Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

wangeweza kenya kwanza.

usione ukadhani,

wataalamu wangapi wapo upinzani kiasi cha kutuhakikishia maendeleo? au mnyika na zitto na mdee?

nchi haijengwi kwa kulipua mabomu
 
Mbowe awaponda wenzake
*Asema wapo kwa maslahi ya tumbo
*Kuungana sawa na kufika mbinguni

Na Eliya Mbonea, Iramba

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Freeman Mbowe (CHADEMA), amesema uwezekano wa viongozi wa kambi ya Upinzani nchini kuungana ni mgumu sawa na tajiri kuona ufalme wa Mbingu.

Alitoa kauli hiyo jana, alipokuwa akihutubia wakazi na wanafunzi wa chuo na sekondari ya Kinampanda mjini hapa, baada ya kuulizwa swali lililotaka kujua sababu ya wagombea urais wa kambi hiyo kutoungana na kuwa kitu kimoja.

Bw. Mbowe alisema chama chake kimekuwa cha kwanza katika historia ya upinzani nchini kuweka mbele dhana ya ushirikiano baina ya wapinzani.

"Vyama vichache vimepandikizwa na CCM kwa maslahi ya tumbo, CHADEMA mwaka 1995 haikusimamisha mgombea, badala yake iliungana na NCCR-Mageuzi, mwaka 2000 tukawaunga mkono CUF, jitihada zetu zote za kushirikiana zimekuwa hazizai matunda, hivyo mwaka huu tumesimamisha mgombea," alisema.

Aliongeza kuwa viongozi wengi wa Upinzani hawawezi kuungana kwa dhamira ya kuwatetea Watanzania, kwani wapo kwa ajili ya maslahi binafsi.

"Msifikirie kuwa kila mgombea urais au Mwenyekiti wa chama yupo kwa ajili ya kupigania mustakabali wa nchi, wamegeuza siasa kama biashara na wanaitumia kama vyanzo vya mapato," alisema mgombea huyo.

Alisema lazima CCM ikubali lawama za kulifikisha Taifa katika hali mbaya na ya kutisha, na kuwafanya wananchi wajione kuwa matatizo yao ni tofauti ya rangi za bendera badala ya kuwaeleza kuwa tatizo kubwa ni umasikini.

Akizungumzia nafsi yake, Bw. Mbowe aliwaeleza wananchi kuwa hakuingia kwenye siasa kwa ajili ya kutafuta ajira, kwani anachopigania si maslahi ya CHADEMA bali ya wananchi wote. "CHADEMA si mama yangu naweza kuiacha wakati wowote," alisisitiza msimamo wake.

Alisema kamwe hataacha kutumia busara na hekima za Mwalimu Nyerere katika kujenga utaifa, kwani kipindi chote cha miaka 44 bado misingi ya utaifa aliyoicha Mwalimu haijatekelezwa.

SASA MASWALI YA KUJIULIZA :
Kama vyama vingine vya upinzani (isipokuwa chadema)vipo kwa ajili ya matumbo, WHY DID HE JOIN THEM ? Doesnt this LOGICALLY make him one of them ??

Kuungana ni sawa na kufika mbinguni ? Anaijua mbingu huyu au anasema tu ? Je ashafika huko since waungane ?

Anaendelea kusema kwamba vyama vimepandikizwa na CCM, then DOES IT MAKE ANY SENSE KWA YEYE KAMA MWENYEKITI WA CHADEMA KUUNGANA NA VYAMA VILIVYOPANDIKIZWA NA CCM ? AU NA YEYE AMEPANDIKIZWA ?? WHO SHOULD WE TRUST HERE ??

(Kuna bonge la nyuzi litashuka kuhusu uchaguzi mkuu, hiyo itaangushwa anytime)!!

Tujumuike katika kuchangia !
 
Saa ingine Mbowe hayuko makini ktk kauli..I doubt uwezo wake kuwa raisi na Mkuu wa Majeshi!
 
...............Anaendelea kusema kwamba vyama vimepandikizwa na CCM, then DOES IT MAKE ANY SENSE KWA YEYE KAMA MWENYEKITI WA CHADEMA KUUNGANA NA VYAMA VILIVYOPANDIKIZWA NA CCM ? AU NA YEYE AMEPANDIKIZWA ?? WHO SHOULD WE TRUST HERE ??.........

Kada
...........hizi politics za vyama ukizifuatilia sana utaumiza kichwa chako saaana.....Hakuna Chama cha Ku-Trust.....their history tells us all........ukiwafanyia vetting hawa wanasiasa be it in CCM or UPINZANI......trust me you will come out with few individuals better.....lol

We need a Good Dictator in this country.......atatokea wapi.....ni kazi yetu kumu-identify na kumpigia support ashike usukani.....nchi itarudi ktk mstari.

.....vichwa wachapa kazi tunavyo (ref: the last JF music CD)............i do admire watendaji kama Magufuli.....una hakika utapata unacho hitaji....ofcourse kutakuwa na waathirika lakini itakuwa ni minimum!

hebu Tumuangalie huyu ndg yetu Mbowe na Biashara zake...ni vipi ameweza fanikisha.......na ni wapi ameshindwa....nini (mafanikio) kaifanyia Chadema kama taasisi......halafu angalia anayozungumza sasa!!!....then combine uone unapata kitu gani
 
nashindwa hata kuelewa kauli za mbowe ! Leo anasema hivi kesho vile, sasa sijui ni flip flop au vipi !

waswahili tunasema "sio kiongozi makini", lakini yeye binafasi yupo mstari wa mbele kukosoa wenzake !

ahhh, hivi vyama kweli sasa vinatuumiza vichwa vyetu !
 
Alitoa kauli hiyo jana, alipokuwa akihutubia wakazi na wanafunzi wa chuo na sekondari ya Kinampanda mjini hapa, baada ya kuulizwa swali lililotaka kujua sababu ya wagombea urais wa kambi hiyo kutoungana na kuwa kitu kimoja.

sire, sire! excuse me sire! which "yesterday"?... Huu ushirikiano wao ulianza lini?
 
Mbowe sio mtu wa kuaminiwa hata kidogo ! Kama watu wanamuamini Mbowe (kwamba ni mkweli) basi naamini moja kwa moja watakuwa wanaamini aliposema kwamba wapinzani (except chadema) wapo kwa ajili ya matumbo yao na wamepachikwa na ccm, NI MANENO YA KWELI !

Sasa basi, kama ni maneno ya kweli kwamba wapinzani wamepachikwa iweje NAE AUNGANE NAO ?? If so, is he one of them ??(kufidia matumbo yao na waliopachikwa na ccm?)
 
Hii habari ni ya lini kwani? Maana naona Mbowe anatajwa kama mgombea urais, mbona mapema mno, uchaguzi si mpaka 2010 sasa anaanza kuitwa mgombea urais 2008?
That aside, he has a point, kwa kifupi hapo ame-summarize upinzani ulivyo bongo, sera za maana kwa faida ya wananchi hakuna ni kuwaza Ikulu tuuuu, hapa nakumbuka Mrema alivyoondoka NCCR kuingia TLP ili awe mgombea urais, what is that?!
 
Wanaojua na kuweza kuongoza hawaongozi, wasiojua na kuweza ndiyo hawa.Mbowe, Kikwete, Mrema and all the other jokers we have.
 
Habari za mwaka 47, za mgombea uraisi ambao Kikwete alishinda kwa asilimia 80, ambao tena Mbowe alimpongeza kwa ushindi ule wa kishindo.

Then leo tunaletewa makala tujadili mambo ya kale, the same old stories which cannot change anything to the lives of our country, mwendelezo wa stutus quo wa hoja katuni.

Mbowe ni shujaa hilo halina ubishi, yamewashinda kina Tambwe, kina Akwilombe, Kina Lamwai, Kina Marando, Kina Msabaha(yule aliyedai katekwa).Lakini watu kama kina Freeman wanakomaa nao.

Tanzania ya leo inahitaji watu kama kina Freeman katika harakati. watu ambao no matter what happens in the path of struggle, they are ready to dare take another step forward in the march for our countrie's bright future.people who dont fear fear, but fear fear them.

Sasa naanza kuona kwamba wakati wa Mbowe kung'ara kisiasa ndo umewadia, ukiona watu wanakuandama bila sababu za msingi ujue kwamba wewe ni tishio, always the forces of status quo will try to fight back.Chuma cha pua hakiwi chuma cha pua mpaka kipitie kwanza kwenye tanuri la moto, haya yote na shutuma zisizo na kichwa wala miguu zao lake litakuwa ni mheshimiwa aliyepikwa akaiva ready kuing'oa CCM na kuandika historia mpya. nanukuu "subirini muone vijana wetu watafanya nini" Mwl jk Nyerere
 
Kitendo cha PM Pinda kuzindua tawi la ccm katika chuo huko iringa JANA na kupata wanachama kadhaa kimenifanya nitafakari na kujiuliza je vyama vya upinzani vinafanya juhudi gani kuanzisha matawi na kusajili wanachama wapya au wanasubiri kukurupuka 2010.
Kwa upande wa kukemea ufisadi/maovu wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa. Na sasa ni vema vikajikita kutekeleza Mpango Mkakati wa kuongeza wanachama. Bila wanachama hakuna chama na ikifika 2010 wanaanza kuhaha! Decentralize madaraka, anzia misenyi bukoba hadi Nanyumbu Mtwara.Toka kinondoni dar hadi nkasi, rukwa. Toka longido hadi mbinga bila kusahau kanda ya kati kwa mzee malecela. Tumia rasilimali chache zilizopo kuunganisha nguvu na kuvuna wanachama.
Pia muda umefika wa kupigania yafuatayo kabla ya 2010:
1) kutungwa sheria ya kuruhusu wagombea binafsi kama ilivyoamriwa na mahakamaa kuu
2) kutunga sheria kali dhidi ya takrima kwenye uchaguzi
3) kupigania tume huru ya uchaguzi
4) kuweka mkakati dhidi ya mkuu wa kaya, pm,mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya na wakurugenzi watendaji wa wilaya kutumia rasilimali za walipa kodi kwa shughuli za chama. Mfano kutumia gari ya serikali na posho toka kasima ya serikali kwenda kufanya kazi za chama eneo furani
5) kupigia kelele vyombo vya usalama kwa kupendelea chama tawala na kunyanyasa upinzani
Bila masuala haya kupatiwa ufumbuzi tusitegemee maajab 2010.
Hiyo ndoto yangu ya usiku wa leo
 
tanzania.jpg

Vyama vya upinzani bado sana..

Kunyoosha kidole au kukosoa si kazi kubwa kama kuendesha nchi. Baada ya kusema hivyo, napenda kusema ya kwamba, hizi zote ni kazi zinazoitaji kwenda sambamba. CCM pamoja na yote yanayotokea hivi sasa, bado ni chama madhubuti zaidi kuongoza nchi yetu kwa sasa. Tusijidanganye na mapenzi yetu ya vyama vya siasa, upizani (Chadema ,CUF nk..) hawako tayari kuchukua madaraka ya nchi kwa sasa. Ukweli ni kwamba vyama vya upinzani viko katika hali nzuri zaidi kujijenga na kuleta changamoto zaidi kwenye bunge letu katika hiki kipindi na kipindi kijacho.

Kukosolewa na kujirekebisha kwa chama ndiko kuna imarisha chama, kwa hiyo wale wana JF ambao hawataki kusikia vyama vyao vinakosolewa wanavidhoofisha vyama vyao.

Kuna mambo mengi tu tunayoweza kujivunia sisi watanzania, haya mambo yameletwa na wananchi chini ya uongozi wa CCM. Leo tunazungumzia ufisadi ambao ni pigo kubwa sana kwa jamii. Vyombo vya habari vimefanya kazi nzuri kuhamasisha wanachi kwa ujumla katika hili jambo. Sasa umefika wakati wa kuangalia mambo mengine muhimu pia. Wana JF na waandishi wa habari msijisahau mkawa kama nchi za magharibi na utangazaji wa habari mbaya tu(negative publicity) kuhusu Afrika au Tanzania (specifically). Au ni kwasababu ya kuishi au kusoma magharibi? Wana JF tuchambue mambo kwa uwazi zaidi kwa faida ya Jamii na sio vyama vya siasa.

Kuongoza nchi sio lelemama, nitatoa mfano mfupi tu wa HAMAS kule Palestine, hawa wamekua nguzo muhimu sana katika mapambano ya kivita zidi ya waisraeli, lakini walikua hawako tayari kutawala, sasa hivi,HAMAS wameshikilia GAZA na wanashindwa kuiendesha na kuendeleza mapambano vizuri kama zamani, wanapoteza wafuasi wao wengi (well this is another issue). Je ni kweli tuko tayari kumpa nchi jini huyu tusiyemjua??🙂
 
Kunyoosha kidole au kukosoa si kazi kubwa kama kuendesha nchi. Baada ya kusema hivyo, napenda kusema ya kwamba, hizi zote ni kazi zinazoitaji kwenda sambamba. CCM pamoja na yote yanayotokea hivi sasa, bado ni chama madhubuti zaidi kuongoza nchi yetu kwa sasa.

Bado hujasema hicho ambacho ccm wamekifanya! uzuri uko wapi? huko kwenu hakuna mifano?

Tusijidanganye na mapenzi yetu ya vyama vya siasa, upizani (Chadema ,CUF nk..) hawako tayari kuchukua madaraka ya nchi kwa sasa. Ukweli ni kwamba vyama vya upinzani viko katika hali nzuri zaidi kujijenga na kuleta changamoto zaidi kwenye bunge letu katika hiki kipindi na kipindi kijacho.

Msijidanganye na nani?

Kukosolewa na kujirekebisha kwa chama ndiko kuna imarisha chama, kwa hiyo wale wana JF ambao hawataki kusikia vyama vyao vinakosolewa wanavidhoofisha vyama vyao.

Haya umeyasikia wapi kuwa kuna watu hawataki kusikia vyama vya vikikosolewa.

Kuna mambo mengi tu tunayoweza kujivunia sisi watanzania, haya mambo yameletwa na wananchi chini ya uongozi wa CCM. Leo tunazungumzia ufisadi ambao ni pigo kubwa sana kwa jamii. Vyombo vya habari vimefanya kazi nzuri kuhamasisha wanachi kwa ujumla katika hili jambo. Sasa umefika wakati wa kuangalia mambo mengine muhimu pia. Wana JF na waandishi wa habari msijisahau mkawa kama nchi za magharibi na utangazaji wa habari mbaya tu(negative publicity) kuhusu Afrika au Tanzania (specifically). Au ni kwasababu ya kuishi au kusoma magharibi? Wana JF tuchambue mambo kwa uwazi zaidi kwa faida ya Jamii na sio vyama vya siasa.

Mambo mengine muhimu pia ni yapi hayo?

Kuongoza nchi sio lelemama,

Kama kuongoza nchi sio lelemama kwa nini msi-resign na kuwaachia wale wenye uwezo wa kuongoza?

nitatoa mfano mfupi tu wa HAMAS kule Palestine, hawa wamekua nguzo muhimu sana katika mapambano ya kivita zidi ya waisraeli, lakini walikua hawako tayari kutawala, sasa hivi,HAMAS wameshikilia GAZA na wanashindwa kuiendesha na kuendeleza mapambano vizuri kama zamani, wanapoteza wafuasi wao wengi (well this is another issue). Je ni kweli tuko tayari kumpa nchi jini huyu tusiyemjua??:-)

Unatumia wingi hapa ukimaanisha wewe na nani?
 
tanzania.jpg

Vyama vya upinzani bado sana..

Kunyoosha kidole au kukosoa si kazi kubwa kama kuendesha nchi. Baada ya kusema hivyo, napenda kusema ya kwamba, hizi zote ni kazi zinazoitaji kwenda sambamba. CCM pamoja na yote yanayotokea hivi sasa, bado ni chama madhubuti zaidi kuongoza nchi yetu kwa sasa. Tusijidanganye na mapenzi yetu ya vyama vya siasa, upizani (Chadema ,CUF nk..) hawako tayari kuchukua madaraka ya nchi kwa sasa. Ukweli ni kwamba vyama vya upinzani viko katika hali nzuri zaidi kujijenga na kuleta changamoto zaidi kwenye bunge letu katika hiki kipindi na kipindi kijacho.

Kukosolewa na kujirekebisha kwa chama ndiko kuna imarisha chama, kwa hiyo wale wana JF ambao hawataki kusikia vyama vyao vinakosolewa wanavidhoofisha vyama vyao.

Kuna mambo mengi tu tunayoweza kujivunia sisi watanzania, haya mambo yameletwa na wananchi chini ya uongozi wa CCM. Leo tunazungumzia ufisadi ambao ni pigo kubwa sana kwa jamii. Vyombo vya habari vimefanya kazi nzuri kuhamasisha wanachi kwa ujumla katika hili jambo. Sasa umefika wakati wa kuangalia mambo mengine muhimu pia. Wana JF na waandishi wa habari msijisahau mkawa kama nchi za magharibi na utangazaji wa habari mbaya tu(negative publicity) kuhusu Afrika au Tanzania (specifically). Au ni kwasababu ya kuishi au kusoma magharibi? Wana JF tuchambue mambo kwa uwazi zaidi kwa faida ya Jamii na sio vyama vya siasa.

Kuongoza nchi sio lelemama, nitatoa mfano mfupi tu wa HAMAS kule Palestine, hawa wamekua nguzo muhimu sana katika mapambano ya kivita zidi ya waisraeli, lakini walikua hawako tayari kutawala, sasa hivi,HAMAS wameshikilia GAZA na wanashindwa kuiendesha na kuendeleza mapambano vizuri kama zamani, wanapoteza wafuasi wao wengi (well this is another issue). Je ni kweli tuko tayari kumpa nchi jini huyu tusiyemjua??

Nadhani tumekumbana kule facebook!
Mimi ndugu yangu nimeshaweka wazi kuwa tumempa Mh Rais muda ili awashughulike mafisadi!
Na asipofanya hivyo...Mimi si wa kulaumiwa!
Halafu si ana facebook page?
Ama ni fake?
Hilo ni juu yake!
Tunataka ripoti ya kamati ya madini!
LASTLT FYI: SINA CHAMA!
 
Najua hiyo picha huyu bwana ameitoa kule facebook ambapo nimeanzisha group inayosema.."African corrupt leaders should be held Accountable"
Halafu kwenye group nikaanzisha mada yenye kuanza mjadala wa namna viongozi wetu wanavyodili na ufisadi!
Hata hivyo nimekupata!
Pia ninashangazwa sana kuona kuwa kuna watu wasiopenda haki itendeke!
 
Bila kuwataja hao watu wasiotaka haki isitendeke inaonesha uoga au heshima kwa hao watu?
 
Back
Top Bottom