Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Fikra dhaifu huweza kutawala kwa muda wote ule ambao fikra hizo zinaonekana na hudhaniwa kuwa zina nguvu. (M. M. Original quote). Watu wenye kukubali fikra dhaifu wakidhania zina nguvu, huweza kuzitetea fikra hizo hata kwa kumwaga damu. Hata hivyo fikra zenye nguvu zinapotokea lazima zigongane na fikra zile zinazoonekana zina nguvu na kumbe ni dhaifu. Mgongano huo ni wa lazima na usioepukika.

Unapotokea mgongano huo njia mojawapo ya fikra dhaifu kujitutumia ni kudai kuwa hizo fikra mpya na zenye nguvu ni fikra zile zile za awali isipokuwa zimebadilishwa tu na watu na hivyo kuziuza tena kwa lugha nyingine. Zinapozidi kutishiwa fikra dhaifu badala ya kushambulia zile fikra zenye nguvu na kujaribu kuzishinda huanza kushambulia wabeba fikra zenye nguvu na kuwafanya wawe duni!

Hapa ndipo tunavuka kutoka mgongano wa kifikra na kuwa mgongano wa watu, vyombo na taasisi. Yote hata hivyo ni sehemu ya mapambano yale yale ya fikra. Ni jukumu la wale wanaoamini kuwa fikra zao zina nguvu kusimama kidete na kutosalimu amri, au kupiga magoti ya msamaha, au kurudi nyuma kwa woga!

a. Upinzani hakuna Tanzania?

Mtoa mada katangaza kwa ujasiri kuwa "Upinzani hakuna Tanzania ni Uwongo mtupu".

Naomba niangalia kwanza kichwa cha habari mkinikubalia, ili niweze kuonesha japo kwa wenye uwezo wa kuona kuwa kauli hiyo ndani yake inapingana yenyewe (has internal contradition).

= upinzani hakuna Tanzani = Sasa kama hakuna upinzani hakuna cha kujadili. Unaweza vipi kujadili kitu ambacho hakipo kihalisia au kinadharia? Mtu akija nyumbani kwako na kusema "hakuna mlango" aidha anasema kweli au anadangaya. Kwa sababu ni rahisi kumuonesha mlango ulipo au mahali ambapo mlango haupo.

= Ni uongo mtupu = Sasa kama upinzani haupo unawezaje kuwa uongo? Aidha upinzani upo na ni "uongo" au haupo na siyo uongo kwa sababu uongo hauwezi kuwa hewani! Sasa kama mtu anasema "mlango haupo, ni matundu tu kwenye mlango" hawezi kuwa anasema kweli kwa sababu aidha mlango ni mbovu, unaning'inia kwenye kona, umevunjika, au una matatizo fulani.

b. Upinzani upo au vyama vya upinzani havipo?

Mtoa hoja alipoanza kuzungumza akaanza kuonesha anachozungumzia hasa. Lakini anajichanganya kwa sababu aidha anazungumzia Upinzani, baadhi ya viongozi wa upinzani, au vyama vya upinzani. Hebu tuangalia mkanganyo huu dhahiri na wa wazi.

Sasa, ndugu yetu zomba anasema "vyama vyoote vya upinzani Tanzania". Sasa kwa kudai kwanza kuna vyama vya upinzani, anadai mambo mawili kwamba vipi, na ni vya upinzani. Hivyo, kwa kukiri kwake mwenyewe anasema "upinzani" upo na ushahidi ni wake ni kuwepo kwa vyama vyake. Hilo peke yake linafuta sehemu ya kwanza ya kichwa chake cha habari kisemacho "upinzani hakuna".

Hata hili nalo linajibu swali lake, kuwa kama vyama vya upinzani vipo na vilianzishwa na system, anachosema kuwa system ndiyo ilianzisha upinzani. Sasa kauli yake hii ina ukweli mkubwa kuliko anavyodhania. Na tuungalie:

Ni kweli kuwa tume iliyokuwa inakusanya mawazo kuhusu mfumo wa vyama vingi ilitokana na CCM na maamuzi ya CCM. Mmojawapo wa wajumbe wake alikuwa ni Philip Marmo na nakumbuka tulivyofanya mazungumzo kuhusu ili mwaka 1990 kule Mbulu.

Matokeo yake tukaambiwa kuwa asilimia 80 ya Watanzania walitaka tuendelee na mfumo wa chama kimoja na ni asilimia 20 tu waliotaka tubadilishe. Kwenye "wengi wape" Tanzania tungeendelea kuwa na mfumo wa chama kimoja kwani miaka kumi na tano baadaye asilimia 80 ya wapiga kura waliichagua CCM na hivyo kwa namna moja kuakisi mawazo ya wakati ule japo kwa sababu tofauti.

Hivyo, kitendo cha serikali ya chama kimoja iliyokuwa na labda ambayo bado inakubalika na wananchi wengi kuamua kubadili mfumo wa kisiasa hata kama ni kutokana na nguvu zilizokuwa nje ya uwezo wake, na kukubali upinzani urudi tena nchini kilikuwa ni kitendo cha wao kuanzisha upinzani. So factually, yuko sawa ni mfumo (system) ya CCM iliyoanzisha upinzani.

Lakini kuna jambo jingine ambalo Mtoa hoja ameshindwa kutuonesha. Je mawazo ya upinzani yaani yaliyo kinyume na CCM tunayoyashuhudia leo hii na ambayo yametufikisha hapa leo ni mazao ya CCM? Je ni CCM waliotuambia tuibua maswala ya rada, Buzwagi, Richmond, ufisadi BoT n.k Kama CCM wamefanya haya basi wamerukwa na akili na kwa hakika akili zao hazina akili!

Mawazo ya upinzani hayapandikizwi na hayawezi kuanzishwa na mtu yeyote, yanatokea ndani ya mtu huyo au jamii hiyo. Kwa hilo tunaweza pia kuwapa sifa CCM. Ni kweli ni wao wamewapa watu sababu ya kuwa na mawazo ya upinzani.

Kama CCM ingekuwa inatawala vizuri, inasimamia fedha zetu vizuri, inashughulikia matatizo ya wananchi, haielei mafisadi, inatoa nafasi sawa kwa wote n.k kusingekuwa na mtu mwenye mawazo ya kipinzani. Lakini kwa vile wao (CCM) wako kinyume na maadili mema na bora ya uongozi wamesababisha watu kuwa na mawazo ya upinzani.

Hivyo kwa hilo pia mtoa hoja yuko sawa.

Lakini ndugu yetu sidhani kama tatizo lake ni upinzani per se, bali ni viongozi waupinzani. Kama hilo ndilo tatizo lake, basi naomba kutoa hoja kuwa mada ibadilishwe na iwe juu ya "viongozi wa upinzani wako kwenye System" au "Hakuna viongozi wa upinzani wasiokuwa kwenye system" kwani mada ilivyo sasa siyo tu imepotoka bali pia haina ukweli wa kimantiki, kihistoria na kihalisia.

Upinzani Tanzania upo, na si uongo kwani hilo ni kweli. Kama anataka tuzungumzie viongozi na jinsi walivyopatikana na walivyo sasa tunaweza kuendelea na mjadala huo!!!!

peace!

Kama hii dunia isingekuwa na vichwa kama hivi nadhani watu wengi wangebaki kwenye stone age na kulaumu system (ice age) kwa hali zao mbaya na matatizo yao yasiyoisha.

Mwanakijiji asante kwa post. Nafurahi kusoma insight badala ya ngonjera za Mdhihiri kwenye report za bunge.
 
mwafrika wa kike, kulikoni? I thought I am onyour ignore list! ulinihukumu bila kunipa fursa ya kujiteteya! Jee, huijuwi system ni nini?
 
IMAO, Jee, huijuwi system ni nini?

Sasa mbona unanitukana? IMAO mwenyewe😀! Hauko kwenye system, haujui system...IMAO na System yako mwenyewe.

Upinzani upo, mwongo ni wewe mwenye thematics usiyoielewa mwenyewe...it is beyond your system of Ideas.

You have failed to convey the Subject matter with your platitude!
You have shown lack of coherence apparently with your nebulous subject.
Its Hypocritical, deceptive,invented and furthermore daub!

Wewe Unajua system ndio nini?
 
Sasa mbona unanitukana? IMAO mwenyewe! Hauko kwenye system, haujui system...IMAO na System yako mwenyewe.

Upinzani upo, mwongo ni wewe mwenye thematics usiyoielewa mwenyewe...it is beyond your system of Ideas.

You have failed to convey the Subject matter with your platitude!
You have shown lack of coherence apparently with your nebulous subject.
Its Hypocritical, deceptive,invented and furthermore daub!

Wewe Unajua system ndio nini?
Loooh, kwanza, kama unaona nimekutukana naomba unisamehe sana.

nakuomba unisamehe, sina niya ya kukutukana wewe wala mwingine yeyote.

Nawaomba wana JF wanaopitia hapa, wamueleweshe huyu mtu ni nini maana ya IMAO.

Kwa nijuavyo mimi, ilikuwa ni furaha na kuisifu post yako, na kwa kifupi nilicheka sana, ndiyo maana nikakwambia IMAO, yaani, I laughed My Ass Of.

Kama kwa muono wako ni tusi, naomba nisamehe saaana. Au huijuwi system ni nini?
 
Zomba hili la kutuambia upinzani haupo Tanzania na umeweka na system,miye haliingii akilini kabisa. Tuna wabunge 40 toka vyama vya upinzani,kule Unguja na Pemba zikapigwa kura za maruwani wakati wa uchaguzi moja,mbunge wa CCM kapata kura 450,kama utakumbuka. Kashfa za BOT,buzwagi,Richmonduli zikaletwa na wapinzani bungeni.Wale wachama cha kijani,wakashikwa na woga wa kuongea,watetea haki wakaongea bila woga. Hoja yako haina nguvu,ukizingatia marehemu ndiye alikupa info wewe pekee yako. How can we trust you. Njoo na hoja zenye mantiki,sio unazuka tu
 
shukurani, natanguliza shukurani zangu kwa at least kutowa muono wako.

Kweli kabisa haliwezi likakuingiya akilini, si akili zote zenye uwezo wa kubadilisha mawazo hasa kwa wakipendacho. Tumeona watu wengi wakiteteya maovu na mabaya kwa kuwa ni yao.

reeya postss zangu za hapo juu, labda utaelewa nina maana gani.

Na wapi nilisema kuwa ni mimi tuu niliyeambiwa hayo? Ni mimi nilyeweza kuyaweka wazi na kuna wengi wameambiwa na wengi wanayajuwa hayo.
 
Ahaa haa, ah wapi wazuishie wengine bwana, nani alikwambia mimi nilitumia pesa kuchaguliwa DARUSO? Zusha lingine ndugu yangu. Kwanza CCM yenyewe ilivyogoigoi ina habari hata na DARUSO?
Kitila ni kijana wa ccm tena wa siku nyingi,ata kule daruso kugombea alitumwa na umoja wa vijana wa ccm, ndio maana ata baada ya lumaliza tu urais wake aligombea uongozi wa umoja wa vijana na kimsingi alikuwa anaelekea kuachiwa uenyekiti wa vijana wa ccm tatizo ni ukosefu wake tu wa subira.Nachojua ata mwenyekiti wa sasa wa uvccm ni rafiki yake mkubwa na wanapendana sana hawa kwa kiwango ambacho ata alimwachi kitila uenyekiti wa East Afrika Youth Forums.Hakuna mahali unaweza msikia Kitila au Mwenyekiti wa UVCCM wanapingana,ata ukiangalia mada za kitila humu jambo hukuti mahali anaipaka jumuhia ya vijana
 
Kitila kwani umemsahau huyo mtoto wa mafisadi ooops "mkulima" anavyozusha mambo hapa kuanzia zile kashfa za kutunga kwa kina Slaa na mgogoro wa chadema etc.

Wengine tulikuwa tumeamua kumpa mkono aongee nao (talk to the hand) maana pumba zake hapa muda mwingine ni kupoteza muda kuzijibu. Katika yote eti ccm wampe Kitila pesa agombee DARUSO then nini kifanyike!? Mambo mengine yanatia kichefuchefu kusoma ati?
Acha kudandia treni kwa mbele,ulikuwepo enzi hizo Kitila anagombea urais wa Daruso?.Kitila alipewa na ccm hela ambazo offcourse sio nyingi,nakumbuka ilikuwa ni kama shilingi laki nane,na hizo ndio zilimfanya aweze kumrithi patrick maleva urais wa daruso.Kuna jamaa mmoja kwa jina la Samweli ndio aligombea na Kitila .yeye hakuwa na pesa ila alimchachafya sana Kitila.
 
Fisadi Mtoto umekuja na kasi sana . Mimi ni mtu wa kuangalia kumbukumbu.Nilizo nazo zinaonyesha kwamba waliwahi kuja hapa wakata issue ambao walikuwa kazini kweli kweli .Achilia wewe unaye babaisha lakini yaliwafika wakiondoka kimya kimya .Na wewe naanza kukuhesabia post utakimbia soon maana unao watetea watakuangusha sasa hivi . Tuendelee ila utakumbuka maneno yangu hii ni JF inahitaji utulivu kila utakapo kuandika .
 
Saluti wakuu wangu,

Kwa kweli pengine hoja zinaweza kuwa zinapishana sehemu ndogo tu na pengine mwanzilishi wa thread anasumbuliwa na matatizo flani kifikra ambayo kwa shule iliyotukuka kutoka wajenga hoja wa JF basi tunaweza kupata tiba kwa huyu jamaa.Labda tujiulize maswali yafuatayo,

Je,Nini maana na dhima ya chama chochote cha upinzani?

Je,ili chama cha upinzani kiitwe CHAMA CHA UPINZANI muundo au anzishwaji wake unatakiwa uwe au usiwe katika Mazingira gani?

Je,Chama cha upinzani kulingana na mazingira ya Tanzania hakistahili kuongozwa na watu kutoka kanda fulani ikiwa vimekidhi masharti yote ya usajili?

Je,kwa sasa ili uone kama Tanzania kuna upinzani unadhani vinatakiwa vifananaje?
 
Acha kudandia treni kwa mbele,ulikuwepo enzi hizo Kitila anagombea urais wa Daruso?.Kitila alipewa na ccm hela ambazo offcourse sio nyingi,nakumbuka ilikuwa ni kama shilingi laki nane,na hizo ndio zilimfanya aweze kumrithi patrick maleva urais wa daruso.Kuna jamaa mmoja kwa jina la Samweli ndio aligombea na Kitila .yeye hakuwa na pesa ila alimchachafya sana Kitila.

Habari hii ingetolewa na mwanaccm mwingine hapa tofauti na wewe ingeaminiwa. Kama inatoka kwako ambaye mara kwa mara unaonekana ukiwa na Manji jr (wana JF wanajua anachofanya Manji kwa watu kama wewe) basi ni vigumu sana kukuamini.
 
Mwafrika wa kike ,Kula tano.
Kumbe huyu fisadi mtoto ndio zake hizo? pamoja na tano zangu Mwafrika wa kike nakulaumu kwa kuchelewa kutuhabarisha juu ya huyu jamaa (wa Manji jr.) maana tusingepoteza muda wetu kujibu hoja zake za kichovu.
 
Yeye Mwenyewe anajua hicho na huwa anatabia ya kujisahau sana kuwa wengi hapa wanajua hilo pia. Wengi wanaomjua walikuwa wamempuuzia na mimi nilikuwa namfichia siri kabla hajaanza kwenda personal na kuleta habari za uongo na upuuzi dhidi ya Kitila hapa.

Kuna mengi tu hapa yapo juu ya huyu ndugu subiria ikifika weekend yote yatawekwa hapa hadharani kama kawaida ya JF.
 
Upinzani wa kweli upo na huenda upinzani uliowekwa na kitu kinachoitwa "System" upo pia. Mimi siujui upinzani uliowekwa na system, lakini kutolijua jambo haina maana kuwa halipo! Ndio maana chama tawala kimeendelea kuuzidi maarifa upinzani wa kweli ktk masuala makubwa! Haya ya BOT,Buzwagi na Richmond na mengineyo yatakayokuja yamedhihirisha upinzani wa kweli Tanzania upo.
 
Acha kudandia treni kwa mbele,ulikuwepo enzi hizo Kitila anagombea urais wa Daruso?.Kitila alipewa na ccm hela ambazo offcourse sio nyingi,nakumbuka ilikuwa ni kama shilingi laki nane,na hizo ndio zilimfanya aweze kumrithi patrick maleva urais wa daruso.Kuna jamaa mmoja kwa jina la Samweli ndio aligombea na Kitila .yeye hakuwa na pesa ila alimchachafya sana Kitila.

Wewe ona aibu wewe, najua huu uongo hapo ulipo unakuasha mpaka chini! Uchaguzi wa DARUSO utumie laki nane wakati wetu kwa kazi gani? Nimeshakwambia zusha lingine maana kwa hili wanaojua ukweli jinsi nilivyochaguliwa wanazidi kukudharau na wataacha bure kusoma posts zako!
 
Midas kwa namna ya CCM inavyo tumia pesa kama ambazo zinaelezwa hapo juu na matumizi ya Usalama na Polisi kuiba kura lazima wabakie madarakani .Na katiba pia ujue imezima mengi so wakishindwa si wa ajili ya u system hapana hata kidogo . Pesa na matumizi mabaya ya madaraka .Upinza sasa upo labda hapo nyuma unaweza kuwa ulikuwa na matatizo lakini Upinzani upo .
 
Nini ajenda ya upinzani kuhusu maendeleo ya nchi..Tunajua wamekuwa wakikichambua chama tawala..Je wao watafanya nini wakiingia Ikulu??
 
Nini ajenda ya upinzani kuhusu maendeleo ya nchi..Tunajua wamekuwa wakikichambua chama tawala..Je wao watafanya nini wakiingia Ikulu??

1. Kwanza hawatakuwa mafisadi.
2. Hawataingia mikataba iliyojaa uozo kama sasa
3. Hawatawanyanyasa wapinzani wa wakati huo (sisiem) kwa kuwapiga mabomu au kuwatisha wanachama wake.
4 Wabunge watafanya kazi bila kushurutishwa au kutishwa na chama chao.
5. Watajenga nchi kizalendo, madini na rasimali nyingine zitagawanywa sawa kwa kila raila na kipaumbele kitakuwa kwa masikini.

6. Mpiga debe kama wewe hawatakuwepo maana kazi watakazofanya zitakuwa zinatosha kuwatangaza pia hata haita nyamazishwa JF

7. Hata JF itakosa cha kukosoa badala yake itakuwa inaifia
8. Tanzania itakuwa Super Tiger Economy
 
Nini ajenda ya upinzani kuhusu maendeleo ya nchi..Tunajua wamekuwa wakikichambua chama tawala..Je wao watafanya nini wakiingia Ikulu??

Unaonaje kama ungeuliza swali hilo baada ya kusoma sera zao kisha kukosoa au kutaka ufafanuzi pale inapohitajika?Kwanza kujumuisha "VYAMA VYA UPINZANI" as if unamzungumzia mtu mmoja kunalifanya swali lako kuwa gumu zaidi.Lakini unaweza kurahisisha majibu pia kwa kuangalia NINI KINA-MISS KATIKA SERA,MIPANGO,ITIKADI,etc za CCM then uzilinganishe na chama cha upinzani kimoja baada ya kingine.

Lakini tukiachana na habari za sera ambazo siku zote zinaweza kuwa nzuri bali utekelezaji wake,tuangalie LEADING FIGURES katika vyaa husika.Nikurahisishie hapo:Hivi unaweza kukumbuka mara ngapi JK ameahidi KUCHUKUA HATUA DHIDI YA WALA RUSHWA (kwa kumbukumbu ya karibu ni siku ile aliposema anawajua lkn anawapa muda wajirekebishe,then pale dodoma kwenye mkutano mkuu wa ccm ambapo alidai kuwa kuna watu thelathini kama sijakosea ambao watafikishwa mbele ya sheria) NA HATUJAONA LOLOTE HADI LEO?Iko wapi ile orodha ya vigogo wa madawa ya kulevya?Look how Dr SLAA na ZITTO,hawakuishia kutoa ahadi za kuwataja mafisadi bali waliwataja hadharani.

Pengine kwa kifupi,hilo linaweza kukupa mwanga wakati unatofautisha mambo
 
Back
Top Bottom