROKO 92

Senior Member
Jun 17, 2019
122
225
MSAADA NMB

NAHITAJI KUFUNGUA ACCOUNT YA NMB

Chap chap account
Je ninahitajika kua na vigezo gani wakati wa kufungua, niwe na nini na nini vitavyoniwezesha kufungua?
Na mimi niko pugu, je office gani iliyopo karibu na mimi ya NMB ambayo naweza kwenda?
 
W

wakurochi

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
1,978
2,000
NMB kufungua account ni rahisi kupata kadi ni miezi kwanini wakati benki nyingine ni fasta tu.

Nimeibiwa ya kwangu huo mlolongo wenu unakatosha tamaa ingawa kwenye mobole banking mko vizuri.
 
BABA PAROKO 92

BABA PAROKO 92

Senior Member
Jun 17, 2019
122
225
Ndugu nisaidie kujua vigezo na documents zipi znahitajika kufungua account na kiingilio ni kiasi gani cha kuanzia?
NMB kufungua account ni rahisi kupata kadi ni miezi kwanini wakati benki nyingine ni fasta tu.

Nimeibiwa ya kwangu huo mlolongo wenu unakatosha tamaa ingawa kwenye mobole banking mko vizuri.
 
W

wakurochi

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
1,978
2,000
Unaanzia kwa kiongozi wa mtaa mjumbe anakupa form au barua unaenda serkali ya mtaa yaani kwa mtendaji eneo lako halafu bank. Ndivyo nivyopata mimi labda kama kuna badiliko ila uwe na passport 2 ililuwa elfu 10 nenda na 20 itatosha
Ndugu nisaidie kujua vigezo na documents zipi znahitajika kufungua account na kiingilio ni kiasi gani cha kuanzia?
 
NJUGHU

NJUGHU

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
380
250
Habarini wanajamvi,NMB mmekuwa mkitoa mikopo lakini kuna kitu huwa hakiwi Na maelezo,hivi processing fee Na insurance huwa ni asilimia ngapi maana hamtufafanulii Wateja mpaka kuhisi tunapigiwa humo.
 
D

Dringia

Member
Sep 17, 2016
62
125
Kufungua chap chap A/C unahitajika uwe na kitambulisho chako cha kura, au Uraia, au Lessen, au Passport ya kusafiria pamoja na tsh 10,000. Unaweza kufika katika Tawi la NMB GONGO LA MBOTO, Karibu na stand
MSAADA NMB

NAHITAJI KUFUNGUA ACCOUNT YA NMB

Chap chap account
Je ninahitajika kua na vigezo gani wakati wa kufungua, niwe na nini na nini vitavyoniwezesha kufungua?
Na mimi niko pugu, je office gani iliyopo karibu na mimi ya NMB ambayo naweza kwenda?
 
mugah di mathew

mugah di mathew

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
1,350
2,000
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1.
Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
Naomba vigezo na masharit ya kupata mkopo wa tsh 200,000 na 5,000,000
 
D

daz capital

Member
Oct 15, 2017
40
95
naomba kujua jinsi ya kubadili namba ya simu ninayotumia kwenye nmb mobile na kuweka namba nyingine tofauti na ya awali ninayotumia
 
full of faith

full of faith

JF-Expert Member
Jun 7, 2018
247
250
Personal loan
Mkopo 10,800,000 Tshs.
Processing fee+ Insurance fee= 729,000 Tshs.Je,hii 729,000Tshs. ni gharama halisi au nimeibiwa?!
Pia naomba kufahamishwa kuhusu percentage ya processing fee na Insurance fee.
Asante.
 
kiboko samson

kiboko samson

Member
Oct 14, 2013
46
125
Je MTU akiwa na mkopo bank tofauti na NMB hawezi kupata advance salary NMB ata kama mshahara wake unapitia NMB ?
 
B

Babeshi Mwamba

Senior Member
Jan 7, 2013
195
195
Tunaomba mfungue TAWI NANYAMBA-MTWARA tunapata tabu sana mpaka Huduma za Kibenki,
Asante.
 
noiselessly hunter

noiselessly hunter

JF-Expert Member
Oct 20, 2013
3,123
2,000
Personal loan
Mkopo 10,800,000 Tshs.
Processing fee+ Insurance fee= 729,000 Tshs.Je,hii 729,000Tshs. ni gharama halisi au nimeibiwa?!
Pia naomba kufahamishwa kuhusu percentage ya processing fee na Insurance fee.
Asante.
Huu ni wizi WA wazi,
Umeomba milioni kumi na laki name,wanakata 729000 sasa hizo zilizobaki ndo ulizoomba?
Hapo nmb mnnatuibia na kutudhulumu wateja kwa sababu ya umaskini wetu na shida zetu,hiyo sio haki,kama mnapita humu na kusoma mjue mnnalofanya no dhambi kubwa.
Dawa ni kutokukopa tu
 
full of faith

full of faith

JF-Expert Member
Jun 7, 2018
247
250
Mkuu kwa ada hiyo nimeghaili kukopa kabisa.Yaani 729,000/- hata mkopo sijafanyia chochote!!!
Huu ni wizi WA wazi,
Umeomba milioni kumi na laki name,wanakata 729000 sasa hizo zilizobaki ndo ulizoomba?
Hapo nmb mnnatuibia na kutudhulumu wateja kwa sababu ya umaskini wetu na shida zetu,hiyo sio haki,kama mnapita humu na kusoma mjue mnnalofanya no dhambi kubwa.
Dawa ni kutokukopa tu
 
Michael Mtitu

Michael Mtitu

Verified Member
Oct 6, 2012
630
500
naomba kujua jinsi ya kubadili namba ya simu ninayotumia kwenye nmb mobile na kuweka namba nyingine tofauti na ya awali ninayotumia
1. Nenda ATM yeyote ya NMB, chomeka kadi yako
2. Bofya chini, kulia
3. Chagua badili namba ya SIMU
4. Ingiza namba mpya ya SIMU unayotaka
5. Ingiza pasword uliyokuwa ukitumia awali ku-access huduma za bank kwenye simu, maliza.
Baada ya hapo utapokea ujumbe kwenye simu yako kuwa umefanikiwa kubadili namba ya NMB Mobile kutoka Mf. 0752XXXXXX kuwa 0683XXXXXX.
 
diana chumbikino

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
429
500
1568786189132.png
BENKI ya NMB imezindua 'NMB Afya loan', huduma mpya itakayotoa mikopo ya gharama nafuu kwa hospitali binafsi, vituo vya afya, zahanati, wasambazaji na maduka ya dawa nchini. Ikishirikiana na Shirika la Stichting Medical Credit Fund (MCF), NMB itatoa mikopo kuanzia Sh. milioni bili hadi Sh bilioni tano huku MCF ikitoa dhamana ya asilimia 50 kwa mikopo yote itakayotolewa kupitia huduma hiyo ya kipekee nchini.

NMB Afya Loan inaifanya benki hiyo kuwa taasisi ya kifedha ya kwanza hapa nchini kutoa huduma hiyo ambayo kwa kushirikiana na MCF, ufadhili wa huduma ya afya, kupanua na kuimarisha ubora wa utoaji wa huduma hiyo muhimu kwa wananchi ni sehemu ya matarajio makuu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Mkuu katika kitengo cha Wateja Binafsi, biashara ndogo na za kati, Filbert Mponzi alisema leo Jumanne jijini Dar es Salaam, huduma hiyo ya mikopo imefika kwa wakati mwafaka na utachangia kuongeza upatikanaji wa huduma nafuu za afya na kujenga mifumo endelevu kwasababu upatikanaji wa mitaji unakuwa rahisi zaidi.

“Huduma hii itawawezesha watoa huduma ya afya kupata fedha pamoja na kupata utaalum wa kiufundi, ambao utasaidia kutambua wauzauji na vifaa vya matibabu bora pamoja na upatikanaji wa vifaa vya tiba kwa ajili ya uboreshaji wa huduma zao. Kuna fursa nyingi katika sekta ya afya nchini na sisi kama NMB, tumeliona hili na tumejikita kuwapa nafasi hospitali, vituo vya afya wasambazaji wa vifaa vya tiba kujiendeleza,” Mponzi alinukuliwa.

Naye Mkurugenzi wa MCF Tanzania, Dk Heri Marwa alisema kuanza utekelezaji wa huduma hiyo mpya ni muhimu katika kutimiza malengo ya MCF ya kuhakikisha Watanzania wengi wanapata huduma nafuu za afya na tiba. "Upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya uwekezaji ni changamoto kubwa katika nchi nyingi barani Afrika na inazuia utoaji huduma nafuu za afya hususan tukiangalia mifumo endelevu ya afya.

Kwa huduma hii tunafurahi kwamba hospitali nyingi binafsi, vituo vya afya vitapata na uwezo wa kuwekeza kwenye vifaa vya afya vya kisasa,” alisema Dk. Heri Marwa
 
Top Bottom