Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Vyama vyoooote vya upinzani Tanzania "vilianzishwa na system", na hii niliambiwa na rafiki yangu aliyekuwa mwenyekiti wa NCCR kabla ya mrema, mzee Kassim Maguto (M/Mungu amsamehe dhambi zake na amuweke pema peponi, Amin.).

Vyama ambavyo havikuwa kwenye system vilishindwishwa kuanza, havikusajiliwa mpaka leo hii.

kwa kifupi, upinzani kwa sasa hakuna kabisa Tanzania, kuna kina sisi huku nje tunaeshangilia siasa kama mpira tuu, tukijuwa nini kinachoendelea na kuna wengi sana wenye kupandisha hasira na ghadhabu, wasiojuwa nini kinaendelea.

Narudia, upinzani kwa sasa hakuna Tanzania. Si CUF, si Chadema, Si NCCR wala si kingine chochote chenye usajili ambacho hakina viongozi ambao wapo kwenye system.

kwa kifupi, si mbowe, si lipumba, si sharif, si mrema, wote hao ni system (according to Marehem Kassim Maguto) ambae na yeye mwenyewe alikiri kuwa ni system wa miaka mingi na alinipa siri kuwa aliitwa Ikulu kuelekezwa waanzishe vyama vya upinzani na wakawa wanafundishwa kila kukicha ni nini cha kufanya na funds zote zikatoka huko, kwa vyama vyote vilivyosajiliwa.

kuna baadhi ya wanachama (wengi tuu) ambao masikini hawalijuwi hili, wapo kwa nia moja ya upinzani na wapo tayari kufa lakini masikini roho zao, laiti wangelijuwa hili nadhani wasingekuwa na hamu hata ya siasa.

Enyi kina Lipumba, Sharifu, Mbowe na Mrema wacheni dhulma hii, haya mnayajuwa lakini mtasababisha watu wauwane bure wakati nyinyi mnajuwa nini mnakifanya. Hebu rudini kwa mola wenu kabla ya watu wasiyoyajuwa haya hawajaanza kughadhibika na kumwaga damu.

Na hayo yote yalipangwa na kuanzishwa na nyerere, ndio maana ufisadi haufi Tanzania na aliyeuanzisha huo ufisadi ni nyerere.

Naapa kuwa hayo yote niliyoyasema ni kweli tupu.

Jee, hamjuwi system ni nini?

Huh!? are you serious? 😕 Yaani haya yote yaliyofanyika kwa kelele za wapinzani kuhusiana na mikataba feki ya madini na kashfa nzito BoT na hatimaye kujua nani aliyekuwa anasema ukweli kati ya upinzani na CCM wewe unaona bureee kabisa! 😕 Ama kweli ukistaajabu ya hayawani utaona ya taahira!
Kidumu chama cha mapinduzi!? huh!? 😕 naona hata kinyaa kuitamka CCM kwa jinsi wanavyoiangamiza Tanzania.

KITILA KITILA KITILA

KUMBUKA PESA ULIZOPEWA WAKATI WA UCHAGUZI DARUSO ULIZOPEWA NA CCM LEO UPO CHADEMA

WEWE UNYAMAZE.

Ahaa haa, ah wapi wazuishie wengine bwana, nani alikwambia mimi nilitumia pesa kuchaguliwa DARUSO? Zusha lingine ndugu yangu. Kwanza CCM yenyewe ilivyogoigoi ina habari hata na DARUSO?
 
Kitila kwani umemsahau huyo mtoto wa mafisadi ooops "mkulima" anavyozusha mambo hapa kuanzia zile kashfa za kutunga kwa kina Slaa na mgogoro wa chadema etc.

Wengine tulikuwa tumeamua kumpa mkono aongee nao (talk to the hand) maana pumba zake hapa muda mwingine ni kupoteza muda kuzijibu. Katika yote eti ccm wampe Kitila pesa agombee DARUSO then nini kifanyike!? Mambo mengine yanatia kichefuchefu kusoma ati?
 
Huh!? are you serious? 😕 Yaani haya yote yaliyofanyika kwa kelele za wapinzani kuhusiana na mikataba feki ya madini na kashfa nzito BoT na hatimaye kujua nani aliyekuwa anasema ukweli kati ya upinzani na CCM wewe unaona bureee kabisa! 😕 Ama kweli ukistaajabu ya hayawani utaona ya taahira!
Kidumu chama cha mapinduzi!? huh!? 😕 naona hata kinyaa kuitamka CCM kwa jinsi wanavyoiangamiza Tanzania.

Yes Iam.

No yote yaliyofanywa na upinzani siyaoni bure kabisa, nimetaja kwa majina, viongozi ambao naona ni bure kabisa na hawana maana ya kuwepo kwenye uongozi wa sasa wa vyama vya upinzani, kwa sababu ni watu wa system.

Na ukitaka kuiokowa Tanzania kwanza unaanza na hao vibaraka wa ccm waliopo kwenye upinzani na ndio viongozi, bila ya hivyo ni kazi bure tuu, hata ashike lipumba leo, au mbowe, au mrema ni kazi bure tuu. Hayo ndio nisemayo mimi.
Au huijuwi system ni nini?
 
bwanamkubwa Zomba weakness ya upinzani huwezi kulaumu viongozi ambao wako upande huo na uwanja ni mkubwa sana kwa hiyo kama unaona hawafai wewe jitupe ndani tuu na mambo yako yakiwa yameshiba sisi tutakuwa nyuma yako tusiopenda uongozi lakini kusema hawafai haisaidii kituu...ingia mzee ufanye mambo then majeshi yakikubaliana na Zomba utatuona,na hao unao walaumu wengi wao hawana hata support yeyote na wamekwisha au hawapo tena,tuangalie future na kuwatoa mafisadi kama Slaa & zitto wanavyofanya maana atleast hao kwangu upinzani wao umeonyesha substance...sio story za kina Kassim magutto(RIP) au lipumba tunayemwona siku ya kuchukua fomu za uraisi tuu
 
bwanamkubwa Zomba weakness ya upinzani huwezi kulaumu viongozi ambao wako upande huo na uwanja ni mkubwa sana kwa hiyo kama unaona hawafai wewe jitupe ndani tuu na mambo yako yakiwa yameshiba sisi tutakuwa nyuma yako tusiopenda uongozi lakini kusema hawafai haisaidii kituu...ingia mzee ufanye mambo then majeshi yakikubaliana na Zomba utatuona,na hao unao walaumu wengi wao hawana hata support yeyote na wamekwisha au hawapo tena,tuangalie future na kuwatoa mafisadi kama Slaa & zitto wanavyofanya

Koba:

Kuwa nyuma ya mtu hayo mambo ya Mombasa. Sema utafuata nyayo au kuwa bega kwa bega.
 
..naona una ogopa sana mtu kuwa nyuma yako,kwani kulitokea nini?
 
Kitila kwani umemsahau huyo mtoto wa mafisadi ooops "mkulima" anavyozusha mambo hapa kuanzia zile kashfa za kutunga kwa kina Slaa na mgogoro wa chadema etc.

Wengine tulikuwa tumeamua kumpa mkono aongee nao (talk to the hand) maana pumba zake hapa muda mwingine ni kupoteza muda kuzijibu. Katika yote eti ccm wampe Kitila pesa agombee DARUSO then nini kifanyike!? Mambo mengine yanatia kichefuchefu kusoma ati?

Nakwambia hawa watu wameamua kuwa wajinga kuliko ujinga wenyewe, tutakwenda nao hivyohivyo!
 
Vyama vyoooote vya upinzani Tanzania "vilianzishwa na system", na hii niliambiwa na rafiki yangu aliyekuwa mwenyekiti wa NCCR kabla ya mrema, mzee Kassim Maguto (M/Mungu amsamehe dhambi zake na amuweke pema peponi, Amin.).

Vyama ambavyo havikuwa kwenye system vilishindwishwa kuanza, havikusajiliwa mpaka leo hii.

kwa kifupi, upinzani kwa sasa hakuna kabisa Tanzania, kuna kina sisi huku nje tunaeshangilia siasa kama mpira tuu, tukijuwa nini kinachoendelea na kuna wengi sana wenye kupandisha hasira na ghadhabu, wasiojuwa nini kinaendelea.

Narudia, upinzani kwa sasa hakuna Tanzania. Si CUF, si Chadema, Si NCCR wala si kingine chochote chenye usajili ambacho hakina viongozi ambao wapo kwenye system.

kwa kifupi, si mbowe, si lipumba, si sharif, si mrema, wote hao ni system (according to Marehem Kassim Maguto) ambae na yeye mwenyewe alikiri kuwa ni system wa miaka mingi na alinipa siri kuwa aliitwa Ikulu kuelekezwa waanzishe vyama vya upinzani na wakawa wanafundishwa kila kukicha ni nini cha kufanya na funds zote zikatoka huko, kwa vyama vyote vilivyosajiliwa.

kuna baadhi ya wanachama (wengi tuu) ambao masikini hawalijuwi hili, wapo kwa nia moja ya upinzani na wapo tayari kufa lakini masikini roho zao, laiti wangelijuwa hili nadhani wasingekuwa na hamu hata ya siasa.

Enyi kina Lipumba, Sharifu, Mbowe na Mrema wacheni dhulma hii, haya mnayajuwa lakini mtasababisha watu wauwane bure wakati nyinyi mnajuwa nini mnakifanya. Hebu rudini kwa mola wenu kabla ya watu wasiyoyajuwa haya hawajaanza kughadhibika na kumwaga damu.

Na hayo yote yalipangwa na kuanzishwa na nyerere, ndio maana ufisadi haufi Tanzania na aliyeuanzisha huo ufisadi ni nyerere.

Naapa kuwa hayo yote niliyoyasema ni kweli tupu.

Jee, hamjuwi system ni nini?

2gsecxt.jpg
 
Tukitumia nadharia za wenzetu wa nchi zilizoendelea kupima kuwepo kwa vyama vya kisiasa kutokana na itikadi ya vyama, kutakuwepo na ukweli fulani kuwa hakuna vyama vya upinzani.

Siasa za nchi nyingi za kiafrika zimejaa Personality Cult. Pamoja na kazi nzuri anayofanya Dr. Slaa, hawezi kushinda kiti cha ubunge nje ya mkoa wake. Jacob Zuma pamoja na ufilauni wake bado anachaguliwa kuwa Rais wa ANC na baadaye anaweza kuwa Rais wa SA.

Ukisoma itikadi ya CCM katika website yao na kuangalia kile wanachofanya wakiwa madarakani, mwenye akili timamu haoni kwanini chama hiki kipo madarakani na kwanini upinzani unashindwa ku-capitalize.

Waliopo JF wanaweza kumchagua mtu kwa kufuata sera zake na sio personality yake. Lakini sehemu kubwa ya Tanzania ambayo nambari wani (CCM) inawika, personality ya mtu bado inatumika sana katika masuala ya kisiasa.

Kwa maoni yangu inabidi tuwe realistic na tusijaribu kuchukua mifano ya Labor party na kuiweka Tanzania.

Vilevile siasa ni ku-capitalize nafasi uliyopewa. Nafasi kubwa watanzania asa wa bara waliyopata kubadili mfumo wa kisiasa ilikuwa 1995 wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi. Mrema na NCCR-Mageuzi walikuwa na nafasi ya kudai mabadiliko makubwa ya katiba kabla ya kwenda kwenye uchaguzi.

Kuchukua ruzuku kwa vyama vya upinzani na kukubali katiba iliyotungwa na CCM kumefanya mabadiliko ya kisiasa na kujenga personality ambayo ni muhimu katika siasa yetu nje ya chama tawala kuwa vigumu.

Kwa Tanzania bara kuwa na wabunge wapinzani chini ya 10 kwa nchi yenye idadi ya zaidi ya watu 36 millioni masikini na wenye njaa ni onyesho la mapungufu.
 
Just being Curious....
Vyama vyoooote vya upinzani Tanzania "vilianzishwa na system", na hii niliambiwa na rafiki yangu aliyekuwa mwenyekiti wa NCCR kabla ya mrema, mzee Kassim Maguto (M/Mungu amsamehe dhambi zake na amuweke pema peponi, Amin.).
Vyama ambavyo havikuwa kwenye system vilishindwishwa kuanza, havikusajiliwa mpaka leo hii.
What if it's true - Angalieni neno moja muhimu sana hapo juu -VILIANZISHWA.
Maanake pamoja na kumpenda sana Nyerere lakini naogopa kukiri kwamba hakuweza kufanya hivyo!
 
WEWE UNYAMAZE.

Mtoto wa Mkulima,

Heshima mbele mkuu, hii ni below the belt mambo binafsi ya Mkuu Kitila, sio hoja hapa na hasa kwenye hii topic, ichambue hoja ya Zomba na wengine bila personal, haifai ndugu yangu, tunahitaji kuwashawishi wananchi hapa waanze kuingia na majina yao kamili, sasa wewe ukiweka huu mfano tena wa kuingilliana personal inatisha wengine wanaotaka kuingia wazima wazima,

Wewe na wengine hapa mnaheshimika sana, na pia Mkuu Kieleweke, punguzeni munkari kidogo tule elimu nzito hapa, tena ya bure!

Mkuu Zomba,

Kama ninakuelewa vizuri una maana hawa viongozi wetu wanafiki ni reflection yetu sisi wananchi au? Maana tunaowachagua kuanzia upinzani mpaka CCM, ni sisi wenyewe wananchi na kama sikosei huwa tunachagua viongozi tunaofanana nao, either kwa uwezo wao wa kufikiri au kwa matendo, kama ni viongozi wanafiki wapo pande zote mbili, wewe angalia ishu ya Zitto, na kusimamishwa bunge, kwanza wote walinyamaza kimyaa, mpaka waliposikia rais ameazisha kamati ya madini ndio wakaanza kujitokeza, sasa hivi ya Balali wote wako kimyaaa, sasa ngoja Balali arudi na kuwachoma moto utaona kila mmoja atajitokeza kumpongeza,

That is what we are, fraud people in a fraud nation, kama ni kusafisha tuanzie na wananchi yaani sisi wenyewe, Obama amesema jana kuwa mbadiliko ya kweli ni lazima yaanzie chini, na kupanda juu. Wewe Zomba ulipoongea na huyo mzee mnafiki kwa maneno yake mwenyewe, ulipaswa kumpa vipande vyake pale pale na kutufahamisha public kuhusiana na aliyokuambia ili wananchi wenye uchungu na nchi wayafanyie kazi, na hasa hapa JF ambapo rais anayesafiri kila siku huitwa exactly what he is kama Waziri Membe alivyoi-quote JF Vasco Da Gama,

Hao viongozi kama wapo kweli, basi ni reflection yetu sisi wenyewe yaani wananchi!
 
Fikra dhaifu huweza kutawala kwa muda wote ule ambao fikra hizo zinaonekana na hudhaniwa kuwa zina nguvu. (M. M. Original quote). Watu wenye kukubali fikra dhaifu wakidhania zina nguvu, huweza kuzitetea fikra hizo hata kwa kumwaga damu. Hata hivyo fikra zenye nguvu zinapotokea lazima zigongane na fikra zile zinazoonekana zina nguvu na kumbe ni dhaifu. Mgongano huo ni wa lazima na usioepukika.

Unapotokea mgongano huo njia mojawapo ya fikra dhaifu kujitutumia ni kudai kuwa hizo fikra mpya na zenye nguvu ni fikra zile zile za awali isipokuwa zimebadilishwa tu na watu na hivyo kuziuza tena kwa lugha nyingine. Zinapozidi kutishiwa fikra dhaifu badala ya kushambulia zile fikra zenye nguvu na kujaribu kuzishinda huanza kushambulia wabeba fikra zenye nguvu na kuwafanya wawe duni!

Hapa ndipo tunavuka kutoka mgongano wa kifikra na kuwa mgongano wa watu, vyombo na taasisi. Yote hata hivyo ni sehemu ya mapambano yale yale ya fikra. Ni jukumu la wale wanaoamini kuwa fikra zao zina nguvu kusimama kidete na kutosalimu amri, au kupiga magoti ya msamaha, au kurudi nyuma kwa woga!

a. Upinzani hakuna Tanzania?

Mtoa mada katangaza kwa ujasiri kuwa "Upinzani hakuna Tanzania ni Uwongo mtupu".

Naomba niangalia kwanza kichwa cha habari mkinikubalia, ili niweze kuonesha japo kwa wenye uwezo wa kuona kuwa kauli hiyo ndani yake inapingana yenyewe (has internal contradition).

= upinzani hakuna Tanzani = Sasa kama hakuna upinzani hakuna cha kujadili. Unaweza vipi kujadili kitu ambacho hakipo kihalisia au kinadharia? Mtu akija nyumbani kwako na kusema "hakuna mlango" aidha anasema kweli au anadangaya. Kwa sababu ni rahisi kumuonesha mlango ulipo au mahali ambapo mlango haupo.

= Ni uongo mtupu = Sasa kama upinzani haupo unawezaje kuwa uongo? Aidha upinzani upo na ni "uongo" au haupo na siyo uongo kwa sababu uongo hauwezi kuwa hewani! Sasa kama mtu anasema "mlango haupo, ni matundu tu kwenye mlango" hawezi kuwa anasema kweli kwa sababu aidha mlango ni mbovu, unaning'inia kwenye kona, umevunjika, au una matatizo fulani.

b. Upinzani upo au vyama vya upinzani havipo?

Mtoa hoja alipoanza kuzungumza akaanza kuonesha anachozungumzia hasa. Lakini anajichanganya kwa sababu aidha anazungumzia Upinzani, baadhi ya viongozi wa upinzani, au vyama vya upinzani. Hebu tuangalia mkanganyo huu dhahiri na wa wazi.

Vyama vyoooote vya upinzani Tanzania

Sasa, ndugu yetu zomba anasema "vyama vyoote vya upinzani Tanzania". Sasa kwa kudai kwanza kuna vyama vya upinzani, anadai mambo mawili kwamba vipi, na ni vya upinzani. Hivyo, kwa kukiri kwake mwenyewe anasema "upinzani" upo na ushahidi ni wake ni kuwepo kwa vyama vyake. Hilo peke yake linafuta sehemu ya kwanza ya kichwa chake cha habari kisemacho "upinzani hakuna".

"vilianzishwa na system",

Hata hili nalo linajibu swali lake, kuwa kama vyama vya upinzani vipo na vilianzishwa na system, anachosema kuwa system ndiyo ilianzisha upinzani. Sasa kauli yake hii ina ukweli mkubwa kuliko anavyodhania. Na tuungalie:

Ni kweli kuwa tume iliyokuwa inakusanya mawazo kuhusu mfumo wa vyama vingi ilitokana na CCM na maamuzi ya CCM. Mmojawapo wa wajumbe wake alikuwa ni Philip Marmo na nakumbuka tulivyofanya mazungumzo kuhusu ili mwaka 1990 kule Mbulu.

Matokeo yake tukaambiwa kuwa asilimia 80 ya Watanzania walitaka tuendelee na mfumo wa chama kimoja na ni asilimia 20 tu waliotaka tubadilishe. Kwenye "wengi wape" Tanzania tungeendelea kuwa na mfumo wa chama kimoja kwani miaka kumi na tano baadaye asilimia 80 ya wapiga kura waliichagua CCM na hivyo kwa namna moja kuakisi mawazo ya wakati ule japo kwa sababu tofauti.

Hivyo, kitendo cha serikali ya chama kimoja iliyokuwa na labda ambayo bado inakubalika na wananchi wengi kuamua kubadili mfumo wa kisiasa hata kama ni kutokana na nguvu zilizokuwa nje ya uwezo wake, na kukubali upinzani urudi tena nchini kilikuwa ni kitendo cha wao kuanzisha upinzani. So factually, yuko sawa ni mfumo (system) ya CCM iliyoanzisha upinzani.

Lakini kuna jambo jingine ambalo Mtoa hoja ameshindwa kutuonesha. Je mawazo ya upinzani yaani yaliyo kinyume na CCM tunayoyashuhudia leo hii na ambayo yametufikisha hapa leo ni mazao ya CCM? Je ni CCM waliotuambia tuibua maswala ya rada, Buzwagi, Richmond, ufisadi BoT n.k Kama CCM wamefanya haya basi wamerukwa na akili na kwa hakika akili zao hazina akili!

Mawazo ya upinzani hayapandikizwi na hayawezi kuanzishwa na mtu yeyote, yanatokea ndani ya mtu huyo au jamii hiyo. Kwa hilo tunaweza pia kuwapa sifa CCM. Ni kweli ni wao wamewapa watu sababu ya kuwa na mawazo ya upinzani.

Kama CCM ingekuwa inatawala vizuri, inasimamia fedha zetu vizuri, inashughulikia matatizo ya wananchi, haielei mafisadi, inatoa nafasi sawa kwa wote n.k kusingekuwa na mtu mwenye mawazo ya kipinzani. Lakini kwa vile wao (CCM) wako kinyume na maadili mema na bora ya uongozi wamesababisha watu kuwa na mawazo ya upinzani.

Hivyo kwa hilo pia mtoa hoja yuko sawa.

Lakini ndugu yetu sidhani kama tatizo lake ni upinzani per se, bali ni viongozi waupinzani. Kama hilo ndilo tatizo lake, basi naomba kutoa hoja kuwa mada ibadilishwe na iwe juu ya "viongozi wa upinzani wako kwenye System" au "Hakuna viongozi wa upinzani wasiokuwa kwenye system" kwani mada ilivyo sasa siyo tu imepotoka bali pia haina ukweli wa kimantiki, kihistoria na kihalisia.

Upinzani Tanzania upo, na si uongo kwani hilo ni kweli. Kama anataka tuzungumzie viongozi na jinsi walivyopatikana na walivyo sasa tunaweza kuendelea na mjadala huo!!!!

peace!
 
Duh,kijiji unaweza kuandika,hapa mimi nikiandika sentensi mbili tuu napoteza focus yote...nasubiri kitabu chako,unajua siku hizi TZ hakuna waandishi wa vitabu na sijui Historia yetu nani ataitunza kama hatuandiki
 
Koba na wewe unasoma kwa haraka sana.. yaani mwenzio naweza kuandika haraka lakini nasoma pole pole kweli.. wakati mwingine inabidi niyafunge kamba macho na kuyavuta yafuate maandishi!
 
...ni kweli nina hiyo tabia na ime nicost mambo mengi sana mpaka mengine nikisema huwezi amini,hata kitabu sometimes naruka pages wakati nasoma.
 
Koba na wewe unasoma kwa haraka sana.. yaani mwenzio naweza kuandika haraka lakini nasoma pole pole kweli.. wakati mwingine inabidi niyafunge kamba macho na kuyavuta yafuate maandishi!

Na wewe acha kutufunga kamba bana...hizi M.M. originals wewe una uhakika kama ni wewe tu ktk dunia nzima uliyesema hivyo na kwa nini sisi tukuamini?
 
Fikra dhaifu huweza kutawala kwa muda wote ule ambao fikra hizo zinaonekana na hudhaniwa kuwa zina nguvu. (M. M. Original quote). Watu wenye kukubali fikra dhaifu wakidhania zina nguvu, huweza kuzitetea fikra hizo hata kwa kumwaga damu. Hata hivyo fikra zenye nguvu zinapotokea lazima zigongane na fikra zile zinazoonekana zina nguvu na kumbe ni dhaifu. Mgongano huo ni wa lazima na usioepukika.

Unapotokea mgongano huo njia mojawapo ya fikra dhaifu kujitutumia ni kudai kuwa hizo fikra mpya na zenye nguvu ni fikra zile zile za awali isipokuwa zimebadilishwa tu na watu na hivyo kuziuza tena kwa lugha nyingine. Zinapozidi kutishiwa fikra dhaifu badala ya kushambulia zile fikra zenye nguvu na kujaribu kuzishinda huanza kushambulia wabeba fikra zenye nguvu na kuwafanya wawe duni!

Hapa ndipo tunavuka kutoka mgongano wa kifikra na kuwa mgongano wa watu, vyombo na taasisi. Yote hata hivyo ni sehemu ya mapambano yale yale ya fikra. Ni jukumu la wale wanaoamini kuwa fikra zao zina nguvu kusimama kidete na kutosalimu amri, au kupiga magoti ya msamaha, au kurudi nyuma kwa woga!

a. Upinzani hakuna Tanzania?

Mtoa mada katangaza kwa ujasiri kuwa "Upinzani hakuna Tanzania ni Uwongo mtupu".

Naomba niangalia kwanza kichwa cha habari mkinikubalia, ili niweze kuonesha japo kwa wenye uwezo wa kuona kuwa kauli hiyo ndani yake inapingana yenyewe (has internal contradition).

= upinzani hakuna Tanzani = Sasa kama hakuna upinzani hakuna cha kujadili. Unaweza vipi kujadili kitu ambacho hakipo kihalisia au kinadharia? Mtu akija nyumbani kwako na kusema "hakuna mlango" aidha anasema kweli au anadangaya. Kwa sababu ni rahisi kumuonesha mlango ulipo au mahali ambapo mlango haupo.

= Ni uongo mtupu = Sasa kama upinzani haupo unawezaje kuwa uongo? Aidha upinzani upo na ni "uongo" au haupo na siyo uongo kwa sababu uongo hauwezi kuwa hewani! Sasa kama mtu anasema "mlango haupo, ni matundu tu kwenye mlango" hawezi kuwa anasema kweli kwa sababu aidha mlango ni mbovu, unaning'inia kwenye kona, umevunjika, au una matatizo fulani.

b. Upinzani upo au vyama vya upinzani havipo?

Mtoa hoja alipoanza kuzungumza akaanza kuonesha anachozungumzia hasa. Lakini anajichanganya kwa sababu aidha anazungumzia Upinzani, baadhi ya viongozi wa upinzani, au vyama vya upinzani. Hebu tuangalia mkanganyo huu dhahiri na wa wazi.

Sasa, ndugu yetu zomba anasema "vyama vyoote vya upinzani Tanzania". Sasa kwa kudai kwanza kuna vyama vya upinzani, anadai mambo mawili kwamba vipi, na ni vya upinzani. Hivyo, kwa kukiri kwake mwenyewe anasema "upinzani" upo na ushahidi ni wake ni kuwepo kwa vyama vyake. Hilo peke yake linafuta sehemu ya kwanza ya kichwa chake cha habari kisemacho "upinzani hakuna".

Hata hili nalo linajibu swali lake, kuwa kama vyama vya upinzani vipo na vilianzishwa na system, anachosema kuwa system ndiyo ilianzisha upinzani. Sasa kauli yake hii ina ukweli mkubwa kuliko anavyodhania. Na tuungalie:

Ni kweli kuwa tume iliyokuwa inakusanya mawazo kuhusu mfumo wa vyama vingi ilitokana na CCM na maamuzi ya CCM. Mmojawapo wa wajumbe wake alikuwa ni Philip Marmo na nakumbuka tulivyofanya mazungumzo kuhusu ili mwaka 1990 kule Mbulu.

Matokeo yake tukaambiwa kuwa asilimia 80 ya Watanzania walitaka tuendelee na mfumo wa chama kimoja na ni asilimia 20 tu waliotaka tubadilishe. Kwenye "wengi wape" Tanzania tungeendelea kuwa na mfumo wa chama kimoja kwani miaka kumi na tano baadaye asilimia 80 ya wapiga kura waliichagua CCM na hivyo kwa namna moja kuakisi mawazo ya wakati ule japo kwa sababu tofauti.

Hivyo, kitendo cha serikali ya chama kimoja iliyokuwa na labda ambayo bado inakubalika na wananchi wengi kuamua kubadili mfumo wa kisiasa hata kama ni kutokana na nguvu zilizokuwa nje ya uwezo wake, na kukubali upinzani urudi tena nchini kilikuwa ni kitendo cha wao kuanzisha upinzani. So factually, yuko sawa ni mfumo (system) ya CCM iliyoanzisha upinzani.

Lakini kuna jambo jingine ambalo Mtoa hoja ameshindwa kutuonesha. Je mawazo ya upinzani yaani yaliyo kinyume na CCM tunayoyashuhudia leo hii na ambayo yametufikisha hapa leo ni mazao ya CCM? Je ni CCM waliotuambia tuibua maswala ya rada, Buzwagi, Richmond, ufisadi BoT n.k Kama CCM wamefanya haya basi wamerukwa na akili na kwa hakika akili zao hazina akili!

Mawazo ya upinzani hayapandikizwi na hayawezi kuanzishwa na mtu yeyote, yanatokea ndani ya mtu huyo au jamii hiyo. Kwa hilo tunaweza pia kuwapa sifa CCM. Ni kweli ni wao wamewapa watu sababu ya kuwa na mawazo ya upinzani.

Kama CCM ingekuwa inatawala vizuri, inasimamia fedha zetu vizuri, inashughulikia matatizo ya wananchi, haielei mafisadi, inatoa nafasi sawa kwa wote n.k kusingekuwa na mtu mwenye mawazo ya kipinzani. Lakini kwa vile wao (CCM) wako kinyume na maadili mema na bora ya uongozi wamesababisha watu kuwa na mawazo ya upinzani.

Hivyo kwa hilo pia mtoa hoja yuko sawa.

Lakini ndugu yetu sidhani kama tatizo lake ni upinzani per se, bali ni viongozi waupinzani. Kama hilo ndilo tatizo lake, basi naomba kutoa hoja kuwa mada ibadilishwe na iwe juu ya "viongozi wa upinzani wako kwenye System" au "Hakuna viongozi wa upinzani wasiokuwa kwenye system" kwani mada ilivyo sasa siyo tu imepotoka bali pia haina ukweli wa kimantiki, kihistoria na kihalisia.

Upinzani Tanzania upo, na si uongo kwani hilo ni kweli. Kama anataka tuzungumzie viongozi na jinsi walivyopatikana na walivyo sasa tunaweza kuendelea na mjadala huo!!!!

peace!
Mwanakijiji, unaandika (haraka) kuliko unavyosoma, kama ulivyokubali mwenyewe hapo juu!

Mimi nakuomba usome ninacho-kiandika, sina haja ya kusoma yoooooote, uliyoyaandika, kwa kuwa hujuwi unachokiandika, kwa sababu "unaandika haraka kuliko unavyosoma" na wala si lazima kusoma unayo-yaandika kama hujuwi nilicho-kiandika.

Cha muhimu ni hoja yangu, kuwa, "upinzani hakuna" na sababu zangu ni: "viongozi wa upinzani, mrema , lipumba, mbowe na sharifu, wote ni system. Na nimetaja kwa majina.

Au hujuwi system ni nini?
 
Uelevu wangu wa system lazima uwe kwenye system ili uwe na system na hata ukisimama mwenyewe unaweza kuwa system-Zomba hayumo kwenye hizo za kwanza(he is intuitive)anadondokea kwenye single system-Au wewe zomba haujui System?
 
IMAO, Jee, huijuwi system ni nini?
 
Back
Top Bottom